Unilever yaendelea kuwazawadia wanafunzi shule mbambali Dar

February 02, 2016
Mwanafunzi wa darasa la tano wa shule ya msingi Maarifa, Gongo la Mboto, jijini Dar es Salaam  Ester Lawrence akipokea fulana kutoka kwa Balozi wa Blue Band Neema Upendo shuleni hapo jana akiwa ni mmoja wa washindi wa shindano la Blue Band ‘Kula Tano’ linalowamasisha wanafunzi kutambua umuhimu wa kula vyakula vyenye virutubisho. Kushoto ni mwalimu wa michezo Edith Katundu.

SERIKALI ITAENDELEA KUWAFUNGIA MAGETI WATUMISHI

SERIKALI ITAENDELEA KUWAFUNGIA MAGETI WATUMISHI

February 02, 2016
Serikali haitokuwa tayari kuwaona watumishi wa umma wachache wakinufaika na kufaidi pesa za walipa kodi hususani wa kipatao cha chini na wale maskinini.
  IMG_0652

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla.

Hayo yamesema wilayani hapa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla alipokuwa akiwahutubia wananchi wa wilaya hiyo.
Dkt. Kigwangalla alisema serikali ya awamu ya tano inawataka watumishi wote nchini kufanya kazi za kuwahudumia wananchi na kuacha uzembe kwani awamu hii haiwezi kuwavumilia watumishi wa namna hiyo.
“Serikali haitowavumilia watumishi wazembe, hivyo tutaendelea kuwafungia mageti na kuwashughulikia wale wazembe, tunataka watumishi wa umma wafanye kazi ya kuwahudumia wananchi kwa ufanisi, mtumishi akizembea tutamtumbua majipu, akichelewa tunamfungia geti na akiiba tunafilisi pamoja na kumpeleka jela,hii ndiyo serikali ya hapa kazi tu,” alisema Dkt. Kigwangalla.
Aidha alisema serikali ya awamu ya tano inataka kero za wananchi zifanyiwe kazi na kutekeleza ahadi zote za ilani ya uchaguzi ya ccm zinatimizwa.
“Hatutomuonea mtu,lakini tutafanyia kazi pale penye matatizo,tunataka Tanzania mpya ya mwaka 2015 inakua,hatutaki hadithi wala ahadi,” alisema naibu waziri.
Hata hivyo aliwataka wazazi wote wenye watoto wenye umri wa kwenda shule kuwapeleka watoto wao kuanza masomo kwani elimu kwa sasa ni bure na hakuna michango yoyote.
“natoa wito kwa walimu wote wasitoze michango yeyote wala ushuru kwa wazazi wanaowapeleka kuwaandikisha watoto shule kwani shule zimepatiwa pesa za kuendeshea shule hizo,” alieleza Dkt. Kigwangalla.
Dkt. Kigwangwalla aliwakumbusha watumishi wa umma kujipanga na kama watagundulika ni majipu bali hawatosita kuwatumbua hadi kina kitoke,usaha na damu kutoka bila huruma.

MANISPAA YA ILEMELA YAWEKA MSIMAMO WAKE DHIDI YA WAFANYABIASHARA WA HOTEL NA NYUMBA ZA KULALA WAGENI.

February 02, 2016
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo John Wanga akitoa ufafanuzi kwa Wanahabari juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni.
Wafanyabiashara wa Hotel na Nyumba za Kulala Wageni katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, Wametakiwa kufanya biashara zao kwa mjibu wa kanuni na sheria za biashara zao ikiwemo kulipa ushuru na kodi mbalimbali kama ilivyoidhinishwa na Serikali.

Kauli hiyo imetolewa hii leo na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo John Wanga, katika Kikao cha Viongozi wa Manispaa ya Ilemela na Wafanyabiashara hao, juu ya Ufafanuzi wa Sheria ya Kodi ya Malazi, ambayo imeanza kukusanywa kwenye Hotel pamoja na nyumba zote za kulala wageni.

“Kama una wajibu wa kulipa kodi Majengo, leseni ya biashara, mabango, ushuru wa malazi, ushuru wa huduma na kodi nyingine zote zilizo kisheria, ni vyema ukalipa bila kushurutishwa. Kutokufanya hivyo utatufanya twende kwenye ule mkono mwingine ambao tusingependa sana kuutumia ambao ni kushurutishana”. Amesema Wanga.

Hata hivyo licha ya agizo hilo, Wafanyabiashara katika Manispaa hiyo wameiomba Serikali kuwapunguzia mzigo wa Kodi walionao kwa kuwa hivi sasa wanakabiriwa na mzigo mkubwa wa kodi pamoja na Ushuru jambo ambalo wamesema ni tofauti na ahadi ya kuondoa kero ya kodi mbalimbali aliyoitoa Mhe.Rais John Pombe Magufuli wakati wa Kampeni zake.

“Kodi zimekuwa nyingi sana kwa sisi wafanyabiashara wa Hotel na Guest Houses (nyumba za kulala wageni), kwa mfano kodi ya majengo, leseni ya biashara, ardhi, mabango na nyinginezo. Yaani nyumba moja inakuwa na kodi zaidi ya 11 sasa itafika sehemu tutashindwa kufanya biashara. Sisi tuko tayari kulipa kodi ya majengo, ardhi na leseni hivyo serikali iangalie namna ya kutusaidia”. Alisema Nuru Ramadhan ambae ni mmoja wa wamiliki wa nyumba ya kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela na kuungwa mkono na wenzake.

Hawa Waziri ambae ni Mwanasheria wa Manispaa ya Ilemela, amewasihi Wafanyabiashara hao kuwa tayari kulipa kodi zilizopo kisheria, ikiwemo Kodi ya Malazi huku wakiendelea kujenga hoja Serikalini ili Sheria hizo zifanyiwe marekebisho bungeni na hatimae kupunguzwa.

Awali Wafanyabiashara wa Hotel na Nyumba za Kulala Wageni, walikuwa wakilipa Kodi ya Malazi ambayo ni asilimia 20 ya mapato yanayotokana na malipo ya kila mteja, kabla ya kodi hiyo kusitishwa na Serikali ambapo hata hivyo imerejeshwa tena na Wafanyabiashara hao wanatakiwa kulipa kodi ya asilimia 10 ya mapato yanayotokana na mteja badala ya 20 kama ilivyokuwa awali.
Kikao juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni kikielendelea
Afisa biashara Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza akitoa ufafanuzi juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni
Hawa Waziri ambae ni Mwanasheria wa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza akitoa ufafanuzi kwa wanahabari juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni
Cyprian Oyier ambae ni mmoja wa wafanyabiashara wa hotel Manispaa ya Ilemela akiwasilisha hoja zake katika kikao juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni
Lemmy Muganyizi Mboyelwa ambae ni mmoja wa wamiliki wa nyumba ya kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela akiwasilisha hoja zake katika kikao juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni
Nuru Ramadhani ambae ni mmoja wa wamiliki wa nyumba ya kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela akiwasilisha hoja zake katika kikao juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni
Melikior Fundi Minsa ambae ni mmoja wa wamiliki wa nyumba ya kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela akiwasilisha hoja zake katika kikao juu ya tozo ya Kodi ya Malazi kwa wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni
Wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela wakiwa katika kikao cha ufafanuzi juu ya kuanza kutumika kwa kodi ya Malazi
Wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela wakiwa katika kikao cha ufafanuzi juu ya kuanza kutumika kwa kodi ya Malazi
Kushoto ni Stella Lwakatare ambae ni Afisa Biashara Mkuu katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza akifafanua jambo kwenye kikao cha Wafanyabiashara wa hotel na nyumba za kulala wageni katika Manispaa ya Ilemela juu ya kuanza kutumika kwa kodi ya Malazi.
Katikani ni Mkurugenzi wa Manispaa hiyo John Paul Wanga na Kulia ni Peter Revelian ambae ni Mwekahazina wa Manispaa ya Ilemela.
Watumishi wa idara mbalimbali katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo
LIGI KUU MZUNGUKO WA 17 KUENDELEA KESHO

LIGI KUU MZUNGUKO WA 17 KUENDELEA KESHO

February 02, 2016
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara mzunguko wa 17 unatarajiwa kuendelea kesho Jumatano kwa michezo sita kuchezwa katika viwanja mbalimbali, huku kila timu ikisaka pointi tatu muhimu kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Kesho Jumatano, Simba SC watakua wenyeji wa maafande wa Mgambo Shooting kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, JKT Ruvu watawakaribisha Mbeya City katika uwanja wa kumbukumu ya Karume Ilala, huku Mtibwa Sugar wakicheza dhidi ya Toto Africans katika uwanja wa Manungu – Turiani.
Jijini Mbeya, Tanzania Prisons watakua wenyeji wa vinara wa ligi hiyo Young Africans katika uwanja wa Sokoine, Wana kimanumanu African Sports watacheza dhidi ya Mwadui FC uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku wakata miwa wa Kagera Sugar wakiwakaribisha Majimaji FC katika uwanja wa Kamabarage mjini Shinyanga.
Alhamisi ligi hiyo itaendelea kwa kuchezwa mchezo mmoja tu, Wagosi wa Kaya Coastal Union watawakaribisha Ndanda FC katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Michezo ya viporo ya Azam FC imepangiwa ratiba, mchezo dhidi ya Tanzania Prisons utachezwa Februari 24 uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, huku mchezo dhidi ya Stand United ukichezwa Machi 16 katika uwanja wa Azam Complex.
MALINZI AMPONGEZA KIKWETE

MALINZI AMPONGEZA KIKWETE

February 02, 2016
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanznaia (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Rais wa awamu ya nne Jakaya Kikwete kwa kukubali uteuzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) na GAVI utakaomfanya kuwa bingwa wa chanjo na balozi wa mradi wa Africa United Duniani.

“Familia ya mpira wa miguu inajua umuhimu wa chanjo na hasa katika maendeleo ya vipaji na wanamichezo kwa ujumla na jinisi chanjo inavyoweza kuwapa watoto siyo tu fursa ya maendeleo bali pia haki ya kuishi” ilisema sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi.

Katika barua hiyo, Malinzi ameelezea furaha ya TFF kuona kiongozi wa Tanzania akiongoza mapambano ya kuokoa afya na uhai wa kizazi cha sasa na kijacho katika Afrika na dunia kwa ujumla.

“TFF itaunga mkono juhudi zako ili kufanikisha malengo yaliyowekwa na ushirika wa chanjo” ilimalizia barua hiyo ambayo nakala yake imetumwa kwa Rais wa Caf, Issa Hayatou.

fastjet yaongeza ndege ya tano

February 02, 2016




Dar es Salaam, Januari 28, 2016-Fastjet Tanzania imeongeza ndege nyingine aina ya Airbus A319 kwenye  idadi ya ndege zake nne  na hivyo kuliweka shirika hilo la ndege la gharama nafuu kuendelea na mipango yake ya kupanuka.

“Ndege za fastjet kwa hivi sasa ni nne na zote zinatumika  na ongezeko la ndege ya tano  ni jibu kwenye mikakati yetu ya  kupanuka pamoja na hitaji la kuongeza uwezo wa kubeba kwenye safari zetu za ndani na za kimataifa”, alisema  Meneja Mkuu wa fastjet Tanzania, John Corse.

Ndege hiyo ya nyongeza  inafanya jumla ya nafasi inayokuwepo kwa siku kwenye safari kwa ajili ya wateja kufikia 1,000.

Fastjet ilianza safari zake nchini mwaka 2012na hivi sasa inajiendesha kwa kutumia ndege tano  aina ya A319 kwenye mtandao wake wa safari ambao unahusisha Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro na Zanzibar na kuifanya ijikite kuufanya usafiri wa anga ndani ya Tanzania watu wote waumudu.

Hali kadhalika ilianzisha safari za kimataifa  kwenda Entebbe nchini Uganda, Nairobi Kenya,  Harare Zimbabwe, Johannesburg Afrika Kusini na Lusaka nchini Zambia katika kipindi cha miaka mitatu ya kuendesha shughuli zake.

“Tangu tuanze safari zetu  tumeshabeba abiria zaidi ya 1,800,000 ambapo utafiti wetu unaonesha kuwa  zaidi ya theluthi moja  ya abiria wetu walikuwa ndio mara yao ya kwanza kumudu  kusafiri kwa ndege”, anasema Corse.

Aliendelea kusema, “kuongeza ndege  nyingine  kwenye safari zetu  kunatupa fursa muhimu ya kuongeza masafa kwa  njia zetu zilizopo  ili kukidhi  mahitaji ya wateja, na na inasaidia kwenye lengo letu la kuongeza njia moja ya kimataifa kwenye mtandao wetu kwa mwaka huu 2016”.

Hali kadhalika, Corse anabainisha kuwa  ndege hiyo mpya  inamanisha kuwa fastjet ni sawia na ni kubwa katika kutosheleza kupanuka kwa shughuli za fastjet.

Ndege hiyo A319  ambayo ni Airbus  ni ya injini mbili  ambazo zinatoa kiwango cha juu cha ufanisi pamoja na kiwango cha chini kabisa cha madhara kwenye mazingira, ikiwa ni nyongeza kwenye  viwango vya juu vya hali ya kuliwaza ndani ya ndege hiyo ya kisiasa.

Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba  abiria  156 ambaop wanamudu viwango vya chini vya kuendesha mtindo wa maisha wa gharama nafuu ambao unaendeshwa na Fastjet Tanzania.

Baadhi ya  njia muhimu ambazo ndege hiyo mpya itakuwa inahudumia  ni njia mpya iliyoanzisjhwa hivi karibuni kati ya Dar es Salaam na Nairobi, Kilimanjaro na Nairobi  na Dar es Salaam kwenda Zanzibar ambazo zote zilianza kwa mara ya kwanza Januari 11, 2016. njia hizi mpya  zote ni kielelezo muhimu muda mrefu kwenye upanuzi wa  njia za fastjet kitaifa na kimataifa.

Fastjet inatarajia kuongeza ndege zaidi kwenye njia yake ya Kenya  kutokana na mahitaji ya wateja kuongezeka kunakosababisha na kumudu, usalama, kasi na huduma kwa wakati, na hali kadhalika  imeshajionesha kuwa  kuna matarajio ya  kuzindua  safari kati ya Zanzibar na Nairobi  na hali kadhalika kati ya Dar es Salaam na Mombasa baadaye mwaka 2016.

“Usafiri wa anga unaoumudu ni muhimu kwenye  kukuza uchumi wa Tanzanoa, hususani kwenye   kukuza sekta za biashara na utalii”, alisema Corse.

Hali kadhalika Corse alibainisha  kuwa ndege hiyo mpya inamaanisha kwamba ndege za  Fastjet zitatosheleza kiasi cha kutosha  kusaidia kwenye changamoto za usimamizi na uendeshaji  iwapo  ndege moja miongoni mwake  itakuwa haifanyi kazi au kama ipo kwenye matengenezo au ukarabati wa lazima.

Mwisho

photo Krantz Mwanteple C.E.O & Founder, MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Website: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Whatsapp: 0712579102 "HABARI MAKINI KWA WATU MAKINI"

DC KINONDONI, PAUL MAKONDA APOKEA SARUJI MIFUKO 1640 KUTOKA KWA WADAU WA MAENDELEO KWA AJILI YA UJENZI WA SHULE ZA SEKONDARY

February 02, 2016
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Duma, Areeq Amran Mohamed (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda mfuko mmoja wa saruji kati ya 640 aliyoitoa kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Shule za Sekondari za wilaya hiyo Dar es Salaam leo asubuhi. Katika makabidhiano hayo Makonda alipokea mifuko 500 ya saruji kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo na Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk.Alex Malasusa aliyetoa mifuko 500. 
 Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo (kulia), akimkabidhi saruji hiyo DC Makonda.
 Lori lilibeba saruji hiyo likiwa eneo la tukio.
 DC Makonda na wageni wake wakiwa eneo la tukio kabla ya makabidhiano ya saruji hiyo.
 Mhe. Bulembo akihojiwa na waandishi wa habari baada ya kukabidhi msaada huo.
Wanahabari wakizungumza na watoa msaada huo.