KESI YA BILIONEA WA MADINI YA TANZANITE UPANDE WA MASHTAKA KUWASILISHA TAARIFA ZA MASHAHIDI.

May 07, 2014


Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya mfanyabiashara bilionea wa madini ya Tanzaniete Erasto Msuya wakiingizwa mahakamani.
Na Ripota wetu , Moshi
UPELELEZI katika kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Erasto Msuya aliyeuwawa Agosti 07 mwaka jana, umekamilika ambapo May 20, mwaka huu, upande wa mashitaka unataarajiwa kuwasilisha taarifa za mashahidi waliyoyandika polisi (Commital Proceedings) mbele ya mahakama ya hakimu mkazi Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Mwendesha Mashitaka, Wakili wa serikali,  Florentina Sumawe, jana aliiambia mahakama  ya hakimu  mkazi mbele ya hakimu ,Munga Sabuni kuwa tayari upelelezi umeshakamilika na kwamba kinachosubiriwa ni Jalada lenye taarifa za mashahidi wa Jamhuri inayoandaliwa na Mahakama kuu kuwasilishwa mahakamani hapo.
 "Ikupendeze mheshimiwa Hakimu, kwamba Upeleelzi wa kesi hii
imekamilika, leo tulitarajia kusoma taarifa za mashahidi wa upoande wa mashitaka lakini haitakuwa hivyo kutokana na jalada hilo kuwa mahakama kuu, hivyo tunaiomba mahakama yako tukufu kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya zoezi hilo," alieleza Wakili Sumawe.
Akiahirisha kesi hiyo Hakimu mkazi, Munga Sabuni alisema kwa
kuzingatia taratibu za kisheria chini ya kesi za makosa ya jinai,
mahakama yake imesikiliza kwa umakini ombi la upande wa Jamhuri na hivyo basi kesi hiyo itafikishwa mahakamani hapo May 20 kwa ajili ya kutajwa.
Marehemu Erasto Msuya (43), aliuwawa kikatili Agosti 07, kwa kupigwa risasi 13, majira ya saa 6:30 mchana kando ya barabara kuu ya Arusha-Moshi, eneo la Mijohoroni,Wilaya ya Hai, Karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kufa papo hapo.
Wanaoshtakiwa 7 kuhusika ni mshtakiwa namba 1, Sharif Mohamed Athuman (31) mchimbaji mdogo wa madini na mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha, Mshitakiwa Shaibu Jumanne Saidi "Mredi" (38), mkazi wa Songambele Wilaya ya Simanjiro na Mussa Juma Mangu (30), mkazi wa Shangarai kwa mrefu mkoani Arusha.
Wengine ni  Mfanyabiashara wa madini na mkazi wa Arusha, Jalila Zuberi Said (28),mkazi wa Babati, Sadiki Mohammed Jabir "Msudani" au "Mnubi"(32), mkazi wa Dar es salaam na Lang'ata Wilayani Hai na Karim Kihundwa (33) mkazi wa Kijiji cha Lawate, Wilaya ya Siha.
Mwisho.

JESHI LA POLISI NIGERIA LATANGAZA DONGE NONO.

May 07, 2014
NA MWANDISHI WETU,ABUJA.

Jeshi la polisi nchini Nigeria limetangaza kitita cha dola za Marekani laki tatu kwa mtu atakaetoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa wanafunzi wa kike waliotekwa na Boko Haram.
 
Utekaji wa wanafunzi hao zaidi ya 200 umesababisha vilio ndani na nje ya Nigreia, na kuongeza shinikizo kwa serikali ya nchi hiyo kuwarudhisha wasichana hao. 

Hasira ziliongezeka jana, kufuatia taarifa kuwa wasichana wengine wanane walitekwa kutoka kijiji hicho cha mabli walikotekwa wa awali.

Polisi imeorodhesha nambari sita za simu katika taarifa yao na kuwataka raia wa Nigeria kupiga kwenye nambari hizo kwa taarifa.
Marekani imetuma kundi la  wanajeshi na wataalamu wengine kusaidia upatikanaji w awasichana hao. 

utekaji huo na mashambulizi mengine ya Boko Haram vimeughubika mkutano wa dunia wa kiuchumi kwa bara la Afrika, unaoanza jioni hii mjini Abuja.

PRESIDENT KIKWETE MEETS FORMER BRITISH PM GORDON BROWN AND MARK SUZMAN OF THE GATES FOUNDATION IN ABUJA, NIGERIA, TODAY

May 07, 2014


President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete shakes hands with Rt. Hon. Gordon Brown (MP), UN Special Envoy for Global Education and Former British Prime Minister in the sidelines of the World Economic Forum on Africa in Abuja, Nigeria, May 7, 2014.
President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete in a bilateral meeting with Rt. Hon. Gordon Brown (MP), UN Special Envoy for Global Education and Former British Prime Minister in the sidelines of the World Economic Forum on Africa in Abuja, Nigeria, May 7, 2014.
President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete shakes hands with Mr Mark Suzman, President of Global Policy and Advocacy and Country Programmes of the Gates Foundation after holding bilateral talks in the sidelines of the World economic Forum on Africa in Abuja, Nigeria, today May 7, 2014. Photos by State House.

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI IDARA MAALUM ZA SMZ

May 07, 2014


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dkt.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Idara Maalum za SMZ katika mkutano wa utekelezaji mpango kazi wa robo tatu ya mwaka  Machi-Julai 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Unguja leo asubuhi.
 Baadhi ya makamanda wa Idara maalum za SMZ wakimsikiliza  Waziri wa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ,Mhe,Haji Omar Kheri (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji mpango kazi wa robo tatu ya mwaka  Julai-Machi 2013/2014,mbele ya  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dkt.Ali Mohamed Shein,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Unguja leo asubuhi. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO CHA KIMATAIFA (AIPS) WAMALIZIKA JIJINI BAKU

May 07, 2014


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
A; MKUTANO MKUU AIPS
WIKI iliyopita kulifanyika Mkutano Mkuu wa Chama cha Kimataifa cha Waandishi wa Habari za Michezo (AIPS) jijini Baku, Azerbaijan.
Mkutano huo ulishirikisha viongozi wa vyama 116 vya waandishi wa habari za michezo duniani, ambapo Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kiliwakilishwa na Katibu Mkuu, Amir Mhando.
Katika mkutano huo msisitizo mkubwa umewekwa kwa nchi wanachama kutilia mkazo program za kuwaendeleza waandishi chipukizi wa habari za michezo, lakini pia AIPS yenyewe nayo pamoja na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Afrika (AIPS-Afrika) vimechukua jukumu la kusaidia kwa wale watakaokidhi vigezo wanavyohitaji.
Hivyo kila nchi mwanachama itatuma wasifu wa majina ya wanahabari chipukizi wasiozidi watano, ambao AIPS yenyewe itaangalia wale watakaofaa na kuwaandalia mafunzo baadaye mwaka huu.
Kwa upande wa AIPS Afrika yenyewe itaendesha mafunzo kwa wanahabari chipukizi 25, ambayo yatafanyika Morocco, lakini kipaumbele cha kwanza kitakuwa kwa nchi 16 zitakazocheza fainali za mataifa ya Afrika mwakani nchini humo na nafasi zingine zitabaki kwa nchi ambazo hazitaenda Morocco.
 Mafunzo ni ya wazi kwa waandishi wowote chipukizi wasiozidi umri wa miaka 25, hata wale waliopo kwenye vyuo vya uandishi wa habari wataruhusiwa kuomba. Tanzania imewahi kupata nafasi moja mwaka 2011, ambapo Mwita Mwaikenda wakati huo akiwa mwanafunzo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alishiriki mafunzo hayo yaliyoandaliwa na AIPS akiwa miongoni mwa Waafrika watatu tu waliopata nafasi hiyo.
 Utaratibu kuhusiana na suala hili utaelezwa vizuri baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji ya TASWA kitakachofanyika Jumatatu wiki ijayo kujadili masuala mbalimbali.
 B: Ziara Uganda
Kulifanyika kikao cha viongozi wa nchi wanachama wa AIPS ambao wanatoka Afrika Mashariki, ambapo nchi za Burundi, Kenya, Tanzania na Uganda zilishiriki na kukubaliana kufanyike ziara ya kimafunzo itakayohusisha waaandishi wa habari za michezo Septemba 25-29 mwaka huu Kampala, Uganda. Rwanda licha ya kutoshiriki mkutano wa AIPS, lakini tulikubaliana nayo ialikwe.
Katika makubaliano hayo kila nchi itakuwa na washiriki wasiopungua 20 na wasiozidi 35, ambapo pia litafanyika kongamano kuhusiana na masuala mbalimbali ya waandishi wa habari za michezo kwa ukanda huo na siku ya mwisho litafanyika bonanza la michezo mbalimbali. Taarifa zaidi za ziara hiyo itatolewa siku za usoni.
C; Ushirikiano wa kimafunzo
 Baadhi ya nchi zilizoshiriki mkutano huo wa 77 wa AIPS, zilikubaliana kuanzisha utaratibu wa kubadilishana utaalamu wa kitaaluma kwa nchi mbalimbali, kwa kuwatoa baadhi ya wanahabari kwenda nchi zilizo katika makubaliano hayo kujifunza kwa gharama za nchi mwenyeji. 
Hata hivyo makubaliano hayo, yataanza kufanya kazi baada ya kila nchi kupata baraka za Kamati ya Utendaji na kutuma majibu kwa waratibu kwamba wanaafiki. Kamati ya Utendaji ya TASWA katika kikao chake kijacho hilo litakuwa moja ya ajenda.
Nawasilisha
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
07/05/2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA VIONGOZI WA CCM NA WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA MGOLOLO (W) MUFINDI, IKULU DAR.

May 07, 2014


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Viongozi wa CCM Wilaya na Mufindi wlioongazana na baadhi ya Wafanyakazi wa Kiwanda cha Mgololo, wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo Mei7, 2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Viongozi wa CCM Wilaya na Mufindi wlioongazana na baadhi ya Wafanyakazi wa Kiwanda cha Mgololo, wakati walipofika Ofisini kwa Makamu Ikulu Jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa CCM Wilaya ya Mufindi na baadhi ya wafanyakazi wa Kiwanda cha Mgololo, waliofika Ofosini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa mazungumzo.

RAIS KIKWETE AWASILI ABUJA, NIGERIA, KUHUDHURIA MKUTANO WA UCHUMI DUNIANI

May 07, 2014


 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea shada la maua mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Nnamdi Azikiwe jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuria  Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa).
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na maafisa mbalimbali wa Tanzania na Nigeria jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa).
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na maafisa mbalimbali wa Tanzania na Nigeria jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa). 
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na maafisa mbalimbali wa Tanzania na Nigeria jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa).
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na maafisa mbalimbali wa Tanzania na Nigeria jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa).
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na  Waziri wa Nishati wa Nigeria Profesa Chinedu Ositadinma Nebo na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe Daniel Ole Njoolay baada ya kupokewa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Nnamdi Azikiwe jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa).
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na maafisa mbalimbali wa Tanzania na Nigeria jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa).




Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Daniel Ole Njoolay, Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Mhe. Mohammed Aboud Mohammed  baada ya kuwasili jijini Abuja, Nigeria, usiku wa Mei 6, 2014 ambako atahudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum for Africa).  PICHA NA IKULU

*MKUTANO WA WIZARA YA AFYA WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM LEO, MPANGO WA KUTOA HUDUMA PAMOJA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA WAJA

May 07, 2014

 Kaimu Mkurugenzi wa Huduma  za Kinga,kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk,Neema Rusibamayila akifungua mkutano wa tatu wa   wa siku tatu wa magonjwa yasiyopewa  kipaumbele leo unaoendelea kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam.
 Afisa  wa Program  wa Magonjwa  yasiyopewa  kipaumbele Kitaifa  kutoka Shirika  la  Afya la Dunia(WHO) Alphonsina  Nanai akizungumza jambo leo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa tatu wa siku tatu  wa magonjwa hayo unaoendelea   kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam.
 Meneja Mpango  wa Taifa wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele,Dk, Upendo Mwingira (kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk,Neema Rusibamayila(katikati) na kulia  ni Afisa  wa Program  wa Magonjwa  yasiyopewa  kipaumbele Kitaifa  kutoka Shirika  la  Afya la Dunia(WHO) Alphonsina  Nanai wakifuatilia mkutano wa tatu wa  siku tatu  wa magonjwa hayo unaoendelea   kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam.
 Mmoja  wadau  wa  mkutano wa tatu wa   wa siku tatu wa magonjwa yasiyopewa  kipaumbele, Tesome  Kanno kutoka (ITI) akijadili jambo  leo wakati wa mkutano huo , unaoendelea  kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Huduma  za Kinga,kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk,Neema Rusibamayila  (wa pili kushoto) akiwa  katika picha ya pamoja  baada ya kufungua mkutano wa tatu wa   wa siku tatu wa magonjwa yasiyopewa  kipaumbele leo unaoendelea  kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam.
 Baadhi wa wadau wakifuatilia mkutano wa tatu wa   wa siku tatu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele, Tesome  Kanno, unaoendelea  kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam.
Baadhi wa wadau wakifuatilia mkutano wa tatu wa   wa siku tatu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele, Tesome  Kanno, unaoendelea  kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam. Picha na Magreth Kinabo - Maelezo
*******************************************
Serikali inaandaa mpango wa kutoa huduma za magonjwa yasiyopewa kipaumbele(NTD,s) kwa pamoja ili kuweza kufikia watu wengi kwa kupunguza gharama.
Hayo yamasemwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma  za Kinga,kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk,Neema Rusibamayila wakati akifungua mkutano wa tatu wa   wa siku tatu wa magonjwa yasiyopewa  kipaumbele leo unaoendelea  kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares Salaam.

“ Tumekutana na wadau mbalimbali katika mkutano huu lengo ni  tunataka kuandaa mpango wa  kutoa huduma na dawa kwa magonjwa yasiyopewa kiupaumbele kwa pamoja badala ya ugonjwa mmoja pekee.Tunaweza kupata matokeo zaidi na kusaidia  kuwafikia  watu wengi  kwa kuwa utarahisisha utendaji kazi, utoaji elimu na dawa,” alisema Dk. Neema.
Dk. Neema aliyataja magonjwa hayo kuwa ni Usubi, Trakoma, Kichocho, Minyoo, Mabusha na Matende.
Aliongeza kuwa  hivi sasa huduma hiyo imeweza kufikia  wilaya 108  kati ya 160.Hivyo  changamoto iliyopo ni kufikia mikoa saba.
Alisema mpango huo ulianza mwaka 2012 na unaendelea hadi mwaka 2017, ambapo mafanikio yameonekana mfano katika kupambana na ugonjwa wa usubi utafiti ulifanyika umeonesha kuwa kati ya wilaya tisa ni wilaya mbili ndizo zitaendelea kupatiwa dawa.  
Naye Meneja Mpango  wa Taifa wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele(NTD,s),Dk, Upendo Mwingira alisema changamoto nyingine iliyopo katika kubabiliana na magonjwa hayo ni baadhi ya jamii kuwa na uelewa mdogo juu ya magonjwa hayo ambayo dalili zake si rahisi kuonekana kwa macho  kwani huonekana baada ya muda mrefu mfano Matende na Mabusha.
Alisema  baadhi ya jamii   huwa mwitiko mdogo  wakati wa utoaji wa huduma, hivyo Dk. Upendo aliitaka jamii kujitokeza kwa wingi wakati wa utoaji wa huduma hizo.
 Alizitaja  baadhi ya athari ya magonjwa hayo kuwa ni ulemavu wa kudumu na miongoni mwa sababu zinazochangia kuwepo kwa matataizo hayo ni umasikini.
 Dk. Upendo