MHE. RIDHIWAN KIKWETE AVUNJA UKIMYA, AZUNGUMZIA KUHUSU MAKONTENA NA MALI ANAZODAIWA KUMILIKI...

December 25, 2015

Ndugu zangu waandishi wa habari, nimeamua kuwaita ili kuzungumza nanyi kuhusu baadhi ya mambo yaliyokuwa yanasemwa katika vyombo vya habari kuhusu mimi.

Awali ya yote napenda kusema kuwa habari hizo ni UONGO mtupu, ni mambo yanayozushwa na waandishi wa habari hizo kwa nia ya kuchafua jina langu kwa sababu wanazozijua wanaoandika. UKWELI ni kwamba haya ni mambo yenye kufanywa kwa nia na dhamira mbaya dhidi yangu na hata familia yangu.

Hivi karibuni, kwa mfano, lipo gazeti moja liliandika na kutoa picha yangu na mtu mmoja waliyedai ni Mhe. Paul Makonda eti akinifunga kamba za viatu. Katika maelezo yake mwandishi akadai kuwa Mhe. Makonda alipata uteuzi kuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni kwa sababu hiyo. Huu ni uongo usiokuwa na hata chembe ya ukweli. Napenda watanzania wajue kuwa hakuna wakati wowote Baba yangu alipokuwa Rais wa nchi yetu alinihusisha kwa namna yeyote ile katika uteuzi wa mtu yeyote katika Serikali. Hivyo basi kujaribu kunihusisha na uteuzi wa Mhe. Paul Makonda kuwa Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni ni jambo lisilokuwa na ukweli wowote.

Pili, Yule mtu anae onekana katika ile picha siyo Mhe. Paulo Makonda  bali ni Bwana Deogratius Kessy anayefanya kazi katika kampuni ya ushonaji na mavazi ya Bwana Sheria Ngowi. Nilishona safari suti kwenye kampuni hiyo. Nilipokwenda kuchukua nguo yangu na nilipovaa ili kuona kama imeshonwa vizuri, Bwana Sheria Ngowi alitaka nivae viatu vya ngozi. Bahati mbaya nilikuwa nimevaa sandals hivyo  akaamua kunipa viatu vya dukani kwake nivae. Wakati bwana Deogratius Kessy akinisaidia kuvaa viatu ndipo ile picha ikapigwa nampiga picha wa kampuni ya Bwana Sheria Ngowi , inashangaza na kusikitisha kuona picha hiyo inatumiwa kupotosha ukweli kwa kutoa maelezo ya uongo. Ni dhahiri kwamba mwandishi aliamua kufanya hivyo kwa maksudi mazima ya kutoa sifa mbaya kwangu na kwa Mheshimiwa Paul Makonda. Hivi ndivyo uhuru wa habari unavyostahili kutumika ?

Siku za nyuma gazeti lingine liliandika eti kuwa nilihojiwa kuhusu sakata la makontena bandarini. Napenda kuwaambia ndugu waandishi wa habari  kuwa sijawahi kuhojiwa na mtu yeyote, chombo chochote au kamati yeyote kuhusu madai hayo. Ni uongo usiokuwa na ukweli wowote. Ni mambo ya kugushi na uzushi kabisa, Ninayasema maneno haya kwa kujiamini na kama mwandishi ana uthibitisho wa  madai yake autoe hadharani watu wauone. Aidha, nasema kama yupo mtu aliyenihoji ajitokeze kukanusha ninayoyasema, Namtaka aseme wazi.  Nawahakikishia kuwa mtu huyo hayupo na wala  hatakuwepo.

Ndugu waandishi na watanzania wenzangu, inaelekea kuna mtu au genge la watu mahali Fulani ambao wameamua na kudhamiria kuchafua jina langu na la familia yangu kwa kutumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Tangu Serikali ya awamu ya tano ianze jitihada za kuwabana watu wanaokwepa kulipa kodi za Serikali bandarini wapo watu wamekuwa wakifanya jitihada za kunihusisha na watu Fulani wanaotuhumiwa kuhusika na ukwepaji huo. Wapo baadhi ya watu wamekuwa wakidai eti baadhi ya makontena hayo ni yangu. Na, wapo waliodai eti kuwa nimekuwa nawasaidia baadhi ya wafanyabiashara hao kukwepa kodi kwa kutoa maagizo kwa maofisa wa forodha wasiwatoze kodi inayostahili kulipwa.
Napenda kuwafahamisha kuwa sijawahi kuagiza bidhaa zozote kutoka nje hivyo sijawahi kuwa na kontena lolote ambalo nililowahi kutakiwa kulipia ushuru nikakwepa.Aidha, sijawahi kumuombea msamaha wa kutokulipa au hata kupunguziwa kodi mfanyabiashara yeyote au mtu yeyote aliyeingiza kontena nchini kutoka nchi za nje.Kama mtu ana ushahidi autoe hadharani mimi niuone na dunia iuone. Nawahakikishia ushahidi huo haupo na wala hautokuwepo. Labda uwe wa kugushi na wakifanya hivyo wataumbuka.

Napenda pia kutumia nafasi hii kusema kuwa sina na wala sijawahi kumiliki lori au basi wakati wowote katika maisha yangu. Aidha, sina hisa au ubia na mtu yeyote au kampuni yeyote ya malori au mabasi. Nayasema haya kwa sababu wapo wabaya wangu wanaoeneza maneno ya kunihusisha na kumiliki malori na mabasi. Pia kunihusisha na baadhi ya makampuni yanayomiliki na kuendesha biashara ya malori na mabasi.  

Ndugu wanahabari, napenda kusema kwa kurudia na kusisitiza kuwa sina lori wala basi hata moja na sina ubia na wafanyabiashara ama makampuni yoyote yanayofanya shughuli hizo. kama yupo mtu yeyote ana ushahidi wa kuhusika kwangu auweke hadharani watu wauone. Napenda ieleweke kuwa kama ningekuwa na ubia wa namna hiyo nisingekuwa na sababu ya kuficha. Niogope kitu gani ? Ukweli ni kwamba sizuiliwi kufanya biashara kama nikipenda kufanya hivyo , Hata kwa nafasi yangu ya sasa ya uongozi yaani mbunge bado sina kizuizi. Mbona Bungeni wapo wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo. Isingekuwa ajabu kwangu kufanya biashara hivi sasa mimi pamoja na kuwa mbunge ni mwanasheria wa kujitegemea na nimeiweka katika TAMKO langu la mali na madeni la viongozi kwa mujibu wa sheria ya maadili ya viongozi.

Nimewavumilia sana lakini sasa nimechoka, nimeona leo nivunje ukimya. Nimeona niseme kidogo kwani bila ya kufanya hivyo nitaliacha genge la watu wenye nia mbaya na mimi waonekane wanasema kweli. Wahenga wanasema msema pweke hushinda! Nikiendelea kukaa kimya uongo wao utageuka kuwa ukweli dhidi yangu.

Naambiwa hapa nchini siku hizi kila jengo jipya linalojengwa linasemekana ni la Ridhiwani, kituo kipya cha petrol ni cha Ridhiwan.
Nimeanza kuona athari za uongo huo, Siku moja kuna mtu alikuja kuniomba nimpangishe katika lile jengo la PSPF pale stesheni. Nilipomuuliza nitampangishaje akasema mbona watu wamemwambia ni jengo langu!? Siku nyingine nikakutana na jamaa mmoja mwenye asili ya kiasia akiwa anahema. Akasema ananiomba sana niache kutaka kupora kampuni yake,nikamuuliza kampuni gani hiyo? Na kwanini anasema hivyo? Akanijibu, anasikia wakisema kampuni yake ni ya ridhiwani wakati kampuni hiyo hata yeye kairithi kwa baba yake na yeye alirithi kwa baba yake zaidi ya miaka hamsini iliyopita, Nikamwambia kuwa habari hiyo si kweli,  sina mpango huo na wala sina sababu ya kufanya hivyo. Hayo ni maneno yanayoenezwa na wabaya wangu walioamua kunipakazia kwa sababu wazijuazo wao. Tukaachana ,sijui kama ameamini kama sina mpango wa kumpora kampuni yake. Siku moja Mzee wangu mmoja wa kwetu kijijini alinilalamikia kuwa nina roho mbaya kwa vile sitaki kumpa kazi mwanae kwenye kampuni yangu ya malori wakati yeye ni dereva mzuri, Nilipomueleza Yule mzee kuwa sina lori hata moja akashangaa na kusema mbona watu wanasema nina malori mengi. Ndugu zangu mnaiona fitina kubwa inavyotengenezwa katika jamii kuhusu maneno haya, Wapo wanaoniona mimi FISADI, Wapo wanaoniana mimi nina Roho mbaya, Wapo wanao niona mie nataka kupora mali zao. Baada ya Baba kustaafu maneno yamekuwa mengi na yanazidi kupata kasi. kila kukicha wanazua jambo jipya.  Nimeoa niyaseme haya ili watu wajue  ukweli wa upande wangu.

Naomba nimalize kama nilivyoanza kwamba yanasemwa mengi lakini ni  maneno ya uzandiki, uzushi na ni uongo mtupu usiokuwa na chembe ya ukweli. Wale wanaosema, kuandika, na kueneza maneno hayo wanajua kuwa wanasema UONGO, ila wanafanya hivyo kwa vile wana nia mbaya dhidi yangu na familia yangu , Naomba watanzania muyapuuze maneno hayo, naomba watanzania wenzangu muupuuze uongo huo.
siko hivyo, sina mali hizo na wala sifanyi hayo wanayodai nafanya na wala sina mpango wa kuyafanya.

Imetolewa na:-
      Ridhiwan J. Kikwete
Mbunge wa Jimbo la Chalinze.
chanzo:Michuziblog
WAZIRI NAPE NNAUYE AWATAKA WATANZANIA KUENDELEA KUMUOMBEA RAIS DK JOHN POMBE MAGUFULI, KAZI YA KUTUMBUA MAJIPU NI NGUMU NA INA VIKWAZO VINGI

WAZIRI NAPE NNAUYE AWATAKA WATANZANIA KUENDELEA KUMUOMBEA RAIS DK JOHN POMBE MAGUFULI, KAZI YA KUTUMBUA MAJIPU NI NGUMU NA INA VIKWAZO VINGI

December 25, 2015

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye aliyekuwa mgeni rasmi akimuwakilisha Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan akizindua rasmi albam mbili za kwaya ya Wakorintho wa Pili kwenye tamasha la Krismas lililofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee leo, ambapo mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika ya Kusini Rebecca Malope amefanya onesho kubwa lililovuta hisia za mashabiki wengi waliohudhuria katika tamasha hili akishirikiana na waimbaji mbalimbali wa hapa nyu mbani na nchi jirani ya Kenya.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Nape Nnauye amewaomba watanzania kuzidi kumuombea Rais Dk . John Pombe Magufuli kwa kazi ya kutumbua majipu ambayo amekwishaianza kwani kazi hiyo ni ngumu na ina vikwazo vingi, lakini pia amewataka watanzania na waumini wa madhehebu mbalimbali kuwaombea wasaidizi wake ili waweze kuwa bega kwa bega na Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli ili kutekeleza kazi hii kwa ufanisi na kisha watanzania wafaidi matunda na rasilimali zao wenyewe.

Waimbaji kutoka Kenya walikuwa ni Faustine Munishi na Sara K na Solomon Mukubwa kutoka jiji la Nairobi huku waimbaji wa hapa nyumbani wakiwa ni Rose Muhandom Upendo Nkone, Christine Shusho, Edson Mwasabwite, Joshua Mlelwa na wengine wengi, Tamasha hilo pia lilikuwa na lengo la kumshukuru mungu kwa nchi yetu ya Tanzania kufanya uchaguzi kwa amani, Kulia ni Akex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ambayo ndiyo imeandaa tamasha hilo.(PICHA NA JOHN BUKUKU- FULLSHANGWEBLOG-DAR ES SALAAM)
Akex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ambayo ndiyo imeandaa tamasha hilo. akimkaribisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye ili kuzungumza na wananchi katika tamasha hilo kushoto ni Mbunge Martha Mlata na MC Mwakipesile mshereheshaji wa Tamasha hilo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye akiwahutubia wananchi na mashabiki waliohudhuria katika tamasha hilo katikati ni Akex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ambayo ndiyo imeandaa tamasha hilo na kushoto ni MC Mwakipesile.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye akiimba moja ya mapambio na kuitikiwa na mashabiki wa nyimbo za injili waliohudhuria katika tamasha hilo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye pamoja na maaskofu na viongozi mbalimbali wakishiriki katika sala maalum ya maombi iliyofanyika katika tamasha hilo,
Wamumini na mashabiki mbalimbali wa muziki wa injili wakishiriki katika maombi maalum ya kumshukuru mungu yaliyofanyika kwenye tamasha hilo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs Rhobi Nape Nnauye wakicheza pamoja na mwimbaji Upendo Nkone kutoka kulia ni Mbunge Martha Mlata na Alex Msama wakishiriki kucheza.
 
Mwimbaji Rebecca Malope akiimba katika tamasha hilo.
Waimbaji wa mwimbaji Rebecca Malope akiimba katika tamasha hilo.
Mwimbaji Rebecca Malope akiimba kwa hisia huku meza kuu pamoja na mashabiki wake wakiwa wamesimama.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs Rhobi Nape Nnauye akicheza na mwimbaji Rebecca Malope wakati wa tamasha hilo. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs Rhobi Nape Nnauye akicheza na mwimbaji Rebecca Malope wakati wa tamasha hilo kulia ni mbunge wa viti maalum mkoa wa mbeya Mary Majelwa na kulia ni Mbunge Martha Mlata.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs Rhobi Nape Nnauye pamoja na maaskofu mbalimbali wakiwa wamesimama wakati mwimbaji Rebecca Malope akifanya vitu vyake katika tamasha hilo.
Mwimbaji Christine Shusho na Mbunge Martha Mlata wakiimba pamoja wakati wa Tamasha hilo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye na mkewe Mrs Rhobi Nape Nnauye,Alex Msama na Mkewe na baadhi ya wabunge kulia ni Martha Mlata na kushoto ni Mary Majelwa wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwimbaji Faustine Munishi kutoka nchini Kenya akiiimba katika tamasha hilo.
Wanakwaya wa Wakorintho wa pili wakiimba wimbo wao mara baada ya kuzinduliwa kwa albam zao katika tamasha hilo.
Mwimbaji kutoka nchini Kenya Solomon Mukubwa akiimba na mwimbaji mwenzake kutoka kushoto Sara K. huku mbunge Martha Mlata akishiriki kuimba nao.
Mwimbaji Joshua Mlelwa naye amefanya mambo makubwa jukwaani katika tamasha hilo.

Mwimbaji Rose Muhando pamoja na waimbaji wake wakifanya vuti vyao jukwaani.
December 25, 2015

Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Ali Maswanya akikabidhi misaada mbalimbali Mwenyekiti wa kamati ya shule ya kulelea watoto Yatima cha Mugeza Mseto Manispaa ya Bukoba Bi. Evelyne Mwijage juzi. Kampuni ya Tigo ilitoa misaada kwenye kituo hicho
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Ali Maswanya akikabidhi misaada mbalimbali Mwenyekiti wa kamati ya shule ya kulelea watoto Yatima cha Mugeza Mseto Manispaa ya Bukoba Bi. Evelyne Mwijage juzi. Kampuni ya Tigo ilitoa misaada kwenye kituo hicho



Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Ali Maswanya akiongea na wanahabari,viongozi  na watoto wa kituo cha kulelea watoto Yatima cha Mugeza Mseto Manispaa ya Bukoba.

Meneja wa Mauzo Mkoa wa Kagera, Sadoki Phares akiongea na wanahabari, viongozi na  watoto wa kituo cha kulelea watoto Yatima cha Mugeza Mseto Manispaa ya Bukoba.

Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Tigo Kanda ya Ziwa, Beatrice Kinabo(kushoto) na Meneja wa Duka la Tigo Bukuba, Lilian Mwise (aliyebeba mtoto).


Watoto wa Kituo cha kulelea watoto cha Mugeza Mseto Manispaa ya Bukoba wakifuatilia kwa makini.

Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Ali Maswanya akitembea na watoto wa kituo cha Mugeza mara baada ya kukabidhi misaada.A

Watoto wa Kituo cha kulelea watoto cha Mugeza Mseto Manispaa ya Bukoba wakifuatilia kwa makini.
Wasaalam photo Krantz Mwanteple C.E.O & Founder, MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Website: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Whatsapp: 0712579102 "HABARI MAKINI KWA WATU MAKINI"

RAIS DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI KIMBILIO LA WATANZANIA - WAZEE WANENA ZANZIBAR

December 25, 2015
-- ---- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 765 253 445 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''

RAIA WAAMILIFU WALILIA HUDUMA BORA KWA WAKULIMA

December 25, 2015

Na Krantz Mwantepele,

“Huku tupo tu tunahangaika na kilimo, tunalima kila mwaka, lakini ukweli ni kwamba kilimo chetu wala hakina faida basi tu bora siku ziende”

Lilikuwa ni jibu toka Alex Jonh maarufu kwa jina la “Mafuriko” mmoja wa wanaharakati na waraghbishi wa kijiji cha Lugunga, kilichopo wilaya ya Mbogwe, mkoani Geita baada ya kuulizwa swali kuhusu maendeleo ya kijiji chao na mmoja wa waandishi wa habari za mitandao Ali Masoud maarufu kwa jina la Kipanya.

Kijiji hiki kina wakazi wanakadiriwa kuwa na wakazi 3,685 wengi wao wakiwa ni wakulima wadogo wadogo. Kilimo kinaajiri karibu 75% ya wakazi wa vijijini. Lakini ni ukweli pia, ni kilimo ambacho bado kinategemea jembe la mkono na mvua na hivyo kuathiri sekta hiyo kwa kiasi kikubwa. Tukiacha hiyo pia upatikanaji wa pembejeo kwa mifumo iliyomo kwenye sera ya kilimo, bado ni changamoto kubwa.

Waraghbishi wengi ni wakulima, ingawa wapo pia walimu, viongozi wa dini, wenyeviti wa vijiji, na watendaji wa kata lakini ukweli unabaki  kwamba wengi wao wanategemea kilimo. Changamoto wanazokutana nazo wakulima ndiyo sababu inayopelekea kilimo kutokuwa cha faida hali inayowakatisha tamaa na kusema bora liende.


Mraghbishi Alex John maarufu kwa jina Mafuriko akiongea na mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Herieth Makwetta alipotembelea kijijini hapo 



Akielezea masikitiko yake kuhusu hali yetu, mraghbishi Alex John ama Mafuriko anasema:

“Ndugu zangu sisi huku tumesahaulika kabisa, kilimo chetu tunacholima ni kilimo cha bora liende maana hatuna kabisa elimu yoyote hapa kijijini. Kila mtu analima na kupanda anavyojua maana tumeshazoea maisha ya hivi.”

Katika ufafanuzi wake Mafuriko ameendelea kusema kuwa kijiji chao kina ardhi yenye rutuba na inayokubali mazao mengi yakiwemo mahindi, maharage, mpunga na karanga lakini licha ya kuwa na ardhi nzuri kama hiyo bado kilimo hakina faida kwao.

Mchora Katuni Ali Masoud (mwenye miwani) akizungumza na waraghbishi na wananchi wa kijiji cha Lugunga

Lakini ni sababu gani inayowafanya wakose faida katika kilimo chao licha ya kuwa na ardhi nzuri inayokubali zaidi ya mazao ya aina tatu. Hapo ndipo waraghbishi walipoanza kuelezea changamoto wanazokabiliana nazo.

Akifafanua ukubwa wa tatizo linalowakabili wakulima wa kijiji hapo raia mwamilifu na mraghbishi Gabriel Jonathan anasema:

“Unajua ndugu mwaandishi hapa kijijini tatizo ni moja, asilimia kubwa ni wakulima na wakulima wengi hawana elimu. Unaona, wengi wao wameishia darasa la saba na wengine hawajasoma kabisa, hivyo hata kilimo chao wanalima ili mradi msimu upite hata akilima heka mbili akatoa gunia tano kwake anaona sawa.”

Ni kweli kilimo ni suala la kitaalamu na hivyo kuna uhitaji mkubwa wa ufahamu kwa mkulima, na hapo ndipo serikali inapomwajiri Afisa Kilimo. Ambaye kimsingi ndio mwenye jukumu hilo katika kuhakikisha anawatembelea wakulima na kuwasaidia kitaalamu ili waweze kuzalisha mazao mengi na yenye ubora.

Hali hii iliibua hamu ya kutaka kujua iwapo kijijini hapo yupo Afisa wa Kilimo ama Bwana Shamba kama anavyojulikana na wengi, katika hali ya kutokuridhishwa na kiwango cha huduma anachotoa mtaalamu huyo wa mashamba, mraghbishi Mafuriko alisema,

“Bwana Shamba yupo tena yupo sana lakini hana ushirikiano kabisa na wakulima wa Lugunga, kwanza hakai hapa kijijini. Pili wengine hawamjui kabisa yaani kwa wiki anaweza kuja mara mbili au msimuone mwezi mzima ila mshahara analipwa”

Akiongezea kuhusu upatikanaji wa Afisa huyo Yohana Julius alisema:

“Tunasikia anaishi Masumbwe na anapoishi hatujui ni mtaa gani na wala mimi simjui licha ya kwamba nakaa hapa katikati (Center) hata nikikutana naye bila kuambiwa simjui je mwananchi anayeishi Mahameni itakuwaje”

Mahameni ni kitongoji kilichopo pembeni ya kijiji cha Lugunga ambapo pia bwana Shamba wa kijiji hicho anatakiwa kufika katika kutimiza wajibu wake.

Mraghbishi Gabriel (wa kwanza kushoto) akiwa na wananchi wenzake wa kijiji cha Lugunga, wakisikiliza maswali toka kwa mwandishi


Umbali wa kutoka Masumbwe hadi Lugunga ni kilometa 17 hali inayodhihirisha kuwepo umbali mrefu kati ya anapoishi Afisa kilimo huyo Dickson Silvester na kituo chake cha kazi.

Kukaa tu na kulaumu hakusaidii sana hivyo ni jukumu la waraghbishi kujua nini wanachotakiwa kufanya,  

“Mimi naona hapa tuandamane mpaka ofisi ya Mkurugenzi, yeye ni mwajiri wake na inawezekana akawa hana hata taarifa ya nini kinafanyika huku, alisikika mmoja wa wananchi aliyetambulika kwa jina moja la Hassan.

Katika hatua nyingine wananchi hao wakapaza sauti kwa kumtaka afisa kilimo huyo kurudi kuishi kijijini na kuongeza kuwa kama alikubali kuja kufanya kazi na kupokea mshahara basi akubali kuishi katika kijiji hicho cha Lugunga kama wanavyoishi wananchi alioenda kuwatumikia.

Safari ya kujua ukweli wa kwanini afisa kilimo huyo haishi katika kituo chake cha kazi ilizidi kusonga mbele na ndipo mwandishi wa makala hii alipomtafuta kwa njia ya simu na kufanya naye mahojiano yaliyodumu kwa dakika kumi na tano.

Katika mahojiano hayo afisa kilimo huyo Dickosn Silvester alikiri kuwa yeye ndiye afisa kilimo wa kijiji cha Lugunga na kukanusha taarifa za kuwa haishi katika kituo chake cha kazi.

“Mimi ni afisa kilimo wa Lugunga kweli na ninaishi hapo hapo Lugunga Center aliyekwambia siishi hapo ni nani? Mana huo ni uzushi”, alisikika akisema Dickson kwa njia ya simu wakati akiongea na mwandishi wa makala hii.

Baada ya kupata majibu ambayo hayakuniridhisha kutoka kwa afisa kilimo huyo nilirudi Lugunga kwa njia ya simu na kumtafuta mwenyekiti wa kitongoji cha Lugunga Kati (Center) bwana Mashiba Dioniz ili kupata ukweli yalipo makazi ya afisa kilimo huyo.

“Mimi ndiye mwenyekiti wa kitongoji cha hapa Senta, kwakweli mwandishi huyo afisa kilimo hana makazi hapa mimi nazijua kaya zangu zote, Ila huwa namuona mara moja kwa wiki basi ila kusema anaishi hapa ni uongo kabisa.’ Alisema Bwana Mashiba mwenyekiti wa Lugunga.

Lakini waraghbishi hawa si tu wanajaribu kufuatilia upatikanaji wa huduma za ugani katika kijiji chao, ila wameendelea kutoa elimu kwa wanakajiji wengine wa kijiji hapo. Mfano mmoja ni migogoro baina ya wakulima wenyewe. Na kwa kuwa waraghbishi hawa hawaitishi mikutano ya vijiji mara nyingi wamekuwa wakitumia maeneo ya migogoro kama sehemu yao ya kutolea elimu.

Akifafanua hilo Felix Daudi, mraghbishi mwingine katika kijiji hicho anasema,
“Kuna kesi tunakutana nazo ambazo tunazitumia pia kutoa elimu. Moja ya kesi hizo ni zile na mtu kuacha mifugo yake bila uangalizi na mwishowe inaingia kwenye mashamba ya watu na kuanza kula mazao. Utakuta mtu hajui wapi akapeleke tatizo lake ama akishaikamata mifugo hiyo afanye nayo ni nini,”

Hivyo ni vizuri watendaji wa serikali wakashirikiana na waraghbishi na muda mwingine kuwapatia ujuzi mdogo mdogo. Hii itasaidia kufanikisha shabaha ya Maendeleo kwani pande zote watakuwa wanategemeana. Na si katika hali hii ambayo watu wanashutumiana.  Hivyo ni jukumu letu sote kucheza nafasi zetu katika kusukuma gurudumu la maendeleo.


                        Moja ya mashamba ya mpunga yaliyopo katika kijiji cha Lugunga



                       CHANZO ; MWANAHARAKATI MZALENDO BLOG 

MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA MAULID DAR

December 25, 2015
 Waumini wa Dini ya Kiislam wakiandamana jijini Dar es Salaam leo jioni, wakati wa kuadhimisha Sikukuu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.W.A).PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG.