TAIFA STARS MABORESHO YAREJEA DAR

December 06, 2014

Kikosi cha Taifa Stars Maboresho kinarejea leo Dar es Salaam kutoka Bulyanhulu mkoani Shinyanga ambapo kiliweka kambi kwa ajili ya mechi ya kimataifa dhidi ya Burundi itakayochezwa Desemba 9 mwaka huu.

Timu hiyo ambayo leo asubuhi imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ndege ya Fastjet saa 12.30 jioni na kwenda moja kwa moja kambini hoteli ya Tansoma.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kesho (Desemba 7 mwaka huu) itafanya mazoezi asubuhi na jioni kwenye viwanja vya Gymkhana wakati keshokutwa (Desemba 8 mwaka huu) itafanya mazoezi jioni kwenye Uwanja wa Taifa.

Nayo timu ya Taifa ya Burundi inatua nchini keshokutwa (Desemba 8 mwaka huu) saa 10 jioni kwa ndege ya Kenya Airways. Kikosi hicho kitafikia hoteli ya Tiffany Diamond kitakwenda moja kwa moja Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo kitafanya mazoezi kuanzia saa 11 jioni.

Kiingilio cha mechi kati ya Tanzania na Burundi itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni kitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya raungi ya chungwa, bluu na kijani wakati VIP B na C ni sh. 5,000 tu.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

WEMA SEPETU, DIAMOND WATARUDIANA NA KUFUNGA NDOA!

December 06, 2014
! Mtabiri maarufu Bongo, Maalim Hassan Yahya ambaye ni mrithi wa kazi za marehemu Shehe Yahya amesema kuwa, penzi la mastaa wa Kibongo,Wema Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond’ bado halijafika mwisho, watarudiana na kufunga ndoa. Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Akizungumzia penzi la wawili hao ambao siku chache zilizopita wameripotiwa kumwagana alisema, hali hiyo ni ya mpito tu haimaanishi kuwa hiyo ndiyo tamati ya mapenzi yao, sababu nyota zao zinategemeana japo ya Wema ina nguvu kubwa kuibeba ya Diamond.Staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu. “Msifikiri kwamba penzi lao ndiyo limefika mwisho, hakuna kitu kama hicho ni mara ngapi wameachana na kurudiana hata hili la sasa natabiri watarudiana,” alisema Malim.

MBOWE:TUTAZUIA UCHAGUZI WA MITAA MAHAKAMANI IKIWA................

December 06, 2014


Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kama hali ya kuwaengua wagombea wa chama hicho katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa itaendelea kama ilivyo sasa, basi wataupinga uchaguzi huo mahakamani.
Mbowe alisema hayo jana katika mkutano wa hadhara wa operesheni mshikemshike mzizima uliofanyika Vijibweni Kigamboni.
“Tangu kampeni zianze kumekuwa na tabia ya kuengua wagombea wetu kiholela. Tumeshaweka angalizo mahakamani na kama hali ikiendelea hivyo tutaupinga uchaguzi mahakamani.”
Alisema baada ya kuibuka kwa tabia ya wagombea kuenguliwa aliwasiliana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimsihi alitizame kwa kina suala hilo kwa sababu wagombea walienguliwa kimakosa.
“Alisema atalifanyia kazi lakini naona bado hali hiyo inaendelea na alisema atazungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuhusu jambo hili.
Nilipowasiliana naye mara ya pili alisema kama tunataka ushindi uchaguzi uwe wa haki. Kuona hivyo tumekwenda kutoa angalizo mahakamani,” alisema.
Aliongeza, “Tukutane katika uchaguzi na tuone nani ni bingwa kati ya CCM na Ukawa baada ya kutumia njia za mkato kama wao wanavyofanya.
Hata sisi hatutaki ushindi wa dezo ila wakitumia dola kutuyumbisha kamwe hatutokubali maana polisi wamekuwa wakitumika kama mawakala wa uchaguzi. Hilo halitakubalika.”
Aliwataka wananchi kutokaa mbali na vituo vya kupigia kura mara baada ya kuwachagua viongozi wanaowataka huku akisisitiza, “Msikubali kura zikahesabiwe sehemu nyingine watazichakachua.
Hata katika sheria za Uchaguzi hakuna sehemu inayosema baada ya kupiga kura, mpigakura anatakiwa kukaa umbali wa mita 100 kutoka katika kituo cha kupiga kura. Tumeweka mawakala nchi nzima kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa.”
Alisema hakuna dhambi mbaya kama wananchi kushindwa kuleta mapinduzi ndani ya nchi yao, hasa nchi kama Tanzania ambayo ina kila aina ya umasikini.
CHANZO:CHADEMA BLOG

WAGANDA WAMSHANGAA ZARI KUMGANDA DIAMOND

December 06, 2014

Mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya Uganda vimemgeuka nyota wa vipindi vya runinga na Mwanamuziki Zari ‘The Boss Lady’ kwa madai kwamba amemganda mwanamuziki wa Tanzania Diamond Platnumz.
Gazeti la udaku la Red Pepper, mitandao ya ugvision.com, bigeye.ug na mingineyo, imedai kuwa nyota huyo amemganda mwanamuziki huyo tangu alipopata upenyo wa kurekodi naye singo jijini Dar es Salaam.
Mitandao hiyo ilimshambulia Zari kwa kumwambia kuwa kavuruga uhusiano baina ya Wema na mkali huyo wa video ya ‘Ntampata Wapi’, huku ikiponda picha ambayo Zari aliiweka mitandaoni ikimwonyesha akiwa na Diamond.
Mitandao hiyo imeponda kuwa Zari ana tabia ya kuwanadi wanaume anaotoka nao.
Wiki tatu zilizopita Zari amekuwa bega kwa bega na mwanamuziki Diamond, baada ya kutengeneza wimbo wa pamoja katika studio za Tuddy Thomas. Zari alionekana akipiga picha kadhaa na nyota huyo kabla ya kumsindikiza katika tuzo za CHOAMVA, Afrika Kusini na baadaye kurudi naye nchini.

Diamond ambaye alinyakua tuzo tatu za Channel O 2014, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla inayoandaliwa na Zari, ijulikanayo kama ‘Zari All White Ciroc Party’, itakayofanyika Desemba 18, mwaka huu.
NHIF Yanyakuwa Tuzo tatu za Ubunifu Hifadhi ya Jamii Barani Afrika

NHIF Yanyakuwa Tuzo tatu za Ubunifu Hifadhi ya Jamii Barani Afrika

December 06, 2014

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya Bw. Khamis Mdee akipokea tuzo  tuzo tatu za ubunifu
katika sekta ya hifadhi ya Jamii Barani Afrika zinazosimamiwa na
Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Duniani (ISSA) unnamed1 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya Bw. Khamis Mdee akiwa na maofisa wengine wa mfuko  huo wakiwa katika picha ya pamoja. unnamed5 
Mandhari ya jiji la Cassablanca Morocco
……………………………………………………………………………………………….
Mwandishi Maalum Casablanca, Morocco
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF umenyakua tuzo tatu za ubunifu katika sekta ya hifadhi ya Jamii Barani Afrika zinazosimamiwa na Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Duniani (ISSA).
Halfa ya kukabidhi tuzo hizo ilifanyika Jijini Casablanca nchini Morocco usiku wa tarehe 3 Desemba, 2014 katika hoteli ya Serana jijini Casablanca ambapo washiriki zaidi ya 360 kutoka taasisi 75 katika mataifa 45 ya Afrika zilihudhuria.
Tuzo ambazo NHIF ilikabidhiwa ni katika eneo la utoaji wa huduma zamatibabu za kibingwa maeneo magumu kufika, kazi ambayo mfuko  umefanyakwa kushirikiana na wataalamu wa hospitali za rufaa nchini. 
tuzonyingine ni katika eneo la TEHAMA katika utayarishaji madai na hudumaza matibabu kwa wanachama wastaafu.
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo wa Kanda ya Afrika ambacho piakilijadili mambo muhimu kuhusu sekta ya hifahi ya jamii na kutambuakazi za ubunifu uliongozwa na Waziri wa kazi Mheshimiwa GaudensiaKabaka pamoja na Viongozi waandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi naUdhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii nchini (SSRA) na baadhi ya Watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini.
Tangu kuanza kutolewa kwa ambazo hushindaniwa kila baada ya miakamitatu, NHIF imeng’ara mara zote.Mwaka 2008 ilipata tuzo ya cheti chaheshima cha ubunifu mjini Kigali kwa kuwashirikisha wadau wake katikautoaji wa elimu kwa makundi mbalimbali ngazi ya mkoa. Mwaka 2011ulikuwa mshindi wa kwanza wa jumla barani Afrika na mwaka huu umeibuka tena na ushindi huo muhimu unaoitangaza Tanzania kimataifa kupitia Bima ya Afya.

Mbali ya NHIF, Tanzania pia imengara kwa kuzoa jumla ya tuzo 6 mbapoMamlaka ya Udhibiti ya SSRA, Mfuko wa Pensheni wa PPF na Mfuko wa PSPSpia ilijizolea tuzo moja moja kwa kila mmoja hivyo kufanya Tanzaniakuwa na jumla ya tuzo 6 na kuifanya kuwa kinara katika ukanda wa nchiza Afrika mashariki na ya Kati.
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika nchi nne ilipata heshima ya pekeekwa kazi zao za ubunifu. Mifuko hiyo ni kutoka Cameroon yenyewe iliyonyakua tuzo 8, Gabon, Maurtania, wenyeji Morocco.
Washindi wa jumla wa kwa mwaka 2014 ni wenyeji Morocco na Jirani zaowa Mauritania ambao kwa pamoja wamepata tuzo ya jumla kwa kutoa huduma bora, kuongeza uwigo wa wanaonufaika na huduma za mifuko hiyo hasa wasio na uwezo, matumizi ya TEHAMA na huduma kwa wateja na ufanisi kwa ujumla.

MAONYESHO YA KIMATAIFA YA ELIMU KUANZA DISEMBA 17-21, 2014 JIJINI DAR

December 06, 2014

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Abdulimalik Mollel, akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani)
 
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
 
Kampuni ya Global Education Link (GEL) kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Wizara ya Elimu na Ufundi pamoja na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) wameandaa maonyesho ya kwanza ya kimataifa ya elimu (TIEE) yanayotarajiwa kufanyika Disemba 17 hadi  21 mwaka huu katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Global link Education, Abdulmalik Mollel, alisema lengo la maonyesho hayo ni kutambulisha wadau wa elimu kwa pamoja ili kuweza kutoa huduma ya pamoja kwa wananchi na kuwaelimisha juu ya mambo muhimu yaliyopo katika kila sekta.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Tred), Jacqueline Mneney, akizungumza jambo.
 
Alisema ushiriki wa asasi mbalimbali kwa kushirikiana na sekta binafsi utakuwa na chachu ya mabadiliko ya elimu kwa kupitia mpango wa matokeo makubwa sasa.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Jacqueline Mneney, alisema wakati umefika kwa Watanzania kujua umuhimu wa maonyesho ya Elimu maana yamekuja kutatua matatizo mbali mbali waliyokuwa wakiyapata wazazi pindi wanapokuwa wanawatafutia shule na vyuo watoto wao.
 
Aidha alisema maonyesho hayo yataleta manufaa makubwa na changamoto chanya hasa katika kuongeza ushindani katika sekta ya elimu ambayo itasaidia mpango wa matokeo makubwa sasa.
 
Maonesho hayo yanatarajiwa kupata washiriki zaidi ya 500 na wananchi mbalimbali zaidi ya 350,000 kutoka ndani na nje ya nchi.
 
Kauli mbiu ya maonesho hayo ni ‘KUWEKA JITIHADA ZA PAMOJA KATIKA KUBORESHA MFUMO WA ELIMU TANZANIA NI NJIA THABITI YA KULETA MAENDELEO ENDELEVU KATIKA TAIFA.’
 MAMA SALMA KIKWETE AFANYA KAMPENI KATIKA KATA ZA MTANDI NA MWENGE HUKO LINDI MJINI

MAMA SALMA KIKWETE AFANYA KAMPENI KATIKA KATA ZA MTANDI NA MWENGE HUKO LINDI MJINI

December 06, 2014


 Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, CCM, anayewakilisha Lindi Mjini, Mama Salma Kikwete akisalimiana na viongozi wa Kata ya Mtandi iliyoko Lindi Mjini wakati alipotembelea Kata hiyo kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni katika uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini kote tarehe 14.12.2014. unnamed1 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM anayewakilisha Lindi mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akionyesha ishara ya vidole viwili kuashiria kuunga mkono pendekezo la muundo wa serikali mbili nchini wakati alipozungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Kata ya Mtandi tarehe 5.12.2014. unnamed2 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM anayewakilisha wilaya ya Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Kata ya Mtandi katika mkutano uliofanyika katika Mtaa wa Maisara kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa nchini unaotarajiwa kufanyika tarehe 14.12.2014. unnamed5 
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM anayewakilisha wilaya ya Lindi Mjini na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Kata ya Mtandi katika mkutano uliofanyika katika Mtaa wa Maisara kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa nchini unaotarajiwa kufanyika tarehe 14.12.2014. unnamed6 
Mama Salma Kikwete, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi anayewakilisha Lindi Mjini akishiriki kucheza na baadaye kuwahutubia wananchi wa Kata ya Mwenge huko Lindi Mjini wakati akishiriki kuwapigia kampeni za uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini kote tarehe 14.12.2014. unnamed7 unnamed8 
Baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni kwenye Kata ya Mwenge huko Lindi Mjini Mama Salma Kikwete anaonekana akimbeba mtoto Juma Selemani ambaye naye alikuwa miongoni mwa watu waliohudhuria mkutano wa kampeni.
…………………………………………………..
Na Anna Nkinda – Lindi
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Lindi mjini wametakiwa kutokubali kurubuniwa kwa kitu chochote kile ili wawapigie kura wagombea wa vyama vya upinzani  bali  waungane kwa pamoja katika kampeni na kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo.
Mwito huo umetolewa jana na  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma Kikwete wakati akiwanadi kwa wananchi wagombea wa chama hicho wanaowania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa Wenyeviti na Wajumbe wa Serikali za Mitaa katika Kata ya Mwenge.
Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema lengo la chama chochote cha Siasa ni kushika Dola kuanzia ngazi ya mtaa  hadi Taifa hivyo  basi wanachama hao wasikubali kurubuniwa bali waendelee kukitetea na kukipigania Chama chao ili kipate  ushindi katika mitaa yote 117 ya Kata hiyo.
“Viongozi wanaogombea tena wamechaguliwa kutokana na kazi yao nzuri. Nanyi ambao kura zeu hazikutosha wakati wa mchakato wa kuchagua msilaumu, bali muwapiganie  wagombea wote na kuhakikisha wanashinda angalieni maslahi ya chama kwanza  mambo binafsi baadaye”, alisema Mama Kikwete.
Aidha Mama Kikwete aliwaomba wananchi wa wilaya hiyo kutumia maarifa na ujuzi waliopewa na Mwenyezi Mungu wa kutambua mema na mabaya na kutokubali kudanganywa na kundi la watu wachache ili waipoteze amani yao.
Mama Kikwete alisema, “Wenzenu wamepiga hatua kubwa za maendeleo  katika mikoa yao huku Lindi Mwenyezi Mungu katupa neema maendeleo yanakuja sasa. Wanakuja huku kuwadanganya ili mfanye vurugu na kurudisha maendeleo yenu nyumba, msifuate mkumbo na kuchezea  amani kwani vurugu zinarudisha nyuma maendeleo”.
Aliwasihi wananchi waliohudhuria mkutano huo kuhakikisha watoto wao wanaenda shule ili wapate viongozi wazuri wa baadaye ambao watawaletea maendeleo kwani bila ya kuwa na elimu ni vigumu kupata maendeleo.
MNEC huyo pia aliwashukuru wanaume waliowaruhusu wake zao kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na kuwapongeza wanawake kwa kutokukubali kubaki nyuma na kuomba kugombea nafasi hizo.
Mama Kikwete yupo wilayani humo kwa ajili ya shughuli za kichama ikiwa ni pamoja na kushiriki  kwenye kampeni na kuwanadi wagombea wa chama hicho wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji  utakaofanyika tarehe 14 mwezi huu.
MICHUANO YA WANAWAKE TAIFA CUP KUANZA DESEMBA 28

MICHUANO YA WANAWAKE TAIFA CUP KUANZA DESEMBA 28

December 06, 2014

Twiga+Stars
Michuano ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake ya Proin Women Taifa Cup inaanza rasmi Desemba 28 mwaka huu kwa mechi ya ufunguzi kati ya timu za mikoa ya Mara na Mwanza itakayochezwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kombaini za mpira wa miguu za mikoa yote ya Tanzania Bara zitashiriki mashindano hayo yatakayochezwa kwa raundi mbili mwanzoni, na baadaye hatua ya robo fainali hadi fainali.
Mashindano hayo yanayodhaminiwa na kampuni ya Proin Promotions Limited, kuanzia hatua ya robo fainali, mechi zote zitafanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja Biashara wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Peter Simon Shankunkuli aliishukuru kampuni ya Proin ambao ni watengenezaji, wazalishaji na wasambazaji wa filamu za kitanzania kwa kuwezesha mashindano hayo kufanyika kwa mara ya kwanza
Proin Promotions imekua ikivumbua vipaji mbalimbali vya uigizaji na sasa imeamua kujikita katika mpira wa miguu ili kuweza kuvumbua vipaji kwa wachezaji wa kike.
Shankunkuli alisema nafasi bado zipo kwa wadhamini watakaoguswa na mashindano hayo, kwa kuwasiliana na TFF au Proin Promotions Limited kwa maelezo zaidi.
Waziri Mwakyembe awapongeza fastJet Kwa Huduma Nzuri kwa Wateja.

Waziri Mwakyembe awapongeza fastJet Kwa Huduma Nzuri kwa Wateja.

December 06, 2014

vvvvv3 
Ofisa wa Mahusiano na Masoko wa kampuni ya ndege ya FastJet Lucy Mbogoro akitoa maelezo kwa ujumbe kwa Waziri wa Uchukuzi Harrison Mwakyembe na ujumbe wake wakati wa maadhimisho ya siku ya anga duniani kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bunge ya Miundombinu, Peter Serukamba.
vvvvv6
Wafanyakazi wa kampuni ya ndege ya Fast Jet wakiwa kwenye picha ya pamoja
vvvvvv2
Wafanyakazi wa kampuni ya FastJet wakipita mbele ya mgeni rasmi ambae ni Waziri wa Uchukuzi Mh.Harrison Mwakyembe wakati wa maadhimisho ya siku ya anga duniani
vvvvvv4
Waziri wa Uchukuzi Harrison Mwakyembe akizungumza na wafanyakzi wa kampuni ya ndege ya FastJet wakati wa maadhimisho ya siku ya anga duniani ambapo aliipongeza kampuni hiyo kwa kutoa huduma kwa bei rahisi kwa wasafiri pembeni yake ni Mwenyekiti wa Bunge ya Miundombinu, Peter Serukamba.
vvvvvv5
Meneja Biashara wa FastJet, Jean Uku akitoa maelekezo kwa Waziri wa Uchukuzi HarrisonMwakyembe kuhusiana na utendaji kazi wa kampuni hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya anga duniani pembeni ya Mwakyembe ni Mwenyekiti wa Bunge ya Miundombinu, Peter Serukamba.
vvvvvvvvvvv
Waziri wa Uchukuzi HarrisonMwakyembe akizungumza na wafanyakzi wa kampuni ya ndege ya FastJet wakati wa maadhimisho ya siku ya anga duniani ambapo aliipongeza kampuni hiyo kwa kutoa huduma kwa bei rahisi kwa wasafiri.
 Serikali kuendelea kunufaisha Vijana katika kutengeneza ajira

Serikali kuendelea kunufaisha Vijana katika kutengeneza ajira

December 06, 2014
JJJJJJ2 JJJJ3 JJJJJ1
Serikali imeahidi kuendelea kusaidia kuwajengea Vijana uwezo wa kujitambua na kufanya kazi kwa hari ikiwemo kujitolea.
Hayo yamebainishwa katika Hotuba ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana wakati wa hafla ya madhimisho ya Siku ya Kimataifa yakujitolea iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Akihutubi baadhi ya Vijana wanaofanya kazi za Kujitolea katika taasisi mbalimbali Kajugusi amesema vijana wanapaswa kufanya kazi za kujitolea ili kujenga uwezo wa utendaji kazi na kupata uzoefu utakaopelekea kuajirika kwa ulahisi.
“Jengeni tabia ya kujitolea kwa kuwa kutawajenga na kuwapa fursa kubwa ya kupata ajira zenye staha zitakazo kidhi matarajio yenu”
Aidha Mkurugenzi huyo alitoa rai kwa vijana kujunga tabia ya kujifunza na kutumia kwa manufaa yao na taifa kwa jumla wake
Kajugusi aliongeza kuwa Serikali ipo mbioni kuboresha mkakati wa Taifa wa kushirikisha Vijana katika shughuli za maendeleo hapa nchini ambapo vijana watapa fursa ya kushiriki moja kwa moja katika kutekeleza mipango ya maendeleo ya nchi yao.
Kwa upande wake Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Matifa (UNIC) Bibi. Stella Vuzo amesema kuwa kadri vijana wanavyofanya kazi za kujitolea ndipo wanapopata fursa ya kujijengea uwezo utakapoelekea waajirike katika sjira zenye staha
Aliongeza kuwaidi ya vijana asilimia 80 wanajitolea katika taasisi mbalimbali duniani kote, ambapo kati yao asilimia 30 ujitolea ndani ya nchi zao hivyo kusaidia kuongeza nguvu kazi katika shughuli za maendeleo.
Akisoma ujumbe mahususi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwa ajili ya maadhimisho hayo, Bibi. Vuzo alisema kuwa Katibu Mkuu huyo anawashukuru zaidi ya watu 6,300 wanaofanya kazi kwa kujitolea katika Umoja wa Mataifa na na 11,000 wanaojitolea kupitia Mtandao kwa kuweza kuwasidia zaidi ya mamilioni ya watu katika kufanya mabadiliko kwa kuwapa sauti katika maendeleo endelevu na jitihada za utunzaji wa amani duniani kote’Alisema Stella Vuzo.
Siku ya Kujitolea duniani uadhimishwa kila mwaka tarehe 5 Desemba duniani kote ambapo kwa Tanzania kitaifa maadhimisho haya yamefanyika jijini Dar es Salaam