AMIRI JESHI MKUURAIS DKT MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WANAFUNZI KUNDI LA 59/15 IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

November 26, 2016


  Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea baada ya kutunuku  kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 26, 201
 Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikagua gwaride la heshima linaloundwa na Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kabla hajawatunuku kamisheni katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 26, 201


 Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kwenye hati  ya  kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kabla hajawatunuku katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 26, 2016


Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea baada ya kutunuku  kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 26, 201,PICHA NA IKULU

JAMII YATAKIWA KUWAHESHIMU NA KUWASAIDIA WAZEE NCHINI

November 26, 2016
Mratibu wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya METDO Tanzania  Mathias Canal akimkabidhi Kaimu Mkuu wa Kituo cha Wazee KIILIMA Bi Gladness Lwiza baadhi ya mahitaji kwa ajili ya wazee waishio kituoni hapo.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya METDO Tanzania (Mining and Environmental Transformation for Development  Organization) Bw Ashraf Omary akimsikiliza kwa makini mzee aliyelala kutokana na homa kali inayomsumbua
Kushoto ni Dkt Peter Shija Mganga Mfawidhi kutoka zahanati ya Ibosa akisisitiza jambo kwa Afisa ustawi wa Jamii Wilaya ya Nyamagana ambaye pia ni katibu wa TAWSO Mwanza Bi Abigali Mhingo
 Meneja Mradi wa METDO Tanzania Bw Hussein Sungura akisaini kitabu cha wageni kwa niaba ya uongozi wa METDO Tanzania katika kituo cha Wazee KIILIMA Manispaa ya Bukoba, Mkoani Kagera
 Hiki ndicho Choo kinachotumiwa na wazee waishio kambi ya KIILIMA-Bukoba
Moja ya Mzee katika Kituo cha Wazee KIILIMA akiwa amelala kutokana na homa kali iliyokuwa inamsumbua
 Mahitaji yamepokelewa kwa furaha na wazee wote kupitia uongozi wao
Pichani katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu, Kushoto kwake ni Mathias Canal Mratibu wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya METDO Tanzania, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Kagera Ndg Charles Mafimbo, Kulia kwa Mkuu wa Mkoa ni Hussein Sungura Meneja Mradi METDO Tanzania na Mkurugenzi wa METDO Tanzania Ndg Ashrafu Omary
Mkurugenzi wa Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya METDO Tanzania (Mining and Environmental Transformation for Development  Organization) Bw Ashraf Omary akifanya usafi katika jiko la watumishi wa kituo cha wazee KIILIMA
 Mjadala ukiendelea baada ya kazi kumalizika Kijijini KIILIMA kambi ya wazee
Kaimu Mkuu wa Kituo cha Wazee KIILIMA Bi Gladness Lwiza akipanda mti kwa ajili ya kumbukumbu
Tafakuri pana kwa Mzee Wilson Ziraimanikabla ya kukabidhiwa mahitaji na uongozi wa METDO Tanzania
 Nyumba ya kulala wazee wa kituo cha KIILIMA kilichopo Kata ya Nyakato Mkoani Kagera
 Viongozi wkibadilishana mawazo mara baada ya kuzuru kituo cha Wazee KIILIMA
Kijana ni mzee ajaye na Mzee ni kijana aliyekuwa
Hili ndilo jiko linalotumiwa na viongozi wa kituo cha KIILIMA kilichopo nje kidogo ya Manispaa ya Bukoba
Katikati ni Dkt Peter Shija Mganga Mfawidhi kutoka zahanati ya Ibosa akipata maelezo ya awali kwa Moja ya mzee aishie kambini KIILIMA kabla ya kumfanyia vipimo
Mathias Canal Mratibu wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya METDO Tanzania akipanda mti wa matunda aina ya Mlimao kwa ajili ya kumbukumbu ya kuzuru kituo cha Wazee KIILIMA

RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI AONGOZA MAHAFALI YA CHUO KIKUU CHA KAMPALA JIJINI DAR ES SALAM

November 26, 2016
 Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akiwatunuku wahitimu wa kozi mbalimbali katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Kampala cha jijini Dar es Salaam kwenye sherehe za mahafali.
 Baadhi ya waadhiri wa chuo hicho wakiwa kwenye mahafali hayo.
 Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (kushoto) na mgeni rasmi katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Kampala cha jijini Dar es Salaam akiteta jambo na Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Muhammad Ndaula katika mahafali hayo yaliyofanyika jana.
 Baadhi  ya wahitimu wa ngazi ya digree kozi ya afya wakila kiapo cha kuhitimu fani hiyo.
 Sehemu ya wahitimu wakiwa katika mahafali hayo.
 Sehemu ya wahitimu wakiwa katika mahafali hayo.
 Sehemu ya wakufunzi na wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kampala wakiwa kwenye mahafali.

Mahafali yakiendelea


Msafara wa mahafali ukiongozwa na Rais msaafu wa Awamu ya Pili, Mwinyi mara baada ya sherehe za mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU) cha jijini Dar es Salaam.kumalizika.

Na Mwandishi Wetu

RAIS mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amewataka wahitimu wa vyuo vikuu nchini kuacha tabia ya kuchagua kazi za kufanya mara baada ya kuhitimu elimu yao. Mwinyi alisema tabia hiyo imepitwa cha wakati hasa katika dunia ya sasa yenye changamoto kubwa ya ajira.

Rais Mwinyi alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na wahitimu wa kozi mbalimbali kwenye sherehe za mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU) cha jijini Dar es Salaam.

Alisema kitendo cha baadhi ya wahitimu hasa wa vyuo vikuu kupendelea kuchagua kazi za kufanya kimekuwa kikiwapotezea muda na fursa anuai, hivyo kuwataka kuacha tabia hiyo ambayo kwa kipindi hiki imepitwa na wakati.

Alisema wahitimu hawana budi kuanza kufanya kazi zozote zinazojitokeza mbele yao na kutumia fursa hiyo kuelekea kwenye mafanikio kadri walivyojipangia katika 
maisha yao. 

"...Nawapongeza wahitimu kwa hatua hii, sasa mnaingia katika maisha mapya na ya vitendo msiende kuchagua kazi za kufanya, anza na kazi yoyote inayojitokeza mbele 
yako kisha uitumie kutimiza ndoto zako," alisema katika hotuba yake kwa wahitimu hao.

Aidha Rais huyo mstaafu aliwataka wahitimu hao kuwa wachapakazi, wabunifu na kutumia ipasavyo ujuzi na elimu waliopewa katika ngazi mbalimbali ili 
kuweza kuisaidia jamii na taifa kwa ujumla. 

Alisema kuwa Serikali ya Tanzania imejipanga kuhakikisha wanafunzi wote wenye sifa na vigezo vya kujiunga na chuo wanapata nafasi hiyo bila vikwazo kupitia 
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB). 

Akihimiza matumizi ya lugha ya Kiswahili hasa kufundisha programu katika vyuo vikuu, Mwinyi alivitaka vyuo vikuu kuanza kufundisha programu za lugha hiyo ili
kuchochea matumizi yake kama yanavyofanya mataifa mengine kwenye vyuo vyao iwemo China, Urusi, USA, Iran na mengineyo.

Alisema Afrika lazima iwe na lugha moja ya kuwaunganisha watu wake na lugha pekee inayozungumzwa na mataifa mengi ya Afrika ni Kiswahili hivyo kuna kila sababu ya kujivunia lugha hiyo na kuitumia ipasavyo. "...Naahidi katika mahafali yajayo nitatoa hotuba yangu kwa lugha ya Kiswahili na salamu zangu zote nitazitoa kwa kiswahili," alisema Mwinyi.

Awali akizungumza katika mahafali hayo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampala (KIU), Profesa Ndaula Muhammad alisema jumla ya wahitimu 1079 wamehitimu masomo yao katika ngazi ya Shahada, Stashahada na Asatashahada katika fani mbalimbali.

ATAKA MALENGO 17 YA SDGs KUFIKISHWA NGAZI ZA CHINI ZA UTEKELEZAJI

November 26, 2016
Mkurugenzi wa Mifumo Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Henry Katabwa ametaka Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) kuhusishwa kwenye michakato ya maendeleo ya serikali za mitaa, hasa kwenye programu zinazotekelezwa kwenye ngazi za chini kabisa ambapo ndiko wananchi wenye hali duni kimaendeleo wanapatikana. Kauli hiyo aliitoa wakati akifunga warsha ya malengo ya maendeleo endelevu kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango kutoka mikoa saba ya kanda ya ziwa. Alisema malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs) yamehusishwa kwenye mpango wa maendeleo wa miaka mitano hivyo ni vyema kuhakikisha hata katika ngazi za chini utekelezaji wa program unazingatia malengo hayo. “Kuna haja ya kuhakikisha kwamba, shabaha ya malengo haya inahusishwa kwenye michakato ya maendeleo ya serikali za mitaa na hasa kwenye miradi ya program zinazotekelezwa kwenye ngazi za chini kabisa, ambako ndiko wananchi wenye hali duni ya kimaendeleo wanapatikana” alisema 
Mwenyekiti wa warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango nchini ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi idara ya Mipango na Uratibu mkoa wa Mara, Eldom Anyosisye akitoa neno la ukaribisho wakati wa kufunga warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango nchini iliyomalizika mwishoni wa juma mjini Dodoma chini ya ufadhili wa Shirika UNDP.

Pia alisema serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na mradi wa uimarishaji wa wa sekta ya umma inaendelea kuboresha mfumo wa ukusanyaji takwimu ili uweze kukusanya takwimu katika ngazi zote za serikali za mitaa ili zitumike kuandaa mipango ya maendeleo. Akisoma maazimio kwa niaba ya washiriki wa warsha hiyo, Afisa Mipango wa wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, Innocent Maduhu alisema sheria ya Bajeti ya mwaka 2015 izingatiwe na kila mhusika atekeleze wajibu na majukumu yake. Pia yafanyike mapitio ya mgawanyo na matumizi ya fedha za mapato ya ndani kwa lengo la kupata uhalisia sambamba na kuweka mkazo katika kutafuta rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo. 
Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Anna Mwasha akizungumza jambo kabla ya mgeni rasmi kufunga warsha hiyo iliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.

Aidha wajumbe hao waliazimia kila sekta iwezeshwe vitendea kazi na rasilimali muhimu ili ziweze kutimiza majukumu yake pia mifumo ya upangaji mipango na utoaji taarifa ihuishwe ili iendane na Malengo ya Maendeleo Endelevu. Pia wametaka yafanyike mafunzo rejea ya mifumo kwa watumishi na kwa wakati na rasilimali katika sekta ya Kilimo ziongezwe kwa lengo la kuongeza na kuboresha uzalishaji na kupata malighafi kwa ajili ya viwanda. Sambamba na halmashauri zote kuboresha mifumo ya ukusanyaji mapato na kubuni vyanzo vipya pamoja na kudhibiti mapato na matumizi, uwepo mpango au mkakati maalumu wa kuendeleza Mikoa na Halmashauri zilizopo nyuma kimaendeleo. “Mbinu za uibuaji na upangaji wa miradi ya maendeleo kutoka ngazi ya chini ufanyike upya katika halmashauri zote” alisema Maduhu. 


Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mifumo Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Henry Katabwa akitoa hotuba ya kufunga warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango nchini iliyomalizika mwishoni wa juma mjini Dodoma chini ya ufadhili wa Shirika UNDP.
Afisa Mipango wa wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera, Innocent Maduhu akiwasilisha maazimio ya warsha ya SDGs yaliyoandaliwa na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango nchini mbele ya mgeni rasmi (hayupo)wakati wa hafla ya kufunga warsha ya siku tatu iliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
Meza kuu ikifuatilia kwa makini maazimo ya SDGs yaliyoazimiwa na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango nchini wakati wa hafla fupi ya kufunga warsha hiyo ya siku tatu iliyomalizika mwishoni mwa juma mjini Dodoma, kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi OR-TAMISEMI, Injinia Enock Nyanda, mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mifumo Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Henry Katabwa na Mkurugenzi wa Kupunguza Umaskini na Kuinua Uchumi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Anna Mwasha.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mifumo Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Henry Katabwa akizungumza na Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango nchini walioshiriki warsha ya siku tatu ya SDGs wakati wa hafla fupi ya kufunga warsha hiyo iliyomalizika mjini Dodoma mwishoni mwa juma.
Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Shomari Maknandi akiwasilisha mada kuhusu Ugatuzi wa madaraka (D by D) na utoaji wa huduma kwa wananchi kwenye warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango nchini iliyomalizika mwishoni wa juma mjini Dodoma chini ya ufadhili wa UNDP.
Afisa Mipango wa Halmashauri ya Kibondo mkoani Kigoma, Anganile Mwasongwe akiwasilisha maoni wakati wa hafla fupi ya kufunga warsha ya kufunga warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango nchini iliyomazika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki chini ya ufadhili wa Shirika la UNDP.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi Manispaa ya Bukoba, Richard Salu akichangia maoni wakati wa kuwasilisha maazimio ya SDGs kwa mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi ya kufunga warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango nchini iliyomazika mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyofadhiliwa na Shirika la UNDP.
Pichani juu na chini ni Maafisa Maendeleo ya Jamii na Mipango nchini walishiriki warsha ya siku tatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) iliyomalizika miwshoni mwa juma mjini Dodoma.

Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango ambao ndio waratibu wa warsha hiyo.
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Mifumo Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Henry Katabwa akiondoka katika ukumbi wa mikutano wa Hazina ndogo baada ya kufunga warsha hiyo
-- Zainul A. Mzige, Operation Manager, MO BLOG, www.modewjiblog.com +255714940992.