PEREIRA: ASEMA ATAPAMBANA NA WALIOPANDIKIZWA KUPANGA SAFU KATIKA UCHAGUZI WA CCM.

PEREIRA: ASEMA ATAPAMBANA NA WALIOPANDIKIZWA KUPANGA SAFU KATIKA UCHAGUZI WA CCM.

June 07, 2017
unnamed
Katibu wa NEC,  Idara ya Organazesheni CCM Taifa, Nd. Pereira Ame Silima akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM  Mkoa wa Kusini Unguja, kichama, Ramadhan  Abdallah  Ali “ Kichupa”  mara baada ya kuwasili katika Ofisi za  Mkoa huo zilizopo Dunga  Wilaya ya Kati Unguja.
1
Katibu wa NEC,  Idara ya Organazesheni CCM Taifa, Nd. Pereira Ame Silima akitoa nasaha kwa viongozi wa CCM Mkoa na Wilaya za Kusini na Kati Kichama katika ziara ya kiongozi huyo visiwani Zanzibar.
2
Baadhi ya viongozi na Watendaji wa ngazi mbali mbali za Chama na jumuiya zake  Mkoa wa kusini na Wilaya zake kichama. ( PICHA NA AFISI KUU CCM ZANZIBAR).
…………………………
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka viongozi na watendaji wa zamani wa ngazi za matawi waliowania tena nafasi za uongozi katika uchaguzi unaoendelea hivi sasa ndani ya chama hicho kutoshiriki kwenye vikao vya kuchuja na kujadili fomu za wagombea wa nafasi za uongozi.
Tahadhari hiyo imetolewa na Katibu wa NEC, Idara ya Organazesheni CCM Taifa, Nd. Pereira Ame Silima katika mwendelezo wa ziara yake huko Mkoa wa Kusini kichama Unguja, alisema mtu aliyewania nafasi ya uongozi ndani ya chama hicho hana haki ya kujadili na kuchuja fomu za wagombea wenzake kwani kufanya hivyo ni kinyume na Katiba ya Chama hicho.
Alisisitiza kwamba katika zoezi hilo ni lazima kila kiongozi asimamie taratibu za uchaguzi ili kuepuka malalamiko yasiyokuwa ya lazima.
“ Kuna baadhi ya matawi kumetokea changamoto za baadhi ya wagombea kujadili na kupitisha fomu za wagombea wenzao jambo ambalo ni kinyume na taratibu za Kikatiba hivyo hatuwezi kuvumilia vitendo hivyo ni bora uchaguzi urejewe katika maeneo yaliyoripotiwa ukiukaji wa miongozo yetu”, alisema Nd. Pereira.
Nd. Silima alisema dhamira ya chama hicho ni kuhakikisha chaguzi zote zitakazofanyika ndani ya chama na jumuiya kuhakikisha wanapatikana viongozi bora waliopatikana kwa mujibu wa matakwa ya Kikatiba na sio watu binafsi.
Katibu huyo aliweka wazi msimamo wake kwamba atapambana  vikali na baadhi ya watu waliopandikizwa katika uchaguzi huo ili wapange safu na makundi ya viongozi wanaowataka wao kwa baadhi ya ngazi za uongozi .
Aidha  aliwasihi viongozi hao kumpa ushirikiano wakati wa utekelezaji wa majukumu ya kiutendaji hasa katika jukumu la kufanikisha uchaguzi unaoendelea na kuhakikisha unakamilika kwa kiwango kilichokusudiwa.
“  Lengo la ziara yangu ni kujitambulisha kwenu kwani toka nilipoteuliwa sijawahi kuja kwenu kubadilishana mawazo  pia naomba ushirikiano katika Idara yangu ya organazesheni ambayo jukumu lake la msingi ni kusimamia  shughuli zote za chaguzi za chama na dola pamoja na masuala ya takwimu za wanachama.”, alisema Silima.
Akiwasilisha  taarifa ya maendeleo ya uchaguzi  wa chama hicho kwa ngazi za Matawi, Kaimu Katibu wa Wilaya ya Kusini Kichama Unguja, Hafidh Hassan Mkadam  alieleza kuwa changamoto iliyojitokeza katika zoezi hilo ni baadhi ya Viongozi wa ngazi husika kufanya uteuzi bila ya kuzingatia kanuni ya uchaguzi na katiba ya CCM, hali iliyopelekea baadhi ya matawi kurejea zozezi hilo.
MARAIS WASTAAFU ALI HASSAN MWINYI NA JAKAYA KIKWETE WAONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA BALOZI SISCO MTIRO JIJINI DAR ES SALAAM

MARAIS WASTAAFU ALI HASSAN MWINYI NA JAKAYA KIKWETE WAONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA BALOZI SISCO MTIRO JIJINI DAR ES SALAAM

June 07, 2017
1
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mh. Dk. Jakaya Kikwete akiweka mchanga kaburini wakati aliposhiriki katika mazishi ya Marehemu Balozi Sisco Mtiro yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kisutu  leo mchana na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na wananchi Marehemu Balozi Mtiro alifariki Jumatatu iliyopita kwenye hospitali ya Agha Khan jijini Dar es salaam.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
2
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi akiweka mchanga kaburini wakati aliposhiriki katika mazishi ya Marehemu Balozi Sisco Mtiro yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kisutu  leo mchana na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na wananchi Marehemu Balozi Mtiro alifariki Jumatatu iliyopita kwenye hospitali ya Agha Khan jijini Dar es salaam.
3
Mtoto wa Marehemu Omari Sisco Mtiro akiweka mchanga kaburini wakati aliposhiriki katika mazishi ya Marehemu Balozi Sisco Mtiro yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kisutu  leo mchana na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na wananchi.
4
Waziri Mkuu mstaafu Mzee Salim Ahmed Salim akiweka mchanga kaburini wakati aliposhiriki katika mazishi ya Marehemu Balozi Sisco Mtiro yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kisutu  leo mchana na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na wananchi Marehemu Balozi Mtiro alifariki Jumatatu iliyopita kwenye hospitali ya Agha Khan jijini Dar es salaam.
5
Jaji Mkuu Mstaafu Othman Mohamed Chande akiweka mchanga kaburini wakati aliposhiriki katika mazishi ya Marehemu Balozi Sisco Mtiro yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kisutu  leo mchana na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na wananchi Marehemu Balozi Mtiro alifariki Jumatatu iliyopita kwenye hospitali ya Agha Khan jijini Dar es salaam.
6
Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange akiweka mchanga kaburini wakati aliposhiriki katika mazishi ya Marehemu Balozi Sisco Mtiro yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kisutu  leo mchana na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na wananchi Marehemu Balozi Mtiro alifariki Jumatatu iliyopita kwenye hospitali ya Agha Khan jijini Dar es salaam.
7
Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Mstaafu Mzee Othman Rashid akiweka mchanga kaburini wakati aliposhiriki katika mazishi ya Marehemu Balozi Sisco Mtiro yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kisutu  leo mchana na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na wananchi Marehemu Balozi Mtiro alifariki Jumatatu iliyopita kwenye hospitali ya Agha Khan jijini Dar es salaam.
MASAUNI, IGP SIRRO WAWATAKA WANANCHI WILAYA YA KIBITI,RUFIJI KUFUNGUKA DHIDI YA VITENDO VYA UHALIFU NAWAHALIFU

MASAUNI, IGP SIRRO WAWATAKA WANANCHI WILAYA YA KIBITI,RUFIJI KUFUNGUKA DHIDI YA VITENDO VYA UHALIFU NAWAHALIFU

June 07, 2017
unnamed
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Bungu, wilayani Kibiti Mkoa wa Pwani, kuhusiana na masuala mbalimbali ya kupambana na wahalifu wilayani humo. Masauni ambaye aliambatana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro aliwataka wananchi hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuwasambaratisha wahalifu hao
1
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akipokea maoni ya wananchi wa Kijiji cha Jaribu Mpakani wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi wilayani humo. IGP ambaye aliambatana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) walizungumza na wazee, viongozi wa dini na watu maarufu kutoka Wilaya Rufiji na Kibiti kuweka mikakati ya kuimarisha zaidi ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
2
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wazee, viongozi wa dini na watu maarufu (hawapo pichani) kutoka Wilaya Rufiji na Kibiti kuhusu masuala mbalimbali na  kuweka mikakati ya kuimarisha zaidi ulinzi na usalama wa raia na mali zao. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, na kushoto ni Mkuu wa Wilaya Kibiti, Gulam Hussein. 
3
Wazee, viongozi wa dini na wa vyama vya siasa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati alipokuwa akizungumza na wananchi hao katika Ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Sekondari ya Kibiti, mkoani Pwani. Masauni na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro pamoja na wananchi hao waliweka mikakati ya kuimarisha zaidi ulinzi na usalama wa raia na mali zao kupitia maoni ya wajumbe waliohudhuria kikao hicho. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MAKALA : ASANTE OMOG,TUMEREJEA ALIKOTUTOA RC LIBOLO

June 07, 2017
Na Honorius Mpangala.

Mchezo wa soka ni mchezo ambao ili ufanikiwe hauhitaji jitihada za mtu mmoja ila jitihada za timu nzima kuanzia wachezaji,viongozi na benchi la ufundi. Klabu ya Simba imeweza kutembea katika tafsiri hiyo ya mafanikio ya soka yanahitaji ushirikiano wa timu nzima ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Ni kitu ambacho wapenzi na wadau wengi wa soka hawajafahamu dhana ya viraka vilivyopo katika mpira na mwisho vinaunda mpira mwenyewe. Viraka vya mpira ni sehemu ya kuelezea muunganiko unaohitajika katika watu ili kuleta mafanikio ya kitu kizima na pia utofauti wa rangi katika viraka huelezea timu mbili tofauti katika uwanja zinazocheza mchezo wenyewe.

Msimu wa 2016/2017 umekua bora sana kwa klabu ya simba na kufanya klabu imalize ligi nikiwa nafasi ya pili na kufanikiwa kubeba kombe la Azam Sport Federation Cup ( ASFC) msimu huu katika fainali Kali dhidi ya Mbao fc ya Mwanza.

Maandalizi ya klabu ya Simba waliyoyafanya ndiyo matunda ya walichokipata na kitawaletea mafanikio zaidi kama wakiendekea nacho kwa misimu mingine inayokuja.

Moja ya eneo ambalo klabu ya simba ilikua na changamoto na kujikuta wanashindwa kujishika vizuri ilikua katika eneo la benchi la ufundi,naweza kusema Benchi la simba limetibiwa ipasavyo.

Joseph Omog huyu mkameruni ni moja ya makocha wazuri na wenye kuamini katika nidhamu ya mchezaji mmoja na baadae nidhamu ya klabu kwa ujumla. Hakuna asiyefahamu mafanikio aliyoyapaya Omog akiwa na klabu Fc Leopard ya Congo Brazzaville alipoifikisha katika fainali ya kombe la shirikisho katika fainali waliyocheza dhidi ya Sc vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Omog alijitangaza katika mashindano ya afrika kama ilivyo kwa George Lwandamina wa yanga alivyojitangaza kupitia Mashindano ya ligi ya mabingwa. Kabla ya ujio wa Omog klabu ya simba ilikua klabu iliyokua ikicheza soka safi lisilo na faida kwao kutokana na upungufu wa nidhamu ya mchezo kupitia utimamu wa mwili na kuhimili mikiki mikiki ya ligi kwa dakika tisini za mchezo.

Omog ni kocha mkali anayejua kusimamia nidhamu,aliondoa hali ya utoto na kuweka mkazo wa kutafuta matokeo kwa faida ya klabu na sio mtu pekee.
Awali ilionekana kama utani wakati simba waenda kuweka kambi yao katika hostel za seminary pale bingwa Morogoro na kuweka mazingira ya kujidhatiti kwa klabu.

Kulikua na utofauti mkubwa kati ya uongozi wa benchi la ufundi chini ya Omog na ilivyokua kwa Jackson Mayanja ambako tuliona mikwaruzano ya chini chini kati yake na wachezaji,mfano kile kilichotokea kati ya Mayanja na Hassan Isihaka na Hamis Kiiza.

Zoezi la usajili walilolifanya kwa upande wa wachezaji walifanikiwa japo sio kwa asilimia kubwa na hilo ni kutokana na aina yetu ya utafutaji wa wachezaji wa kutoka nje ambapo walitumia majaribio.

Usajili wa Javier Belasa Bukungu ulipondwa sana na vyombo vya habari lakini amekuja kuwa thibtishia yeye ni mtu wa tofauti ndani ya uwanja.

Mafanikio makubwa kwa klabu ya simba ilikua pale walipojidhatiti kuivamia mtibwa sugar na kuwasajili Shiza Kichuya,Mzamiru Yassin na Mohammed Ibrahim ilikua usajili bora ambao umeleta matunda kwasababu katika mechi ya FA Mohammed Ibrahim ndo mfungaji wa bao la kuwapeleka fainali na Kichuya akafunga la kuipa Ubingwa wa FA achilia mbali magoli yake mawili ya mechi dhidi ya yanga ambayo yalimtengenezea jina zaidi na zaidi Kichuya.

Wakati ligi ikiendelea na kuona jinsi gani imekua ngumu simba walifanya makosa ambayo hawakuyajua awali kama wanakosea, Safu ya ushambuliaji Ikiongozwa na Laudit Mavugo ilikua inazidiwa magoli na viungo wakiongozwa mzamiru,Mo na Kichuya huku wakiwaacha Mavugo,Fred Blagnon na Ibrahim Ajib wakiwa na idadi ndogo ya magoli.

Simba walimwamini sana Mavugo kuliko Blagnon kwasababu tu mienendo ya uwanjani kati ya hawa wawili ila kiukweli mienendo ya Blagnon inafaida zaidi kuliko Mavugo hii iko wazi ila kinacho mfanya awe nyuma ya Mavugo ni chenga na visigino.

Mfumo mpya wa uhasibu kupunguza hati zenye mashaka katika halmashauri

June 07, 2017

Mkuu wa Kitengo cha Tehama na mawasiliano kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) bwana Desderi Wengaa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wakufunzi wa mfumo wa Uhasibu na utoaji taarifa za fedha.Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya wakufunzi wa mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kutoka mikoa ya Ruvuma, Lindi, Mtwara, Pwani, Tanga na Dar es salaam wakishiriki mafunzo hayo yaliyofunguliwa jana 
Mtoa mada wa mafunzo ya wakufunzi wa mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa njia ya kielektroniki kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI bwana Hamis Zikatimu akitoa mada wakati wa mafunzo hayo yanayofanyika mkoani Mtwara.
Mgeni rasmi Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara bwana Elias Nyamusami.(aliyeketi katikati akiwa katika picha ya pamoja na washiriki kutoka mkoa wa Tanga. Aliyeketi kushoto kwa Mgeni rasmi ni Mkuu wa Kitengo cha Tehama na mawasiliano kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) bwana Desderi Wengaa na kulia kwa Mgeni rasmi ni bwana Lucas Mrema ambaye ni mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI

Mgeni rasmi Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara bwana Elias Nyamusami.(aliyeketi katikati akiwa katika picha ya pamoja na washiriki kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3).

……………………..

Na Mathew Kwembe,Mtwara

Serikali imesema kuanza kutumika kwa mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ifikapo julai mosi, 2017, kutapunguza changamoto za halmashauri kupata hati zenye mashaka pindi zinapokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Mfumo huo utaiwezesha Serikali kupeleka rasilimali fedha moja kwa moja kwenye vituo vya afya kwa ngazi za halmashauri. Vituo vya kutolea huduma ambavyo vitapokea fedha hizo vinajumuisha Zahanati, Vituo vya Afya, na Hospitali za Wilaya. Zoezi hilo litaenda sambamba na inavyotekelezwa kwenye sekta ya elimu, Serikali za Vijiji na Ofisi za Kata.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bwana Alfred Luanda ameyasema hayo jana mjini Mtwara wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wakufunzi wa mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma kwa wahasibu kutoka halmashauri za mikoa sita ya Mtwara, Lindi, Ruvuma,  Tanga, Pwani na Dar es salaam.

MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 43, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO JUNI 07, 2017.

June 07, 2017
 Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Najma Giga akiongoza kikao cha 43 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 07, 2017.
 Naibu Waziri Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angeline Mabula akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 41 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 5, 2017.
 Naibu Waziri Wizara ya Fedha na Mipango Mhe.Dk Ashatu Kijaji akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 43 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 7, 2017.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini Dk Medard Kalemani akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 43 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 7, 2017.
  Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Prof Makame Mbarawa akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 43 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 7, 2017.
 Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe.Mwigulu Nchemba akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde  katika kikao cha 43 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 7, 2017.
  Mbunge wa Kigamboni (CCM) Mhe,Faustine Ndugulile  akiuliza swali katika kikao cha 43 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Juni 7, 2017.

OSCAR HAULE AIBUKA MSHINDI WA MILIONI 20 ZA BIKO LEO ASUBUHI

June 07, 2017
Balozi wa Biko Tanzania Kajala Masanja akionyesha namba ya ushindi wa Sh Milioni 20 aliyopata mkazi wa Arusha, Oscar Haule, katika droo iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam.

BENKI YA FINCA, DAR CITY F.C ZA SAINI MKATABA WA UDHAMINI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

June 07, 2017

Meneja Masoko wa Benki ya Finca, Nicholous John katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa udhamini  wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 5 na Klabu ya soka ya Dar City F.C. Kulia ni Rais wa Klabu hiyo Azimkhan Akber Azimkhan na Mwenyekiti wa Chama cha Soka  mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Almasi Kasongo.
BIMA YA JAMII KUTOKA VODACOM TANZANIA NA JUBILEE INSURANCE YAZINDULIWA MKOANI MWANZA

BIMA YA JAMII KUTOKA VODACOM TANZANIA NA JUBILEE INSURANCE YAZINDULIWA MKOANI MWANZA

June 07, 2017
#BMGHabari Kampuni ya mawasiliano nchini ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya bima ya Jubilee Insurance, kwa pamoja zimezindua huduma ya bima ya afya ili kuwawezesha wananchi kupata matibabu kwa gharama nafuu katika mkoa wa Mwanza. Huduma hiyo ambayo pia inapatikana kote nchini, inajulikana kama "Jamii, Ngao ya Afya" ambapo itawawezesha wateja wa Vodacom waliojiunga na hudumaya M-Pesa kupata matibabu kote nchini katika hospitali na vituo vya afya vilivyoidhinishwa kutoa huduma hiyo. Huduma ya matibabu ya Jamii huwawezesha watumiaji wa Vodacom kupata matibabu kwa gharama nafuu ambapo kwa mwanachama mmoja atalipa shilingi 7,000 kwa miezi mitatu, miezi sita atalipa shilingi 23,000 na kwa mwaka atalipa shilingi 44,000 ambapo atanufaika na huduma bora zama tibabu. Ni rahisi sana kujiunga na huduma ya bima ya afya ya "Jamii" kutoka Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Jubilee Unsurance, wasiliana na mtoa huduma kwa wateja kwa kupiga nambari 0743 888 111 ama 0755 88 55 15
Diwani wa Kata yaKirumba, Alex Ngusa, akizungumza jana kwa niaba ya Naibu Meya wa Jiji la Mwanza kwenye uzinduzi wa Bima ya Afya ya Jamii katika viwanja vya Igoma Jijini Mwanza.

Asma Athuman ambaye ni Meneja Mafunzo kutoka Vodacom mkoani Mwanza, akifafanua jambo kwenye uzinduzi wa Bima ya Afya ya Jamii katika viwanja vya Igoma Jijini Mwanza.

Asma Athuman ambaye ni Meneja Mafunzo kutoka Vodacom mkoani Mwanza, akifafanua jambo kwenye uzinduzi wa Bima ya Afya ya Jamii katika viwanja vya Igoma Jijini Mwanza.
 
Wakazi wa Jiji la Mwanza wakimsikiliza kwa makini, Asma Athuman ambaye ni Meneja Mafunzo kutoka Vodacom mkoani Mwanza, wakati akifafanua jambo kwenye uzinduzi wa Bima ya afya ya Jamii katika viwanja vya Igoma Jijini Mwanza.
 
Maureen Ndekana kutoka USAID akizungumzia huduma ya Jamii kwenye uzinduzi wa Bima ya Afya ya Jamii katika viwanja vya Igoma Jijini Mwanza.

Victoria Chale ambaye ni Meneja Mauzo na Usambazaji kutoka Vodacom Mwanza akiwahamasisha wakazi wa Jiji la Mwanza kujiunga na huduma ya afya ya Jamii-Ngao ya Afya ambapo wananchi wengi walihamasika kujiunga na huduma hiyo

  • Noel Mazoya ambayeni Meneja Masoko, huduma za kifedha kutoka Vodacom Tanzania, akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma ya afya ya Jamii-Ngao ya Afya kwenye viwanja wa Igoma Jijini Mwanza

Wakazi wa Jiji la Mwanza wakishuhudia uzinduzi wa huduma ya Jamii-Ngao ya Afya katika viunga vya Igoma Jijini Mwanza jana

Shukurani za pekee ziwaendee Vodacom Tanzania, Jubilee Insurance, ADGE Point kwa ufadhili wa watu wa Marekani USAID kwa kuwafikia wakazi wa mkoa wa Mwanza katika kunufaika na huduma ya Bima ya afya ya Jamii ambapo kwa mwezi mzima timu ya usajili wa huduma hiyo itazunguka maeneo mbalimbali ikiwemo minadani ili kuwasajili wananchi wote.
Pia ahsante kwa 102.5 Lake Fm Mwanza, kwa kujumuika kwenye kuhakikisha wananchi wote wa Mwanza wanaifahamu huduma hii ya "Jamii-Ngao ya Afya". Kwa msaada zaidi piga simu nambari 0743 888 111 ama 0755 88 55 15