KATIKA PICHA; SIMBA ILIVYOIMALIZA POLISI MORO KWAO MOROGORO

February 15, 2015

MSHAMBULIAJI WA SIMBA, ELIUS MAGURI (KUSHOTO) AKIPAMBANA NA BEKI WA POLISI KATIKA MECHI YA LIGI KUU BARA KWENYE UWANJA WA JAMHURI MJINI MOROGORO, LEO. MAGURI ALIFUNGA BAO LA PILI WAKATI SIMBA IKIIBUKA NA USHINDI HUO WA MABAO 2-0.






 CHRISTIAN BELLA AACHA HISTORIA VALENTINE'S DAY, DAR LIVE

CHRISTIAN BELLA AACHA HISTORIA VALENTINE'S DAY, DAR LIVE

February 15, 2015

Christian Bella akiimba na mashabiki wimbo wa Usilie.
Bella akiwakonga mashabiki jukwaani.
Bella akimpa maiki mmoja wa kinamama waliojitokeza jukwaani kuimba Wimbo wa Nani Kama Mama.
Wanenguaji wa Malaika Music wakifanya yao jukwaani.
Baadhi ya mashabiki wakijiachia kwa kucheza Wimbo wa Nakuhitaji wa Christian Bella.
Umati wa mashabiki wakimfuatilia Bella (hayupo pichani) alipokuwa akiimba Wimbo wa Usilie.
MFALME wa masauti 'Christian Bella' akiwa na bendi yake ya Malaika Music wameandika historia mpya ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live, Mbagala.
Bella alianza kwa kuimba nyimbo zake kali za mapenzi kama vile Msaliti, Usilie, Nakuhitaji sambamba na kutambulisha wimbo wake mpya wa Nashindwa. Burudani ilinoga zaidi pale alipomaliza kwa Wimbo wa Nani Kama Mama huku akiimba pamoja na wakinamama wote waliojumuika naye jukwaani.
(Habari/Picha: Richard Bukos)
 MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AKABIDHI TUNZO YA RAIS YA MZALISHAJI BORA MWAKA 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AKABIDHI TUNZO YA RAIS YA MZALISHAJI BORA MWAKA 2014

February 15, 2015
 2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wadau mbalimbali kwenye Ghafla ya  utoaji Tunzo ya Rais ya mzalishaji bora Mwaka 2014 wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na          Jumuiya ya wafanyabiashara (Cti). Ghafla hiyo imefanyika jana usiku Februari 14,2015 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia maonesho mbalimbali kwenye Ghafla ya  utoajio Tunzo ya Rais ya mzalishaji bora Mwaka 2014 wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na          Jumuiya ya wafanyabiashara (Cti). Ghafla hiyo imefanyika jana usiku Februari 14,2015 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhi kikombe kwa washindi bora wa Tunzo ya Rais ya mzalishaji bora Mwaka 2014 uongozi wa Kiwanda cha Saruji Tanga, wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Jumuiya ya wafanyabiashara (Cti). Ghafla hiyo imefanyika jana usiku Februari 14,2015 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
5
Washiriki waliohidhudhia kwenye Ghafla ya  utoaji Tunzo ya Rais ya mzalishaji bora Mwaka 2014 wakimsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal alipokua akizungumza kwenye ghafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Jumuiya ya wafanyabiashara (Cti). Ghafla hiyo imefanyika jana usiku Februari 14,2015 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. (Picha na OMR)
6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal katikati akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa Tunzo ya Rais ya mzalishaji bora Mwaka 2014, wakati wa ghafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Jumuiya ya wafanyabiashara (Cti). Ghafla hiyo imefanyika jana usiku Februari 14,2015 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
7
 Tanzania yaipongeza China kwa misaada ya kimaendeleo.

Tanzania yaipongeza China kwa misaada ya kimaendeleo.

February 15, 2015
1
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatafa Bernard Membe akitoa hotuba kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika sherehe ya mwaka mpya wa Kichina jana katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
2
Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt Lu Youqing akitoa hotuba ya kumkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatafa Bernard Membe kutoa hotuba kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika sherehe ya mwaka mpya wa Kichina jana katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
6
Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt Lu Youqing (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadick Meck Sadiki(kulia) wakicheza ngoma ya iliyoimbwa kwa lugha ya Kishwahili na Kichina inayosema tupige jahazi iende mbali wakati wa sherehe ya mwaka mpya wa Kichina iliyofanyika jana katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
.4
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatafa Bernard Membe akizugumza jambo na Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt Lu Youqing wakati wa sherehe ya mwaka mpya wa Kichina iliyofanyika jana katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
5
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatafa Bernard Membe(kushoto) na Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt Lu Youqing (katikati) wakati wa sherehe ya mwaka mpya wa Kichina iliyofanyika jana katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es SALAAM, Sadick Meck Sadiki.
7
Baadhi ya wageni waliaohudhuria sherehe ya mwaka mpya wa Kichina iliyofanyika jana katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
(Picha na Eleuteri mangi- MAELEZO)
………………………………………………………………………….
Na Magreth Kinabo na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatafa Bernard Membe, ameipongeza Serikali Jamhuri ya China kwa msaada wake wa kuhakikisha Tanzania imefungua idara ya maalum ya upasuaji wa moyo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). Hayo yamesemwa na Waziri Membe jana katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika sherehe ya mwaka mpya wa Kichina. “Tuna mengi ya kusema kuhusu misaada ya maendeleo inayoletwa na ndugu zetu Wachina Sasa hivi muhimbili, kwa mfamo wametusaidia kufungua idara maalum ya upasuaji wa moyo, ambayo sasa unaweza kufanya upasuaji wa moyo jambo ambalo lilikuwa hadithi ya kufikirika katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. “Lakini sasa hivi Watanzania wanaweza kwenda kutibiwa ugonjwa wa moyo kwa kupasua na kufanyiwa matibabu. Tunawapongeza Serikali ya China kwa kuleta msaada mkubwa wa aina hii nchini Tanzania,” alisema Waziri Membe. Katika sherehe hizo za mwaka mpya,Jumuiya ya Wachina waishio nchini Tanzania waliungana pamoja na wageni wengine kusherehekea siku kuu hiyo, ambayo itaanza rasmi February 18, mwaka huu. Waziri Membe akifafanua kuhusu mwaka huo, alisema kuwa utajulikana kama mwaka wa kondoo, ambapo mwaka jana 2014 ulijulikana kama mwaka wa farasi. Jumuiya hiyo wamechagua siku hiyo ya Februari 14 kwa kuwa ni mwisho wa wiki tofauti na siku yao rasmi ya mwaka mpya ambayo itaangukuia Jumatano ambayo ni katikati ya wiki na kuwanyima wengine fursa ya kuhudhuria na wanasherehekea siku yao ya mwaka mpya 2015. Aliongeza misaada mingine ya maendeleo ilitolewa na nchi hiyo ni miradi ya maji Dodoma na Chalinze mkoani Pwani, mradi ya kilimo Dakawa mkoani Morogoro, Uwanja wa Taifa wa Michezo na Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, uliopo jijini Dar es Salaam. Kwa upande wake Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt Lu Youqing alisema sherehe hiyo kama alama ya kufahamu utamaduni wa nchi hiyo, imeshafanyika kwa mafanikio mkubwa kwa miaka sita nchini Tanzania na inapendeza, ambayo ni mfano mzuri wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta ya utamaduni.
“Uhusiano wa Tanzania na China sasa uko katika kipindi kizuri cha Juu, mwaka 2014 uliopita ni miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na China. Kwa nusu karne uhusiano nchi hizi mbili zinasaidiana na urafiki wa baina ya nchi hizi mbili umepata maendeleo makubwa,” alisema Balozi Dkt Youqing. Balozi huyo aliishukuru Serikali Tanzania kwa kuunga mkono sherehe hiyo na aliwaomba wananchi wa nchi hizo kushirikiana na kusaidiana ili kupata maendeleo pande zote mbili. Serikali hiyo ya China imepongezwa kwa kuwa nchi mfano wa kuigwa kwa kutoa misaada mbalimbali Barani Afrika,ambapo imesaidia kutatua migogoro na kutoa dola za Marekani milioni 35 kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa ebola na kutoa madaktari 200 ili kukabiliana na janga hilo katika nchi za Liberia,Guinea pamoja na Sierra Leone
MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR AREJEA NCHINI AKITOKEA QATARI KWA ZIARA YA KIKAZI.

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR AREJEA NCHINI AKITOKEA QATARI KWA ZIARA YA KIKAZI.

February 15, 2015

1
Makamu wa Kwanza wa Rais  wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akishuka ndege katika uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume  baada ya kumaliza ziara ya Kiserikali nchi Qatar.
2
Makamu wa Kwanza wa Rais wa  Zanzibar Maalim  Seif Sharif Hamad akivishwa shada la maua  alipowasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume  akitokea  nchini Qatar.
3
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui akisalimiana na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alipowasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume akitokea nchini Qatar, wa kwanza (kushoto) Waziri wa Nchi katika Ofisi yake  Fatma Abdulhabib Ferej. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
4
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar mara baada ya kuwasili kutoka ziara yake ya Qatar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
5
Mwandishi wa habari wa Radio Adhana FM Said  Mussa Makame akimuuliza swali Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar.
7
Maalim Seif Sharif Hamad akiagana na wananchi waliofika Uwanja wa ndege wa Zanzibar kumpokea  akitokea  Qatar.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

BALOZI WA PROMOSHENI YA JAYMILLIONS YA VODACOM'JAY'AWALIPIA ABIRIA WOTE NAULI WA KITUO CHA MAWASILIANO JIJINI

February 15, 2015

Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary Daud”Zembwela”(kushoto)akimkabidhi fedha mmoja wa abiria wa basi linalofanya safari zake kutoka kituo cha mabasi cha mawasiliano cha ubungo kwenda Mwananyamala jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuwalipia abiria wenzake nauli ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wateja wa kampuni hiyo kutuma neno Jay kwenda 15544 ili kujua kama wameshinda.
Mkazi wa jijini Dar es Salaam Mudy Seleman(kushoto)akikabidhiwa fedha kwa ajili ya nauli na Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary Daud”Zembwela” wakati wa kuhamasisha wateja wa kampuni hiyo kutuma neno Jay kwenda 15544 ili kujua kama wameshinda iliyofanyika katika kituo cha mabasi cha Mawasiliano ubungo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi waliokuwa wakisubiria usafiri katika kituo cha mabasi cha mawasiliano ubungo jijini Dar es Salaam wakipiga picha ya pamoja na Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary Daud”Zembwela”(kushoto)baada ya kuwalipia nauli wakati wa kuhamasisha wateja wa kampuni hiyo kutuma neno Jay kwenda 15544 ili kujua kama wameshinda iliyofanyika katika kituo hicho.
Meneja uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akitoa elimu kwa mmoja wa abiria wa basi liendalo Gongolamboto kutoka kituo cha mabasi cha mawasiliano ubungo jijini Dar es Salaam juu ya Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo ambapo wateja wanatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544 ili kujua kama wameshinda.
Baadhi ya abiria wakiwa na watoto wao katika kituo cha mabasi cha Mawasiliano ubungo jijini Dar es Salaam, wakifafanuliwa jambo na mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Joyce Mhina kuhusiana na Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo wakati Balozi wa promosheni hiyo alipoenda kituoni hapo kutoa elimu kuhusiana na promosheni hiyo na kuwalipia wasafiri wote bure wa daladala nauli kulingana na sehemu wanayo kwenda ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wananchi kushirikia katika promosheni hiyo.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary Daud”Zembwela”(aliyesimama)akitoa elimu juu ya promosheni hiyo kwa abiria waliopanda daladala zinazofanya safari za mlandizi kutoka kituo cha mabasi cha mawasiliano ubungo jijini Dar es Salaam na aliwalipia nauli abiria wote bure ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wananchi kushirikia katika promosheni hiyo.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Kondakta wa basi linalofanya safari zake kutoka kituo cha mabasi cha Mawasiliano ubungo kwenda Kawe jijini Dar es Salaam, Hamis Omari(kushoto)akikabidhiwa nauli ya abiria wote waliopanda gari lake na Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary Daud”Zembwela”(kulia) wakati alipokuwa akihamasisha wateja wa kampuni hiyo kituoni hapo kutuma neno Jay kwenda 15544 ili kujua kama wameshinda. Ambapo abiria wote waliokuwepo kituoni hapo walilipiwa nauli kulingana na safari zao.

Balozi wa promosheni ya Jaymilioni inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hillary Daud‘Jaymillions’ mwishoni mwa wiki alikuwa kivutio kwa wananchi wengi alipotembelea eneo kituo cha mabasi cha Ubungo Mawasiliano na kuwahimiza wananchi kuchangamkia fursa  zinazojitokeza katika maisha yao ambapo pia   alitoa ofa ya kuwalipia nauli wasafiri waliokuwa wamepanda mabasi kuelekea sehemu mbalimbali za jiji waliokuwa kituono hapo.  

Ziara hiyo ilileta msisimko mkubwa wa wananchi waliokuwa eneo hilo ambapo  baadhi yao walilazimika kuacha shughuli zao kumwangalia balozi huyo na wengine kuomba kupiga naye picha ikiwemo waliompiga picha kwa kutumia simu zao zao mkononi.
Balozi huyo  alitumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi kuwa wanaotumia mtandao wa Vodacom wahakikishe kila siku  wameangalia kama namba zao zimeshinda mamilioni ya fedha kwa kutuma neno JAY kwenda namba 15544 na aliwataka wale ambao hawako kwenye mtandao wa Vodacom wajiunge nao ili  washiriki kwenye promosheni hii kubwa iliyolenga kubadilisha maisha ya watanzania wengi kuwa mamilionea.

“Leo nimewafuata huku kuwapatia ofa na kuwafikishia ujumbe kwa maana naona wengi wenu bado hamjachangamkia fursa hii kwa kuangalia iwapo  namba zenu zimeshinda kila siku,bado tunayo mabilioni ya fedha kwa ajili yenu hivyo changamkia fursa hii muweze kujishindia mamilioni ya fedha katika kipindi hiki cha promosheni.Kila siku kuna mshindi 1 wa shilingi  milioni 100,000,washindi 10 wa milioni 10 na washindi 100 wa shilingi milioni 1 hivyo kazi kwenu na Vodacom”.Alisema

Naye Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia, aliwahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni hii kwa kuhakikisha wametuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza nafasi zao za kushinda pia alisema kuwa njia nyingine ya kushinda ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo  mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-

  Alisema kuwa tangu promosheni hii ianze mapema mwezi uliopita  mteja mmoja ameishajishindia milioni 100,  wateja 2  wamekwishajishindia milioni 10 na wateja kumi na moja wameisha jishindia shilingi milioni moja kila mmoja  na  maelfu ya wateja wengine tayari wamejishindia muda wa maongezi.

Wateja wa Vodacom ambao tayari wamejipatia mamilioni ya fedha kupitia promosheni hii ni Uwezo Magedenge mfanyakazi nyumba ya wageni  wilayani Kilolo mkoani Iringa ambaye amejishindia milioni 100. Waliojishindia milioni kumi kila mmoja wao Hynes Petro Kanumba mkulima kutoka Inyonga mkoani Rukwa na James Mangu mfanyabiashara  kutoka wilayani Magu.

 Washindi wa milioni moja  ni Chiphold Wanjara mjasiriamali wa Kutoka Mwanza ,Janeth Nganyange wa Njombe,Evarista Minja mwanafunzi kutoka Mwanza,Stanley Bagashe Mwalimu  wa Shinyanga,Ramadhani Maulid Mkulima kutoka Dodoma, ,Lucas Masegese wa Shinyanga,Ayub Makonde mfanyabiashara wa Mbeya,Hyasinti Mlowe Fundi gereji kutoka Njombe,Florian Gwayu mchapishaji kutoka Arusha,Modesta Millanzi mjasiriamali kutoka Peramiho mkoani Ruvuma na Nobert Minungu mwanafunzi kutoka Mbwanga mkoani Dodoma.


“Promosheni hii itadumu kwa muda wa siku mia moja hivyo  juma  hili inaingia katika wiki ya nne na bado kuna mabilioni ya fedha yamewasubiri watanzania,wanachopaswa kufanya ni kuhakikisha  kila siku wameangalia kama namba zao zimeibuka na ushindi kwenye droo ya siku kwa kutuma neno Jay kwenda namba 15544.”Alisisitiza.