NYALANDU AKAGUA MADHARA YA MAMBA MLA WATU MASASI

May 23, 2015


 WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akimsikiliza diwani wa Nhavila, wilayani Masasi, Meja Ramadhan Chilumba, jana, katika sehemu ya mto, wakati waziri huyo alipotembelea mto Ruvuma katika kijiji cha Manyuli ambako alitembelea watu waliojeruhiwa na wengine kuuawa na
mamba, alipokwenda kutoa kifuta machozi kutoka wizarani kwake.

 Katibu Tawala wilaya ya Masasi, Dunford Peter akimwonyesha ramani Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ya sehemu ya mto huo, wakati waziri huyo alipotembelea mto Ruvuma katika kijiji cha Manyuli ambako alitembelea watu waliojeruhiwa na wengine kuuawa na mamba, alipokwenda kutoa kifuta machozi kutoka wizarani kwake.

 Diwani wa Nhavila, wilayani Masasi Meja Ramadhan Chilumba akimsaidia Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kupanda kingo za mto, alipotembelea mto Ruvuma mpakani na Msumbiji kutoa kifutajasho kwa watu waliojeruhiwa na kuuawa na mamba katika mto huo.

 Diwani wa Nhavila, wilayani Masasi Meja Ramadhan Chilumba akimwongoza Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alipotembelea mto Ruvuma katika kijiji cha Manyuli wilayani Masasi, mpakani na Msumbiji alikokwenda kutoa kifutajasho kwa watu waliojeruhiwa na kuuawa na mamba katika mto huo.

 Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na wanakijiji wa Manyuli wilayani Masasi ambako alitembelea watu waliojeruhiwa na wengine kuuawa na mamba, alipokwenda kutoa kifuta machozi kutoka wizarani kwake.

 Wanakijiji wa Manyuli, wilayani Masasi wakimsikiliza Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alipozungumza nao jana, alitembelea watu waliojeruhiwa na wengine kuuawa na
mamba, alipokwenda kutoa kifuta machozi kutoka wizarani kwake.

Waziri wa maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akikabidhi hundi ya fidia kwa Katibu Tawala wilaya ya Masasi Dunford Peter ili zigawiwe kwa watu walioathiriwa na mamba katika vijiji vilivyo kando ya mto Ruvuma jana, ikiwa ni mpango wa serikali kufidia watu waliojeruhiwa ama kuuawa na mamba nchini.
MITAZAMO HASI KITAMADUNI CHANZO CHA MAUAJI YA WATU WENYE ALBINISM

MITAZAMO HASI KITAMADUNI CHANZO CHA MAUAJI YA WATU WENYE ALBINISM

May 23, 2015
DSC_0569
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Bi. Zulmira Rodgrigues, akiwasilisha mada katika warsha ya siku tatu iliyofanyika katika kijiji cha Nyakahungwa wilayani Sengerema mkoani Mwanza kuhusu ushirikishaji jamii katika kuandaa na kutekeleza mikakati itakayochangia kuzuia na kutokomeza unyanyasaji na dhulma zinazofanywa dhidi ya watu wenye albinism iliyoshirikisha waganga wa asili, wauguzi na wakunga, viongozi wa dini, walimu pamoja na watu maarufu iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)
Na Modewjiblog team, Mwanza
Mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) yanayoendelea nchini yanatokana na mitazamo hasi kitamaduni miongoni mwa wanajamii.
Hayo yameelezwa na washiriki wa warsha ya siku tatu inayoendelea katika kijiji cha Nyakahungwa kata ya Nyakahungwa wilayani Sengerema yenye lengo la kubadili mitazamo iliyojengeka katika jamii na kusababisha madhara makubwa kwa watu wenye albinism iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Warsha hiyo ni miongoni mwa mlolongo wa warsha nne zitakazofanyika katika wilaya za Sengerema, Mwanza, Kahama na Bariadi kwa kuzishirikisha jamii kuibua masuala mbalimbali yanayobagua, kunyanyapaa na kuwatenga watu wenye albinism katika maeneo husika.
Warsha hizo zinafanyika katika kipindi ambacho kumetokea mauaji ya mtoto wa kike, msichana na kijana wenye albinism wilayani Sengerema wakati tarehe 14 Mei 2015 mwanamke mmoja alikatwa mkono wilayani Bariadi.
DSC_0522
DSC_0532
Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Sengerema, Bw. Bushaija Vicent (kulia), akitoa takwimu za idadi ya za wanafunzi wenye albinism katika wilaya yake kwa Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO Bi. Zulmira Rodgrigues.
Kwa mujibu wa Afisa Maendeleo Jamii wilayani Sengerema Bwana Bushaija Vicent kati ya shule za msingi 191 wilayani humo ni Shule zenye watoto wenye albinism ni 14, Idadi yao ni 16 katika shule ya awali watoto 4 wana albinisim, vyuo mbalimbali Sengerema vijana 4 wana albinism na katika Shule za sekondari 48, watoto wenye albinism 4.
Akitoa mada kuhusu uhamasishaji jamii katika masuala ya albinism, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO Bi Zulmira Rodgrigues amesema miongoni mwa masuala ambayo warsha italenga ni kutafakari kwa kina kwa nini watu wenye albinism wanauawa, kubaguliwa, kutengwa na mambo yanayosababisha Tanzania kuongoza katika mauaji hayo ikilinganishwa na nchi nyingine ambazo pia zina watu wenye albinism.
“Watu wenye albinism hawauwawi katika sehemu nyingine duniani, kwa nini Tanzania? Ikiwa mauaji hayo yako kwa wingi nchini Tanzania basi kuna tatizo kubwa ambalo linatakiwa kufanyiwa kazi, na si serikali, UNESCO wala taasisi yoyote ambayo inaweza kuleta mabadiliko hayo isipokuwa jamii yenyewe,” alisema Rodrigues.
Tatizo kubwa lililotajwa kuhusiana na mauaji ya watu wenye albinism ni utamaduni uliojengeka katika fikra za watu na kuwa na imani kwamba watu wenye albinism si watu wa kawaida, hawana hadhi na hawastahili kuishi.
Watu wenye albinism ni watu wa kawaida wanaostahili heshima na kulindwa kama binadamu wengine kulingana na kanuni na sheria za nchi na za kimataifa zinazopinga ubaguzi wa rangi, jinsia, tabaka na kukatisha maisha ya mtu. Tofauti ni kwamba rangi yao inatokana na ukosefu wa vinasaba asili vijulikanavyo kama melanin, vyenye uwezo wa kuzalisha rangi ya nywele, macho na ngozi.
Utamaduni uliojengeka katika jamii wa kuwabagua, kuwatenga na kuwapuuza watu wenye ulemavu wa ngozi kumehalalisha mauaji ambayo kwa hivi sasa imekuwa biashara ya kuuza viungo vya watu wenye albinism kwa waganga wa asili kwa lengo la kupata utajiri, cheo na madaraka.
“Mara nyingi waganga wa asili wamekuwa wakitajwa kuwa ndio chanzo cha mauaji hayo kwa ajili ya imani potofu ya kujipatia utajiri, vyeo na madaraka. Biashara hiyo inaonekana kushamiri kwa kuwa hakuna mifumo mahsusi kudhibiti maafa hayo,” alisema mmoja wa washiriki anayeshughulikia masuala ya usalama.
DSC_0545
Mratibu na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO Bi. Rose Haji Mwalimu, akichangia mada kuhusu ushirikishaji jamii katika kuandaa na kutekeleza mikakati itakayochangia kuzuia na kutokomeza unyanyasaji na dhulma zinazofanywa dhidi ya watu wenye albinism iliyoshirikisha waganga wa asili, wauguzi na wakunga, viongozi wa dini, walimu pamoja na watu maarufu iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO). Katikati ni Mratibu ambaye pia ni Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias na Kulia ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Bi. Zulmira Rodgrigues.
Akichangia mada wakati wa majadiliano yanayokusudiwa kuzalisha mikakati ya kukomesha maovu hayo, Mratibu na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO Bi Rose Haji Mwalimu alisema kwamba wakati umefika wa kutambua kitu gani kizuri katika tamaduni zilizopo zitakazoweza kusaidia kuleta mafanikio na kuachana na zile ambazo hazina tija na zinasababisha maafa katika maendeleo na ustawi wa jamii.
“Ni kweli kuna changamoto nyingi katika jamii zinazosababishwa na kuhalalisha tamaduni zinazolenga kupotosha badala ya kujenga. Tukiendelea kuzikumbatia tutajikuta tunajenga taifa lisiloona mbali kimaendeleo kuhadaiwa na watu wenye ubinafsi kutoka nje na ndio maana Tanzania imekuwa soko kubwa au shamba lenye rutuba ya kupandikiza mbegu ambazo mavuno yake hupatikana kwa urahisi”, alisema Bi Mwalimu.
Katika warsha hiyo washiriki walibaini maeneo makuu matatu ya kuyawekea mpango kazi. Maeneo hayo ni Kuzuia mauaji, ubaguzi, unyanyapaa na kuwatenga, eneo la pili ni kuwalinda watu wenye albinism katika maeneo ya makazi, mashuleni, katika jamii na familia zao na la tatu ni hatua za kisheria wale wote watakaoonekana kuhusika moja kwa moja au kwa namna nyingine katika kuwatendea maovu watu wenye ulemavu wa ngozi kuanzia ngazi za kimataifa, kitaifa, kifamilia na shuleni.
DSC_0553
Mganga wa jadi kutoka kijiji Nyanzenda, wilayani Sengerema, Maimuna Musa akizungumzia jinsi anavyotoa huduma za kutibu watoto magonjwa mbalimbali ya watoto ikiwemo na huduma ya kuzuia mwanamke asizae mtoto mwenye ulemavu wa ngozi.
DSC_0549
Mganga wa jadi kutoka kijiji cha Nyakasungwa, Omary Mongongwa akitoa msimamo kuhusu uwezo wa tiba kwa waganga wa jadi unavyotofautiana na kuwasihi waganga wenzake wa jadi wanapojadili wazungumzie kazi za mtu binafsi na utendaji wake na si kuusemea moyo wa mganga mwingine.
DSC_0596
Mzee maarufu kutoka kijiji cha Bukokwa, Felician Buhumbi, akifafanua hatua zilizokuwa zikichukuliwa wakati wa Ukoloni dhidi ya waganga asili wenye kupiga ramli chonganishi wakati wa warsha ya siku tatu iliyofanyika katika kijiji cha Nyakahungwa wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
DSC_0511
Sehemu ya washiriki wa warsha hiyo ya siku tatu iliyowashirikisha, Waganga wa Jadi, Viongozi wa dini, walimu shule za msingi na sekondari, wazee maarufu, Wakunga, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Shirika la Under the Same Sun, Baraza la taifa la dawa asilia, Afisa wa polisi wa dawati la jinsia pamoja na Maafisa wa mkoa wa Mwanza na wa wilaya ya Sengerema.
DSC_0652
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Bi. Zulmira Rodgrigues aliyeambatana na mbunge wa viti maalum CCM anayetetea maslahi ya watu wenye albinism, Mh. Al-Shaymaa Kwegyir wakiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki.
 RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR NDUGU SEIF SHARIFF HAMAD.

RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR NDUGU SEIF SHARIFF HAMAD.

May 23, 2015
seif1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) leo, Jumamosi, Mei 23, 2015 amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Seif Shariff Hamad ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) katika Ikulu Ndogo, Dodoma. Rais Kikwete akimwaga Mheshimiwa Hamad baada ya kumalizika kwa kikao hicho.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: UANDIKISHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA KUANZA RASMI KESHO JUMAPILI MKOANI RUKWA

May 23, 2015

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 23 Mei 2015  kuelezea juu zoezi la uandikishiaji wa Wananchi kwenye daftari la kudumu la Mpigakura litakaloanza rasmi kesho tarehe 24 Mei 2015 Mkoani Rukwa. Kulia kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa.
Mkutano na waandishi wa habari ukiwa unaendelea. Kwa taarifa kamili SOMA HAPA CHINI:-
 (Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa@Rukwareview.blogspot.com)
Jamii yaombwa kuuenzi Utamaduni wa Mtanzania

Jamii yaombwa kuuenzi Utamaduni wa Mtanzania

May 23, 2015
PR1
Mkurugenzi wa Maendeleo ya nUtamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko (kushoto) akiwa katika maandanano ya kuadhimisha siku ya Uanuai wa Utamaduni Dunia jijini Dar es Salaam juzi ambapo maaandamano hayo yalianzia katika viwanja vya maonyesho ya Biashara vya Mwalimu Nyererere Sabasabasa kupitia mtongani kwa Aziz Aly na kurudi kiatika viwanja hivyo.Kulia ni balozi wa India nchini Mhe.Debnath Shaw.
PR2
Baadhi ya vikundi vya sanaa na wananchi wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha siku ya uanuai wa Utamaduni Dunia maandamano hayo yalianzia katika viwanja vya maonyesho ya Biashara vya Mwalimu Nyererere Sabasabasa jijini Dar es Salaam kupitia mtongani kwa Aziz Aly na kurudi kiatika viwanja hivyo.Siku hiyo ya Uanuai wa Utamaduni uadhimishwa tarehe 21 May kila mwaka Duniani kote ikiwa na lengo la kukukuza na kuibua kazi za sanaa na utamaduni.
PR3
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Biashara Tanzania (Tan Trade) Bibi. Jacqueline Maleko akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Uanuai wa Utamaduni Duniani. Hafla iliyofanyika mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko na wa mwisho kushoto ni Balozi wa India nchini Tanzania Bw. Debnath Shaw.
PR4
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko Mkurugenzi kizungumza wakiti wa ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Uanuai wa Utamaduni Duniani. Hafla iliyofanyika mapema wikiendi hii jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Mamlaka ya Biashara Tanzania (Tan Trade) Bibi. Jacqueline Maleko na mwisho kushoto ni Balozi wa India nchini Tanzania Bw. Debnath Shaw.
PR5
Wapiga vyombo vya muziki na ngoma kutoksa kikundi cha Tanzania wkichakarika wakati wa zoezi la kutumbia kwenye hafla ya ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya uanuai wa Utamaduni.
PR6
Wanakikundi cha sanaa kutoka nchini India wakitumbuiza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uanuai wa Utamaduni Duniaa ambayo nufanyika kila tarehe 21 mwezi wa tano kila mwaka.
PR7
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermsa Mwansoko akicheza Bao na Balozi wa India nchini Bw. Debnath Shaw wakati wa maadhimisho ya siku ya Uanuai wa Utamaduni Duniani ambapo kitaifa imefanyika jijini Dar es Salaam.Maadhimisho hayo yameambatana na maonyesho ya wajisariamali wa bidhaa za kiutamaduni na kuratibiwa kwa ushirikianao baiona ya Wizara yenye dhamana ya Utamaduni na Tan Trade.
PR8
Mkurugenzi wa Maendeleo ya nUtamaduni KUTOKA Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko akiwa akiangalia namna wanafunzi wa shule
…………………………………………………………………
Na: Genofeva Matemu – Maelezo Wadau mbalimbali wa sekta ya Utamaduni nchini wameiomba jamii kuuenzi utamaduni wa Mtanzania kwa kuzingatia matumizi ya vitu vinavyoendana na tamaduni za Tanzania ili kudumisha na kuenzi mila na desturi za Tanzania. Kauli hiyo imeibuliwa na wadau wa sekta ya Utamaduni walioshiriki katika ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya Uanuai wa Utamaduni Duniani inayoadhimishwa kila tarehe 21 ya mwezi Mei ambapo Tanzania imeadhimisha siku hiyo katika Uwanja wa Mwalimu Nyerere Sabasaba jana jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bibi. Jacqueline Maleko ameiomba serikali kujenga kituo cha Utamaduni kitakachotumika kuendeleza, kudumisha na kuhamasisha matumizi ya vitu vya asili ya Tanzania hivyo kuendeleza tamaduni zetu. “Utamaduni wa mtanzania ni urithi wenye mashiko kama utadumishwa na kuhamasisha jamii kutumia vitu vya asili kama vile nyimbo, ngoma, uchongaji, mashahiri, uchoraji, filamu Sanaa, vyakula na mavazi kwa kuviendeleza na kuvinadi ndani na nje ya Tanzania” Amesema Bibi Maleko. Akitoa maoni yake kuhusu utamaduni wa Tanzania Mwalimu Gasper Maro kutoka Shule ya Msingi Magomeni amesema kuwa shule za msingi zimekuwa zikijitahidi kuuenzi utamaduni wa Tanzania kwa kuwahamasisha wanafunzi kuimba nyimbo za jadi na kucheza ngo ma za makabila mbalimbali ili kuweza kujua tamaduni za kila kabila lililopo nchini Tanzania, Hata hivyo mwalimu Maro amesema kuwa utamaduni wa Tanzania kwa sasa unashuka kutokana na kizazi cha sasa kuiga tamaduni za nchi nyingine na kudharau tamaduni zao hivyo kuwaomba maafisa utamaduni nchini kuandaa programu mbalimbali zitakazokuwa zikihamasisha jamii kuishi kwa kufuata tamaduni za Tanzania. Kwa upande wake mwanafunzi Agustino George Pius kutoka Shule ya Msingi Magomeni amesema kuwa utamaduni wa Tanzania umekua ukibadilishwa na vijana kutokana na maendeleo ya teknolojia hasa katika upande wa mavazi, vyakula, pamoja na staili ya maisha wanayoishi vijana wa sasa. Naye Afisa Utumishi kutoka Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bw. Elius Ngemela ameitaka jamii kutambua kuwa utamaduni ni utambulisho wa nchi ambao kama utatumika vizuri utasaidia kukuza uchumi wa nchi na kutoa ajira katika jamii hivyo kuuthamini na kuudumisha kwa maendeleo ya nchi yetu.

MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOA WA TANGA (CUF) AMINA MWIDAU ATEMBELEA HOSPITALI YA WILAYA YA PANGANI

May 23, 2015

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Pangani,Mugiri Emili akisisitiza jambo kwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga kupitia (CUF) Amina Mwidau wakati akipotembelea hospitali hiyo kuwafariji wagonjwa na kugawa zawadi mbalimbali ikiwemo sabuni,sukari ikiwemo mahitaji muhimu na kukabidhi jengo la kupumzikia wagonjwa alilolijenga kwa gharama za sh.milioni tano na mbunge huyo.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga kupitia (CUF) Amina Mwidau (mkoba wa bluu) akisalimiana na wakina mama wakati alipotembelea hospitali ya wilaya ya Pangani jana kuwaona wagonjwa kuwafariji na kugawa zawadi mbalimbali ikiwemo sabuni,sukari pamoja na mahitaji muhimu na kukabidhi jengo la kupumzikia wagonjwa alilolijenga kwa gharama za sh.milioni tano na mbunge huyo.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga kupitia (CUF) Amina Mwidau akizungumza na wakina mama waliokuwa wakisubiri huduma za matibabu kwenye hospitali ya wilaya ya Pangani jana wakati alipotembelea hospitali ya wilaya ya Pangani jana kuwaona wagonjwa kuwafariji na kugawa zawadi mbalimbali ikiwemo sabuni,sukari pamoja na mahitaji muhimu na kukabidhi jengo la kupumzikia wagonjwa alilolijenga kwa gharama za sh.milioni tano na mbunge huyo.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga kupitia (CUF) Amina Mwidau kulia kushoto kwake ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wlaya ya Pangani,Mugiri Emili wakielekea wodini kwa ajili ya kuwatazama wagonjwa ,kugawa zawadi mbalimbali ikiwemo sabuni,sukari pamoja na mahitaji muhimu na kukabidhi jengo la kupumzikia wagonjwa alilolijenga kwa gharama za sh.milioni tano na mbunge huyo.
Katikati ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga kupitia (CUF) Amina Mwidau akitoa maelekezo namna ya ugawaji wa zawadi kwa wagonjwa wakati alipotembelea hospitali ya wilaya ya Pangani jana kwafariji wagonjwa na kugawa zawadi mbalimbali ikiwemo sabuni,,sukari,poda na kukabidhi jengo la kupumzikia wagonjwa ambalo limejengwa na mbunge huyo kwa gharama za sh.milioni tano kushoto kwake ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani,Dennis Ngaromba.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CUF) Amina Mwidau akimsalima mtoto mchanga kwenye hospitali ya wilaya ya Pangani wakati alipokuwa akiwatembelea wagonjwa kuwajulia hali kuwapa zawadi na kukabidhi jengo la kupumzikia hospitalini hapo lilolojengwa na mbunge huyo kwa gharama za shilingi milioni tano.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CUF) Amina Mwidau akigawa zawadi kwa mgonjwa Aisha Juma kwenye hospitali ya wilaya ya Pangani mara baada ya kuwatembelea wagonjwa jana kuwafariji na kukabidhi jengo la kupumziki wagonjwa hao kwenye hospitali hiyo ambalo limejengwa na mbunge huyo kwa gharama za kiasi cha shilingi milioni tano.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CUF) Amina Mwidau akiwa kwenye picha ya pamoja na wahuduma wa hospitali ya wilaya ya Pangani jana mara baada ya kuwatembelea wagonjwa hospitalini hapo kugawa zawadi na kukabidhi jengo la kupumzikia wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu ambalo limejengwa na mbunge huyo kwa gharama za kiasi cha shilingi milioni tano.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CUF) Amina Mwidau akimkabidhi Jengo la kumpumzikia wagonjwa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Dennis Ngaromba ambalo limejengwa na mbunge huyo kwa kiasi cha shilingi milioni tano litakaotumiwa na wagonjwa wanaokwenda hospitalini hapa kupata matibabu ,Picha na Mpiga Picha wetu,Pangani.

Bayport Financial Services kukopesha watu viwanja

May 23, 2015
Mkurugenzi wa Bayport Financial Services, John Mbaga, pichani, akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya viwanja katika mradi wa Vikuruti, Kibaha, mkoani Pwani. Uzinduzi huo ulifanyika Ijumaa ya Mei 22, katika Hoteli ya Serena na kuhudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwamo viongozi wa serikali. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.


Bayport yazindua huduma mpya ya mikopo ya viwanja kwa Watanzania wote


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaama

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, inayojihusisha na mikopo, imeanzisha huduma mpya ya kukopesha viwanja watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni za kawaida na wajasiriamali wa aina zote.

Kuanzishwa kwa huduma hiyo mpya kumetokana na taasisi hiyo kupania kuboresha maisha ya Watanzania, likiwamo kundi la wajasiriamali ambalo limeendelea kusahauliwa na kampuni nyingi kupewa mikopo.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, akizungumza katika uzinduzi huo, jijini Dar es Salaam.


Akizungumza mwishoni mwa wiki katika uzinduzi uliofanyika katika Hoteli ya Serena, Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport Financial Services, John Mbaga, alisema kuwa ni kusudio lao kutoa fursa ya watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni na wajasiriamali kupata nafasi ya kutimiza ndoto za kumiliki ardhi nchini Tanzania.

Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya Kibaha, Obed Katonga, kulia akijadiliana jambo na Meneja Uzalishaji wa Bayport Financial Services, Mashaka Mgeta kulia kwake na Mkuu wa Kanda ya Pwani, David Ndiega.


“Huduma yetu katika mradi wa Vikuruti, Kibaha, mkoani Pwani, fomu zake zinapatikana katika matawi yote ya Tanzania Bara, ambapo kwenye matawi yetu yote fomu hizo zitakuwapo, huku fomu hizo za kukopeshwa viwanja zikipatikana kwa wiki mbili, kuanzia Mei 22 hadi Juni 10 mwaka huu.


“Si lazima uwe mtumishi wa umma ili uwe na sifa ya kukopeshwa viwanja, ila hata wajasiriamali nao wamekumbukwa katika huduma hii nzuri kwa Watanzania wote, hivyo ni wakati wao sasa kuiunga mkono taasisi hii ili iweze kuwakomboa na kuwakwamua pia,’ alisema Mbaga.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paulo Makonda mwenye shati jeupe mbele akiwa katika uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya viwanja kutoka kwenye taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, jana jijini Dar es Salaam. Mwenye miwani ni Ruth Bura, mtumishi wa taasisi hiyo anayehusika na mambo ya Bima.


Akimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Kibaha katika uzinduzi huo, Afisa Mipango wa wilaya hiyo, Obed Katonge, alisema kwamba Bayport imebuni huduma nzuri inayofaa kuungwa mkono na Watanzania wote, hasa kwa kuingia kwenye sekta ya ardhi inayopanda thamani siku hadi siku duniani kote.
Wadau wanafuatilia uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport Financial Services, John Mbaga, akiendelea kufafanua katika uzinduzi wa mikopo ya viwanja, katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport Financial Services, John Mbaga, kushoto akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paulo Makonda. Uzinduzi huo ulihudhuriwa na watu mbalimbali, wakiwamo viongozi wa serikali.
Meneja Masoko wa Property International, Zora Moore, akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya mikopo ya viwanja, huku wao wakiwa ni kampuni iliyohusika na upimaji wa viwanja hivyo vya Vikuruti, Wilayani Kibaha, mkoani Pwani.
Mambo yamekwenda poa. Ndivyo wanavyoonekana kusema Mkurugenzi Mtendaji wa Bayport Financial Services, John Mbaga kulia na Meneja Masoko wake na Mawasiliano wa taasisi hiyo, Ngula Cheyo, katika uzinduzi wa mikopo ya viwanja. Uzinduzi huo ulifanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa Clouds Tv na Radio, Salehe Masoud, akibadilishana mawazo na mdau wa maendeleo wilayani Handeni, mkoani Tanga, Kambi Mbwana, mwenye shati jeupe na Mwandishi wa redio ya Times FM, Phillip Daudi.
Staff wa Bayport Financial Services wakijadiliana katika uzinduzi wa huduma yao.
Wadau wanafuatilia kwa makini kilichokuwa kinaendelea katika uzinduzi huo.
Baada ya kuzindua, wadau walikuwa wakibadilishana mawazo kama hivi.


“Serikali hususan kwenye wilaya yetu ya Kibaha tumepokea huduma hii kwa mikono miwili, ukizingatia kuwa wilaya yetu ni kati ya maeneo yanayokuwa kwa kasi, hivyo tunaamini tutaendelea kushirikiana na Bayport kwa ajili ya kuwapatia mwangaza wateja na wananchi wote kwa ujumla,” alisema Katonge.

Habari; napenda kuiwasilisha kwako stori ya uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya viwanja kutoka Bayport Financial Services, yenye maskani yake, jijini Dar es Salaam, Tanzania. Wageni mbalimbali walialikwa akiwamo Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Paulo Makonda. Uzinduzi huo ulifanyika jana ijumaa ya Mei 22 katika Hoteli ya Serena. Tunaomba sapoti yako ili Watanzania waone na waweze kuchangamkia fursa hii ya mikopo ya viwanja kutoka mradi wa vikuruti, uliopo Kibaha. Kambi Mbwana, +255 71205949
Naye Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kuanzishwa kwa huduma hiyo mpya ni njia ya kunapanua wigo wao na shabaha ya kuwafaidisha wateja wao na Watanzania wote kwa huduma na bidhaa zilizothibitishwa kwa ubora zaidi. “Bayport ilikaa na kufanya tafiti kadhaa zenye nia ya kujenga jamii na kuinua uchumi wa Watanzania wote, hivyo tukaona ipo haja ya kufungua ukurasa huu wa kukopesha viwanja, huku wateja wetu wakitakiwa kulipa kila mwezi katika vipindi vya miezi 24, ambapo kiwanja cha chini kabisa kinapatikana kwa Sh 1,700,000 na nzuri zaidi wateja wetu wanaweza kuona huduma nyingine nzuri za mikopo kwa kupitia tovuti yetu ya www.kopabayport.co.tz ,” alisema Cheyo.


Naye Meneja Bidhaa wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, alisema makato ya kiwanja chenye thamani ya Sh 1,400,000 kwa mjasiriamali ni 105,181.55, wakati mtumishi wa umma akilazimika kukatwa Sh 73,684.49, huku akiongeza kuwa mtu anaweza kupata kiwanja kwa malipo ya fedha taslimu. “Naomba Watanzania wajitokeze kwa wingi kukopeshwa viwanja hivi ili watimize ndoto zao za ujenzi wa nyumba, maana Bayport imekuja kwa ajili ya kuboresha maisha ya Watanzania wote, maana tangu sasa kila mtu anaweza kuwa baba au mama mwenye nyumba,” alisema Cheyo.


Mbali na huduma ya mkopo wa viwanja, Bayport pia inatoa mikopo mbalimbali ya bidhaa, mikopo ya fedha taslimu, bima ya elimu kwa uwapendao, huku mikopo yote hiyo ikiweza kupatikana kwa njia ya mtadao wa www.kopabayport.co.tz.
Click here to Reply, Reply to all, or Forward 6.07 GB (40%) of 15 GB used Manage Terms - Privacy Last account activity: 1 hour ago Details 22 more Kambi Mbwana's profile photo Kambi Mbwana Recent photos View photo in message View photo in message View photo in message Show details Compose: New Message MinimizePop-outClose To
NEED FOR INCLUSIVE QUALITY EDUCATION FOR ALL DOMINATES WORLD EDUCATION FORUM

NEED FOR INCLUSIVE QUALITY EDUCATION FOR ALL DOMINATES WORLD EDUCATION FORUM

May 23, 2015
WordEduForum-01-L
Opening of World Education Forum 2015, Seoul. UN Secretary-General Ban Ki-moon centre, at the opening of the World Education Forum 2015, in Seoul. He is flanked by Hwang Woo-yea (left), Deputy Prime Minister and Minister of Education of the Republic of Korea; and Irina Bokova, Director-General of the UN Educational, Scientific and Cultural Organization (UNESCO). 19 May 2015. Seoul, Republic of Korea. (UN Photo/Evan Schneider).
Tanzania’s Minister for Education and Vocational Training (MoEVT), Honourable Dr. Jumanne Shukuru Kawambwa with a delegation of four most senior officials from Tanzania Mainland and Zanzibar and a representative from the Civil Society are attending the Third World Education Forum (WEF) from 19-22 May 2015 in Incheon, Republic of Korea. The 2015 WEF is the third after the Jomtien WEF of 1990 and the Dakar WEF of 2000. The 2015 forum takes stock of achievements and challenges since the Dakar WEF and deliberates on the education agenda for the next fifteen years (2015-2030).
Tanzania was represented by a high profile delegation that consisted of two the Permanent Secretaries (from the Ministry of Education and Vocational Training and from the Prime Minister’s Office-Regional Administration and Local Governments), the Commissioner for Education from MoEVT as well as the Deputy Principal Secretary from MoEVT Zanzibar. The Civil Society is represented by HakiElimu which is a member organization of the Tanzania Education Network (TEN/MET).
UNESCO is taking the lead in coordinating WEF with the collaboration of UNDP, UNHCR, UNFPA, UNICEF, UN Women and the World Bank (WB). The opening ceremony was attended by a number of high profile key speakers including Ms. Irina Bokova the Director General of UNESCO, representatives from the Government of the Republic of Korea and Mr Ban Ki-moon, the United Nations Secretary General, to mention but a few.
The 2015 WEF seeks to take stock of achievements and shortfalls in the implementation of the Millennium Development Goals since the year 2000. The forum will also agree on a joint position for the education goal and targets in the post millennium development period (post 2015 development agenda). The agreements from the forum will be adopted by UN Member States at a Summit in September 2015;
The forum will further agree on a framework to support the implementation of the future education goal which focuses on equitable and inclusive quality education and lifelong learning for all by 2030.
UNESCO Dar es Salaam office, in collaboration with UNICEF, the WB and DFID are pleased to support the successful participation of the United Republic of Tanzania to the 2015 World education Forum