March 02, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MSIKITI KIBOJE UWANDANI ZANZIBAR LEO

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Alhajj Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wananchi wa kijiji cha kiboje uwandani alipowasili katika kijiji hicho leo Februari   2-2014 kwa ajili ya kufungua msikiti wa Masjid Fatima Binti Rasuuli uliojengwa na baadhi ya wafadhili kwa kushirikiana na Muwakilishi wa Jimbo la Uzini Mhe. Mohammed Raza.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Alhajj Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Rais mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi wakiondosha kitambaa kuzindua rasmi msikiti wa Masjid Fatima Binti Rasuuli leo Februari 2-2014 uliojengwa katika kijiji cha kiboje uwandani Zanzibar.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Alhajj Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kufungua rasmi msikiti wa Masjid Fatima Binti Rasuuli leo Februari 2-2014 katika kijiji cha kiboje uwandani Zanzibar.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Alhajj Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wananchi wa kijiji cha kiboje.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Alhajj Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wananchi wa kijiji cha kiboje uwandani baada ya kufungua rasmi msikiti wa Masjid Fatima Binti Rasuuli uliopo katika kijiji cha kiboje uwandani Zanzibar leo Februari 2-2014.
 

Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Kabi akiongoza Dua ya pamoja baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Alhajj Dkt. Mohammed Gharib Bilal kufungua msikiti wa Masjid Fatima Binti Rasuuli uliopo katika kijiji cha kiboje uwandani Zanzibar leo Februari 2-2014.     (Picha na OMR)
March 02, 2014
CCM YAZIDI KUTESA KAMPENI ZA UBUNGE KALENGA
 Mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa (32), akiwapungia wananchi huku akiwa amebebwa alipowasili kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Mangalali,  Kata ya Ulanda, Iringa Vijijini leo mchana.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba akiongoza msafara wa mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa aliyebebwa walipowasili kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Mangalali.
March 02, 2014

AFISA WA JESHI LA WANANCHI AITOA KIMASOMASO TANZANIA,KILIMANJARO MARATHONI.

Kilimanjaro Marathoni imeshirikisha watu wa rika zote.
Mshindi wa kwanza wa Full Marathoni kwa upande wa wanawake Frida Lodepa wa Kenya.
Mshindi wa kwanza wa Half Marathoni ,Jackline Sakilu akihitimisha mbio.
March 02, 2014

WEMA SEPETU AFANYA SHINDANO LA KUSAKA VIPAJI VYA KUIGIZA KWA WATOTO ENEO LA LEADERS JIJINI DAR LEO

Msanii wa Bongo Movie, Wema Sepetu na pia alikuwa ni jaji wa shindano la kusaka vipaji kwa watoto waliokuwa na umri kuanzia miaka minne(4) mpaka kumi na tano (15) akizungumza na mshiriki wa shindano hilo la kusaka vipaji kwa wanaojua kuigiza. Shindano hili limefanyika leo kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam na kuwapata watoto watatu waliokuwa wanaitajika.
Jaji Wema Sepetu akiwa na Jaji mwenzake Aunt Ezekiel walipokuwa wanawafanyia usahili watoto waliofika kwenye shindano la kusaka vipaji vya watoto wanaoweza kuigiza.

SIMBA SC YAZINDUKA,YAWAFUMUA RUVU SHOOTING 3-2, TAMBWE APIGA MBILI

March 02, 2014
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
SIMBA SC imezinduka baada ya jioni hii kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo uliochezwa sambamba na mvua mwanzo hadi mwisho, hadi mapumziko tayari Simba SC walikuwa mbele kwa mabao 2-0.
Mrundi Amisi Tambwe aliifungia Simba SC bao la kwanza dakika ya 25 baada ya kuwahi mpira uliotemwa na kipa Abdallah Rashid kufuatia shuti la mpira wa adhabu la Said Ndemla.
Mtambo wa mabao; Amisi Tambwe akishangilia baada ya kufungfa bao la pili leo
March 02, 2014

WANANCHI WAFUNGA BARABARA YA MBEYA CHUNYA BAADA YA MWENZAO KUKAMATWA / MTUHUMIWA AKIMBIA NA PINGU ZA POLISI

Mkuu wa wilaya ya Chunya Deotatus Kinawiro akihutubia wananchi wa Chalangwa

Mkuu wa wilaya ya Chunya Deotatus Kinawiro akipokea nyaraka toka kwa afisa mpelelezi wilaya ya Chunya
March 02, 2014

UCHAGUZI MKUU WA TASWA WAFANYIKA DAR LEO, JUMA PINTO KUENDELEA KUONGOZA TASWA

 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi Tanzania Taswa, Juma Pinto, akijieleza mbele ya wajumbe na wanachama wa Taswa wakati akiomba kura kurejea kukiongoza chama hicho kwa muhura wa pili. Uchaguzi Mkuu wa Taswa umefanyika leo mchana kwenye Ukumbi wa NSSF Water Front. Katika uchaguzi huo Juma Pinto ameibuka kidedea na kuchaguliwa kuwa mwenyekiti kwa awamu nyingine.
 Akiomba kura...

George John, akitangaza kujiondoa kuendelea kuwania nafasi ya Katibu Msaidizi.

Katibu Mkuu wa Taswa, Amir Mhando, akiomba kura.
 Patrick Nyembela, akiomba kura kwa niaba......
 Shija, akiomba kura kuwa Mweka hazina....

Wajumbe wakitafakari....
 Meza kuu.....
 Baadhi ya wajumbe na wagombea Ujumbe.....
March 02, 2014

SHY-ROSE AIOMBA SERIKALI YA TANZANIA KUWEZESHA WATANZANIA WAIFAHAMU EAC NA FAIDA ZAKE 1069410_488216681262565_60269170_n
Katibu wa Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Shy-Rose Bhanji (pichani) amerejea nchini baada ya ziara ya siku 10 ya Wabunge wa EALA nchini Kenya na hicho ndicho alichokisema kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nimerejea nchini baada ya ziara ya siku 10 nchini Kenya. Ziara hii ya wabunge wa EALA ilikuwa kwa mwaliko wa Serikali ya Kenya lengo likiwa kuhamasisha wananchi wa Kenya kupata ufahamu mkubwa juu ya Mtangamano wa Jumuiya na faida zake. Tulipata nafasi ya kuonana na wananchi, wafanyabiashara, wabunge, maseneta, magavana, asasi za kiraia na makundi mengine.