SERIKALI KUBORESHA KIWANGO CHA VYOO BORA KUFIKIA 2025

May 09, 2017


Na Ally Daud-WAMJW DODOMA
SERIKALIi imedhamiria kuboresha kiwango bora  vyoo mjini na vijijini  kutoka asilimia 35 hadi asilimia 55 kufikia mwaka 2025 ili kujenga taifa lenye afya bora na lisilo na maambukizi ya magonjwa yatokanayo na uchafu wa vyoo.
Akizungumza hayo kwenye uzinduzi wa  kampeni ya utunzaji wa mazingira ijulikanayo kama “NIPO TAYARI” Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali imepania kufikisha asilimia ya ubora wa vyoo mpaka kufikia 2030.
“Hatua hii itafikiwa endapo kwa pamoja tutasukuma mbele ajenda ya usafi wa mazingira kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hasa katika ujenzi wa vyoo bora,utupaji salama wa taka ngumu,upatikanaji wa maji salama kwa mikono miwili” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa yapo mafanikio yaliyofikiwa katika kupunguza kasi ya watu kujisaidia ovyo tabia ambayo ni kisababishi cha maambukizi ya magonjwa mengi katika jamii.
Mbali na hayo Waziri Ummy alitoa rai kwa wanasiasa wenginekushirikiana na wananchi katika majimbo yao ilikusukuma kwa vitendo ajenda ya Usafi wa Mazingira  nchini .
Kwa upande wake Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Suleiman Jaffo amesema kuwa  watanzania wa wa mijini na vijijini wawe mstari wa mbele katika kuhakikisha wanatumia vyoo bora kila kaya ili kuepuka magonjwa ya kuambukiza.
Naye Naibu Waziri wa maji na umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe amesema kuwa ili kuendana na kasi hiyo wamejipanga kuhakikisha shule zote za msingi na sekondari nchini zinapata maji safi na salama kwa wakati sahihi.

MUFINDI YA ENDELEA KUTEKELEZA SERA YA KUWA NA ZAHANATI KWENYE KILA KIJIJI.

May 09, 2017


Na Afisa Habari Mufindi
Halmashauri ya Wilaya ya Maufindi imeendelea kutekeleza sera ya serikali ya kuhakikisha kila Kijiji kinakuwa na Zahanati kwa kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye  zahanati za Vijiji vinne kati ya vitano zilizopo kata ya Ihalimba Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.
 Uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi umetekelezwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mh. Festo Mgina, Diwani wa kata Ihalimba Mh. Award Mahanga sanjari na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Prof. Riziki Shemdoe.
Taarifa hiyo imevitaja vijiji vilivyo nufaika na huduma hiyo muhimu kwa usatawi wa afya ya jamii kuwa, ni pamoja na Kijiji cha Wamimbalwe uwekaji wa Jiwe la msingi, uzinduzi wa Zahanti ya Kijiji cha Vikula, uzinduzi wa zahanati ya Kijiji cha Nundwe pamoja na uwekaji wa jiwe la Msingi kwenye azahanati tarajiwa ya Kijiji cha Ihalimba.  
Awali akiwahutubia wakazi wa Vijiji hivyo, Mwenyekiti wa Halmashauri Mh Festo Mgina, alitoa rai kwa wananchi kujiepusha na tabia hatarishi zinazochochea maambukizi ya Virusi vya ukimwi huku akiutaja Mkoa wa Iringa kuwa na asilimia kubwa ya maabukizi ya  09.1 wakati asilimia ya kitaifa ni 05.6 Pekee. 
Aidha, Kiongozi huyo mwenye dhamana ya juu ya uongozi katika halmashauri hiyo, amekemea vitendo vya ubakaji kwa Watoto ambavyo vinashamili kwa kasi Wilayani Mufindi.
Mnamo mwaka 2015 wakati wa ufunguzi wa Bunge la Tanzania, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazania Mh. Dk. John Pombe Magufuli, aliahidi kuwa serikali ya awamu ya Tano itahakikisha sera ya kuwa na zahanati kwenye kila kijiji na kituo cha afya kwa kila kata inatekelezwa kwa vitendo.
TEMBO WANNE WAVAMIA CHUO KIKUU CHA UDOM INASEMEKANA HUENDA NI NJIA YAO WALIYOIPITA MIAKA ILIYOPITA

TEMBO WANNE WAVAMIA CHUO KIKUU CHA UDOM INASEMEKANA HUENDA NI NJIA YAO WALIYOIPITA MIAKA ILIYOPITA

May 09, 2017
TEMB1
Tembo wanne leo wametinga Chuo Kikuu cha  UDOM Mkoani Dodoma na kuleta tafrani kubwa kwa wanafunzi wafanyakazi na wakazi wa maeneo hayo,  Inaaminika ni mapito yao au shoroba na tembo husifika kwa kutunza kumbukumbu kama njia aliipita miaka 50 iliyopita anaweza kurudia palepale na inawezekana ndilo lililotokea leo hii. Askari wa Mamlaka ya Wanyamapori  wanaendelea kuwadhibiti ili wasilete madhara kwa wananchi.
TEMB2 TEMB3 TEMB4

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU KASIMU MAJALIWA BUNGENI DODOMA LEO

May 09, 2017

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa zamani, Lawrence Masha kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Kiembesamaki, Ibrahim Raza kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 9, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 9, 2017. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge, Job Ndugai kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 9, 2017. Katikati ni Mbunge wa zamani, Hezekia Wenje. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge, Job Ndugai kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 9, 2017.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Sengerema, William Ngereja kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma, Mei 9, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika Mstaafu, Mhe. Anne Makinda, leo.

Balozi Seif akutana na Kamati ya Kitaifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar

May 09, 2017
Na Othman Khamis Ame, OMPR
Kamati ya Kitaifa ya Kukabiliana na Maafa  Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi imekutana Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kutathmini Mvua za Masika na muelekeo wa kukabiliana na changamoto zilizoanza kuibuka.
Tathmini hiyo imekuja kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika Maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Unguja na Pemba na kuathiri Nyumba 325 Mkoa Kusinin Pemba, Nyumba 667 kuhamwa  ndani ya Mkoa Mjini Magharibi pamoja na kubomoka kwa miundombinu ya Bara bara na baadhi ya Madaraja hasa Kisiwani Pemba. 
Akitoa Taarifa za awali za athari ya mvua zilizojitokeza kwa mwaka wa 2017 tokea kuanza kwa msimu wa Mvua za  Masika, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Nd. Ali Juma Hamad alisema athari ya Mvua hizo zimesababisha maporomoko ya ardhi yaliyosababisha kufukia  kwa baadhi ya Nyumba na Bara bara.
Nd. Ali alisema ziara za Viongozi wa Serikali zimegundua athari kubwa ya uharibifu wa miundombinu ya Bara bara na nyumba kutokana na mvua hizo hasa katika Mkoa wa Kusini Pemba na kusababisha kifo cha Mtoto Mmoja Ramadhan Mohamed baada ya kuangukiwa na ukuta wa Madrasa Chanjani Chake Chake Pemba.
Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Kanda ya Zanzibar Nd. Mohamed Khamis Ngwali  alisema bado Visiwa vya Unguja na Pemba viko katika msimu wa mvua hali ambayo wananchi wanapaswa kufuatilia Taarifa zainazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa.
Nd.Ngwali  alisema viwango vya mvua katika visiwa vya Zanzibar  viongezeka kama vilivyotangazwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania mnamo Tarehe 28 Mwezi uliopita na kuanza kunyesha mara moja siku iliyofuata.
Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya Kinga Wizara ya Afya  Dr.Fadhil Abdulla  alieleza kwamba Wizara ya Afya tayari imeshajiandaa na changamoto yoyote inayoweza kujitokeza endapo kutaibuka kwa maradhi ya mripuko katika kipindi hichi cha msimu wa mvua za masika.
Dr. Fadhil  alisema udhibiti wa vyakula vinavyouzwa katika maeneo ya wazi bado mgumu na ndio uliochangia kuibuka kwa maradhi ya Kipindupindu mwaka jana kwa asilimia 16%.
Alisema katika kukabidhiana na udhibiti wa mfumko wa maradhi ya kuambukiza Wataalamu wa Afya tayari wameshapima wagonjwa  22 walioonyesha ishara ya kusumbuliwa na maradhi ya matumbo ya kuharisha.
Akiahirisha  Kikao hicho Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema ipo haja ya kuandaliwa mikakati ya muda mrefu ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza kila mwaka wakati wa msimu wa mvua za Masika.

Mwakilishi na Mbunge wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Wakabidhi Vifaa Kwa Shughuli za Kijamii Jimbon

May 09, 2017
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza nas Wananchi wa Shehia tatu za Bungi, Ubago na Tunguu wakati wa kukabidhi vifaa kwa ajili ya shehia hizo tatu kwa matumizi ya Kijamii wakati wa shida na raha, Vifaa walivyokabidi majiko ya gesi 3, sinia 800  mitungi ya gesi 6 na mabusati. kwa ajili ya matumizi yao katika shughuli za kijamii, hafla hiyo ya makabidhiani imefanyika katika Tawi la CCM Tunguu Wilaya ya Kati Unguja. Na kuhudhuriwa na Viongozi wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja. 
Mbunge wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Khalifa Salim Suleiman akizungumza na wananchi wa jimbo lake wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa kwa ajili ya matumizi ya shughuli za kijamii katika jimbo lao ikiwa ni kutimiza ahadi kwa wananchi wa jimbo lao walioitowa wakati wa kampeni ya uchaguzi.hafla hiyo imefanyika katika tawi la CCMTunguu Wilaya ya Kati Unguja.
Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu wakikabidhi vifaa mbalimbali waliohidi kwa wananchi wa jimbo lao wakikabidhi vifaa hivyo kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg Ramadhan Abdallah na Uongozi wa jimbo hilo, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Tawi la CCM Tunguu Unguja. wakikabidhi mabusati na sinia.
Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar wakikabidhi majiko ya gesi kwa ajili ya shia tatu kila shehia imepata jiko moja na mitungi ya gesi miwili. na sinia 200, kwa ajili ya matumizi ya kijamii katika shehia zao.Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika Tawi la CCM Tunguu Unguja. 
Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu wakikabidhi sufuria kwa Uongozi wa Jimbo kwa ajili ya matumizi ya Shehia za Jimbo hilo tatu kila shehia imepata sufuria mbili kubwa.
Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu wakikabidhi mitungi ya gesi kwa Uongozi wa Jimbo kwa ajili ya matumizi ya Shehia za Jimbo hilo tatu kila shehia imepata mitungi miwili ya gesi mikubwa kwa ajili ya matumizi ya shughuli za kijamii katika jimbo lao zilizotolewa na viongozi hao..
Mwenyekiti wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mzee Khatib Ramadhani akitowa shukrani kwa Mwakilishi na Mbunge kwa msaada wao huo kwa ajili ya kuwajali wananchi wa jimbo lao kwa msaada huo na kuahidi kuutumia kwa malengo yaliokusudiwa katika shughuli za kijamii katika shehia husika za jimbo hilo. 
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali dhamira wa msaada huo kwa wananchi wa jimbo lao kuweza kuwasaidia katika matumizi yao ya shughuli za kijamii zinazotokea kwa wananchi hao ili kuweza kuvitumia kupunguza gharama za kukodi vifaa hivyo.

Imetayarishwa na OthmanMapara,zanzinews.com.
email. othmanmaulid@gmail.com.

RAIS DKT MAGUFULI ATOA MSAADA WA MAGARI YA KUBEBEA WAGONJWA (AMBULANCE) KWA WABUNGE WA NKASI, TABORA NA SHINYANGA

RAIS DKT MAGUFULI ATOA MSAADA WA MAGARI YA KUBEBEA WAGONJWA (AMBULANCE) KWA WABUNGE WA NKASI, TABORA NA SHINYANGA

May 09, 2017
unnamed
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akimwangalia Mbunge wa Nkasi Mhe Ali Mohamed Kessy baada ya kumkabidhi gari la kubebea wagonjwa alilopewa msaada na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 9, 2017
A
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akiwakaribisha  Wabunge Mhe Ali Mohamed Kessy (Nkasi Kaskazini)  Mhe. Munde tambwe (viti maalumu – Mkoa wa Tabora) na Mhe Lucy Mayenga (viti maalumu-mkoa wa Shinyanga) kupokea magari ya kubebea wagonjwa waliyopewa saada na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 9, 2017
A 1
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akimwangalia Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Munde baada ya kumkabidhi gari la kubebea wagonjwa alilopewa msaada na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 9, 2017
A 2
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akimwangalia Mbunge wa Viti Maalumu Mhe Lucy Mayenga baada ya kumkabidhi gari la kubebea wagonjwa alilopewa msaada na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 9, 2017
A 4
Wabunge wa Nkasi, Tabora na Shinyanga wakiwasili tayari kukabidhiwa magari la kubebea wagonjwa waliyopewa msaada na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 9, 2017
A 5
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi (kati) akiwa na Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Alphayo Kidata (Kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma Ikulu  Bw. Charles Mwankupili (kulia) na  Wabunge Mhe Ali Mohamed Kessy (mbunge wa Nkasi Kaskazini)  Mhe. Munde tambwe na Mhe Lucy Mayenga (wabunge viti maalumu)  baada ya kuwakabidhi magari la kubebea wagonjwa waliyopewa msaada na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 9, 2017.
PICHA NA IKULU

Mshindi wa MIlioni 10 Biko aahidi kuuaga umasikini

May 09, 2017
Meneja Masoko wa BIko Goodhope Heaven mwenye fulana ya njano akionyesha nyaraka zilizowekwa kiasi cha Sh Milioni 10 kwa ajili ya mshindi wao wa wiki, Emmanuel Philipo aliyeibuka na ushindi wa mamilioni hayo kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko. Kushoto kwa Heaven ni Philipo akifuatiwa na Afisa wa NMB na kulia ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSHINDI wa Sh Milioni 10 wa droo ya nne ya mchezo wa kubahatisha wa BIko IJue Nguvu ya BUku, Emmanuel Philipo, ametangaza rasmi nia yake ya kuuaga umsikini baada ya kukabidhiwa fedha zake jumla ya Sh Milioni 10.

Makabidhiano hayo yalifanyika jana jijini Dar es Salaam kwa kuhudhuriwa na baadhi ya wataalam wa benki ya NMB kwa ajili ya kumuelimisha mashindi huyo wa bahati nasibu ya Biko ili azitumie vizuri fedha zake.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Philipo alisema kwamba ni wakatiwake wa kuuaga umasikini kwa sababu amepata nafasi ya kutimiza ndoto zake kiuchumi kwa kuhakikisha kwamba anakamilisha mradi wake wa garage ya kutengenezea magari katika viunga vya jiji la Dar es Salaam.
Meneja Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage akionyesha namba za kucheza bahati nasibu yao inayofanikisha ushindi wa mamilioni kutoka kwa Watanzania, ambapo droo iliyopita alitangazwa Emmanuel Philipo ambaye jana alipewa kiasi cha Sh Milioni 10.
Mazungumzo yakiendelea baada ya makabidhiano hayo.
Afisa wa NMB akizungumza jambo na mshindi wa Sh Milioni wa Biko, Emmanuel Philipo baada ya kukabidhiwa Sh Milioni 10 zake kutoka Biko.
Afisa wa NMB akimkabidhi nyaraka mshindi wa Sh Milioni 10, Emmanuel Philipo katikati akishuhudiwa na Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven.
Alisema fedha alizopata jumla ya Sh Milioni 10 ni nyingi, huku akizipata kwa sababu ya kushiriki bahati nasibu ya Biko, akiamini kuwa ni mpango wa Mungu kumpatia fedha hizo ukizingatia kuwa ni wengi wanaocheza bahati nasibu.

"Namshukuru Mungu kwa kuniletea zawadi hii kwa kuwatumia wachezeshaji wa biko, hivyo ni wakati wangu wa kufanikiwa kimaisha kwa sababu ndio dhamira yangu kuu kupiga hatua kubwa kimaendeleo kwa kuamua kucheza bahati nasibu hii kwa njia yaujumbe wa maandishi kwa kufanya muamala kwenye simu za Tigo, Vodacom na Airtel ambapo namba ya kampuni niliweka 505050 na ile ya kumbukumbu niliingiza 2456 na kutangazwa mshindi mwishoni mwa wiki.

"Nawaomba Watanzania wenzangu tuendelee kuthubutu katika fursa mbalimbali ikiwamo ya kucheza mchezo wa Biko kwa sababu sio tu zawadi zao mbalimbali kama vile Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000 na Sh MIlioni Moja za papo
kwa hapo zinaeleweka, bali pia hata unapotangazwa mshindi wa Sh Milioni 10, huwa wanakabidhi haraka kwa mshindi wao," Alisema.

Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven alimpongeza Philipo kwa ushindi huo na kumtaka awe balozi mzuri kwa Watanzania wote kwa ajili ya kuwapa elimu ya kuhakikisha kuwa wanacheza Biko ili nao waibuke na mamilioni ya Biko.

Naye Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, alisema ushindi kwenye bahati nasibu yao ni mwepesi na kila mchezaji anaweza kuibuka na fedha kutoka kwenye bahati nasibu yao ya Biko.

"Huu ni muda wa kulala masikini na kumka tajiri, hivyo njia ya ushindi ni kucheza mara nyingi zaidi ambapo kila tiketi moja inayopatikana kwa sh 1000 inatoa nafasi mbili za ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya wiki ya kushinda Sh Milioni 10," Alisema.

Philipo ni mshindi wa nne wa Sh Milioni 10 ambapo jana alikabidhiwa fedha zake kwa ajili ya kuanza matumizi kama walivyokabidhiwa wenzake kutoka
jijini Dar es Salaam na Mwanza.

KIKAO CHA ISHIRINI MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MAY 9, 2017

May 09, 2017

 Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Najma Giga akiongoza  kikao cha Ishirini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 9, 2017.
 Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba akijibu hoja Mbalimbali za Wabunge  katika  kikao cha Ishirini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 9, 2017.
 Mbunge wa Segerea Mhe.Bonnah Kaluwa  akiuliza swali katika  kikao cha Ishirini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 9, 2017.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI Mhe.Selemani  Jafo akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 9, 2017.
 Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Waziri wa mabo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba katika  kikao cha Ishirini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 9, 2017.
 Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza jambo Mbunge wa Arusha Mjini Mhe.Godbless Lema katika  kikao cha Ishirini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 9, 2017.
  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Jumanne Maghembe akizungumza na Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe.Joshua Nassari katika  kikao cha Ishirini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 9, 2017.
 Mbunge wa Mwibara (CCM) Mhe.Kangi Lugora akiuliza swali katika  kikao cha Ishirini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 9, 2017.
Mbunge wa Madaba Mhe.Joseph Mhagama akiuliza swali katika  kikao cha Ishirini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 9, 2017
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Isack Kamwelwe akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 9, 2017.
 Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Maria Kangoye akiuliza swali katika  kikao cha Ishirini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 9, 2017.
 Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.Dk Charles Tizeba akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha Ishirini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 9, 2017.
 Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 9, 2017. 

Picha Zote na Daudi Manongi- Dodoma MAELEZO, DODOMA

RAIS SHEIN ATEMBELEA BANDARI YA NCHINI DJIBOUTI

May 09, 2017
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi  Ukaguzi Nd.Mohamoud Houssein (wa pili kushoto) wakati  alipotembelea  katika Bandari ya Doraleh  Container Terminal jana,ambayo ni maalum kwa upokeaji wa Makontena kutoka kwenye meli mbali mbali  zinazowasili katuika Bandari hiyo,akiwa katika ziara ya kiserikali chini Djibouti na ujumbe aliofuanata nao.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Viongozi mbali mbali  alipowasili katika Bandari ya   Doraleh  Container Terminal  jana ambayo ni maalum kwa upokeaji wa Makontena kutoka kwenye meli mbali mbali zinazowasili katika Bandari hiyo, alipotembelea  akiwa katika ziara maalum ya kiserikali nchini Djibouti akiwa na ujumbe aliofuanata nao
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Viongozi mbali mbali  alipowasili katika Bandari ya   Doraleh  Container Terminal  jana ambayo ni maalum kwa upokeaji wa Makontena kutoka kwenye meli mbali mbali zinazowasili katika Bandari hiyo, alipotembelea  akiwa katika ziara maalum ya kiserikali nchini Djibouti akiwa na ujumbe aliofuanata nao.
 Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi  Ukaguzi Nd.Mohamoud Houssein (katikati) mara baada ya mapokezi alipotembelea  katika Bandari ya   Doraleh  Container Terminal  jana ambayo ni maalum kwa upokeaji wa Makontena kutoka kwenye meli mbali mbali zinazowasili katika Bandari hiyo, alipotembelea  akiwa katika ziara maalum ya kiserikali nchini Djibouti akiwa na ujumbe aliofuanata nao terehe 08/05/2017.
 Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) pamoja na Viongozi wengine wakipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa Mashine  karika Bandari  ya   Doraleh  Container Terminal  jana  ambayo ni maalum kwa upokeaji wa Makontena kutoka kwenye meli mbali mbali zinazowasili katika Bandari hiyo, Dk.Shein yupo nchini Djibouti katika  ziara maalum ya kiserikali   akiwa na ujumbe aliofuanata nao
 Makontena yenye mizogo mbali mbali yakiwa katika eneo maalum lililotengwa na kuwekwa katika Bandari  ya   Doraleh  Container Terminal nchini Djibouti ambapo  Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na ujumbe wake jana walitembelea eneo hilo akiwa katika ziara maalum ya kiserikali.
 Mashine za kuchukulia Makontena katika meli zinazofunga gati katika  Bandari  ya   Doraleh  Container Terminal nchini Djibouti ambapo  Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na ujumbe wake  jana walitembelea eneo hilo akiwa katika ziara maalum ya kiserikali.
 Makontena yenye mizogo mbali mbali yakiwa katika eneo maalum lililotengwa na kuwekwa Mizigo mbali mbali katika Bandari  ya   Doraleh  Container Terminal nchini Djibouti ambapo  Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na ujumbe wake jana walitembelea eneo  hilo   katika ziara maalum ya kiserikali.
  Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akisalimiana  na Mkuu wa Bandari ya Djibouti Bw, Saad Omar  Guelleh  mara alipowasili katika Bandari  ya   Doraleh  Multipurpose nchini Djibouti akiwa katika ziara maalum ya kiserikali alitembelea jana akiwa na ujumbe wake,(kushoto) Waziri wa Vifaa na Usafirishaji Mhe.Mohamed Abdoulkader Moussa.
 Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akitambulishwa na Mkuu wa Bandari ya Djibouti Bw,Saad Omar  Guelleh (katikati) kwa viongozi wakati aliposalimiana nao jana  wakati  alipotembelea katika Bandari  ya   Doraleh  Multipurpose  nchini Djibouti  akiwa katika ziara maalum ya kiserikali  na ujumbe wake,(kushoto) Waziri wa Vifaa na Usafirishaji Mhe.Mohamed Abdoulkader Moussa.
 Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akitambulishwa na Mkuu wa Bandari ya Djibouti Bw,Saad Omar  Guelleh (katikati) kwa viongozi wakati aliposalimiana nao jana  wakati  alipotembelea katika Bandari  ya   Doraleh  Multipurpose  nchini Djibouti  akiwa katika ziara maalum ya kiserikali  na ujumbe wake,(kushoto) Waziri wa Vifaa na Usafirishaji Mhe.Mohamed Abdoulkader Moussa.
 Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akitambulishwa na Mkuu wa Bandari ya Djibouti Bw,Saad Omar  Guelleh (katikati) kwa viongozi wakati aliposalimiana nao jana  wakati  alipotembelea katika Bandari  ya   Doraleh  Multipurpose  nchini Djibouti  akiwa katika ziara maalum ya kiserikali  na ujumbe wake,(kushoto) Waziri wa Vifaa na Usafirishaji Mhe.Mohamed Abdoulkader Moussa.

(Picha na Ikulu)