TCRA YAENDELEA KUHAMASISHA USALAMA MTANDAONI NA UPATIKANAJI NA UPATIKANAJI WA LESENI KIDIGITALI

October 26, 2023

 Na Mwandishi Wetu Arusha


Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeendelea kutoa elimu kwa umma na kuhamasisha juu ya usalama mtandaoni, ikizingatiwa kwamba mwezi huu wa Oktoba ni mwezi wa Usalama Mtandaoni.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha wakati akiwasilisha Taarifa ya Mwenendo wa Sekta ya Mawasiliano, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Jabiri Bakari, alisema kuwa TCRA inaendelea na kampeni ya "Futa Delete Kabisa", ambapo inawakumbusha wananchi kuepuka kusambaza taarifa zozote zile zisizo za uhakika na za uchochezi.

Dkt. Bakari aliwasisitiza wananchi kuwa, pale ambapo wanapokea ujumbe wa kitapeli au simu ya kitapeli kwenye simu zao, watumie namba 15040 kutoa taarifa. Pia aliwakumbusha kuwa, usaidizi ambao mtumiaji wa huduma za mawasiliano ya simu anapaswa kupokea kutoka kwa mtoa huduma wa mawasiliano ni kupitia namba 100 pekee.

"Unapopata taarifa ambayo huna uhakika nayo, ni taarifa ambayo haiendani na mila zetu, ni taarifa ya hovyo, unatakiwa kufuta na kudelete kabisa, kwa sababu unapoisambaza unafanya kosa na inaweza kukuletea matatizo, futa delete kabisa," alisisitiza Dkt. Bakari.

Kuhusu Kampeni ya uelimishaji wadau wa sekta ya mawasiliano inayohusu upatikanaji wa leseni za mawasiliano Kidijitali, Dkt. Bakari alisema kuwa, TCRA imeboresha namna wanaohitaji leseni hizo wanaweza kuzipata kupitia mtandao katika Jukwaa la mtandaoni liitwalo ‘Tanzanite Portal’ ambalo linapatikana kwenye tovuti ya TCRA.

Dkt. Bakari aliwasisitiza watoa huduma wote wa Mawasiliano, kuhuisha leseni zao, kwa mujibu wa Sheria na taratibu. Pia aliwasisitiza wananchi kuhakikisha wakati wote wanapohitaji kupokea huduma za sekta ya mawasiliano wahakikishe wanazipata kutoka kwa watoa huduma wenye leseni ya TCRA.

"Wananchi wahakikishe wanapokea huduma kutoka kwa mtoa huduma ambae ana leseni hai, kwa sababu kuna watoa huduma ambao wanaendelea kutoa huduma wakati leseni yake hajahuisha," alisisitiza Dkt. Bakari.

Wachambuzi wa masuala ya mawasiliano wameipongeza TCRA kwa kazi nzuri inayofanya katika kuelimisha wananchi kuhusu usalama mtandaoni na upatikanaji wa leseni za mawasiliano Kidijitali.

Bi. Asha Mlay, mkazi wa Arusha, alisema kuwa, kampeni ya "Futa Delete Kabisa" ni muhimu sana kwani inawasaidia wananchi kuepuka kushirikishana taarifa za uongo na za uchochezi mtandaoni.

Bw. John Mwita, mtoa huduma wa mawasiliano jijini Arusha, alisema kuwa, mfumo wa Tanzanite Portal ni rahisi kutumia na umewawezesha watoa huduma wa mawasiliano kuhuisha leseni zao kwa haraka na kwa urahisi.

Kwa upande wao Wanahabari wa mtandaoni JUMIKITA kupitia kwa Mwenyekiti wao Shaban Omary Matwebe waliweka bayana kwamba utaratibu wa TCRA kuanzisha Jukwaa la pamoja la leseni mtandaoni ‘Tanzanite Portal’ umewarahisishia pakubwa watoa huduma ya maudhui kwenye mtandao kupata huduma kwa haraka huku gharama za leseni zikiwa zimepunguzwa kwa asilimia hamsini.

“lakini kipekee kwa sababu Serikali imeweka njia nyepesi ya kuapply (kuomba) leseni kupitia mtandao maana yake ni nini, ni wewe tu kuwa na vile viambatanisho, kitambulisho chako cha NIDA na karatasi nyingine chache basi unaomba unapata, tunapongeza sana TCRA kwa jambo hili,” alisisitiza Matwebe.

Mamlaka hiyo iliyoasisiwa miaka 20 iliyopita imepewa jukumu la kusimamia sekta ya mawasiliano katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na imekuwa na utaratibu wa kuchapisha taarifa ya mwenendo wa sekta ya mawasiliano katika kipindi cha kila Robo ya mwaka wa Fedha ili kuhakikisha wadau wa sekta wanapata fursa muhimu ya kwenda sambamba na mageuzi na maboresho yanayotokea kwa kasi katika sekta ambapo kwa Robo ya Kwanza ya mwaka wa Fedha 2023/2024 sekta ya mawasiliano imeendelea kukua kiidadi, kiteknolojia na kiusimamizi.

WAZIRI MKUU AZINDUA MASHINE YA KUCHANGANYA VIRUTUBISHO

WAZIRI MKUU AZINDUA MASHINE YA KUCHANGANYA VIRUTUBISHO

October 26, 2023





Kassim Majaliwa amezindua mashine ya kuchanganya virutubisho kwenye vyakula na kuwaomba wadau wote wa maendeleo kuunga mkono juhudi hizo ili kuwezesha mashine hizo kuzalishwa kwa wingi kutumika katika maeneo yote hapa nchini.

Mashine iliyozinduliwa inatumika kuongeza virutubisho muhimu katika vyakula hususan unga wa mahindi, virutubisho hivyo ni pamoja na vitamin B na folic acid ambayo zinasaidia kwenye ukuaji wa watoto na kuzia kuzaliwa na changamoto za ulemavu ikiwemo mgongo wazi na vichwa vikubwa.

Waziri Mkuu amezindua mashine hiyo leo (Alhamisi, Oktoba 26, 2023) wakati akitembelea mabanda ya maonesho kabla ya kufunga Mkutano Mkuu wa Tisa wa Wadau wa Lishe nchini uliofanyika katika Hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha. “Ninawapongeza sana wote waliowezesha kufikia hatua hii sambamba na mchango wa Shirika la GAIN, SIDO na DIT kwa kuwezesha kazi hii kukamilika.”

Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwasisitiza wadau hao wahakikishe virutubisho vinavyotumika katika mashine hizo vinazalishwa nchini ili kuondokana na utegemezi wa kuviagiza kutoka nje ya nchi.
- Advertisement -


Aidha, Waziri Mkuu amewahakikishia wadau hao kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan siku zote itaendelea kuunga mkono juhudi hizi ili kuhakikisha zinakuwa endelevu. Kadhalika,

Waziri Mkuu amesisitza Ofisi ya Rais – TAMISEMI ihakikishe kuwa mikataba ya lishe kati ya Mheshimiwa Rais na Wakuu wa Mikoa inatekelezwa kikamilifu na kuwa na tija. “Fanyeni ufuatiliaji wa karibu na kutoa taarifa za utekelezaji mara kwa mara.”

“Watendaji Wakuu wote wa Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala na Taasisi za Umma na Binafsi pamoja na Wadau wa Maendeleo na Asasi za Kijamii wekeni malengo ya lishe katika mipango yenu pamoja na kutenga fedha za utekelezaji kila mwaka kwa mujibu wa viwango tulivyojiwekea.”

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama amesema kwa kipindi kirefu nchi imekuwa ikikabiliana na changamoto ya upatikanaji wa vifaa vya kuchanganyia virutubisho kwenye vyakula vyenye bei nafuu, hivyo ameishukuru shirika la GAIN kwa kuwezesha upatikanaji wa vifaa hivyo.

“Serikali imepata mafanikio makubwa hayo kupitia Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) na Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Shirika la GAIN ambalo limewezesha kukamilika kwa kazi hiyo na kuwa wa kwanza kununua na kusambaza mashine hizo katika maeneo tofauti 50 yenye wazalishaji wadogo ambao ndio kundi kubwa linalolisha wananchi wengi.”

Awali, Naibu Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI, Deogratius Ndejembi alisema TAMISEMI itaendelea kusimamia utekelezaji wa huduma za afua za lishe kwa wakuu wa mikoa pamoja na viongozi wa Mamlaka za Seikali za Mitaa kama ilivyoainishwa katika mikataba.

Lengo kuu la Mkutano huo ni kupokea tathmini ya utekelezaji wa masuala ya lishe nchini kwa mwaka uliopita na kutoa fursa nyingine kwa wadau wa lishe kukutana na kupata maelezo ya tathmini ya utekelezaji wa masuala ya lishe katika mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Pili wa Kitaifa wa Lishe (2021/22 – 2025/26) ambao ulizinduliwa mwaka 2021 Mkoani Tanga.
MAKAMU WA RAIS DKT. PHILIP MPANGO AKAGUA VIWANDA MKOANI NJOMBE

MAKAMU WA RAIS DKT. PHILIP MPANGO AKAGUA VIWANDA MKOANI NJOMBE

October 26, 2023









Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Uchambuzi na Ufungashaji Parachichi cha AvoAfrica Bw. Nagib Karmali wakati alipowasili katika Kiwanda hicho kilichopo Makambako mkoani Njombe. (tarehe 26 Oktoba 2023)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akitembelea na kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa katika kiwanda cha Uchambuzi na Ufungashaji Parachichi cha AvoAfrica kilichopo Makambako mkoani Njombe. (tarehe 26 Oktoba 2023)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Uchambuzi na Ufungashaji Parachichi cha AvoAfrica Bw. Nagib Karmali wakati akitembelea na kukagua kiwanda hicho kilichopo Makambako mkoani Njombe. (tarehe 26 Oktoba 2023)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisalimiana na kaimu mkurugenzi wa Kiwanda cha Tanganyika Wattle (TANWAT) Bw. Hemasundar Raju wakati alipowasili katika Kiwanda hicho cha uchakataji wa bidhaa za mbao kilichopo Kibena mkoani Njombe. (tarehe 26 Oktoba 2023)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akitembelea na kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa katika kiwanda cha uchakataji wa bidhaa za mbao cha Tanganyika Wattle (TANWAT) kilichopo Kibena mkoani Njombe. (tarehe 26 Oktoba 2023)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa kaimu mkurugenzi wa Kiwanda cha Tanganyika Wattle (TANWAT) Bw. Hemasundar Raju wakati akitembelea na kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa katika kiwanda hicho cha uchakataji wa bidhaa za mbao kilichopo Kibena mkoani Njombe. (tarehe 26 Oktoba 2023)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha uchakataji wa bidhaa za mbao cha TANWAT mara baada ya kutembelea na kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa katika kiwanda hicho kilichopo Kibena mkoani Njombe. (tarehe 26 Oktoba 2023)
UGANDA NA TANZANIA WAJADILIANA KUJENGA BOMBA LA KUSAFIRISHA GESI ASILIA

UGANDA NA TANZANIA WAJADILIANA KUJENGA BOMBA LA KUSAFIRISHA GESI ASILIA

October 26, 2023







Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga (katikati), Naibu Waziri wa Nishati wa Uganda, Mhe. Peter Lokeris (kulia) na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Kanali Mstaafu Fred Mwesigye, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao kuhusu utekelezaji wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la kusafirisha Gesi Asilia kutoka nchini Tanzania kwenda nchini Uganda kilichofanyika terehe 26 Oktoba 2023, Jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Nishati wa Uganda, Mhe. Peter Lokeris (katikati) na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga (wa tatu kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Tanzania na Uganda, kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Musa Makame, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Kanali Mstaafu Fred Mwesigye, baada kikao kuhusu utekelezaji wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la kusafirisha Gesi Asilia kutoka nchini Tanzania kwenda nchini Uganda kilichofanyika terehe 26 Oktoba 2023, Jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga (kushoto) na Naibu Waziri wa Nishati wa Uganda, Mhe. Peter Lokeris (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja baada kikao kuhusu utekelezaji wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la kusafirisha Gesi Asilia kutoka nchini Tanzania kwenda nchini Uganda kilichofanyika terehe 26 Oktoba 2023, Jijini Dar es salaam.



*Tanzania na Uganda wajadiliana Ujenzi wa Mradi wa Bomba la kusafirisha Gesi Asilia

*Rasimu ya Mkataba baina ya nchi hizo mbili kusainiwa mwezi Novemba, 2023

Serikali ya Tanzania na Uganda zimekubaliana kuwa Rasimu ya Mkataba Mahsusi Baina ya Tanzania na Uganda (Bilateral Agreement) katika utekelezaji wa Ujenzi wa Mradi wa Bomba la kusafirisha Gesi Asilia kutoka Tanzania kwenda Uganda isainiwe Mwezi Novemba, 2023 Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga na Naibu Waziri wa Nishati wa Uganda, Mhe. Peter Lokeris wamekubaliana hayo wakati wa kikao cha majadiliano kuhusu Ujenzi wa Mradi wa Bomba la kusafirisha Gesi Asilia kutoka nchini Tanzania kwenda nchini Uganda kilichofanyika terehe 26 Oktoba 2023, Jijini Dar es salaam.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Kanali Mstaafu Fred Mwesigye, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Musa Makame na wataalamu wengine kutoka Wizara ya Nishati upande wa Tanzania na Uganda.

Akizungumzia hatua zilizofikiwa katika majadiliano hayo, Mhe. Kapinga alisema kuwa Wizara ya Nishati, imekwisha wasilisha nyaraka muhimu kwa wadau wote wanaohusika katika utekelezaji wa mradi huo ikiwemo Wizara ya Fedha na Mipango, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).

Pia Wizara imeshapokea maoni kutoka kwa wadau hao, ambapo tayari Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameridhia kuendelea na hatua zinazofuata.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati wa Uganda, Mhe. Peter Lukeris amesema kuwa mradi huo ni muhimu kwa nchi zote mbili hivyo ni vyema kuanza utekelezaji wa hatua za awali hususani kusaini nyaraka zilizoandaliwa ikiwemo Rasimu ya Mkataba Mahsusi Baina ya Tanzania na Uganda (Bilateral Agreement).

Vilevile ameeleza kuwa kusainiwa kwa mkataba huo utawezesha shughuli zingine za utekelezaji wa mradi huo kuanza na kuleta manufaa kwa mataifa hayo mawili.

Awali akiwasilisha taarifa za mradi huo, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Mramba, alieleza kuwa Timu ya Wataalamu ya pamoja iliandaa nyaraka mbalimbali ambazo ni Rasimu ya Mkataba Mahsusi Baina ya Tanzania na Uganda (Bilateral Agreement), Rasimu ya Kanuni za Manunuzi za Pamoja (Joint Procurement Rules) na Rasimu ya Hadidu za Rejea (Terms of Reference – ToR).

Na baada ya kuandaa nyaraka hizo, timu hiyo ya watalaam ilikubaliana kupata maoni na idhini kutoka Mamlaka zinazohusika na Mradi huo kutoka nchi zote mbili na kuzifanyia kazi kwa hatua zaidi.

TANZANIA NA UN ZASAINI MPANGO KAZI WA PAMOJA

October 26, 2023

 Na. Farida Ramadhani na Saidina Msangi, WF, Dodoma.


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Umoja wa Mataifa (UN) wamesaini Mpango Kazi wa pamoja wa Mwaka 2023/24 wa ushirikiano wa maendeleo kati ya Serikali na Mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Hati za Mpango kazi huo zimesainiwa jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti wa Kundi la Washirika wa Maendeleo nchini, Bw. Zlatan Milišić, katika Kikao cha Pili cha Kamati ya Usimamizi wa Mpango wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Akizungumza katika kikao hicho, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba amehimiza watekelezaji wote wa Mfumo wa Ushirikiano wa Maendeleo Endelevu wa Umoja wa Mataifa (UNSDCF) zikiwemo Taasisi za Serikali, AZAKi, Mashirika yasiyo ya Kiserikali na Umoja wa Mataifa kwa ujumla, kutumia fedha zinazotolewa na washirika wa maendeleo ipasavyo katika kuleta maendeleo nchini.

“Kama wasimamizi wa rasilimali za umma tuna jukumu la kuendeleza ustawi wa wananchi, na kuhakikisha kila shilingi inayotengwa inatumika kwa ufanisi, uwazi, na kwa umakini wa hali ya juu kwa maendeleo ya Taifa” Alisisitiza Dkt. Mwamba.

Alisema Mfumo wa UNSDCF unaweka msisitizo katika ushirikiano thabiti ili kuleta mabadiliko ambapo utekelezaji wake unahitaji ushirikiano endelevu kati ya Tanzania na UN, huku ukiendelea kusisitiza katika maadili, kanuni na viwango vya pamoja vya mfumo wa Umoja wa Mataifa.

“Mkutano huu ni muhimu katika jitihada zetu zinazoendelea za kufikia malengo yetu makubwa yaliyowekwa katika Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu na hasa baada ya hivi karibuni kuhitimisha Jukwaa la Ngazi ya Juu la Kisiasa la Umoja wa Mataifa lililofanyika Julai 2023, nchini Marekani, ambapo pamoja na mambo mengine, kama Taifa tuliwasilisha Ripoti ya Tathmini ya Kitaifa ya Hiari ya mwaka 2023 (VNR) kuhusu Utekelezaji wa Ajenda ya 2030 ya SDGs”, alibainisha Dkt. Mwamba.

Aidha, alitoa rai kwa pande zote kuendelea kuzingatia Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, Sura ya 134 (kifungu cha 30) ambayo pamoja na mambo mengine, inatamka kwamba Waziri wa Fedha atakuwa na mamlaka ya kupokea na kwa niaba ya Serikali ruzuku yoyote itakayotolewa kwa Serikali kutoka kwa Serikali yoyote ya kigeni au mtu mwingine, isipokuwa akikasimisha kwa Afisa yeyote wa Umma aliyetajwa kutekeleza kwa niaba ya Serikali makubaliano yoyote au hati nyingine inayohusiana na mkopo, dhamana au ruzuku.

Aliupongeza Umoja wa Mataifa (UN) kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania na kubainisha kuwa msaada unaotolewa na UN umesaidia Serikali katika kutekeleza sera za kiuchumi na mageuzi ili kukuza ukuaji wa uchumi, kupunguza umaskini, na kuboresha ustawi wa kijamii na kiuchumi wa watu ambapo bila msaada huo baadhi ya mipango ya kupunguza umasikini ingechelewa.

Akizungumzia kikao hicho, Dkt. Mwamba alisema kuwa kikao hicho ni hatua muhimu katika dhamira inayoendelea ya kufikia malengo yaliyoainishwa katika Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti wa Kundi la Washirika wa Maendeleo nchini, Bw. Zlatan Milišić, alisema kuwa kutokana na juhudi za pamoja mafanikio makubwa yameweza kufikiwa katika kipindi cha mwaka mmoja ikiwemo maendeleo ya watu na kujenga mazingira wezeshi.

‘’Tumefanikiwa katika ushirikishaji wa masuala ya kijinsia katika mifumo ya fedha na kutumia kanuni ya kutomwacha yeyote nyuma hasa katika mikakati ya afya. Tulifanikiwa katika kupanua wigo wa utoaji huduma za afya na elimu’’, alisema Bw. Zlatan MiliÅ¡ić.

Aliongeza kuwa walifanikiwa kufanya kazi na Serikali pamoja na washirika wa maendeleo kukusanya rasilimali katika mazingira ya kupunguza usaidizi rasmi wa maendeleo na kufanikiwa kukusanya rasilimali chini ya Mfuko wa Kimataifa (GFTAM), na kuunga mkono mikakati mbalimbali kama vile Mwongozo Maalum wa Kitaifa na mikakati inayohusu Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika na Biashara ya Mtandaoni.

‘’Tumeunga mkono utoaji wa taarifa za makubaliano ya kimataifa ikiwemo kupitia usaidizi kwa Utafiti wa Demografia na Afya (DHS), Sensa ya Watu na Makazi (PHC) na zoezi la Mapitio ya Hiari ya Kitaifa ya 2023’’, aliongeza.

Aidha, alisema kuwa mtazamo wa UN kwa jamii ulisababisha kuongezeka kwa uelewa miongoni mwa makundi mbalimbali ya watu kuhusu haki, wajibu na wajibu wao katika safari ya kuelekea mafanikio ya maendeleo ya taifa.

Alishukuru kwa ushirikiano ambao UN unapata kutoka kwa Serikali ya Tanzania na kueleza kuwa anatumai ushirikiano huo utaendelea katika ngazi zote, huku akiahidi kuwa UN itaendelea kuunga mkono Serikali katika jitihada za kuleta maendeleo.



Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti wa Kundi la Washirika wa Maendeleo nchini, Bw. Zlatan MiliÅ¡ić, wakisaini Mpango Kazi wa Pamoja wa 2023-2024 wa ushirikaiano kati ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, katika kikao cha Pili cha Kamati ya Usimamizi ya Pamoja kati ya Serikali ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, kilichofanyika katika ukumbi wa Kambarage, jijini Dodoma. Anayeshuhudia ni Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Robert Mtengule.


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza wakati akifungua Kikao cha Pili cha Kamati ya Usimamizi ya Pamoja kati ya Serikali ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, kilichofanyika katika ukumbi wa Kambarage, jijini Dodoma.


Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti wa Kundi la Washirika wa Maendeleo nchini, Bw. Zlatan MiliÅ¡ićakizungumza wakati wa Kikao cha Pili cha Kamati ya Usimamizi ya Pamoja kati ya Serikali ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, kilichofanyika katika ukumbi wa Kambarage, jijini Dodoma.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti wa Kundi la Washirika wa Maendeleo nchini, Bw. Zlatan MiliÅ¡ić wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa walioshiriki katika kikao cha Pili cha Kamati ya Usimamizi ya Pamoja kati ya Serikali ya Tanzania na Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, kilichofanyika katika ukumbi wa Kambarage, jijini Dodoma.

 

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)

MAKONDA ATINGA NA BODABODA OFISI ZA CCM DAR, MAPOKEZI YAKE YAWEKA REKODI, ATAKA TAARIFA SAHIHI

October 26, 2023

 Na Said Mwishehe, Michuzi TV


PAUL Makonda apokelwa kwa staili ya aina yake baada ya kutumia usafiri bodaboda wakati akienda Ofisi ndogo za Chama Cha Mapinduzi(CCM)zilizopo Mtaa wa Lumumba jijini Dar ea Salaam ambako yamefanyika mapokezi makubwa.

Mapokezi ya Makonda yamefanyika leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku chache tu Chama Cha Mapinduzi( CCM) kuteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho na leo amepokelewa rasmi na wana CCM mkoa wa Dar es Salaam .

Akitumia usafiri wa bodaboda akiendesha mwenyewe alifika Ofisi za CCM saa nne asubuhi akiwa na waendesha bodaboda kadhaa na baada ya kuwasili aliingia ofisini na kisha kuzungumza na waandishi wa habari pamoja na watumishi wa Idara ya Itikadi na Uenezi.

Pia yamefanyika makabidhiano ya ofisi kati yake na aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi Sophia Mjema ambaye ameteuliwa kuwa mshauri wa Rais katika masuala ya wanawake na makundi maalum.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa ofisi na vitendea kazi, Makonda amesema kwamba anamshukuru Mungu kwa kumpa kibali cha kuwatumikia watanzania katika bafasi hiyo lakini pia anamshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan pamoja na Kamati Kuu kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kukitumikia Chama hicho.

"Namuomba Mungu anipe hekima, busara , uadilifu na maarifa ili kuifanya kazi hii kwa uaminifu na ukamilifu wa hali ya juu ili nisimuabishe Mungu na nisimuabishe Mwenyekiti wa Chama aliyeriki jina lake kwenda Kamati Kuu."

Pamoja na hayo Makonda ametumia nafasi hiyo kuwaomba watumishi na watendaji wa Chama hicho kumpa ushirikiano na kubwa zaidi kumpa taarifa sahihi ambazo zitamuwezesha kutekeleza majukumu yake vizuri.

"Duniani kote watu wanaishi kwa taarifa na taarifa ndio inafanya maamuzi ,ukiwa na chanzo kibovu utafanya maamuzi mabovu na ukiwa na chanzo kizuri utafanya maamuzi sahihi, " amesema Makonda

Hivyo amesema anatarajia atapewa taarifa sahihi ili aweze kufanya ya kumsaidia Katibu Mkuu wa Chama ,kumsaidia Makamu Mwenyekiti,kumsaidia Mwenyekiti wao wa Chama na hatimaye kwa pamoja waweze kukiimarisha na kukijenga Chama kwa wananchi.

Makonda akitumia nafasi hiyo amewashukuru waandishi wa vyombo vya habari nchini kwa kuendelea kushirikiana na CCM na kwamba waandishi wa habari wamekuwa kiunganishi kikubwa kati ya Chama na wananchi , hivyo Chama hicho kitaendelea kushirikiana na vyombo vya habari.

Aidha Makonda amemtakia majukum mema aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Sophia Mjema na kwamba anaamini watashirikiana katika kuyasemea makundi mbalimbali

Makonda akizungumza na waandishi wa habari amehitimisha mazungomzo yake kwa kueleza kwa sasa anaendelea kujifunza kuhusu nafasi yake na atajifunza kupitia watangulizi wake kuanzia Sophia Mjema, Shaka Hamdu Shaka na Nape Nnauye.



SERIKALI YABAINISHA MIKAKATI ENDELEVU KWA AJILI YA KUIMARISHA MFUKO WA UDHAMINI WA KUDHIBITI UKIMWI NCHINI.

October 26, 2023

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga akifafanua jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI kilichofanyika Bungeni Dodoma Tarehe 23 Oktoba 2023 ambapo aliwasilisha Taarifa kuhusu Utekelezaji wa Mkakati Endelevu kwa  ajili ya kuimarisha mfuko wa udhamini wa Kudhibiti UKIMWI Tanzania (AIDS TRUST FUND – ATF).




Picha Ikionesha baadhi ya wajumbe katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI kilichofanyika Bungeni Dodoma Tarehe 26 Oktoba 2023.

NA; MWANDISHI WETU – DODOMA

 

Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, inaendelea kushauriana na Serikali kuhusu kuwa na chanzo endelevu na cha uhakika cha Mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI nchini.

Hayo yamesemwa mapema leo Tarehe 26 Oktoba 2023 Bungeni Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Buange na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga alipowasilisha Taarifa kuhusu Utekelezaji wa Mkakati Endelevu kwa ajili ya kuimarisha mfuko wa udhamini wa Kudhibiti UKIMWI Tanzania (AIDS TRUST FUND – ATF), kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI.

Naibu Waziri Nderiananga alisema, Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) inafanya mapitio ya Mkakati wa Ukusanyaji wa Rasilimali kwa kuzingatia wakati, mwelekeo na mahitaji ya sasa na kupitia upya vigezo na malengo ili kufanya maboresho kwa kuzingatia Mkakati ulioboreshwa wa kukusanya rasilimali.

Akiongelea suala la kukuza mchango wa sekta binafsi katika mapambano dhidi ya UKIMWI, Naibu Waziri Nderiananga alisema, Tume imeanzisha mfumo wa majadiliano na wadau kupitia vikao ili kujadili uendelevu wa rasilimali za afua za UKIMWI nchini.

 “Malengo makuu ya kuanzishwa kwa Mfuko wa ATF ni pamoja na kupunguza utegemenzi wa rasilimali za kufadhili afua za VVU/UKIMWI kutoka nje ya nchi, kuongeza uendelevu wa huduma muhimu za UKIMWI.” Alisisitiza Nderiananga.

Aliendelea kusema kuwa, Serikali imeendelea kutekeleza sheria kwa kutenga bajeti ya Serikali kila mwaka kwa ajili ya mfuko huo, pamoja na kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali kwa mujibu wa mwongozo wa mfuko.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI Mhe. Stansalus Nyongo alisema ni vizuri Serikali ikatenga na kuongeza  fedha za kutosha kwa ajili ya Mfuko huo wa UKIMWI na kuendelea kusema kuwa kamati yake ipo tayari kuhamasiha upimaji wa VVU kupitia mabonanza mbalimbali ya michezo yanayofanyika..

 

 

 

Captions

P1.


P2.


 


WIZARA YA KILIMO YAAHIDI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA WADAU WA KILIMO

October 26, 2023

 Na Fauzia Mussa , Maelezo

WIZARA ya Kilimo ,Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar imesema uwepo wa miradi ya kilimo kunapelekea kuikomboa jamii kiuchumi.

Akizungumza wakati wa ziara ya wadau wa mradi wa Agri connect kuangalia utekelezaji wa mradi huo Afisa Mdhamini Wizara ya Kilimo Pemba Mhandisi Idris Hassan Abdulla amesema kupitia mradi huo jamii imeweza kunufaika kwa kujiongezea kipato pamoja na kupata lishe nzuri kwaajili ya familia.

Alifahamisha kuwa Mradi huo una lengo la kuwainua wakulima wa mbogamboga , viungo,pamoja na wajasiriamali wanaojishuhulisha na utengenezaji wa majani ya chai na kahawa,hivyo Wizara itaenedelea kuunga mkono juhudi za wadhamini wa mradi huo ili kufikia malengo yalioyotarajiwa.

Mapema ameishukuru Jumuiya ya umoja wa ulaya kwa kuwekeza fedha zao katika mradi huo unaolenga kutoa ajira hasa kwa wanawake na vijana.

Kwa upande wake Meneja Mkuu mradi wa viungo Simon Makobe alisema lengo la ziara hiyo ni kuangalia changamoto zinazowakabili watekelezaji wa miradi ya agri connect na kuweza kuzipatia ufumbuzi.

Aidha aliishukuru Wizara ya Kilimo kwa kusimamia shughuli zote zinazofanyika chini ya mradi huo pamoja na Jumuiya ya Ulaya ambayo imeamini kutoa fedha na kuziwekeza kwa wajasiariamali wakiwemo wakulima wa mbogamboga, matunda na viuongo.

Sambamba na hayo aliwataka wakulima kushirikiana kwa pamoja katika kilimo kwa kuzalisha bidhaa zinazofanana ili kurahisisha kupata masoko.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Katibu wa kikundi cha Tumaini la Kijani Ali Shauri na mkulima wa Viungo Aviwa walisema kwasasa wamekuwa wakipunguza gharama za matumizi kwaajili ya mlo kwani kilimo kinawasaidia kupata mahitaji ya chakula na mbogamboga.

"Sasahivi kina mama hawanunui tena mboga,tungule ,bamia,wala nyanya zote tunapata kupitia bustani zetu za nyumbani"Katibu huyo

Walisema kupitia mradi huo jamii imepata elimu juu ya mbinu bora za kilimo hai hivyo kwasasa wanajipatia chakula salama kwani wanarutubisha vilimo vyao kwa kutumia mbolea asili ikiwemo kinyesi cha Ng’ombe.

Aidha walisema awali jamii ilikua ikipanda bustani za maua kama pambo lakini baada ya kupata elimu wameanza kupunguza upandaji wa maua na wengine kuoondoa kabisa nakuweka bustani za mbogamboga (kitchen garden ) pembezoni mwa nyumba zao ili kupunguza gharama za mlo.

Hivyo waliwashauri Vijana na Wanawake kuacha kukaa bila ya kujishughulisha na badala yake kujiunga na vikundi vya ujasiriamali na kuanzisha kilimo kitakachowapatia kipato na kupunguza gharama za maisha.

Mbali na mafanikio hayo wakulima hao wanakabiliwa na uhaba wa maji,pamoja na masoko ya nje.

Ziara hiyo iliyoambatana na ujio wa ujumbe wa jumuiya ya umoja wa Ulaya ,watekelezejai wa miradi ya Agri connect Zanzibar na Tanzania Bara, timu ya ushauri wa mradi Tanzania wakishirikiana na Wizara ya kilimo na fedha Zanzibar ilifanikiwa kutembelea kikundi cha Tumaini la kijani Chuini,Shamba la Viungo na matunda Kizimbani na kiwanda cha kutengeneza majani ya Chai Amani Zanzibar.
Katibu wa kikundi cha Tumaini la kijani Ali Shauri akizungumza na wafadhili wa mradi wa agriconnect kuhusiana na bustani za nyumban (kitchen garden) wakati walipowatembelea kuangalia maendeleo ya mradi huo,huko Chuini Wilaya ya Magharibi “A”.
fisa Mdhamini Wizara ya Kilimo Pemba Mhandisi Idris Hassan Abdulla akizungumza na Waandishi wa habari katika ziara ya kuangalia utekelezaji wa mradi wa Agri-connect.
Mkulima wa viungo(spices) na matunda Aviwa akielezea maendeleo ya kilimo hicho wakati alipotembelewa na wadau wa mradi wa Agri connect huko Kizimbani Wilaya ya Magharibi “A”.
PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO

TCRA :WANANCHI EPUKENI KUSAMBAZA TAARIFA ZISIZO NA UHAKIKA NA ZA UCHOCHEZI

October 26, 2023

 



Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt.Jabir Kuwe Bakari akitoa Muhtasari wa mwenendo wa Sekta ya Mawasiliano katika kipindi cha Julai hadi Septemba leo 25 Oktoba 2023 Jijini Arusha


Na.Vero Ignatus,Arusha

Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imefanya ufuatiliaji wa maudhui ya redio/ televisheni ambapo watoa huduma 80 walikutwa na makosa ya urushwaji wa maudhui yasiyofaa.

Akitoa mwenendo wa sekta ya mawasiliano katika kipindi cha Julai-septemba 2023 kwa waandishi wa habari leo Jijini Arusha Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt.Jabir Kuwe Bakari alisema tayari hatua za kisheria zimechukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kupewa onyo, adhabu na maelekezo kwa kujibu wa sheria.

Dkt.Kuwe amesema TCRA kwa kushirikiana na Wizara ya maendeleo ya Jamii Jinsia wanawake na watoto na makundi maalum, imekamilisha uratibu wa programu maalum ya kuandaa vipindi vya maadili vitakavyorushwa na vituo vya utangazaji 150 vyenye leseni ya kiwilaya kwa lengo la kutoa elimu na kujenga jamii inayozingatia maadili, mila, desturi na utamaduni wa Mtanzania.

Sambamba na hayo TCRA imewakumbusha wananchi kuepuka kusambaza taarifa zozote zile zisizokuwa na uhakika na za uchochezi,kutambua na kiripoti kuhusu udanganyifu mtandaoni,na endapo yeyote akipokea ujumbe wa kitapeli au simu ya kitapeli atume ujumbe kwenda namba 15040.

Aidha TCRA imeendelea kuwasisitiza wananchi upatikanaji wa leseni za kidijitali kupitia mfumo wa Tanzanite Portal ,pamoja na kuhakikisha kuwa watumiaji hao wa huduma za mawasiliano kutoka TCRA ili kuendelea kuwa salama kupata huduma bora

Vilevile katika sekta ya Utangazaji zinaonyesha kuwa visimbizi 3,631,649 vilikuwa hewani hadi mwezi septemba 2023 ikilinganishwa na visimbizi 3,342,626 kwa.mwezi juni 2023 ambapo kati ya hivyo 1,789,090 ni vya dijitali kwa mfumo wa televisheni wa utangazaji wa mitambo ya ardhini na 1,846,559 ni vya mfumo wa televisheni wa setilaiti ambapo Dar inaongoza kuwa na visimbizi 1,390,163 ikifiatiwa na Arusha (287,908) mwanza 282,779 na mbeya (229,570) mikoa yenye visimbuzi vichache kuliko yote ni Manyara( 1,816)


'' Septemba 2023 kulikuwa na laini za simu milioni 67.12 kutoka milion 64.01 mwezi juni 2023 sawa na ongezeko.la 4.86%

kuanzia mwezi julai hadi septemba 2023 simu zilizobainika kuhusika na viashiria vya ulaghai au uhalifu ni 23,328 ikilinganishwa na 23,234 kati ya mwezi April hadi Juni 2023.

Akielezea juu ya sekta za kifedha kupitia mitandao ya simu amesema Tanzania inazidi kiendeleza mfumo jumuishi wa kifedha kutokana na ongezeko kwa watumiaji wa simu za mkononi .

"Takwimu za robo ya kwanza 2023/24 zinaonyesha kuwa huduma za kipesankupitia simu za mkononi zimeongezeka kutoka akaunti 47,275,660 mwezi june 2023 hadi kufikia 51,369,347 kwa mwezi Septemba 2023,ikiwa ni ongezeko la asilimia 8.7%ambapo miamala. Ya kifedha imeongezeka kutoka 420,675,884 kwa kipindi kilichoisha mwezi june 2023 hadi miamala 422,390,546 kufikia septemba 2023"

Dkt. Jabir.amesisitiza umuhimu wa taarifa ya takwimu za. Mawasiliano ni pamoja miongoni mwa faida zake ni kusaidia umma kupata taarifa, kuonyesha maeneo ya fursa mpya kwa wajasiriyamali, kiwasaidia watoa huduma kuweza kuboresha huduma zao, pamoja na kiwawezesha watendaji kichukua hatua stahiki kwenye maeneo ya kufanya iwezeshajj wenye tija katika sekta ya mawasiliano.

Aidha TCRA inatoa rasilimali za mawasiliano bure kwa wabunifu mbalimbali wanaohitaji kufanya majaribio kwenye huduma zao kwa kipindi maalum, kwani mwezi juni 2023 jumla ya wabunifu 4 walipewa rasilimali namba, ambapo hadi kufikia septemba 2923 imetoa rasilimali kwa wabunifu waoatao 9katika namba na. Mmoja ni katika masafa,.

Pamoja na hayo takwimu za watumiaji wa huduma za intaneti zinaonyesha kuendelea kuongezeka kwa watumiaji 1.24% kutoka kwa watumiaji 34,047,407 kwa mwezi juni 2023 hadi kufikia 34,469,022 mwezi septemba 2023.

"Baadhi ya sababu zinazochangia ongezeko hilo la matumizi ya Intaneti ninuwepo wa maudhui ya Kiswahili kwenye matandao wa ikijumuisha kuongezeka kwa programu -tumizi kwa lugha ya kiswahili.

Vilevile katika Sekta ndogo ya Posta katika kipindi cha mwezi julai hadi septemba 2023 vipeto 107,147 kutoka nje ya nchi ambapo huduma hiyo inaendelea kuchagiza ukuaji wa biashara mtandao.