MAKABIDHIANO YA WAZIRI OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI

MAKABIDHIANO YA WAZIRI OFISI YA RAIS NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI

April 12, 2016

ofi1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (Gavu) akikabidhiana Ofisi na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makeme Mwadini katika ukumbi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi IkuluMjini Zanzibar baada ya uteuzi wa Mawaziri na Naibu Mawazi wapya kwa Wizara mbali mbali za Serikali.[Picha na Ikulu.]
ofi2
Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makeme Mwadini akitoa shukurani kwa wafanyakazi wakati wa kukabidhi Ofisi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (Gavu) katika ukumbi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ikulu  Mjini Zanzibar baada ya uteuzi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya kwa Wizara mbali mbali za Serikali.[Picha na Ikulu.]
ofi3
Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makeme Mwadini akitoa shukurani kwa wafanyakazi wakati wa kukabidhi Ofisi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (Gavu) (katikati) katika ukumbi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ikulu  Mjini Zanzibar baada ya uteuzi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya kwa Wizara mbali mbali za Serikali.[Picha na Ikulu.]
ofi4
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa haji Ussi (Gavu) akitoa nasaha zake kwa Wafanyakazi wakati wa makabidhiano ya Ofisi na aliyekuwa Waziri ya Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini leo katika ukumbi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ikulu  Mjini Zanzibar baada ya uteuzi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya kwa Wizara mbali mbali za Serikali,[Picha na Ikulu.]
ofi5
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (Gavu) na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makeme Mwadini (katikati) wakiombewa dua baada ya makabidhiano ya Ofisi katika ukumbi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ikulu  Mjini Zanzibar baada ya uteuzi wa Mawaziri na Naibu Mawaziri wapya kwa Wizara mbali mbali za Serikali.[Picha na Ikulu.]
ofi6
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (Gavu) na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makeme Mwadini (katikati) wakipeana na Makatibu (kulia) Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum na Katibu wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Haroub Shaibu Mussa kwa kuwatakia Kheri na mafanikio  baada ya makabidhiano ya Ofisi katika ukumbi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ikulu  Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
LIGI KUU KUENDELEA KESHO

LIGI KUU KUENDELEA KESHO

April 12, 2016

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania inatarajiwa kuendelea kesho Jumatano, kwa michezo miwili ya viporo kuchezwa katika viwanja vya Manungu Turiani mkoani Morogoro na uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans wanaoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, watakua wenyeji wa Mwadui FC inayokamata nafasi ya sita katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Wakata miwa wa Turiani, Mtibwa Sugar walio katika nafsi ya nne ya msimamo wa ligi kuu watawakaribisha Azam FC walio juu yao nafasi ya tatu, mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Manungu Turiani mkoani Morogoro.

WAZIRI MAHIGA APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MABALOZI WATEULE WA SUDANI KUSINI NA JAMHURI YA CZECH.

April 12, 2016

Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Augustine Mahiga (kulia) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Jamhuri ya Czech, Mhe. Pavel Rezac, na kisha kufanya nae mazungumzo yaliyojikita katika kukuza ushirikiano kati ya Tanzania na Jamhuri ya Czech. 
Waziri Mahiga akizungumza na Balozi Mteule Mhe. Pavel Rezac 
Waziri Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Jamhuri ya Czech Mhe. Pavel Rezac.
Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Augustine Mahiga (kulia) akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudani Kusini, Mhe. Mariano Deng Ngor, na kisha kufanya nae mazungumzo yaliyojikita katika kukuza Ushirikiano katika sekta mbalimbali kati ya Tanzania na Jamhuri ya Sudani Kusini. 
Waziri Mahiga akizungumza na Balozi Mteule Mhe. Mariano Deng Ngor 
Waziri Mahiga (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Jamhuri ya Sudani Kusini Mhe. Mariano Deng Ngor (wa tatu kutoka kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Balozi Samwel Shelukindo (wa kwanza kushoto), Afisa Ubalozi wa Sudani Kusini nchini (wa pili kutoka kulia) na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Eric Ngilangwa (wa kwanza kulia). 

Picha na Reginald Philip.
UJUMBE WA MAWAZIRI NA WAFANYABIASHARA WA CZECH REPUBLIC WAFANYA KONGAMANO LA UWEKEZAJI DAR ES SALAAM

UJUMBE WA MAWAZIRI NA WAFANYABIASHARA WA CZECH REPUBLIC WAFANYA KONGAMANO LA UWEKEZAJI DAR ES SALAAM

April 12, 2016


2
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Misitu  wa Serikali ya Czech Republic Bw. Dusan Benza akizungumza katika kongamano la wafanyabiashara wa nchi hiyo na watanzania lililofanyika leo kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
Mawaziri wawili Kilimo na Viwanda wa Jamhuri ya Jamhuri ya Czech  wakiongozana na wafanyabiashara zaidi ya thelathini wako nchini kwa ajili ya kutafuta na kujionea fursa za uwekezaji  nchini Tanzaniam  Mkutano huo umeandaliwa kwa pamoja na Tanzania Investiment Bank (TIB), Ubalozi wa Szech Republic nchini Kenya na Tanzania House Of Business Company Limited (THB).
Ujumbe huo metembelea wizara ya Kilimo na wizara ya Viwanda na Biashara  na kusaini mikataba ya ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji hapa nchini na nchi ya Szech Republic ili kuunganisha masuala ya kibiasha na uwekezaji na kuwezesha wafanyabiashara wa nchi hizi kuwekeza katika masuala ya biashara, Teknolojia  na Kilimo kwa ujumla.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
3
Balozi wa Heshima na Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic hapa nchini  John Chaggama  akizungumza na mmoja wa viongozi wa ujumbe huo huku   Marian Jureck Waziri wa Kilimo wa Czech akisikiliz kwa makini.
4
Injinia Michal Basovnik  wa kampuni ya Impuls  akitoa mada kuhusu shughuli mbalimbali zinazotolewa na kampuni yao ambayo ina tawi pia nchini Zambia.
5 7
Injinia Martin Adamuska  wa kampuni ya NWT kutoka nchini Czech Republic akifafanua jambo wakati alipokuwa akielezea mambo mbalimbali yanayofanya na kampuni yao lakini pia fursa mbalimbali zinazoweza kuwekezwa.
8
Injinia Petr Pawlica wa wa kampuni ya PAWLICA pia ametoa mada katika kongamano hilo na kuelezea teknolojia ya kampuni hiyo katika masuala ya Kilimo.
9
Bw. Godffrey Kirenga wa SAGCOT CENTER LIMITED akiwaelezea wafanya biashara hao juu ya fursa mbalimbali zilizopo hapa nchini katika uwekezaji wa kilimo.
10
 Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa Tanzania Private Sector Foundation(TPSF) Godfrey Simbeye akizungumza katika kongamano hilo kulia ni  John Chaggama Balozi wa Heshima na Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic nchini Tanzania.
11 12
Kutoka kulia ni Mr Charles Chandika Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tanzania House Of Business Company Limited, Pan Arnold  Mturi Charge de Affairs at the Szech Consolate  nchini Tanzania, Elipina Makungu na Bahija Salim wakijadiliana jambo wakati wa kongamano hilo la wafanya biashara.
13
Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa Tanzania Private Sector Foundation(TPSF) Godfrey Simbeye akizungumza na Pan Arnold  Mturi Charge de Affairs at the Szech Consolate  nchini Tanzania  wakimsikiliza mmoja wa maofisa kutoka wizara ya mambo ya nje wakati akizungumza nao.
14
Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa Tanzania Private Sector Foundation(TPSF) Godfrey Simbeye na  John Chaggama Balozi wa Heshima na Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic nchini Tanzania wakizungumza na Injinia Vladmir Pikora wa benki  ya Czech Export Bank mara baada ya nusu ya kwanza ya majadiliano kati ya wafanya biashara wa Tanzania na Szech Republic katika kongamano lililofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
15
 John Chaggama Balozi wa Heshima na  Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic nchini Tanzania akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu ujio wa wafanyabiashara hao.
16
Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa Tanzania Private Sector Foundation(TPSF) Godfrey Simbeye akizungumza na waandishi wa habari juu ya umuhimu wa ujio wa wafanyabiashara hao na kongamano hilo kwa wafanyabiashara wa Tanzania ya Czech Republic katika masuala mazima ya kibiashara na uwekezaji.
17
Baadhi ya wafanyabiashara kutoka nchini Czech Republic wakiwa katika kongamano hilo lililofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam
18 19
Baadhi ya wafanyabiashara wa Tanzania wakihudhuria kongamano hilo.
20
Baadhi ya waalikwa kutoka taasisi mbalimbali za Tanzania masuala ya biashara na uwekezaji wakiwa katika kongamano hilo.
21
 John Chaggama Balozi wa Heshima na Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic nchini Tanzania akimsikiliza Pan Arnold  Mturi Charge de Affairs at the Szech Consolate  nchini Tanzania.
22
Elipina Makungu na Bahija Salim wakifurahia  jambo wakati wa kongamano hilo la wafanyabiashara wa Czech Republic na Tanzania kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MBUNGE WA VITI MAALUUM WA CHADEMA JIJINI DAR LEO

April 12, 2016

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mh. Freeman Mbowe, wakati walipowasili kwenye viwanja vya Karimjee, kulikofanyika shughuli ya kutoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo, Jijini Dar es salaam. Marehemu Christina Lissu Mughwai, alifikwa na umauti mwishoni mwa wiki iliyopita, kutokana na Maradhi ya Kansa yaliyokuwa yakimsumbua.Kushoto ni Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisaini kitabu cha Maombolezo ya Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, na Mkewe Mama Jannet Magufuli, wakisalimiana na baadhi ya waheshimiwa wabunge waliokuwepo kwenye shughuli ya kutoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo, Jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akimpa pole, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mh. Freeman Mbowe, kufuatia msiba wa Mbunge wa Chama chake, Marehemu Christina Lissu Mughwai.
 Mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ukuwasili kwenye ukumbi wa Karimjee leo, Jijini Dar es salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akimpa, akimfariji Mh. Tundu Lissu, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambaye ni Kaka wa Marehemu Christina Lissu Mughwai.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, akimfariji Mh. Tundu Lissu, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambaye ni Kaka wa Marehemu Christina Lissu Mughwai.Kulia ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, akifuatiwa na Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli.
  Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambaye ni Kaka wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, Mh. Tundu Lissu, akisoma wasifu wa Marehemu, wakati wa shughuli ya kuaga mwili wake, leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam.
 Mtoto wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, Veronica Mallya akitoa taarifa fupi juu ya Mama yake.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akimfariji Mtoto wa Christina Lissu Mughwai, mara baada ya kutoa taarifa ya Mama yake.





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Christina Lissu Mughwai, ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo kwenye Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es salaam. Marehemu Christina Lissu Mughwai, alifikwa na umauti mwishoni mwa wiki iliyopita, kutokana na Maradhi ya Kansa yaliyokuwa yakimsumbua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akiagana Mh. Tundu Lissu, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki ambaye ni Kaka wa Marehemu Christina Lissu Mughwai.