COSTA RICA YAPETA ROBO FAINALI KOMBE LA DUNIA KWA MIKWAJU YA PENATI 5-3 DHIDI YA UGIRIKI

COSTA RICA YAPETA ROBO FAINALI KOMBE LA DUNIA KWA MIKWAJU YA PENATI 5-3 DHIDI YA UGIRIKI

June 29, 2014


 
COSTA Rica wamefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya kombe la dunia kwa kuifunga Ugiriki kwa mikwaju ya penati 5-3 baada ya dakika za kawaida na za nyogeza 30 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Hata hivyo kocha wa Ugiriki,  Fernando Santos alitolewa kwenye benchi kwa kuoneshwa kadi nyekundu kutokana na kumzonga mwamuzi katika mchezo huo ulioenda hatua ya penati.

Sokratis (kushoto) akifunga bao la kusawazisha dakika za lala salama 
 
Costa Rica walilazimika kucheza pungufu baada ya mchezaji wake Oscar Duarte kutolewa nje kwa kadi nyekundu mnamo dakika ya 67 kufuatia kadi mbili za njano.

Kikosi cha Costa Rica: Navas, Gamboa (Acosta 77), Duarte, Gonzalez, Umana, Diaz, Ruiz, Borges, Tejeda (Cubero 66), Bolanos (Brenes 83), Campbell.
Wachezaji wa akiba: Pemberton, Myrie, Barrantes, Francis, Granados, Miller, Calvo, Urena, Cambronero.

Kadi ya njano: Duarte, Tejeda, Granados, Ruiz, Navas.
Kadi nyekundu: Duarte.
GMfungaji wa goli: Ruiz 52.
 
Kikosi cha Ugiriki: Karnezis, Torosidis, Manolas, Papastathopoulos, Holebas, Karagounis, Salpingidis (Gekas 69), Maniatis (Katsouranis 78), Christodoulopoulos, Samaris (Mitroglou 58), Samaras. Subs: Glykos, Tzavelas, Moras, Tziolis, Kone, Mitroglou, Vyntra, Fetfatzidis, Tachtsidis, Kapino.
Booked: Samaris, Maonlas.
Mfungaji wa Goli: Sokrats 90+1 dakika moja nyongeza.
Mwamuzi: Benjamin Williams (Australia)

MATOKEO YA AWALI UCHAGUZI WA SIMBA, AVEVA MWENYEKITI, KABURU MAKAMU WAKE, WAJUMBE BADO MATOKEO

June 29, 2014



 Mgombea nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu wa Simba, Evans Aveva (katikati) Nkwabi, wakiangalia muda kwa pamoja baada ya kupiga kura zao katika uchaguzi huo, wakisubiri matokeo na kutangazwa kwa washindi katika uchaguzi huo uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Bwalo la Poilisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Katika uchaguzi huo matokeo ya awali yalikuwa yakionyesha kuwa, Evans Elieza Aveva, alikuwa akiongoza kwa kujizolea jumla ya kura 1452 kati ya 1845  zilizopigwa na kutoa matumaini kwa wapiga kura wake ya kuibuka kidedea katika uchaguzi huo.

Mpinzani wake Andrew Tupa, hadi tunakwenda mitamboni alikuwa amejinyakulia jumla ya kura 387 wakati kura sita zimeharibika. Hata hivyo, matokeo rasmi ya uchaguzi huo yatatangazwa na Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo chini ya Mwenyekiti Dk Damas Ndumbaro baadaye.

wakati huo Geoffrey Nyange 'Kaburu' ameshinda Umakamu wa Rais Simba SC baada ya kupata kura 1043 akimshinda mpinzani wake wa karibu Jamhuri Mussa Kihwelo 'Julio' aliyepata kura 413 na Swedi Nkwabi kura 300. Hata hivyo, hizo ni taarifa za awali, matokeo kamili yatatangazwa na Kamati ya Uchaguzi baadaye.huo;
 Julio akipiga kura..
 Mwanachama wa Simba, 'Madenge' akipiga kura
 Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Simba, Hassan Dalali, akipiga kura.
 Aliyekuwa msemaji wa Simba Asha Mhaji, akipiga kura 
 Mmoja kati ya wagombea wa nafasi ya Ujumbe, Ibrahim Masoud (kulia) akipozi wakati akisubiri matokeo baada ya kupiga kura.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakipiga kazi wakiwa humo humo ukumbini.
 Mwenyekiti wa Simba aliyemaliza muda wake, Aden Ismail Rage, akitimka eneo hilo mida ya mchana, baada ya kupiga kura.
 Baadhi ya wanachama wa Simba wakifuatilia kila linaloendelea ukumbini hapo.
 Wengine walichoka na kuanza kuuchapa usingizi kwa kuchelewa kupata matokeo.
Baadhi ya wanachama wakifuatilia kwa makini.....