MAALIM SEIF AZIBARIKI KMKM NA SHABA NGAO YA JAMII ZANZIBAR

MAALIM SEIF AZIBARIKI KMKM NA SHABA NGAO YA JAMII ZANZIBAR

September 12, 2014


1 (19)
Makamu wa kwanza wa rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na mmoja wa wachezaji wa timu ya soka ya KMKM wakati akikagua timu hizo kwenye mchezo wa ngao ya jamii baina ya KMKM na Shaba ya Pemba kabla ya ufunguzi wa ligi kuu ya soka ya Grandmalt inayotarajiwa kuanza jumatatu tarehe 15/09/2014, KMKM ilishinda kwa mabao 2:0 dhidi ya shaba ya Pemba.
2 (13)Sehemu ya washabiki waliofurika kwa wingi kwenye uwanja wa Amani mjini Zanzibar kushudia mchezo kati ya kmkm na Shaba kwenye mchezo wa ngao ya Jamii
3 (13)Makamu wa kwanza wa rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akimkabidhi ngao ya jamii nahodha wa timu ya KMKM Khasim Ali mara baada ya kushinda mchezo dhidi ya timu ya Shaba ya pemba kwa magoli 2:0 kushoto mwenye fulana ya njano ni meneja mauzo Tanzania wa kinywaji cha Grandmalt Kassiro Msangi.
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Soka ya Grand Malt ya Visiwani hapa, KMKM juzi walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Shaba kutoka Pemba katika mchezo  wa Ngao ya Jamii uliofanyika kwenye Uwanja wa Amaan.
Ikicheza mbele ya mgeni rasmi, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Seif Shariff Hamad, KMKM ilikabidhiwa zawadi maalum ya ngao na kiongozi huyo wa nchi.
Bao la kwanza la KMKM katika mechi hiyo iliyokuwa na ushindani lilifungwa na Pandu Haji  katika dakika ya 83 huku lile lililowanyamazisha mashabiki wa Shaba waliofika uwanjani hapo liliwekwa kimiani na Faki Mwalimu sekunde chache kabla ya filimbi ya mwisho.
Hata hivyo KMKM walipoteza nafasi nyingi za kufunga katika kipindi cha kwanza kupitia kwa washambuliaji wake Mudrik Muhibu na Mwalimu ambao walishindwa kumalizia nafasi walizotengeneza.
Dakika ya 89 Shaba ilipoteza nafasi ya kusawazisha kupitia kwa mchezaji wake Suleiman Nuhu ambaye akiwa mita chache na kipa wa KMKM, Mudathir Khamis, kwa kupiga juu na kupoteza nafasi ya wazi ya kufunga.
 Mechi hiyo ya Ngao ya Jamii ilifanyika chini ya udhamini wa Kampuni ya Bia ya Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Grand Malt ambao ndio wadhamini wakuu wa ligi hiyo na ulikuwa ni maalumu kwa ajili ya uzinduzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Grand Malt Zanzibar ambayo inatarajiwa kufanyika kuanzia Septemba 15 mwaka huu.
KMKM:  Mudathir Khamis, Pandu Haji, Mwinyi Haji, Makame Haji, Khamis Ali, Ibrahim Khamis, Iddi Kambi/ Am Khamis (dk 45), Juma Mbwana, Abdi Kassim, Mudrik Muhibu/  Faki Mwalim (dk 46) na Maulid Ibrahim/  Nassor Ally (59).
Shaba: Mhando Twaha, Robert Mtuge, Hassa Shaaban, Amour Said, Mahmoud Salmin, Juma Mwalimu, Bakari Suleiman/ Kheri Shaaban (dk 56), Sheha Khamis, Mohammed Nyasa, Jackson Dickson na Suleiman Nuhu.
 NHIF YATETA NA WACHEZAJI, WATENDAJI KLABU YA YANGA

NHIF YATETA NA WACHEZAJI, WATENDAJI KLABU YA YANGA

September 12, 2014

Katibu Mkuu wa Yanga Bw. Beno Njovu akizindua semina ya Mfuko wa Bima ya Afya na Watendaji na wachezaji wa Klabu ya Yanga  iliyofanyika jana makao makuu ya klabu hiyo mtaa Jangwani katikati ni Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti na kushoto ni Christopher Mapunda Meneja wa NHIF Wilaya ya Ilala klabu ya Yanga imekuwa ya kwanza kuanza utaratibu wa kuijunga na mfuko wa Bima ya afya. 8Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti akizu.ngumza na watendaji wa Yanga na wachezaji wakati wa semina hiyo jana 9Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti akizu.ngumza na watendaji wa Yanga na wachezaji wakati wa semina hiyo jana 10Mmoja wa maofisa wa Mfuko wa Bima ya Afya akiwaonyesha makocha wa Yanga baadhi ya picha alizpoiga  nao Kulia ni kocha wa yanga Marcio Maximo. 11Christopher Mapunda Meneja wa NHIF Wilaya ya Ilala akitoa mada wakati wa semina na wachezaji wa timu ya Yanga jana. 12Baadhi ya wachezaji na maofisa pamoja na wanachama wa Yanga wakiwa katika semina hiyo. 13Baadhi ya wanachama wa Yanga wakiwa katika semina hiyo kushoto ni mwanachama wa Yanga Bw Said Hassan Kipara 14 
Mmoja wa maofisa akigawa majarida yanayoelezea faida za Mfuko wa Bima ya Afya ya jamii katika semina hiyo  17 
Ofisa   Mawasiliano mwandamizi  NHIF  Bw. Luhende Andrew Singu akizungumza na wachezaji hao jana wakati wa semina hiyo
TPDC, KAMPUNI ZA WENTWORTH, MAUREL & PROM WASAINI MKATABA WA KUUZIANA GESI

TPDC, KAMPUNI ZA WENTWORTH, MAUREL & PROM WASAINI MKATABA WA KUUZIANA GESI

September 12, 2014


1 (18) 
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (wa nne kushoto)  akipeana mkono na  Mkurugenzi Mtendaji wa  Kampuni ya  WENTWORTH  inayochimba gesi katika eneo la Mnazi Bay Mkoani Mtwara , Robert MacBean (wa tatu kushoto) mara baada ya kusaini Makubaliano ya Mkataba wa Kuuziana Gesi kati yake na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Wengine katika picha ni baadhi wa Watendaji Wakuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC na wawakilishi wa kampuni za WENTWORTH na MAUREL & PROM.
3 (12) 
Wajumbe waliohudhuria kikao cha Kusaini Mkataba wa Kuuziana Gesi kati ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na Kampuni zinazochimba gesi katika eneo la Mnazi Bay Mkoani Mtwara za WENTWORTH Resources Limited na MAUREL & PROM wakisaini MKataba huo. Anayeshuhudia mbele ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo pamoja na wawakilishi wengine kutoka kampuni hizo, TPDC, Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Kampuni zinazochimba gesi katika eneo la Mnazi Bay Mkoani Mtwara za WENTWORTH Resources Limited na MAUREL & PROM zimesaini Mkataba wa Makubaliano wa kuuziana Gesi, ambapo kampuni hizo zitaingiza gesi hiyo katika visima vilivyopo Mnazi Bay Mtwara kwa ajili ya Mradi wa Bomba la Gesi.
Kikao hicho cha Makubaliano kimeongozwa na Waziri wa Nishati na Madini,  Profesa Sospeter Muhongo Wizarani ambapo Waziri Muhongo amesisitiza kuwa, Mkataba huo ni fursa nyingine ya Kiuchumi kwa Tanzania na kuongeza kuwa, Serikali imeazimia kuingia katika biashara ya gesi na hivyo imedhamiria  kufanya biashara yenye maslahi kwa taifa na iko makini katika usimamizi na utekelezaji wa biashara hiyo.

MAFUNZO YA TIKETI ZA ELEKTRONIKI UWANJA WA TAIFA

September 12, 2014
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kesho Jumamosi (Septemba 13 mwaka huu) saa 4 asubuhi litaendesha mafunzo ya matumizi ya tiketi za elektroniki kwa wadau wa mpira wa miguu Dar es Salaam.

Mafunzo hayo Uwanja wa Taifa, na kushirikisha wasimamizi wa mechi, viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na makatibu na maofisa habari wa klabu za Azam na Yanga.

Washiriki wengine wa mafunzo hayo ni Meneja wa Uwanja wa Taifa na msaidizi wake, wasimamizi wa milangoni (stewards), waandishi wa habari wa Dar es Salaam maofisa usalama wa TFF.

Mafunzo hayo yatahitimishwa Jumapili (Septemba 14 mwaka huu) kwa mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Azam na Yanga kuanzia saa 10 kamili jioni. 

Tiketi zimeanza kuuzwa jana (Alhamisi) kupitia M-Pesa, CRDB Simbanking na maduka ya Fahari Huduma.

BONIFACE WAMBURA
MKURUGENZI WA MASHINDANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)