NAIBU SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA UGENI KUTOKA JHPIEGO

NAIBU SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA UGENI KUTOKA JHPIEGO

May 03, 2017
A
Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa JHPIEGO nchini Tanzania Ndg.Jeremie Zoungana, aliyekuja kuzungumza nae na kubadilishana uzoefu wa kazi, kabla ya kuanza kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma
A 1 Naibu Spika  wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (kulia) akizungumza na ugeni uliomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma,ukiongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa JHPIEGO nchini Tanzania Ndg. Jeremie Zoungana (wa pili kulia).
A 2 Naibu Spika  wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Mradi wa USAID wa Boresha Afya, Ndg. Dustan Bishanga (wa pili kushoto) akizungumza leo katika kikao kilichofanyika Ofisini kwake Mjini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

TGNP YAENDESHA SEMINA KUJADILI VIPAUMBELE KATIKA BAJETI YA WIZARA YA AFYA YA MWAKA 2017/2018

May 03, 2017
 Ofisa Programu wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Alphonce Slima, akiongoza semina ya kujadili vipaumbele katika bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 iliyofanyika makao makuu ya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam jana.
 Mdau  Neofita Kunambi akizungumza wakati akichangia mada kwenye semina hiyo.
 Anna Sangai akichangia jambo kwenye semina hiyo.
 Sadick Juma mkazi wa Mbezi Beach, akielezea changamoto ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Muhimbili.
 Janeth Mawinza akielezea changamoto ya matibabu ya homa ya ini ambayo dawa zake hazipatikani nchini hadi zitoke India.
 Moses Benard akizungumzia wajawazito kujinunulia vifaa vya kujifungulia na suala la dawati la ukatili wa kijinsia kuwepo vituo vya polisi.
 Mdau Dalia Kalungwana akichangia jambo.
 Washiriki wakiwa kwenye semina hiyo.
 Semina ikiendelea.
 wananchi wakifuatilia kwa karibu semina hiyo.
Vijana wakifuatilia mada katika semina hiyo.
SERIKALI KUBORESHA UPATIKANAJI WA DAWA KATIKA VITUO VYA HUDUMA ZA AFYA NCHINI

SERIKALI KUBORESHA UPATIKANAJI WA DAWA KATIKA VITUO VYA HUDUMA ZA AFYA NCHINI

May 03, 2017
PIX 4-Dk Kugwangala akiongea
Na Husna Saidi & Nuru Juma- MAELEZO
Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeweka mikakati endelevu ya kuboresha upatikanaji wa dawa kwenye vituo vyote vya huduma za afya nchini.
Hayo yamebainishwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Adrea Kigwangalla akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa viti maalum Oliver Daniel Simguruka kuhusu hali ya upatikanaji wa dawa nchini katika kikao cha saba cha Bunge.
Dkt. Kigwangalla alisema kuwa hali ya upatikanaji wa dawa nchini umeimarika kwa asilimia 83 hivyo kufanya huduma hiyo ya afya kuwa bora.
“Hadi kufikia Aprili 2017 jumla ya shilingi bil.112 mil.198, 920,456 zimeshatolewa na kupelekwa kwenye bohari ya dawa ili kuwezesha vituo vya huduma za afya vya umma kupata mahitaji ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi”, alisema Dkt. Kigwangalla.
Aidha, alisema ongezeko hilo la fedha limesaidia kuongeza hali ya upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya tofauti na miaka iliyopita.
Aliongeza kuwa hadi kufikia Januari 15 mwaka huu Mkoa wa Kagera pekee ulipokea kiasi cha shilingi bil.4 mil.150, 767,216 kupitia fungu namba 52 kutoka kwa Wizara hiyo ili kuboresha huduma ya afya Mkoani humo.
Akizungumzia ujenzi wa bohari za dawa katika kila kanda Dkt. Kigwangalla alisema kuwa Serikali imeendelea kuitatua changamoto hiyo baada ya hapo awali kukabiliwa na changamoto ya fedha katika kujenga bohari za dawa kila kanda.
Kwa upande mwingine aliwaomba viongozi wa ngazi zote waweze kushirikiana katika kudhibiti wizi wa dawa katika vituo vya huduma za afya kwa sababu hili ni jukumu la kila mmoja na pia alitoa wito kwa wananchi kuweza kutoa taarifa za wizi wa dawa ili sheria iweze kuchukuliwa.

Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo Vya Habari Duniani Mei 3,2017

May 03, 2017
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipitia ratiba ya hafla ya Kongomano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wqa Vyombo Vya Habari Duniani yaliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Habari Kilimani Zanzibar. 
Mc wa Kongamano la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani Ndg Suleiman Seif akitowa maelezo la kongamano hilo la kuadhimisha lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Habari Kilimani Zanzibar.  
Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar Ndg Chande Omar akitowa maelezo wakati wa maadhimishi ya Siku ya Uhuru wa Vyombo Vya Habari Duniani ilioadhimishwa Zanzibar katika ukumbi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Kilimani Zanzibar.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania Kajubi Mukajanga akitowa maelezo wakati wa Kongamano hilo la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, yaliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Kilimani Zanzibar. 
Wageni waalikwa na Viongogozi wa Vyombo vya habari Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo. 
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Habari Tanzania Hassan Abdallah Mitawi akitowa maelezo ya hafla hiyo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja kutowa machache na kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kuhutubia Kongamano hilo la kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud akitowa nasaha zake wakati wa kongamano hilo kabla ya kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuhutubia hadhara hiyo ya waandishi wa habari mbalimbali walioko Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akihutubiwa wakati wa Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Vyombo vya Habari Duniani huadhimishwa kila mwaka mwezi wa mei 3, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Habari Kilimani Zanzibar.



Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar Ndg Chane Omar akiwasilisha Mada ya kuhusu Umakini wa Fikra kwa wakati muhimu Nafasi ya Vyombo vha Habari katika Kuimarisha jamii zenye Amani, Haki na Ujumuishwaji, wakati wa kongamano hilo la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Kilimani Zanzibar
MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Ndg Ali Uki akitowa Mada kuhusiana Uchambuzi wa Sheria za Habari Zanzibar wakati wa Kongamano hilo.




MWANDISHI wa Habari Muandamizi Ndg Enzi Talib akichangia mada zilizowakilishwa wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Kilimani Zanzibar


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ali iddi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa vyombo vya habari Zanzibar. 
imetayarishwa na othmanmapara.
zanzinews.com.
email othmanmaulid@gmail.com 

RAS TANGA ATAKA WAANDISHI WA HABARI KUPEWA USHIRIKIANO

May 03, 2017
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi akifungua maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani kimkoa yaliyofanyika kwenye ukumbi wa klabu ya waandishi wa habari mkoani Tanga (Tanga Press Club) leo kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Hassan Hashim kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Lulu George
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Hassan Hashim akizungumza katika maadhimisho hayo leo
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Lulu George akizungumza katika maadhimisho hayo kushoto ni Katibu Msaidizi Alex Abraham
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Hassan Hashim kushoto akifurahia jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi mara baada ya kupokea cheti  cha kuripoti habari za majanga na hali hatarishi jana mafunzo waliyoyapata mkoani Morogoro hivi karibuni katika halfa iliyofanyika
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Lulu George naye akipokea cheti hicho kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Kamishna Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Benedict Wakulyamba kulia ni  Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Hassan Hashim
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Amina Omari naye akipokea cheti hicho
Mwanachama wa Klabu ya waandishi wa Habari na Mwandishi wa Clous TV Mkoani Tanga Zawadi Kika naye akipokea cheti
Mwanachama wa Klabu ya waandishi wa Habari na mwandishi wa gazeti la Citizen Paskal Mbunga naye akipokea cheti
Mmiliki wa Blog ya Tanga Kumekucha na Mwanachama wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Tanga,Salum Mohamed naye akipokea cheti hicho
 Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorah Killo akizungumza jambo kwenye maadhimisho hayo
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Benedict Wakulyamba akizungumza jambo kwenye maadhimisho hayo
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akizungumza umuhimu wa kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na fursa zinazopatikana kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tanga Press Klabu,Lulu George
Afisa Uchunguzi kutoka Takukuru Mkoani Tanga,Frank Mapunda akisisitiza jambo kwenye maadhimisho hayo leo
Afisa kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Sophia akisisitiza jambo kwenye maadhimisho hayo kulia ni Meneja wa Mfuko huo Mkoani Tanga,Ally Mwakababu anayefuatia ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga (Tanga Press Club) Lulu George
 Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakiwemo wadau wa habari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa ziki wakilishwa kwenye maadhimisho hayo leo

  Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakiwemo wadau wa habari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa ziki wakilishwa kwenye maadhimisho hayo leo

 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF),Ally Mwakababu kulia akiteta jambo na Mwandishi wa gazeti la Mtanzania katikati Amina Omari kushoto ni Ofisa wa Mfuko huo mkoani Tanga Sophia
Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga (Tanga Press Klabu)Neema Omary kulia na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Klabu hiyo,Amina Omari wakifuatilia matukio mbalimbai

KATIBU Tawala Mkoa Tanga Mhandisi Zena Said ameziagiza taasisi za Serikali na mashirika ya umma kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari pindi wanapohitaji taarifa kutoka kwenye taasisi hizo kwa ajili ya kuhabarisha umma.
Ameyazungumza hayo leo wakati wa kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani ambapo Mkoa Tanga maazimisho hayo yalifanyika katika ukumbi wa klabu ya waandishi wa habari na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka taasisi za serikali na zisizo za kiserikali.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya waandishi wa habari kutoa malalamiko yao mbele ya Katibu Tawala huyo wa Mkoa ambae alikua mgeni rasmi katika maazimisho hayo ya kuwa zipo baadhi ya taasisi za Serikali kushindwa kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari pindi wanapohitaji kutekeleza majuku yao ya kazi.
Burhan Yakubu ambae ni mjumbe na mwaandishi wa habari  alisema kumekuwepo na utaratibu usioendana na maadili ya kiuwandishi katika Hospitali kuu ya Rufaa ya Bombo kwa kutengeneza urasimu wa kupatikana kibali kutoka kwa katibu tawala Mkoa wakati mwandishi anapohitaji kupatiwa tariifa zozote kutoka katika Hospitali hiyo
“Tumekuwa tukikwama kutekeleza wajibu wetu hasa tunapohitaji kupata taarifa katika Kuu ya Rufaa ya Bombo na kulazimishwa mpaka tupate kibali kutoka kwa katibu Tawala jambo ambalo limekuwa liktkwamisha katika shughuli zetu”Alisema Yakubu.
Akitolea ufafanuzi malalamiko hayo Mhandisi Zena  alisema taasisi zote zinapaswa kutambua kuwa wanahabari wanahaki ya kupatiwa taarifa sahihi kwa lengo la kuihabarisha jamii na hakuna sababu za kuweka vikwazo kwao kwa lengo la kuwakwamisha kutimiza majukumu yao.
Mhandisi Zena alisema zimekuwepo taarifa za malalamiko kwa waandishi kuwa zipo baadhi ya tasisi kama Hospitali ya Rufaa ya Bombo kutokutoa ushirikiano wa kutosha kwa waandishi wa habari pindi wanapotaka kutekeleza wajibu wao kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
“Tusiwawekee mipaka waandishi wakati wanapotaka kutekeleza majuku yao na tayari nimekwisha toa agizo sio Hospitali ya Bombo tu hili ni kwa taasisi zote,hakuna jambo linaloweza kufanyika na mwananchi akaweza kulipata kwa wakati ikiwa hakuna waandishi,tunatambua umuhimu wenu na thamani yenu ni kubwa kwa Taifa Hili.”Alisema
Hata hivyo alitumia fursa hiyo kuwaomba waandishi wa habari kutumia kalamu zao vema na kuwepo na maadili yatakayokuwa na maslahi mapana kwa ajili ya amani ya nchi na kujiepusha na taarifa zitakazoweza kuliingiza Taifa kwenye machafuko.
Katika hatua nyingine Mwandishi wa Tanzania Daima Mkoani Tanga Mbaruku Yusuph alitaka kupatiwa ufafanuzi kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa Tanga,Kamishna Msaidiz,Mwandamizi wa Polisi Benedict Wakulyamba,juu ya usalama wa waandishi wa habari wanapotekeleza wajibu wao hasa katika mikutano ya kisiasa.
Mbaruku alisema hivi karibuni kumeripotiwa kutokea matukio kwa baadhi ya waandishi wa habari maeneo mbalimbali hapa nchini kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji na kushindwa kuwajibika katika harakati zao za kupata habari kwa lengo la kuhabarisha umma na kujenga hofu kubwa kwa baadhi yao juu ya usala wa maisha yao.
Kamanda wakulya alisema jukumu la usalama lipo mikononi mwa jeshi hilo na wajibu wa polisi kutambua uwepo wa waandishi na umuhimu wao katika kila tukio ambapo alitoa rai kwa waandishi hao kuziona dalili za uvunjifu wa amani na kuanza kujiepusha mapema kabla ya madhara makubwa hayaja tokea.