RAIS WA ZIMBABWE,ROBERT MUGABE AWASILI JIJINI ARUSHA,KUFUNGUA KOGAMAO LA 3 LA VIONGOZI VIJANA WA AFRIKA NA CHINA LEO

March 28, 2015
 Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal akizungumza jambo na Rais wa Zimbabwe,Mh.Robert Mugabe mara mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA,mapema leo mchaa.Rais Mugabe anatarajiwa kufungua  Kongamano la Viongozi Vijana wa Afrika na China litakaloanza leo mjini Arusha.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiteta jambo  na Rais wa Zimbabwe,Mh.Robert Mugabe mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA mapema leo mchana.Rais Mugabe anatarajiwa kufungua  Kongamano la Viongozi Vijana wa Afrika na China litakaloanza leo mjini Arusha..
  Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal akimpomkea mgeni wake,Rais wa  Zimbabwe,Mh.Robert Mugabe mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa KIA,mapema leo mchana.Rais Mugabe anatarajiwa kufungua  Kongamano la Viongozi Vijana wa Afrika na China litakaloanza leo mjini Arusha.
 Baadhi ya Wanahabari wakihangaika kupata taswira ya kuwasili kwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ambaye alipokelewa na Makamu wa Rais Dkt.Gharib Bilal na viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Kidini
 Rais wa Zimbambwe Robert Mugabe akiwasili mapema leo mchana 
kwenye uwanja wa ndege wa KIA.Rais Mugabe anatarajiwa kufungua  Kongamano la Viongozi Vijana wa Afrika na China litakaloanza leo mjini Arusha. 
 Afrika walilia kiti cha baraza la usalama

Afrika walilia kiti cha baraza la usalama

March 28, 2015
1
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Vijana viongozi wa Afrika na China wakiwa baadhi ya majarida na mitandao kwenye simu katika mkutano huo unaofanyika kwenye hoteli ya Ngurudoto mkoani Arusha kuanzia leo ambao unafunguliwa na Rais wa Zaimbabwe Mzee Robert Mugabe.
2
Na Mahmoud Ahmad, Arusha
.
NCHI za bara la Afrika zimeendelea kulilia kiti cha uwakilishi katika
baraza la usalama la umoja wa mataifa ili ziweze kujiwakilisha vyema
katika kuzungumzia matatizo yao kuliko ilivyo sasa ambapo nchi hizo
zinasemewa pasipo uwakilishi wake.
Kilio hicho kilitolewa leo na mwakilishi wa vijana kutoka nchi ya
Niger katika kongamano linalofanyika mkoani Arusha la kzungumzia mambo
mbalimbali zikiwemo fursa za ajira na mengineyo kwa vijana wan chi za
bara la Afrika.
Kufuatia kilio hicho ndipo Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa
Kimataifa Bernard Membe alipotolea tamko jambo hilo na kuiomba nchi ya
China ambayo ni mwanachama katika baraza hilo na raifiki wa nchi za
Afrika kufikisha kilio hicho kwanchi zingine wanachama.
Membe amesema mchakato wa maombi ya uanachama katika baraza hilo
ulianza muda mrefu lakini kumekuwa na vikwazo mbalimbali kwa nchi za
Afrika jambo ambalo limekuwa likisababisha mikwamo lakini hata hivyo
nchi hizo hazijakata tama na kwamba zinaendelea kuomba.
Amesema awali lilikuwepo ombi la kupatiwa jambo nafasi mbili za
uwakilishi kwa nchi mbili za Afrika lakini bado imeonekana kuwa ngumu
lakini bado wameendelea kuwasilisha maombi hayo japo kwa hata nafasi
moja ili kuweza kusemewa mambo yao sawa sawa.
Ametaja moja ya kikwazo kikubwa kwa nchi hizo za Afrika kuwa ni lazima
ziwe zinatumia nuklia ambapo suala hilo ni gumu kwa nchi hizo za
Afrikalini waliwasilisha ombi la kuruhusiwa kutumia na kutengeneza
nuklia ili kuweza kumudu kuingia katika baraza hilo lakini hadi sasa
maombi hayo hayajajibiwa.
Amesema kinachofanyika kwasasa katika baraza hilo si sawa kwakua
baraza limekuwa likitumia muda mwingi kujadilia masuala ya nchi 54 za
bara la Afrika huku likikosa majibu sahihi kutoka kwa nchi za bara
hilo kutokana na kukosa uwakilishi wan chi hizo.
Amesema zipo taarifa kuwa baraza hilo liliahidi kutoa nafasi hiyo ya
uwakilishi wa nchi za Afrika kuwa mzunguko ili kutoa nafasi kwa nchi
hizo lakini bado hata ahadi hiyo haijatekelezwa hadi sasa pasipo na
maelezo yoyote.
Nchi zingine zilizo wanachama wa baraza hilo lililoanza tangu mwaka
1945 ni pamoja na Urusi,Marekani,Uingereza,Ufaransa na yenyewe China
huku nchi ya Brazili ambayo ilijitahidi kwa nguvu zake zote lakini
haikufanikiwa kuingia katika baraza hilo.
KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AMPOKEA MAKAMU WA RAIS DR. GHARIB BILAL MKOANI ARUSHA

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AMPOKEA MAKAMU WA RAIS DR. GHARIB BILAL MKOANI ARUSHA

March 28, 2015

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA tayari kwa kumpokea Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe ambaye atafungua mkutano wa Vijana Viongozi wa Afrika na China unaofanyika kwenye hoteli ya Ngurudoto mkoani Arusha ukijumuisha vijana kutoka China na nchi za kiafrika. Dr. Gharib Bilal alipokelewa na katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurlahman Kinana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Arusha.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-NGURUDOTO -ARUSHA)2 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA mkoani Arusha kwa ajili ya mkutano wa Vijana viongozi wa Afrika na China, Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ndugu Felix Ntibenda na kutoka kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Steven Masele Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mkutano huo na Sadifa Hamis Juma Mwenyekiti wa UVCCM Taifa. 9 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana huku wakiangalia vikundi vya ngoma mbalimbali mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA mkoani Arusha.
8
 Rais Kikwete Afungua Mkutano wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam

Rais Kikwete Afungua Mkutano wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam

March 28, 2015
1
Rais Dkt.Jakaya mrisho Kikwete akifungua mkutano wa Viongozi wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNICC) jijini Dar es Salaam leo.
2
Baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini mbalimbali wakimsikiliza kwa makini Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa akiwahutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Viongozi wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam leo.
(picha na Freddy Maro).

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NA UJUMBE WAKE NDANI YA JIMBO LA SAME MASHARIKI.

March 28, 2015


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akipata maelezp mafupi namna  Tangawizi inavyochakatwa na kusindikwa katika kiwanda hicho,ambapo Katibu Mkuu Ndugu Kinana alishuhudia kiwanda hicho kukabidhiwa mashine za kuchakata Tangawizi kutoka SIDO,Kulia ni Mbunge wa Same Mashariki,Mh.Anne Kilango Malecela.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi namna  Tangawizi inavyosindikwa katika kiwanda hicho,ambapo Katibu Mkuu Ndugu Kinana alishuhudia kiwanda hicho kukabidhiwa mashine za kuchakata Tangawizi kutoka SIDO.Kiwanda hicho kilizinduliwa na Rais Kikwete mnamo Oktoba,2012.Katika taarifa iliyosomwa kiwandani hapo inaeleza kuwa kiasi cha fedha zaidi ya shilingi bilioni 500 zimetumika kwa ajili ya ujenzi pamoja na shughuli nyingine za kujenga uwezo ili kuhakikisha kiwanda hicho kinafanya kazi kwa ufanisi.
 Meneja wa SIDO mkoa wa Kilimajaro Bwa.Daniel Njowero akikabidhi nyaraka za mashine mpya za kuchakata Tangawizi kwa Mwenyekiti wa Bodi wa Kiwanda cha Tangawizi,Bwa.Yonaz Yohana Mgonja,huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakishuhudia
 Moja ya shamba la Tangawizi .
 Moja ya jengo la chuo cha VETA kilichopo katika kijiji Maore-Same Mashariki ambalo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alikagua na kujionea ujenzi wake,chuo hicho kinafadhiliwa na Kampuni ya Suzuki ya nchini JAPANI 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza kwenye mkutano mkuu wa jimbo la Same Mashariki,Ndugu Kinana pia alipokea taarifa ya kazi  za chama na taarifa ya Utekelezaji wa ilani.
 Wananchi wakishangilia jambo
  Sehemu ya umati wa Wakazi wa Same Mashariki,kijiji cha Ndungu wakishangilia jambo katika mkutano huo wa hadhara.
 Mmoja wa watoto akiwa amebeba kipeperushi cha kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake ndani ya Jimbo la Same Mashariki
 Wakazi wa Same Mashariki,kijiji cha Ndungu wakifuatilia mkutano huo wa hadhara
 Sehemu ya umati wa Wakazi wa Same Mashariki,kijiji cha Ndungu wakifuatilia mkutano huo wa hadhara
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kusuka nondo za nguzo za daraja la Mang’a Myamba wakati alipokagua ujenzi wa Daraji hilo Same Mashariki mkoani Kilimanjaro.Ujenzi wa Daraja hilo ni ahadi iliyoitoa Rais Kikwete kwa wananchi wa Same Mashariki katika suala zima la utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010
 Ujenzi wa daraja la Mang’a Myamba,Same Mashariki ukiendelea,Ujenzi wa Daraja hilo ni ahadi iliyoitoa Rais Kikwete kwa wananchi wa Same Mashariki katika suala zima la utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010