Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi azindua maadhimisho ya siku ya Bahari Duniani Mkoani Tanga leo

September 27, 2016
 Kulia ni Mgeni Rasmi kwenye Uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Bahari Duniani  ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi, Tumpe Mwaijande kushoto ambaye alimuwakilisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Makame Mbawara katika maashimidho hayo akiingia kwenye viwanja vya Tangamano kunakofanyika maadhimisho hayo katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra,Gilliard Ngewe  kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(Ras)Mhandisi Zena Saidi 
 Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TPA,Focus Mauki kushoto akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi, Tumpe Mwaijande aliyesimama katikati wakati alipolitembelea Banda la Mamlaka ya Bandari (TPA) kunakofanyika maadhimisho ya siku ya Bahari Dunia wa kwanza kulia ni  Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra,Gilliard Ngewe
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),Joseph Msaki kushoto akimueleza jambo Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi, Tumpe Mwaijande wakati alipotembelea Banda lao leo
 Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),Joseph Msaki aksisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi, Tumpe Mwaijande wakati alipotembelea Banda lao leo wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa
 Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika kushoto akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi, Tumpe Mwaijande wakati alipotembelea Banda lao leo
  Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika kushoto akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi, Tumpe Mwaijande ambaye hayupo pichani wakati alipotembelea Banda lao leo
 Tug Master Idara ya Marine Bandari ya Tanga,Mkanga Mbwana akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi, Tumpe Mwaijande wakati alipotembelea Banda lao leo katikati ni Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TPA,Focus Mauki
 Afisa Zimamoto na Usalama wa Bandari ya Tanga (TPA),Athumani Mkubwa akimueleza jambo Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi, Tumpe Mwaijande wakati alipotembelea Banda lao leo katikati ni Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TPA,Focus Mauki
 Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Quality Body Product LTD ambayo inajihusisha na Vifaa vya Uvuvi na Malighafi za Vipodozi,Hussein Walt akimuonyesha mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira, Wizara ya Uchukuzi, Tumpe Mwaijande namna wanayotengeneza bidhaa hizo wakati alipo tembelea Banda lao leo


 Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi kavu na majini  (Sumatra) Mussa Mandia kushoto akisoma vipeperusi kuhusiana na mfuko wa Pensheni wa  PSPF mara baada ya kulitembelea Banda lao lililopo kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga panako fanyika maadhimisho ya siku ya Bahari Duniani katikati ni Afisa wa Mfuko huo,Michael Kazimili na kulia aliyekaa ni Afisa Mwandamizi wa mfuko huo Mkoa wa Tanga,Happines Mbuna
Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi kavu na majini  (Sumatra) Mussa Mandia kushoto akisoma vipeperusi kuhusiana na mfuko wa Pensheni wa PSPF mara baada ya kulitembelea Banda lao lililopo kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga panako fanyika maadhimisho ya siku ya Bahari Duniani katikati ni Afisa wa Mfuko huo,Michael Kazimili na kulia aliyekaa ni Afisa Mwandamizi wa Mkoa wa Tanga,Happines Mbuna
Afisa Mkaguzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Vyombo vya Majini  kutoka Sumatra ,Mhandisi Christopher Mlelwa akimsikiliza mkazi wa Jiji la Tanga ambaye aliitaja kupata ufafanuzi kuhusiana na masuala mbalimbali yanayohusiana na mamlaka hiyo


 Baadhi ya wakazi wa Jiji la Tanga wakifuatilia uzinduzi wa Maonyesho ya Bahari Dunia leo kwenye viwanja vya Tangamano

WAZIRI LUKUVI AWAFUTIA HATI WALIOMIKISHWA ENEO LOTE LA MAKABURI YA KINYEREZI SOKONI

September 27, 2016

bn647561
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, William Lukuvi akisalimia na DAS wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, alipowasili kwenye eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni, kufuatia mgogoro wa wananchi wawili kumilishwa eneo hilo la makaburi lenye ukubwa wa zaidi ya ekari moja. Katika sakata hilo, Waziri Lukuvi ameagiza kufutwa kwa umiliki huo mara moja ifikapo leo jioni, na pia kugiza kusakwa Pascal Kyonya Kazungu na  Ntitonda Chukilizo waliomilikishwa eneo hilo watafutwe na kufikishwa ofisini kwake kesho  Kadhalika amemwagiza Kaimu Mkurugenzi wa Ardhi mkoa wa Dar es Salaam, Leo Komba, kuorodhesha majina ya maofisa ardhi wote walioshiriki kuwamilikisha ardhi hiyo ya eneo la makaburi ili aweze kuwashughulikia kwa kuwachukulia hatua za kisheria. Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Segerea Bona Kalua
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi William Lukuvi akipatiwa maelezo na Mbunge wa Segerea Bona Kalua alipowasili kwenye eneo hilo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni leo. Kushoto ni DAS wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo.
 Waziri Lukuvi akiwa na Diwani wa Kata ya Kinyerezi,  Grayson Celestine alipowasili leo kutatua mgogoro wa kumilikishwa eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni Dar es Salaam,.Kushoto ni Dar wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo
 Waziri Lukuvi akihoji jambo kwa uongozi wa Kata ya Kinyerezi alipowasili kwenye eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni, leo
 Waziri Lukuvi akipata maelezo kutoka kwa uongozi wa Kata ya Kinyerezi alipowasili kwenye eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni, leo. Kulia ni Mbunge wa Segerea Bona Kalua
 Wananchi wa eneo la Kinyerezi Sokoni wakiwa wamemzunguka Waziri Lukuvi alipowasili kwenye eneo la Makaburi hayo leo
 Kaimu Mkurugenzi wa Ardhi jiji la Dar es Salaam,  Leo Komba (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri Lukuvi kuhusu anachofahamu juu ya wananchi wawili kumilikishwa eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni leo
 ” Sasa hapo mimi sima la ziada, Wewe si ndiyo Mkurgenzi?” Sawa kuanzia mda huu, nakuagiza ukafute umilikishwaji ardhi uliofanywa katika eneo la makaburi haya”, alisema Waziri Lukuvi na kuongeza ” Na wale waliomilikishwa hapa nitafutieni kesho waje kwangu wanieleze ilikuwaje hata wakapata kumilikishwa eneo hili, na wale wote walioshiriki kwa namna yoyote katika kufanya hili uniletee majina yao mara moja”.
 Diwani wa Kata ya Kinyerezi, Grayson Celestine, akimshukuru Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi, William Lukuvi baada ya kutoa uamuzi wa kufuta umilikishwaji wa eneo hilo la makaburi kwa watu wawili. 
Waziri Lukuvi akifuatana na DAS wa wilaya ya Ilala wakati akiondoka kwenye eneo hilo la makaburi ya Kinyerezi, ambako amefanikiwa kumaliza mgogoro wa wananchi na watu wawili waliokuwa wamemikishwa eneo hilo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni. Kulia ni Diwani wa Kata ya Kinyerezi Grayson Celestine. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
………………………………………………………….
Jonas Kamaleki, MAELEZO
Wakazi wa Kinyerezi Sokoni, Dar es Salaam wameipongeza Serikali ya awamu ya Tano kwa kufuta hati tatu zilizokuwazimetolewa katika eneo la makaburi liliouzwa kinyume cha sheria.
Pongezi hizo zimetolewa leo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi baada ya kumwagiza kamishna wa ardhi Kanda ya Dar es Salaam kufuta hati hizo mara moja na kulirejesha eneo la makaburi kwa wananchi.
Akiongea kwa niaba ya wakazi wa Kinyerezi, Mwanasheria, Mwinjuma Mzee amesema kuwa Wanakinyerezi wanamshukuru sana Mhe. Waziri kwa kurejesha eneo la makaburi kwa wakazi hao.
“Mhe. Waziri na msafara wake wote tunawashukuru kwa kumaliza mgogogoro huu ambao umedumu kwa muda mrefu na tumemwomba Waziri ashughulikie na maeneo mengine yanayohusu huduma za jamii kama zahanati na shule,” alisema Mzee.
Naye mkazi wa Kinyerezi, Bi. Maimuna Forogo ameelezea furaha yake kwa kumshukuru sana Mhe waziri kwa hatua aliyoichukua ya kubatilisha hati za umiliki wa makaburi.
“Mimi namnshukuru sana Mhe. Waziri na Serikali ya awamu ya Tano kwa ujumla kwa kutujali sisi wananchi, mimi kwenye makaburi haya nilimzika babu yangu sasa wanataka nimpeleke wapi kwanza ni mifupa mitupu,”alisema Maimuna.
Kwa upande wake, Mhe. Lukuvi amesema ameamua kubatilisha hati tatu za viwanja zilizotolewa na watumishi wasiowaaminifu wa Serikali ili eneo hilo liendelee kutumika kwa ajili ya maziko.
“Nimemuagiza kamishna anitafutie wahusika ambao walishiriki katika kumilikisha eneo la makaburi kwa watu ili wachukuliwe hatua za kinidhamu, watu hawa inabidi wafukuzwe kazi kwani kitendo cha kumilikisha eneo la kuzika hakivumiliki,”alisema Waziri Lukuvi.
Ameongeza kuwa watu ambao wanadiriki kuuza makaburi ambayo yametumiwa tangu mwaka 1962 na kwa sasa yapo zaidi ya 500, ni watu ambao hawana hata hofu ya Mungu hivyo kufukuzwa ni halali yao.
Mhe. Lukuvi ametoa wito kwa viongozi wenzake wanapofanya shughuli za mipangomiji nchini kutenga sehemu za huduma za jamii ikiwemo mahali pa kuzikia kwani kila mtu atakufa na anahitaji kuzikwa.  
“Serikali ya awamu ya Tano tumeamua kurekebisha pote palipokuwa pamepinda ili wananchi wapate haki zao,”alisema Lukuvi.
Aidha amewataka waliokuwa wamemilikishwa wafike wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili wampe Waziri uzoefu wanaoutumia kununua maeneo ya huduma za jamii ikiwemo maeneo ya makaburi ili imsaidie kujua jinsi mtandao ulivyo.
Hati tatu zilizofutwa ni 213, 215 na 217 Kitalu B, Kinyereze, Kata ya Segera jijini Dar es Salaam

RAIS DK. MAGUFULI APOKEA MSAADA WA SH. MILIONI 545 KUTOKA SERIKALI YA INDIA KWA AJILI YA WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI LILILOTOKEA MKOANI KAGERA

September 27, 2016

Rais Dkt. John Magufuli akimshukuru Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya baada ya kupokea mfano wa hundi ya Sh. milioni 545, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Msaada huo umetolewa na Serikali ya India kwa ajili ya kuwasaidia  waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera. Kushoto ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kulia ni Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje Balozi Dk. Aziz Mlima 

 Rais Dk. John Magufuli, Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakitazama mfano wa hundi hiyo 
 Rais Dk. John Magufuli akimshukuru Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Sh milioni 545, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais Dk. John Magufuli akizungumza na  Balozi wa India hapa nchini Sandeep Arya baada ya kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya Sh milioni 545, Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kulia ni Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje Balozi Dk. Aziz Mlima
 Rais Dk. John Magufuli akimkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mfano wa hundi hiyo



Rais Dk. John Magufuli akijadiliana jambo na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa baada ya kupokea msaada wa fedha hizo

DC KONGWA AMTUMBUA MENEJA WA MAMLAKA YA MAJI

September 27, 2016

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi akizungumza wakati wa kikao cha Kumng'oa Meneja wa Mamlaka ya Maji safi na salama Wilyani humo
Watumishi wa Mamlaka ya Maji safi na salama WIlayani Kongwa wakizunguza na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Deogratius Ndejembi

NDEGE YA PILI YA BOMBARDIER Q-400 YAWASILI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

September 27, 2016

Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) ikitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.
Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) ikipata Saluti ya maji (Water Canon Salutation) mara tu baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.
Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) ikiegeshwa karibu na pacha wake iliyofika wiki moja uliopita katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.
NAIBU WAZIRI MASAUNI AFUNGUA MKUTANO MKUU WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI, MJINI GEITA LEO

NAIBU WAZIRI MASAUNI AFUNGUA MKUTANO MKUU WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI, MJINI GEITA LEO

September 27, 2016

bara1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Wadau wa Usalama Barabarani pamoja na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Kulia ni Katibu wa Baraza hilo ambaye pia Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna wa Polisi, Mohamed Mpinga. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Mafunzo na Uenezi wa Baraza hilo, Henry Bantu. Mkutano huo unafanyika leo katika Ukumbi wa wa Mikutano wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Geita. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
bara2
Sehemu ya Wadau na Wajumbe wa Baraza la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote chini wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) katika mkutano wa baraza hilo ambao unajadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Mkutano huo unaenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kanisa Katoliki Jimbo la Geita. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
bara3
Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia Kamanda wa Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna wa Polisi, Mohamed Mpinga akitoa taarifa ya matukio mbalimbali ya ajali za barabarani nchini katika mkutano wa Wadau wa Usalama Barabarani pamoja na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka mikoa yote nchini. Mkutano huo ulijadili masuala mbalimbali ya jinsi ya kupunguza ajali za barabarani nchini. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mhandisi Hamad Masauni, na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Mafunzo na Uenezi wa Baraza hilo, Henry Bantu. Mkutano huo unafanyika katika Ukumbi wa wa Mikutano wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Geita. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MAONYESHO YA FILAMU ZA BEIJING 2016 CHACHU KWA UKUAJI WA SANAA NCHINI

September 27, 2016


 Washindi wa kwanza hadi wa tatu wa mashindano ya sauti waliopatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China wakionesha tuzo baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam leo. Washiriki 10 walishinda mashindano hayo. Kutoka kushoto ni Hilda Malecela, Safiya Ahmed na Sadiq Kututwa.


Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura akisalimiana na mmoja wa washindi 10 wa mashindano ya vipaji vya sauti, Abraham Richard, ambao watakakwenda kufanya kazi makao makuu ya StarTimes jijini Beijing, China wakati wa hafla fupi ya Maonyesho ya Matangazo ya Tamthiliya za Runinga na Filamu za Beijing 2016.

 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Anastazia Wambura akizungumza na washindi hao.

 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,. Anastazia Wambura akiwasisitizia jambo mshindi wa kwanza hadi wa tatu baada ya kuwakabidhi tuzo zao.
 Washindi 10 wa mashindano ya vipaji vya sauti, Abraham Richard, ambao watakakwenda kufanya kazi makao makuu ya StarTimes jijini Beijing, China wakiwa katika picha ya pamoja na kutoka (kushoto) Muwakilishi wa Mamlaka ya Halmashauri ya Beijing, Yang Peili,  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa, Dk. Ayoub Riyoba, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura, Muwakilishi wa Ubalozi wa China nchini,  Guo HaoDong, Makamu wa Rais wa Makampuni ya StarTimes,  Guo ZiQi na Kansela wa Utamaduni katika Ubalozi wa China nchini Tanzania, Gao Wei wakati wa hafla fupi ya Maonyesho ya Matangazo ya Tamthiliya za Runinga na Filamu za Beijing 2016.
 Washindi hao 10 wakifurahia baada ya kukabidhiwa  tuzo.

Na Dotto Mwaibale

STARTIMES  imefanya Maonyesho ya Michezo ya Kuigiza ya Runinga na Filamu za Beijing ya mwaka 2016 kwa mara ya pili jijini Dar es Salaam kwa lengo lakuendelea kukuza ushirikiano wa iutamaduni baina ya China na Tanzania.

Akizungumza wakati wa maonyesho hayo yaliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam leo asubuhi, mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura amesema kuwa kwa muda mrefu serikali ya China na Tanzania zimekuwa na 
mahusiano mazuri katika Nyanja za kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.

“Mahusiano mazuri ya kiutamaduni ndiyo yaliyopelekea serikali hizi mbili kuendelea kushirikiana na kuwa marafiki mpaka hivi leo. Uhusiano huo si tu unatunufaisha katika masuala ya kiuchumi bali pia kijamii. 

Kupitia kazi za sanaa kam vile tamthiliya za michezo ya kuigiza na filamu watu huweza kujua na kujifunza tamaduni za kila upande. 

Nawapongeza StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China nchini Tanzania kwa kutuletea maonyesho haya ambayo nina hakika yatakuwa na manufaa makubwa kwa tasnia yetu.” Alisema . Wambura

“Pia ningependa kuwapongeza StarTimes kwa juhudi zao za dhati katika kukuza utamaduni wetu kuipa nafasi lugha ya Kiswahili kuwa mojawapo inayotumika kutafsiri filamu na tamthiliya hizi za 
michezo ya kuigiza. Nimesikia mlifanya shindano la vipaji vya sauti ambapo watanzania kumi walipatikana na watakwenda kufanya kazi katika makao yenu makuu yaliyopo Beijing. 

Hii ni hatua nzuri na jambo la kuigwa kwa kukipa Kiswahili nafasi kubwa. Ninegependa kumalizia kwa kutoa wito kwa washindi waliopatikana kwenda huko China kutuwakilisha vema kama mabalozi wetu na kukifanya Kiswahili kiendelee kutambulika zaidi.” alisema Wambura

Akielezea umuhimu wa maonyesho hayo Makamu wa Rais wa Makampuni ya StarTimes,. Guo ZiQi amebainisha kuwa kihistoria China imedumisha kwa dhati urafiki na mataifa ya Afrika na kushirikisha tamaduni ndio njia madhubuti itakayoenzi mahusiano hayo.

‘’Utofauti ndio unaofanya dunia pawe mahala pazuri pa kuishi na China na Tanzania kwa muda mrefu zimedumisha utamaduni wao unaovutia zaidi. Katika kilele cha mkutano wa jukwaa la ushirikiano baina ya China na Afrika uliofanyika mwaka 2015, Rais wa Jamhuri ya watu wa China, 

 Xi Jinping alionesha nia ya kujizatiti katika kudumisha mahusiano mazuri ya kiutamaduni, kuimarish mafunzo baina ya China na Afrika ili kusonga mbele kwa pamoja na vilevile kuhakikisha mustakabali wa ukuaji wa urafiki baina ya China na Afrika.’’Alisema  ZiQi

‘’Kwa kuendelea kukua kwa mahusiano ya maingiliano ya kiutamaduni baina ya watu wa China na Waafrika, michezo ya kuigiza ya runinga na filamu za Kichina imezidi kujizolea umaarufu na kuwa kichocheo muhimu katika kujenga mahusiano baina ya pande hizo mbili. Kwa hivi sasa Beijing inaongoza China katika uzalishaji wa michezo ya kuigiza ya runinga na filamu. 

Mpaka hivi sasa ina taasisi takribani 3,400 zilizojikita katika uzalishaji wa filamu na vipindi vya uninga na uendeshaji, vikiwa tayari vimekwishazalisha zaidi ya mfululizo wa vipindi vya runinga 3,000 na karibuni filamu 300 kwa mwaka.’’ alisema ZiQi

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Teknolojia na Ufundi ambaye alizungumza kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Wang Xiabo alisema kuwa,‘’mnamo mwaka 2014, Halmashauri ya Mamlaka ya Uandishi wa Habari, Uchapishaji, Redio, Filamu na Runinga ya Beijing ilishirikiana na StarTimes kuzindua msimu wa Maonyesho ya Michezo ya Kuigiza ya Runinga na 
Filamu za Beijing katika nchi za Kiafrika. Lengo kubwa lilikuwa ni kuleta simulizi nyingi za Kichina barani Afrika na kukuza uhusiano katika tasnia za filamu na runinga baina ya pande mbili.’’


‘’Maonyesho haya yamefanyika kwa mafanikio makubwa kwa miaka ya 2014 na 2015 mfululizo. Filamu maarufu za Kichina na mfululizo wa michezo ya kuigiza ya runinga  ambayo imeingizwa sauti kwa lugha ya Kiingereza, Kifaransa na lugha nyinginezo tano za Kiafrika zilionyeshwa na StarTimes kwa miaka hiyo iliyopita,’’ alisema Wang Xiabo kuwa,‘’Katika kipindi hiko tamthiliya kama zilipata mapokezi makubwa sana kutoka kwa hadhira ya barani Afrika.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji waTaifa (TBC),  Ayoub Riyoba, ambao ni washirika wa kampuni ya StarTimes katika urushaji wa matangazo ya dijitali nchini Tanzania amebainisha umuhimu wa filamu hizo hususani katika ukuzaji wa tamaduni baina ya nchi hizo mbili.

‘’Tanzania na China zina historia ndefu ya mahusiano tangu enzi hizo za waasisi wa mataifa haya. Nchi hizi mbili zimekuwa zikishirikiana kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Sisi kama chombo cha habari cha taifa tumekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa tunasaidia jitihada za 
serikali kukuza na kuutangaza utamaduni wetu hususani lugha ya Kiswahili. Kwa takribani miaka miwili iliyopita TBC imekuwa ikionyesha tamthiliya za Kichina zilizoingiziwa sauti kwa lugha ya Kiswahili. 

Kwa kufanya hivyo hivyo tamthiliya hizo zimeonyesha kupokewa vizuri na kupendwa sana na watanzania kwani wamekuwa wakielewa kinachoonekana.’’ alisema Riyoba

‘’Mbali na kukuza lugha yetu ya Kiswahili nchini na nje yanchi, hii pia ni fursa kwa tasnia yetu ya filamu kujifunza kutoka kwa wenzetu ambao wamepiga hatua zaidi. Tasnia yetu bado ni change na inahitaji mengi ya kujifunza ili kusonga mbele na kufikia pale walipo wenzetu na kuwa inazalisha kazi nyingi zaidi za sanaa. 

Ningependa kuchukua fursa hii kuipongeza na kuishukuru serikali ya China kwa jitihada zao wanazozionyesha katika kukuza filamu na lugha yetu ya Kiswahili. Na ningependa kuwaahidi kutokana na ushirikiano huu watazamaji wa TBC wataendelea kupata burudani ya tamthiliya 

na filamu nzuri zaidi ya zilizopita.’’  alisema Mkurugenzi Mkuu wa TBC katika maonyesho hayo Ubalozi wa China nchini Tanzania pia ulikabidhi mfano wa hati za makubaliano ya kwenda kufanya kazi 
jijini Beijing kwa washindi 10 waliopatikana katika shindano la vipaji vya sauti lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

Washindi hao 10 waliopatikana ni; Hilda Malecela(DSM), Safiya Ahmed(ZNZ), Saiq Kututwa(ZNZ), Mathew Philip Mgeni(Arusha), Maisala Abdul(DSM), Rukia Hamdan(ZNZ), Richard Rusasa (DSM), Happiness Stanslaus - Nyamayao (DSM), Jamila Hassan(DSM) na Abraham Richard (DSM).



LHRC WASHEREHEKEA MIAKA 21 NA WATOTO WANAOISHI MAKAO YA TAIFA YA WATOTO WENYE SHIDA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM

September 27, 2016
Wafanyakazi wa LHRC wakijumuika na watoto wanaolelewa katika Makao ya taifa ya watoto wenye shida Kurasini jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 21 tangu kuanzishwa kwake.
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Dk. Helen Kijo-Bisimba (katikati) akiwasaidia watoto kukata keki kusheherekea miaka 21 ya LHRC.
Ofisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida Kurasini, Beatrice Lawrance, akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo.



Na Dotto Mwaibale

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)  kimeiomba serikali kupitia wizara ya Afya ,Jamii Jinsia ,Wazee na Watoto, pamoja na na Wizara ya Katiiba na Sheria ,kufanya marekebisho yaSsheria ya Mtoto  nakutilia mkazo malezi bora ya watoto ikiwemo kuweka kipengele kitakacho toa  adhabu kali  kwa familia itakayo shindwa kutoa malezibora kwa watoto au kutelekeza familia.

Akizungumza katika maadhimisho ya  miaka 21 ya kituo cha sheria na haki za binadamu, yaliyofanyika katika Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida kilichopo Kurasini, Temeke Jijini Dar es salaam,  Mkurugenzi Mtendaji wa  kituo hicho Dk. Helen Kijo-Bisimba alisema kuboreshwa kwa sheria hizo kutasaidia kupunguza wimbi la watoto wasio na makao maalumu  wanao zagaa kuomba omba mitaani, na ameitaka jamii  kushiriki katika kutatua tatizo la watoto wa mitaani linalozidi kushika hatamu kila siku.


Ofisa Mfawidhi wa kituo  hicho,  Beatrice Laurence  ame kishukuru kituo cha sheria na haki za Nina damu kwakuona umuhimu wa kutoka misaada katika kuwa saidia watoto wanao lelewa  hapo  nakuwataka watanzania wengine  badala ya kuelekeza nguvu zao  pekee kwa wathirika wa tetemeko huko Kagera  kuwa kumbuka na  watoto yatima kwani nao  wanayo kahitaji ya kibinadamu.


Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kilianzishwa Septemba 26, 1995 kwa lengo la kufanya utetezi kwa watu wenye uhitaji sambamba na kulinda haki za binadamu nchini.