INDIA NA ZANZIBAR ZATILIANA SAINI YA KUANZISHWA KWA OFISI YA KUTANGAZA UTALII WA ZANZIBAR NCHINI INDIA

INDIA NA ZANZIBAR ZATILIANA SAINI YA KUANZISHWA KWA OFISI YA KUTANGAZA UTALII WA ZANZIBAR NCHINI INDIA

February 17, 2015
Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JIHIL ENTERPRISES ya India Nd. Jilesh H. Babla wakitiliana saini mkataba wa makubaliano ya kuanzishwa kwa ofisi ya uwakala wa Utangazaji Utalii wa Zanzibar Nchini India. (Picha na Makame Mshenga Maelezo-Zanzibar) BAR2 
Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JIHIL ENTERPRISES ya India Nd. Jilesh H. Babla wakikabidhiana mkataba wa makubaliano ya kuanzishwa kwa ofisi ya uwakala wa Utangazaji Utalii wa Zanzibar Nchini India baada ya kumaliza kusaini. (Picha na Makame Mshenga Maelezo-Zanzibar)
BAR3 
Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Nd. Saleh Ramadhan Ferouz akijibu maswali ya waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa tukio hilo. (Picha na Makame Mshenga Maelezo-Zanzibar)
BAR4 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar na Wa 3 kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JIHIL ENTERPRISES ya India Nd. Jilesh H. Babla na viongozi wengine kutoka Wizara ya Habari pamoja na Kamisheni ya Utalii Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja.
(Picha na Makame Mshenga Maelezo-Zanzibar)
……………………………………………………………………………….
Na Abdulla Ali Maelezo-Zanzibar
Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar imetia saini mkataba wa makubaliano ya kuanzishwa kwa ofisi ya uwakala wa Utangazaji Utalii wa Zanzibar Nchini India.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Nd. Ali Mwinyikai wakati wa kutia saini Mkataba huo katika ukumbi wa Wizara hiyo iliyopo Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Mkataba huo umetiwa saini tarehe 17/02/2015 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Nd. Ali Mwinyikai na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JIHIL ENTERPRISES ya India Nd. Jilesh H. Babla.
Katibu huyo amesema kuwa uanzishwaji wa ofisi ya utalii nchini India haukuja kwa bahati mbaya ila ni utekelezaji wa ilani na malengo yaliyopangwa na kutekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyopo madarakani kwa upande wa sekta ya Utalii kwa lengo la kuitangaza zaidi Zanzibar kiutalii.
Amesema ofisi hizo zitafanya kazi kama mabalozi wa kuutangaza Utalii wa nchi zao kwa kuwapatia habari watalii wote ambao wana nia ya kuzitembelea nchi husika pamoja na kutoa ushawishi mkubwa utakaowafanya wananchi wa nchi hizo kuwa na maamuzi sahihi ya kuzitembelea nchi hizo.
Aidha Katibu huyo amesema kuwepo kwa ofisi za Utalii nchini India itasaidia kujenga uhusiano mzuri na wa kudumu baina ya Zanzibar na wadau mbalimbali wa Utalii walioko nchini India jambo ambalo linakosekana katika masoko yaliyopo hivi sasa ispokua soko la Itali.
“Tuna kila sababu za Zanzibar nayo kutumia mfumo huu wa utangazaji wa Utalii kwani unaweza kuleta tija kubwa kwa haraka ukilinganisha na mifumo mengine ya utangazaji”, ameeleza Katibu Mwinyikai.
Amesema mpango huo umelenga kuimilikisha Sekta ya Utalii kwa wanachi wote wa Zanzibar ili kuhakikisha kuwa uwepo wa sekta hiyo unawafaidisha wananchi wa Zanzibar Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni.
Ametanabahisha kuwa kupanuka kwa wigo wa masoko ya Utalii kutaongeza kazi ya utekelezaji wa dhana ya Utalii na kuondokana na utegemezi wa soko la Ulaya ambalo linatishia uhakika wa kuwepo kwake kutokana na athari za Kiuchumi na Kifedha zinazojitokeza siku hadi siku.
Nd. Mwinyikai amefahamisha kuwa kutokana na hali hiyo Serikali ya Zanzibar imeamua kuongeza nguvu na kubadilisha mikakati ya utafutaji wa masoko mengine ikiwa ni pamoja na yale yanayochipukia yakiwemo ya Nchi za China, India, Urusi na Uturuki.
Nae mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Jihil Enterprises ya India ambae pia ni mzaliwa wa Zanzibar anaeishi Mumbai India Nd. Jilesh H. Babla amesema ameamua kuwa wakala wa Utalii wa Zanzibar Nchini India kwa lengo la kuitangaza Zanzibar kiutalii kwani Zanzibar ina vivutio vingi vya Kiutalii zikiwemo Fukwe na Mandhari mazuri ya Kisiwa hicho pamoja na sehemu za kihistoria.
Amesema ameamua maamuzi ya kizalendo kuwa Wakala wa Zanzibar Nchini India kwani hadi sasa hakuna wazalendo wanaoishi nje ya Nchi waliyojitikeza kufanya kazi hiyo pamoja na kuvitaka vyombo vya habari Zanzibar kufikisha ujumbe uliyo sahihi kwa wananchi juu ya Utalii wa Zanzibar ili kukuza Utalii wa nchi na hatimae kupelekea kukua kwa uchumi wa nchini.
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dr. Ahmada H. Khatib amesema wazo la kuwa na Ofisi ya Utalii Nchini India lilitokana na matokeo ya ziara rasmi ya Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliyoifanya Nchini China na India tarehe 27/05/2013 hadi 02/06/2013 ambayo ilijumuisha Mawaziri mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema pamoja na kuwa takwimu za idadi ya watalii wanaotembelea Zanzibar bado zinakumbana na changamoto za kutokuwa sahihi hata hivyo idadi ya sasa inaonyesha kuwa India hutoa watalii zaidi ya 98,000 kwa kila mwaka hivyo ipo haja ya kuwepo kwa wakala wa Utalii wa Zanzibar Nchini humo.
Amefahamisha kuwa makisio ya jumla ya kuendesha Ofisi hiyo Mjini Mumbai, India inakadiriwa kufikia zaidi ya Dola 100,000 za kimarekani kwa Mwaka ambapo Dola zipatazo 27,000 ni za kuendeshea Ofisi hiyo kila mwezi.

MAMA KIKWETE AWATAKA WAKAZI WA MKOA WA LINDI KUIPIGIA KURA YA NDIYO KATIBA PENDEKEZWA

February 17, 2015

Mama Salma Kikwete
Na Anna Nkinda – aliyekuwa Lindi

 Wananchi wa mkoa wa Lindi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuipigia kura ya ndiyo katiba inayopendekezwa kwani ni bora na imegusa maeneo yote kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania.

Rai hiyo imetolewa na  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete wakati akiongea na wananchi waliohudhuria sherehe ya kushangilia ushindi wa uchaguzi wa Serikali za mitaa katika mtaa wa Ruaha kata ya Mingoyo wilayani humo.

Katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana wananchi wa mtaa wa Ruaha waliwachagua Mwenyekiti na wajumbe wote watano kutoka Chama Cha Mapinduzi.

Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema katiba inayopendekezwa imeangalia maeneo yote yanayomgusa binadamu ikiwa ni pamoja na haki za wanawake na watoto, watu wenye mahitaji maalum wakiwemo walemavu na wazee.

“Katiba iliyopo sasa ilitungwa na baadhi ya watu waliokuwa madarakani kwa wakati ule na haikuwahusisha wananchi, lakini hii inayopendekezwa  wananchi wameshiriki kuitunga kwa kutoa maoni yao”, alisema Mama Kikwete.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mwantumu Mahiza aliwahimiza wananchi hao kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili wasipoteze haki yao ya msingi ya  kupiga kura.

Mahiza alisema kama kuna watu waliojiandikisha katika miaka ya nyuma wabebe vitambulisho vyao  ili viweze kunukuliwa na kwa wale wenye umri wa kuanzia miaka 18 wakajiandikishe na walio na umri wa chini ya hapo wasijiandikishe.

Aliwaasa wananchi hao  kutokubali  wageni waliokaa katika maeneo yao  kwa kipindi cha chini ya miezi sita kujiandikisha.

Akisoma taarifa ya CCM tawi la Ruaha Mohamedi Ngashona ambaye ni mjumbe alisema viongozi hao wamejipanga kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa mtaa huo ambazo ni uharakishaji wa ujenzi wa zahanati, ukarabati wa vyumba vya madarasa na ujenzi wa nyumba za walimu.

Kuwatambua kaya maskini na wazee kwa kuwapatia huduma muhimu, uimarishaji wa barabara ya kutoka Mnazimmoja hadi Ruaha na utekelezaji wa sera ya umeme vijijini hasa vilivyopitiwa na mradi wa bomba la gesi.

Katika mkutano huo jumla ya wanachama 43  walijiunga na chama hiyo kati yao wanne walitoka Chama cha Wananchi CUF .

Makamu wa Rais akagua mzani wa Kisasa wa Vigwaza na kufungua barabara ya Msoga - Msolwa km 10

February 17, 2015

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli kushoto akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal kuhusu Mzani wa kisasa wa Vigwaza uliopo Mkoani Pwani ambao umekamilika kwa asilimia 99.8.
Mzani wa Kisasa wa Vigwaza kama unavyoonekana. Mzani huu utapima magari kwa haraka zaidi kwa muda wa sekunde 30 kwa kila gari tofauti na mizani ya sasa inayotumia dakika moja na nusu mpaka mbili.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akihutubia wananchi katika Mzani wa Vigwaza mara baada ya kuukagua.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli pamoja na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Msoga-Msolwa km 10 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akizungumza mara baada ya kutoa pole kwa wananchi wa kijiji cha Msoga, Chalinze mkoani Pwani walioathirika na kimbunga kikali kilichosababisha kubomoka kwa nyumba zaidi ya 40 katika kijiji hicho pekee.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akicheza ngoma pamoja na kikundi cha ngoma cha Msoga kusherehekea ufunguzi wa barabara ya Msoga-Msolwa yenye urefu wa km 10. Barabara hiyo itapunguza msongamano wa magari katika eneo la Chalinze.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na watumishi wa TANROADS mara baada ya kukagua Mzani wa Vigwaza.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli kulia akisalimiana na Waziri wa Elimu ambaye pia ni Mbunge wa Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa kabla ya ukaguzi wa Mzani wa Vigwaza.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli wakielekea kwenda kumpokea Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal katika eneo la mzani wa Vigwaza mkoani Pwani. Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini GCU-Wizara ya Ujenzi
UONGOZI OFISI YA RAIS IKULU NA UTAWALA BORA

UONGOZI OFISI YA RAIS IKULU NA UTAWALA BORA

February 17, 2015

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa  Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora katika mkutano wa siku moja uliozungumzia utekelezaji mpango kazi wa Wizara ya hiyo kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,[Picha na Ikulu.] dkt2 
Uongozi wa  Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora wakiwa katika mkutano wa siku moja uliozungumzia utekelezaji mpango kazi wa Wizara ya hiyo kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.] dkt3 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa  Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora katika mkutano wa siku moja uliozungumzia utekelezaji mpango kazi wa Wizara ya hiyo kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,[Picha na Ikulu.]
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini   alipokuwa akitoa Taarifa ya Utekelezaji wa mpango kazi wa Wizara ya hiyo kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 katika kikao kilichofanyika leo asubuhi ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.) dkt5 
Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya  Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora wakimsikiliza Waziri  Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini   alipokuwa akitoa Taarifa ya Utekelezaji wa mpango kazi wa Wizara kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 katika mkutano uliofanyika leo asubuhi ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar mbele ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.) dkt6 
Katibu Mkuu Wizara ya Ncho Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Salum Maulid Salum (kushoto) na watendaji wengine wakifuatilia kwa makini Taarifa ya Utekelezaji wa mpango kazi wa Wizara kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 iliyotolewa na Waziri  Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini (hayupo pichani) katika mkutano uliofanyika leo asubuhi chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.] dkt7 
Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya  Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora wakimsikiliza Waziri  Dk.Mwinyihaji Makame Mwadini   alipokuwa akitoa Taarifa ya Utekelezaji wa mpango kazi wa Wizara kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 katika mkutano uliofanyika leo asubuhi ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar mbele ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.)

Mengi na kampuni ya A to Z ya jijini Arusha wampiga tafu Lowassa jimboni kwake,wachangia shule iliyoungua

February 17, 2015
 
Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule sekondari ya wavulana ya Engutoto wilayani Monduli wakati alipotembelea leo.Lowassa ambaye alirejelea kauli yake ya kwamba yeye si tajiri bali ni tajiri wa marafiki, alichangia shilingi milioni tatu kwa ajili ya sare za shule kwa wanafunzi ambao nguo zao ziliteketea.Aidha mwenyekiti mtendaji wa makampuni IPP amechangia shilingi milioni 25 kwa ajili ya vitanda.
 
Mmiliki wa kiwanda kikubwa cha A to Z cha Arusha,Anoji Shah (aliesimama) akiwaeleza wanafunzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Engutoto wilayani Monduli umuhimu wa elimu na pia kutangaza msaada wa enzi wa mabweni yote mawili yaliyoteketezwa kwa moto wiki mbili zilizopita.
 
Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule sekondari ya wavulana ya Engutoto wilayani Monduli.