KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE ZA PAC NA LAAC ZAENDELEA NA VIKAO VYAKE LEO MJINI DODOMA

KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE ZA PAC NA LAAC ZAENDELEA NA VIKAO VYAKE LEO MJINI DODOMA

August 30, 2017
_Y2A1391
Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Mussa Mbaruku akizungumza jambo pale kamati hiyo ilipokutana na viongozi kutoka Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, kwa lengo la kuwapitisha Wajumbe wa kamati kuhusu hesabu za fedha za Taasisi husika, katika kikao kilichofanyika leo Mjini Dodoma. kulia ni Mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Juma Aweso
_Y2A1409
Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Japhet Hasunga akiongoza kikao cha kamati hiyo pale  ilipokutana na viongozi kutoka Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, kwa lengo la kuwapitisha Wajumbe wa kamati kuhusu hesabu za fedha za Taasisi husika, katika kikao kilichofanyika leo Mjini Dodoma.
_Y2A1442
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakifuatilia mazungumzo baina yao na Viongozi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi lengo likiwa ni kupitia Mahesabu na Maagizo ya kamati hiyo, katika kikao kilichofanyika leo Mjini Dodoma kikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Naghenjwa kaboyoka(katikati).
_Y2A1472
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Mhe. Vedasto Ngombale (katikati) akiongoza kikao cha kamati hiyo dhidi ya viongozi kutoka Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Hazina na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika kikao kilichofanyika leo Mjini Dodoma.kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Abdallah Chikota na kulia ni katibu kamati wa Bunge, Ndg. Dismiss Muyanja
PICHA NA OFISI YA BUNGE

ZAIDI YA WAKAZI 3000 JIJINI TANGA KUNUFAIKA NA MIRADI YA MAJI YA TANGA UWASA

August 30, 2017
ZAIDI ya wakazi 3000 wanaoishi katika eneo la Jaribu tena na Mwisho wa Shamba kata ya Maweni Jijini Tanga wanatarajiwa kuepukana na adha ya uhaba wa maji safi na salama iliyodumu kwa muda mrefu baada ya Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa mazingira Jijini Tanga kuwa pelekea mradi wa maji.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurungenzi Mtendaji wa Tanga UWASA Mhandisi Joshua Mgeyekwa alisema kuwa mradi huo unaotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.
 
Alisema kuwa gharama za mradi huo hadi kukamilika kwake ni kiasi cha sh Mil98,lakini kutoka na gharama kuwa kubwa waliwashauri  wananchi ili kuona namna watakavyoweza kufanya kazi za kujitolea ili kukamilika kwa wakati.
 
Alisema kuwa ndipo wananchi walipoamua kushiriki katika kazi za kuchimba mitaro ambayo itaweza kutumika kwa ajili ya kupitisha miundombinu ya mabomba kutoka Pongwe hadi katika maeneo hayo yenye uhitaji.

“tunawashukuru wananchi kwa ushirikiano waliounyesha wa kushiriki kwenye uchimbaji huo kwani wameweza kuokoa kiasi cha sh Mil 10 ambazoingebidi tuwalipe vibarua kwa ajili ya uchimbaji wa mitaro hiyo”alisema Mgeyekwa.
 
Alisema kuwa mradi huo umegawanyika katika awamu ambapo katika awamu ya kwanza unatarajiwa kusambaza maji katika umbali wa Km 5.5 kutoka eneo la Pongwe hadi katika mitaa ya Jaributena na Mwisho wa shamba.

Nae Mbunge wa Jimbo la Tanga Mussa Mbaruku alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo kwa haraka kutaweza kusaidia wananchi hao kuepukana na adha ya ukosefu wa maji iliyodumu kwa muda mrefu.
 
“Niwapongeze wananchi wa kata ya Maweni namna walivyoweza kujitolea kushirikina na serikali yao katika kumaliza changamoto zinazowakabili kwani hii inaonyesha kuwa ili kuharakisha maendeleo ya sehemu husika kunahitaji ushirikishwaji wa pande zote”alisema Mbunge Mbaruk.

Kwa upande wake Mtendaji wa Kata wa mtaa wa kichangani Ziada Ali alisema kuwa wakazi wa mtaa huo walilazimika kutembea umbali wa Km 5kwa ajili ya kutafuta huduma hiyo kila siku.
 
Alisema kuwa mradi huo utakapo kuwa umekamilika itakuwa ni faraja kwa wananchi wa mitaa ya Jaribu tena na Mwishi wa shamba pamoja na kuwapunguzu adha ya kwenda mwendo mrefu kwa ajili ya kutafuta huduma ya maji.

Vile vile Mwenyekiti wa Kamati ya Maji  Lucas Nyengo alisema kuwa kwa takribani miaka minne wamekuwa wakiomba kupatiwa huduma hiyo lakini wanashukuru kwa awamu hii kupatiwa mradi huo.

Alisema kuwa kufuatia shida ya maji ilidumu kwa muda mrefu waliamuakuunga mkono jitihada za mamlaka kwa kushiriki katika uchimbaji wa mtaro ili kuharakisha mradi huo.
 
Alisema kuwa kutokana na shida ya maji iliyokuwa inawakabili
walilazimika kununua  ndoo moja kwa kiasi cha sh 500 jambo ambalo ni gharama kubwa ukilinganisha na uhitaji wa huduma hiyo

Tigo yakabidhi kisima chenye thamani ya 18m/- kijiji cha Rorya Mara

August 30, 2017

Mkurugenzi wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kanda ya ziwa, Ally Maswanya akizungumza na wanahabari na wananchi kabla ya kukata utepe wa uzinduzi wa kisima mapema mwishoni wa wiki iliyopita.


Mbunge wa Rorya- Lameck Airo akipampu maji wakati wa sherehe za uzinduzi wa kisima chenye thamni ya Tsh.18/- milioni kilichodhaminiwa na kampuni ya Tigo.


 


Mkuu wa wilaya Rorya- Samson Chacha akitwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha  Nyasoro, Penina Bailes

RAIS DKT MAGUFULI ASITISHA UBOMOAJI WA NYUMBA 300 TUANGOMA JIJINI DAR LEO.

August 30, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda Wamesitisha zoezi la BOMOA BOMOA kwa Nyumba zaidi ya elfu kumi na saba (17, 000) zilizotangazwa KUBOMOLEWA na Baraza la Hifadhi ya Mazingira NEMC.

Hatua ya kusitisha zoezi hilo, Imekuja kufuatia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda kuzungumza na Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kuhusiana na Sintofahamu ya bomoa bomoa hiyo ambayo amemueleza Mhe Rais Magufuli kuwa Taarifa za BOMOA BOMOA ya Nyumba elfu kumi na saba iliyotolewa HAIKUFIKA ofisini Kwake, Jambo ambalo ni tofauti na Taratibu za Utendaji kazi wa Serikali.

Mhe Makonda amesema, hata kama TAMKO hilo limetolewa na watumishi wa Mkoa mfano Wakurugenzi wa Manisapaa au Wakuu wa Wilaya walioko Chini ya Mamlaka ya Mkuu wa Mkoa LAZIMA Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ipate taarifa na iridhie bomoa bomoa hiyo, na pia hata kama Taarifa zimetoka Wizarani inapaswa taratibu za kimaandishi zifuatwe kwa kujulisha Ofisi ya Mkoa.

"haiwezekani mtu kutoa TAMKO la kuvunja Nyumba elfu kumi na saba bila Mkoa kujua, hilo HALIWEZEKANI" amesema Mhe Makonda.

Mhe Makonda amefafanua kuwa AMEONGEA na Mhe Rais Magufuli na Kumuuliza kama ana taarifa za zoezi la Ubomoaji wa Nyumba elfu kumi na saba ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda ALIMUELEZA Mhe Rais Magufuli kuwa HANA taarifa hizo za UBOMOAJI, zaidi Ubomoaji wa Nyumba zilizo kwenye Hifadhi ya Barabara ya kuanzia Ubungo kwenda KIMARA na MBEZI Ubomoaji unaofanywa kwa ajili ya upanuzi wa Barabara ya Morogoro, Ubomoaji wa Nyumba zilizo Jirani na Reli hususani ni zile zinazohusiana na Ujenzi wa Reli Mpya na ya Kisasa.

Kutokana na Sababu hizo, Mhe Makonda amesema Mhe Rais amesikitishwa na TAMKO hilo la kutaka KUBOMOLEWA kwa Nyumba zaidi ya elfu kumi na saba na ametoa pole kwa Wananchi waliokumbwa na TAHARUKI ya TAMKO hilo la Ubomoaji, na kusisitiza kuwa Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli HAKUCHAGULIWA kwa ajili ya KUBOMOA Nyumba za watu na kusisitiza kuwa anataka wananchi WANAOISHI katika maeneo HALALI kuachwa mana AMEPATA taarifa kuwa huenda ZOEZI hilo lingekwenda mbali zaidi mpaka kwa Wananchi WASIOHUSIKA.

Katika HATUA nyingine, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda AMEPIGA MARUFUKU zoezi lolote UBOMOAJI wa Nyumba pasipo Ofisi yake kupewa TAARIFA na kisha KURIDHIA Ubomoaji huo.

Mwisho, Mhe Paul Makonda AMEWATAKA wananchi na wakazi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam kuzingatia SHERIA na wasivamie maeneo au kuuziwa VIWANJA na Matapeli na pia AMEWATAKA wananchi kuchukua TAHADHARI hususani ni katika maeneo yote HATARISHI ambayo sio SALAMA kwa MAKAZI na kuwataka kila Mwananchi Mwenye Familia KUTAFUTA Salama kwa Maisha yake na ya Familia yake.

Mhe Makonda Pia ametoa OMBI Maalumu Kwa Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi la KUBORESHA mfumo wa Ardhi katika Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuanzisha mpango wa kuweka MAAFISA ARDHI katika KATA zote za Mkoa wa Dar es Salaam ambao watakuwa na JUKUMU la KUSIMAMIA, KURATIBU masuala yote ya Ardhi ngazi ya KATA hatua ambayo itasaidia kuondoa Migogoro na UTAPELI kwa Wananchi kuuziwa au kununua Ardhi katika maeneo ambayo HAYARUHUSIWI, ambapo amesema amepata wazo hilo kutokana na uzoefu aliopata akiwa Rais wa umoja wa Vyuo vikuu -TAHILISO ambapo alishirikiana na Bodi ya Mikopo kuanzisha mfumo wa kuwa na MAAFISAMikopo katika vyuo hatua iliyosababisha kuondoa kero ya wanafunzi kufuatilia Mikopo katika Ofisi za bodi ya Mikopo hatua ambayo imekuwa mwarobaini wa tatizo la kufuatilia Mikopo kwa wanafunzi, Mhe Makonda amesema atamwandikia OMBI hilo na kulifikisha Rasmi kwa Mhe Lukuvi ili amsaidie kulifikisha kwa Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili utekekezaji.

Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
30/08/2017 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi wa Tuangoma wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam  na kusitisha bomoa bomoa iliyokuwa ikiendelea katika eneo hilo. Pia  amewaomba kujiepusha na kujenga nyumba za kuishi katika maeneo hatarishi.
MAYANGA AMWITA EMMANUEL MARTIN TAIFA STARS

MAYANGA AMWITA EMMANUEL MARTIN TAIFA STARS

August 30, 2017
Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Mayanga amemwongeza Kiugo wa Young Africans, Emmanuel Martin kwenye kikosi chake kinachojindaa kucheza na Botswana Jumamosi Septemba 2, mwaka huu.
Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam chini ya utaratibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Emmanuel Martin anatarajiwa kujiunga na kambi ya Taifa Stars mara moja leo Agosti 30, mwaka huu na kuanza na mazoezi na wenzake yatakayofanyika jioni kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Emmanuel Martin ameongezwa na Mayanga baada ya mawasiliano kuonesha kwamba huenda akawakosa nyota wa kimataifa Simon Msuva kutoka Difaa El Jadidah ya Morocco na Orgenes Mollel wa FC Famalicao ya Ureno.
Taarifa kutoka Morocco inaonesha kwamba Msuva ana kibali cha muda cha kuingia na kutoka Morocco ‘visa’ ambacho kinamnyima haki ya kutoka na kuingia Morocco mara kwa mara.
Kuna juhudi zinafanywa na timu yake kadhalika Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco kumfanikishia kupata kibali cha muda mrefu ili iwe rahisi kwa mchezaji kutoka na kuingia kama anahitaji katika timu ya taifa.
Kuhusu Mollel taratibu za ruhusa za kimataifa zinafanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria za nchi ya Ureno ambako anacheza soka la kulipwa.
Nyota wengine wote wameripoti Taifa Stars wakiwamo wale wa kutoka nje ya mipaka ya Tanzania kama vile Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Elias Maguli (Dhofar FC/Oman), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya) wakati Farid Mussa wa CD Tenerif ya Hispania anatarajiwa kutua leo.
Wengine ambao wako kambini Hoteli ya Sea Scape iliyoko Kunduchi, Dar es Salaam ni makipa Aishi Manula (Simba SC), Mwadini Ally (Azam FC) na Ramadhani Kabwili (Young Africans).
Pia wamo Walinzi ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphas Maganga (Mbao FC), Kelvin Yondani (Young Africans), Salim Mbonde (Simba SC) na Erasto Nyoni (Simba SC).
Viungo ni Himid Mao - Nahodha Msaidizi (Azam FC), Mzamiru Yassin (Simba SC), Said Ndemla (Simba SC), Shiza Kichuya (Simba SC), wakati Washambuliaji ni Raphael Daud (Young Africans) na Kelvin Sabato (Azam FC).
Benchi la Ufundi la Mayanga linaundwa na yeye mwenyewe ambaye ni Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny Msangi (Meneja), Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt. Gilbert Kigadye (Daktari wa Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).

JKT MGULANI YACHANGIA DAMU HOSPITALI YA RUFAA YA TEMEKE NA KUFANYA USAFI

August 30, 2017
 Mkuu wa   Kikosi  cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) namba 831 KJ Mgulani, Luteni Kanali, Zacharia Godfrey Kitani, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu askari wa kikosi hicho kujitolea damu na kufanya usafi  katika maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 tangu lianzishwe Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),ambayo yatafikia kilele chake kesho kutwa nchini kote. 
MSHINDI WA SHILINGI MILIONI 30 YA DROO YA JUMAPILI YA JACKPOT YA TATU MZUKA AKABIDHIWA FEDHA ZAKE

MSHINDI WA SHILINGI MILIONI 30 YA DROO YA JUMAPILI YA JACKPOT YA TATU MZUKA AKABIDHIWA FEDHA ZAKE

August 30, 2017
1.JPEG
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akifafanua jambo katika kikao na Kamati ya Bunge ya Miundombinu kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Moshi Kakoso na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Mawasiliano wa Wizara hiyo Eng. Angelina Madete.
2JPEG
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Eng. Angelina Madete akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu kuhusu miradi ya maendeleo ya mawasiliano vijijini katika kikao kilichofanyika mjini Dodoma.
3.JPEG
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Moshi Kasoso, akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Kamati hiyo katika kikao kilichowakutanisha na uongozi wa Wizara ya  Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) mjini Dodoma. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Eng. Edwin Ngonyani.
4.JPEG
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Dua Nkurua, akitoa maoni  kuhusu ufikishaji wa mawasiliano vijijini kwa viongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (hawapo pichani) katika kikao na Kamati hiyo mjini Dodoma. Kushoto kwake ni Mjumbe wa Kamati hiyo Mhe. Bhagwanji Meisuria na kulia ni Katibu wa Kamati hiyo Bw. Richard Masuke.
5.JPEG
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Eng. Peter Ulanga akiwaonesha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu maeneo ya vijijini yaliyofikiwa na mawasiliano katika kikao na Kamati hiyo mjini Dodoma. Kulia ni Mhe. Dua Nkurua na kushoto ni Mhe. Rita Kabati wajumbe wa Kamati hiyo.
……………………….
Serikali imesema kuwa imetumia shilingi Bilioni 85 kupeleka mawasiliano vijijini kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kuzipatia ruzuku kampuni za simu za mkononi ili kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata huduma za mawasiliano.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwenye Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu mjini Dodoma.
“Mfuko huu unaendelea kuhakikisha kuwa mawasiliano bora yanafika katika maeneo mengi nchini hususan vijijini na kwenye maeneo ambayo hayana mvuto wa kibiashara ambapo Takwimu zinabainisha kuwa, tayari mawasiliano   yamefikishwa kwenye kata 443, vijiji 1,939  kuanzia mwezi Machi 2013 hadi Julai mwaka huu”, amefafanua Naibu Waziri Ngonyani.
Ameongeza kuwa tayari Mfuko umetiliana saini mkataba na kampuni za simu za mkononi mwezi Agosti mwaka huu kuhakikisha kuwa zinapeleka mawasiliano kwenye kata nyingine 75 na vijiji 154.
Aidha, ametanabaisha kuwa hadi hivi sasa asilimia 94 ya wananchi wanapata huduma ya mawasiliano nchini na kuongeza kuwa, Serikali kupitia mkataba wake na Kampuni ya Simu ya Halotel imefikisha mawasiliano kwenye jumla ya vijiji 3,069 kati ya vijiji 4,000 tangu walipoanza utekelezaji wa jukumu hilo mwezi Novemba, 2015 na wanatarajia kukamilisha kazi hiyo ifikapo mwezi Novemba mwaka huu.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu Mhe. Moshi Kakoso, amezitaka kampuni za simu za mkononi zinazopeleka mawasiliano vijijini na maeneo yasiyokuwa na mvuto wa kibiashara ambazo zinapatiwa ruzuku na Serikali kuhakikisha kuwa zinatoa taarifa sahihi kwa Mfuko huo ikiwemo hatua zilizofikiwa za ujenzi na usimikaji wa minara na uwepo wa mawasiliano kwenye vijiji husika.
 Amewataka UCSAF kujitangaza na kuweka mabango yao kwenye minara yote nchini iliyojengwa kupitia ruzuku ya Serikali ili kuwawezesha wananchi kutambua uwajibikaji wa Serikali katika kufikisha mawasiliano kwa wananchi wake.
Naye, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Eng. Angelina Madete, amesema kuwa Wizara kupitia UCSAF itahakikisha kuwa kila mwananchi anafikiwa na mawasiliano kuendana na jukumu la msingi la Mfuko huo la kufikisha mawasiliano kwa wote.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo Eng. Peter Ulanga, amewahakakikishia wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu kuwa Taasisi yake itashirikiana na wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuhakiki kazi zilizofanywa na kampuni za simu za mkononi za ujenzi na usimikaji wa minara na uwepo wa mawasiliano kwenye vijiji mbalimbali nchini.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MSHINDI WA SHILINGI MILIONI 30 YA DROO YA JUMAPILI YA JACKPOT YA TATU MZUKA AKABIDHIWA FEDHA ZAKE

August 30, 2017
 Balozi wa Mchezo wa Tatu Mzuka, Mussa Hussein (kushoto), akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 30 mshindi wa droo ya Jumapili ya Jackpot ya Tatu Mzuka, Tausi Mashombo jijini Dar es Salaam jana, aliyojishindia kutoka katika mchezo wa Tatu Mzuka ambao umejizolea umaarufu kwa kutoa washindi kila saa. Jackpot hiyo inaendelea Jumapili hii kwa mshindi kujishindia shilingi milioni 80.

NAIBU KATIBU MKUU-BARA AFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE KUTOKA CHAMA CHA CPC CHA CHINA, LEO

August 30, 2017
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM-Bara- Rodrick Mpogolo (kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Xu Lyuping (kulia), katika ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM-Bara- Rodrick Mpogolo (wapili kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Xu Lyuping (kulia), katika ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa KIanali mstaafu Ngemela Lubinga.
 Ujumbe wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM_Bara Rodrick Mpogo na ujumbe wa Naibu Waziri wa mamambo ya Nje wa CPC, wakishangilia baada ya mazungumzo kumalizika. 
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM-Bara- Rodrick Mpogolo akiagana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Xu Lyuping baada ya mazungumzo yao katika ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. (Picha na Bashir Nkoromo).
 Naibu Katibu Mkuu akimsindikiza mgeni wake baada aya mazungumzo hayo
  Naibu Katibu Mkuu akimsindikiza mgeni wake baada aya mazungumzo hayo
  Naibu Katibu Mkuu akimsindikiza mgeni wake baada aya mazungumzo hayo
  Naibu Katibu Mkuu akimsindikiza mgeni wake baada aya mazungumzo hayo