WHO YATOA VIFAA VYA DOLA ZA MAREKANI 46,000 KWA SERIKALI YA TANZANIA KUJIAMI NA EBOLA

February 20, 2015
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (HWO) nchini, Rutaro Chatora (kulia), akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando, moja ya kompyuta na baadhi ya vifaa tiba vyenye thamani ya dola za Marekani 46,000 vilivyotolewa na WHO kwa Serikali ya Tanzania Dar es Salaam leo,  kwa ajili ya maandalizi ya udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza na ebola.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (HWO) nchini, Rutaro Chatora (kulia), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando wakitiliana saini za makabidhiano ya vifaa hivyo.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (HWO) nchini, Rutaro Chatora (kulia), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando wakibadilishana hati baada ya kusaini makabidhiano ya vifaa hivyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando akionesha pampu ya kupulizia dawa kwa mbali za kutibu magonjwa ya kuambukiza.
Wadau wa sekta ya Afya wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Baadhi ya vifaa vilivyotolewa vikiwa katika maboksi.
 
Na Dotto Mwaibale
……………………………………………..
 
SHIRIKA la Afya Duniani (WHO), limetoa msaada wa vifaa tiba kwa Serikali ya Tanzania vyenye thamani ya dola la marekani 46,000 kwa ajili ya maandalizi ya udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza na ebola.
Akizungumza katika hafla fupi ya kupokea msaada huo jijini Dar es Salaam leo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Donan Mmbando alisema vifaa hivyo vimefika wakati muafaka  wakati serikali ikiwa katika mpango maalumu wa kuiandaa nchi kukabiliana na magonjwa hayo.
“Tunalishukuru shirika la WHO kwa msaada huu mkubwa waliotupatia kwani utatusaidia katika kukabiliana na magonjwa hayo hasa wa ebola ambao umeenea zaidi Afrika Magharibi” alisema Dk.Mmbando.
Alisema ilikukabiliana na changamoto ya magonjwa hayo Serikali imetoa mafunzo, kuimarisha maabara za utambuzi wa viashiria vya ugonjwa huo pamoja na vifaa tiba mbalimbali.
Alisema utambuzi wa viashiria vya ugonjwa huo vinafanyika katika maabara kubwa iliyopo katika Hospitali ya Mkoa wa Mbeya pamoja na Muhimbili.
Dk. Mmbando alisema tangu ugonjwa huo uibuke katika nchi kadhaa za Afrika Magharibi umewaathiri watu 23,000 pamoja na kusababisha vifo vya watu 9,000.
Akikabidhi msaada huo Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (HWO), Rutaro Chatora alisema shirika hilo limekuwa likisaidia misaada  ya huduma za afya katika nchi mbalimbali ikiwemo nchi za Guinea, Liberia na Siera Leon.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
RAIS KIKWETE AWA MWENYEKITI MPYA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

RAIS KIKWETE AWA MWENYEKITI MPYA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

February 20, 2015

1
Rais Jakaya Kikwete,Naibu Rais wa Kenya,William Rutto na maafisa
wengine wakiwa kwenye Jengo la mikutano wa kimataifa la Kenyatta
International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya wakimba
wimbo wa taifa la Tanzania katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa
nchi za Afrika Mashariki uliofanyika leo.20/2/2015
2
Kutoka kushoto ni mgeni mwalikwa,Rais wa Sudani Kusini,Salva Kiir,Rais
wa Burundi,Pierre Nkurunziza,Rais Jakaya Kikwete(Tanzania),Rais Uhuru
Kenyatta(Kenya)Rais Yoweri Museveni(Uganda)Rais Paul Kagame(Rwanda)na
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)Dk Richard Sezibera
wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano kwenye  mkutano wa kawaida wa 16 wa
Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika leo.20/2/2015.
3
Rais Jakaya Kikwete (kushoto), akipokea bendera ya Afrika
Mashariki(EAC)kutoka kwa Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta ikiwa ni ishara
ya kumkabidhi Uenyekiti wa  EAC  kwenye  mkutano wa kawaida wa 16 wa
Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika leo.20/2/2015.
 Dk.Ali Mohamed Shein ashiriki MAZIKO YA MREHEMU SALMIN AWaDH

Dk.Ali Mohamed Shein ashiriki MAZIKO YA MREHEMU SALMIN AWaDH

February 20, 2015
4
Rais wa Zanzibar na Mwenmyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai alipofika kutoa pole Nyumbani kwa Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) Magomeni Mjini Unguja leo,
[Picha na Ikulu.]
1
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein alipofika kutoa pole kwa kizuka wa   Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM)  nyumbani kwake Magomeni Mjini Unguja leo.
3
Wananchi kutoka sehemu mbali mbali walijumuika pamoja katika maziko ya Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM)  nyumbani kwake Magomeni Mjini Unguja leo na kuzikwa kijijini kwao Makunduchi  Wilaya ya Kusini Unguja,[Picha na Ikulu
5
Rais wa Zanzibar na Mwenmyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto) pamoja na Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi na Viongozi wengine walipofika kutoa pole kwa wafiwa Nyumbani kwa Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) Magomeni Mjini Unguja leo.
6
Rais wa Zanzibar na Mwenmyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto) pamoja Viongozi mbali mbali walijumika pamoja katika kumswalia Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) katika masjid Nuru Muhammad Mendae Mjini Unguja leo Swala iliyoongozwa Kadhi Mkuu na Sheikh Khamis Haji na kuzikwa kijijini kwao Makunduchi  Wilaya ya Kusini Unguuja.
7
Wananchi kutoka sehemu mbali mbali Bara na Visiwani wakilibeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) wakati wa maziko yaliyofanyika leo Makunduchi  Wilaya ya Kusini Unguja
8
Rais wa Zanzibar na Mwenmyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa nne kushoto) pamoja Viongozi mbali mbali walijumika na Wananchi katika mazishi ya aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) Marehemu Salmin Awadh  aliyezikwa kijijini kwao Makunduchi  Wilaya ya Kusini Unguja.
9
Wananchi kutoka sehemu mbali mbali wa Mjini na Mashamba walijumuika kwa pamoja katika maziko ya Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM)   yaliyofanyika leo Makunduchi  Wilaya ya Kusini Unguja.
10
Rais wa Zanzibar na Mwenmyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akitia udongo wakati alipojumuika na Waislamu mbali mbali na Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa wakati  wa maziko ya aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) Marehemu Salmin Awadh  aliyezikwa kijijini kwao Makunduchi  Wilaya ya Kusini Unguja.

TANZANIA KUIVAA KENYA JUMAMOSI.

February 20, 2015
NA MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM.
 Timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer) kesho jumamosi itacheza mchezo wa marudiano dhidi ya timu ya Taifa ya Kenya, mchezo utakaoanza majira ya saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Escape One Club Msasani jijini Dar es salaam.

Wageni timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni kutoka nchini Kenya wanatarajia kuwasili leo jioni jijini Dar es salaam, tayari kabisa kwa ajili ya mchezo huo wa marudiano siku ya jumamosi na watafikia katika hoteli ya Saphire iliyopo eneo la Gerezani – Kariakoo.

Katika mchezo wa awali uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mombasa, timu ya Taifa ya Tanzania iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 5 – 3 dhidi ya wenyeji timu ya Taifa ya Kenya na kujitengenezea mazingira mazuri ya kusonga mbele katika hatua inayofuata.

Waamuzi wa mchezo huo watakua ni , Beye Mbokh kutoka Senegal, mwamuzi wa pili ni Signate Youssouph (Senegal), mwamuzi wa tatu, Maolidy Tsaralaza kutoka Madagascar, mtunza muda (time keeper)  atakua Hachim Said Nassur (Madagascar) na kamishina wa mchezo atakua Roch Henriette kutoka Visiwa vya Shelisheli.

Tayari waamuzi wa mchezo huo wameshawasili jijini Dar e salaam tangu jana jioni tayari kwa mchezo huo, na endapo timu ya Taifa ya Tanzania itasonga mbele, itakutana na timu ya Taifa ya Misri kati ya Machi 7, 8 na kurudiana kati ya Machi 13, 14, 2015.

Fainali za Soka la Ufukweni zinatarajiwa kufanayika mapema mwaka huu katika Visiwa vya Shelisheli.

SERIKALI KUAJIRI WALIMU 35,000 – WAZIRI MKUU

February 20, 2015

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali imepanga kuajiri walimuzaidi ya 35,000 kwa ajili ya shule za sekondari ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa walimu nchini.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Februari 19, 2015) wakatiakizungumza na mamia ya wakazi wa kata ya Kiwere, mara baada yakukagua ujenzi wa maabara na kuzindua nyumba nne za walimu kwenyeshule ya sekondari ya Kiwere, tarafa ya Kalenga, wilayani Iringa.

Waziri Mkuu alisema walimu hao watagawanywa kwenye shule kulingana namahitaji yaliyokwishawasilishwa na kwamba watakapopata mgao wao hawanabudi kuziangalia kwanza shule zenye miundombinu iliyokamilika kama ilivyo kwa shule hiyo.

Akifafanua kuhusu kasi ya ujenzi wa maabara Waziri Mkuu alisema: “Mkoamzima wa Iringa unahitaji kuwa na maabara 318 na zilizo tayari mpakasasa ni 108. Lakini kuna nyingine 141 ambazo zimekwishaanza kujengwana zimefikia hatua nzuri. Nimeambiwa katika muda mfupi ujao kutakuwa na maabara 249 zilizokamilika,” alisema.
“RC inabidi uwasukume watu wako ili hizi 69 ambazo bado hazijaanzakujengwa zikamilike kabla ya Juni mwaka huu kama ambavyo MheshimiwaRais Jakaya Kikwete alikuwa ameelekeza. Alisema hataongeza tena muda wa ujenzi,” aliongeza.

Alisema elimu ni sekta ya msingi ambayo Serikali imeamua kuipa umuhimuwa kipekee na kuiweka katika moja ya maeneo sita muhimu ya kipaumbele chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa ya Haraka (BRN).
Waziri Mkuu aliwataka wanafunzi wa shule hiyo wasome kwa bidii na wawe wasikivu ili waweze kufanya vizuri zaidi kwenye masomo yao.
Mapema, akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Afisa Elimu wa Wilaya yaIringa, Bw. Leonard Msigwa alisema ujenzi wa nyumba hizo nne ambazozina pande mbili (four duplex houses) umegharimu sh. milioni 323.2. Alisema nyumba hizo zenye vyumba vitatu vya kulala, sebule na jiko,zina uwezo wa kubeba familia nane.

Bw. Msigwa alisema ujenzi wa nyumba ulifanywa shirika la DESWOS laUjerumani kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa pamojana wananchi. Pia walisaidiwa kujengewa tenki la maji na mabweni mawili yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 112 kila moja kwa ajili ya wasichana.
Akifafanua kuhusu hali ya ujenzi wa maabara, Afisa Elimu huyo alisemahadi sasa wamekamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya Kemia na Baiolojialakini bado viko kwenye hatua ya kupaka rangi. Alisema mfumo wa gesi na maji umekwishafungwa ndani ya vyumba vya maabara.

“Ujenzi wa maabara hadi sasa umekwishagharimu sh. milioni 52.8/- nakatika kipindi cha Februari 2015, tumefanikiwa kutengeneza baadhi yasamani za maabara yaani meza 24 na stuli 96 zenye thamani ya sh.8,940,000/-,” alisema.
ASASI YA “AIDS – free” KUSAIDIA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI NDANI YA JESHI LA MAGEREZA

ASASI YA “AIDS – free” KUSAIDIA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI NDANI YA JESHI LA MAGEREZA

February 20, 2015

Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza walioshriki katika mazungumzo rasmi kuhusu Mradi wa “AIDS – free” unaotarajiwa kutekelezwa ndani ya Jeshi la Magereza(wa kwanza kulia) ni Kamishna Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa pili kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa pili kushoto) ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Gedion Nkana(wa kwanza kushoto) ni Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Nsajigwa Mwakenja. mag4 
Maofisa Wasimamizi wa Sekta ya Afya kutoka Jeshi la Polisi wakifuatilia mazungumzo rasmi kuhusu Mradi wa “AIDS – free”(wa kwanza kushoto) ni Dkt. Nyanda Lushina(katikati) ni Mrakibu wa Polisi, Husein Yahya.
mag5 
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(meza kuu) akiongoza mazungumzo rasmi yaliyofanyika Ofsini kwake leo februari 20, 2015 kati ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza na Wasimamizi Wakuu wa Mradi wa “AIDS – free” utakaotekelezwa ndani ya Jeshi la Magereza(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Safari ya Mwisho ya DCP Mstaafu wa jeshi la Polisi Tanzania , Mzee Andrew Michael Kumalilwa huko Tabata Segerea.

February 20, 2015

 Jeneza lenye Mwili wa marehemu Mzee Andrew Michael Kumalilwa ukiwa tayari kushushwa nyumbani kwake Tabata Segerea ambapo misa ya kumuombea na kutoa heshima za mwisho zilifanyika kabla ya Kwenda kuupumzisha Mwili wake katika Nyumba yake ya Milele.
Askari wa Jeshi la Polisi Tanzania wakiwa wamebeba jeneza lenye Mwili wa aliyekuwa DCP Mstaafu wa Jeshi la Polisi Tanzania Mzee Andrew Michael Kumalilwa  wakiingia katika nyumba yake iliyopo Tabata Segerea kwaajili ya Misa na ndugu, jamaa na marafiki kutoa heshima za mwisho kabla ya kwenda kuupumzisha katika Nyumba yake ya Milele ambapo Marehemu alizikwa katika nyumba kwake Tabata Segerea.
 Mtoto wa Kwanza wa Marehemu Andrew Michael Kumalilwa, Patricia Andrew akiwa mwenye huzuni wakati wa msiba wa marehemu Baba yake ambapo marehemu alikuwa mstaafu wa jeshi la Polisi Tanzania akiwa na Cheo cha DCP.
 Jeneza lililokuwa limebeba Mwili wa Marehemu Mzee Andrew Michael Kumalilwa ukitolewa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwaajili ya kuelekea nyumbani Kwake Segerea ambapo mazishi yalifanyika
 Baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi Tanzania wakitoa heshima mbele ya jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Mzee Andrew Michael Kumalilwa ambae alikuwa mstaafu wa jeshi la Polisi kwa ngazi ya DCP
 Ndugu wa marehemu akijadiliana jambo na Mmoja wa Askari wa Jeshi la Polisi wakati wa Kutoa Heshima za mwisho kabla ya kwenda kuupumzisha mwili wa Mzee Andrew Kumalilwa ambae alizikwa nyumbani kwake Tabata Segerea tarehe 14 Februari 2015.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi Tanzania, DCP Simon Siro akitoa maneno mafupi kabla ya kwenda kuupumzisha Mwili wa marehemu Mzee Andrew Kumalilwa katika nyumba yake ya Milele. Marehemu Andrew Kumalilwa alizikwa mnamo tarehe 14 February 2015 huko Nyumbani Kwake Tabata Segerea.

WAZIRI MKUU,MIZENGO PINDA ZIARANI KATIKA JIMBO LA ISIMANI NA KALENGA MKOANI IRINGA

February 20, 2015

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wauguzi wa Kituo cha Afya cha Mlowa katika jimbo la Ismani kabla ya kuzindua kituo hicho akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 19, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipima mapigo ya moyo ikiwa ni ishara ya kuzindua kituo cha afya cha Mlowa katika jimbo la Isimani akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 19, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimjulia hali mmoja wa wagonjwa waliolazwa kwenye kituo cha afya cha Mlowa katika jimbo la Isimani akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 19, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua matrekta madogo maarufu kwa jina la Power Tiller yanayotumika katika shamba la kilimo cha umwagiliaji la Magozi katika jimbo la Ismani wakati alipolitembelea shamba hilo akiwa katika ziara ya mkoawa Iringa Februari 19, 2015. Watatu kulia ni Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kiwere katika jimbo la Kalenga wakati alipotembelea maabara ya Kemia na Fizikia ya shule hiyo akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 19, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama mafunzo kwa vitendo ya kumfanyia upasuaji panya yaliyokuwa yakifanywa na wanafunzi wa kidato cha tatu, Rosemary Kapugi (kushoto) na Faudhia Ndunguru Wapili kushoto) wakati alipotembelea maabara ya Baiolojia ya shule ya sekondari ya Kiwere katika jimbo la Kalenga akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa, Februari 19, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua nyumba za walimu katika shule ya sekondari ya Kiwere katika jimbo la Kalenga akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 19, 2015. Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo, Blandina Nkondola na watatu kulia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Gerlad Guninita.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua nyumba za walimu katika shule ya sekondari ya Kiwere katika jimbo la Kalenga akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 19, 2015. Kushoto ni Mkuu wa Shule hiyo, Blandina Nkondola na wapili kulia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Gerlad Guninita.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (kushoto) na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kiwere katika jimbo la Kalenga mkoani Iringa baada ya kuzindua nyumba za walimu shuleni hapo akiwa katika ziara ya mkoa wa Iringa Februari 19, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

TWIGA STARS KUINGIA KAMBINI JUMAPILI.

February 20, 2015

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania (Twiga Stars), Rogasian Kaijage ametangaza kikosi cha wachezaji thelathini (30) kitakachoingia kambini siku ya jumapili kujiandaa na mchezo wa kufuzu Mataifa Afrika dhidi ya Zambia mwezi Machi mwaka huu.

Kaijage ametangaza program yake ya  mazoezi itakayochukua takribani wiki nne (4) ili kuhakikisha wachezaji wanakua tayari kwa ajili ya mchezo huo utakaochezwa kati ya Machi 21, 22 mwaka huu, huku akipanga kucheza mchezo mmoja wa kirafiki kabla ya kuelekea Lusaka Zambia kwenye mchezo wa awali.

Twiga Stars ambayo itakua kambini katika Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF zilizopo Karume,  imeingia moja kwa moja katika hatua ya pili kucheza na Zambia kufuatia kuwa na matokeo mazuri katika msimamo wa viwango vya soka la wanawake barani Afrika.

Wachezaji walioitwa ni, Asha Rashid, Esther Chaburuma, Fatuma Bushiri, Fatuma Hassan, Fatuma Mustapha, Fatuma Omari, Eto Mlenzi, Mwajuma Abdallah, Sofia mwasikili, Zena Khamis, Mwanahamis Omar, Fatuma Khatibu, Fadhira Hamad, Anastazia Anthony, Shelder Boniface.

Wengine ni Thereza Yonna, Happines Hezron, Amina Ally, Donizia Daniel, Fatuma Issa, Vumilia Maarifa, Maimuna Hamisi, Najiati Abbasi, Stumai Abdallah, Ziada Ramadhani, Zuwena Aziz, Irene Joseph (Mfunzo – Zanzibar), Dawa Haji Vuai (JKU – Zanzibar), Belina Julius na Amina Ramadhani.

Kusaga: Habari za kuuzwa Clouds Media Group ni uzushi wa kupuuzwa

February 20, 2015
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
TAHARUKI iliyosambaa jana kwenye mitandao kijamii juu ya kuuzwa kwa Clouds Media Group, inayomiliki Clouds FM, Clouds Tv na Choice FM, zimepata majibu baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Joseph Kusaga, kuibuka na kukataa habari hizo na kuziita ni uzushi wa kupuuzwa.

Habari za kuuzwa kwa kampuni hiyo dhidi ya mfanyabiashara maarufu na kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rostam Aziz, zilishika nafasi katika mitandao ya kijamii na hatimae kuzua usumbufu mkubwa kwa wafanyakazi, viongozi wa Clouds na Watanzania kwa ujumla.

Akizungumza leo asubuhi (jana) moja kwa moja katika kituo cha Radio cha Clouds FM, Kusaga alisema habari hiyo imetengenezwa na watu walioamua kupoteza muda wao katika mitandao ya kijamii, hali ya kuwa wapo wanaovuna fedha nyingi kwa kupitia njia hiyo ya mawasiliano (social media).

Alisema mara baada ya kuenea kwa habari hiyo, usumbufu mkubwa uliibuka kutokana na watu wenye mapenzi mema na kampuni hiyo kuanza kuhoji juu ya taarifa hizo kama zina ukweli, huku akisisitiza pia si kosa kuuza kwa kuwa ni jambo la kawaida katika mambo ya kibiashara.

“Clouds Media Group ni kampuni iliyoanzia chini kwa ushirikiano wa watu wengi, hivyo kuamua kuiuza kiholela ni jambo la kushangaza, ingawa pia si dhambi kufanya hivyo kwa mtu yoyote kwa sababu ni biashara kama zilivyokuwa biashara nyinginge.

“Naomba Watanzania wote wapuuze habari hizo na kuwataka wale wenzetu walioamua kuitumia mitandao vibaya waache na badala yake wajikite kufanya biashara kwa kupitia mitandao hiyo ambayo inalipa kama itatumiwa vizuri na si kueneza habari za kumuuzia Rostam ukizingatia kuwa hakuna kitu kama hicho na nina miaka sijakutana na mfanyabiashara huyo katika kikao chochote cha kujadili juu ya jambo hilo,” alisema Kusaga.

Aidha Kusaga alitumia muda huo kuwahakikishia Watanzania kuwa Clouds ni chombo huru kisichofungamana na chama chochote cha siasa, huku akisema kwamba katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu haki itatolewa kwa vyama vyote na wanasiasa wote.

“Huu ni mwaka mgumu, hivyo naomba niseme ikitokea suala la kuhoji au kuunga mkono siasa, basi haki itatolewa kwa wanasiasa wote, ukizingatia kwamba chombo chetu hakika chama cha siasa inachokiunga mkono kwa sababu zozote zile,” alisema Kusaga .

Katika hatua nyingine, Kusaga aliwataka Watanzania wote kuunga mkono juhudi za kupambana na dawa za kulevya, huku akisema sakata hilo linaathiri nguvu kazi ya Taifa, hususan kwa baadhi ya wasanii waliojiinga katika matumizi hayo ya dawa za kulevya.

“Sisi Clouds tunaungana na Watanzania wote wanaopambana juu ya matumizi mabaya ya dawa za kulevya, hivyo ni jukumu letu kubwa kuzidi kuelimisha jamii juu ya masuala hayo kwakuwa yanaathiri kwa kiasi kikubwa ndugu zetu, wakiwamo baadhi ya wasanii,” alisema.

Kwa mujibu wa Kusaga, jitihada nyingi zinawekwa katika kubuni mbinu mbalimbali za kuelimisha jamii katika mambo mbalimbali ili kuhakikisha kwamba Tanzania inapiga hatua hatua katika nyanja za kielimu, kisiasa, kiuchumi na kijamii, huku akiwataka watu kufanya kazi bila kuchoka na si kupoteza muda kwa kueneza habari zisizokuwa na ukweli katika mitanda ya kijamii.

Clouds Media Group inayomiliki kituo cha Radio cha Clouds FM, Clouds Tv na Choice FM, ni moja ya makampuni ya wazawa yenye mafanikio makubwa, huku Watanzania wengi wakifuatilia matangazo katika vituo hivyo.

Mwisho