DK. KESSY AWAPIGA MSASA WASIMAMIZI WA MASHAMBA YA MKIKITA NCHINI
Daktari wa Mifugo na Kilimo, Dk. Aloyce Kessy akitoa mafunzo ya jinsi ya kuandaa vitalu vya miche ya papai katika kikao cha mpango kazi kwa watalaamu wa kilimo wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA) watakaokuwa wanasimamia mashamba makubwa yaliyoanzishwa na mtandao huo maeneo ya Ruaha mkoani Iringa, Kibaha na Vikindu mkoani Pwani. Kikao hicho kimefanyika leo eneo la Goba, Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Dk. Kessy akifafanua jambo wakati wa kikao hicho. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mtandao huo, Dk. Kissui S Kissui na Mkurugenzi wa Miradi na Maendeleo ya Biashara wa Mkikita, Edwin Mkwanga
Washiriki wakisikiliza kwa makini wakati Dk. Kessy akitoa mafunzo hayo
Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange akiwaelea watalaaamu hao kuhusu majukumu yao
Watalaamu wa kilimo wa Mkikita wakiwa makini kusikiliza maelekezo ya jinsi ya kuboresha kilimo cha papai
TAMASHA LA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA ARUSHA KUFANYIKA KESHO
wakwanza kulia ni Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha, Mussa Juma katikati ni Mwenyekiti wa TASWA Arusha, Jamila Omar akioongea na waandishi wa habari |
Na Woinde Shizza,Arusha
Tamasha
la waandishi wa habari, kanda ya kaskazini, linatarajiwa kufanyika
jumapili, octobar 15 katika uwanja wa General Tyre ambapo mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
Katika
tamasha hilo, ambalo litashirikisha wanahabari zaidi ya 500, kutoka
mikoa ya Arusha, Tanga, Manyara na Kilimanjaro,limedhaminiwa na shirika
la hifadhi za Taifa(TANAPA) Mifuko ya hifadhi ya Jamii ya LAPF na PSPF,
Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, kampuni ya vinywaji baridi ya Coca
cola na kampuni ya ya vinywaji baridi ya SBC (T) Limited na Palace
Hoteli.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari,
Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha, Mussa Juma, alisema tamasha hilo,
limeandaliwa na TASWA kwa kushirikiana na kampuni ya Arusha media na
maandalizi yote yamekamilika.
Juma alisema katika tamasha
hilo, bingwa atazawadiwa kikombe na fedha taslimu jumla ya shilingi
500,000, mshindi wa pili fedha taslimu 100,000 na kwa upande wea mpira
wa pete mshindi ni kikombe na fedha taslimu jumlaya sh 300,000 na
mshindi wa pili sh 50,000.
Alisema pia kutakuwa na michezo
ya mbio za magunia, kuvuta kamba, mbio za vijiko, riadha na masumbwi
ambapo tayari waambuzi wanaotambuliwa na mashirika mbali mbali ya
michezo watakuwepo.
Hata hivyo, alisema wadhamini wengine
wa tamasha hilo wanatarajiwa kutangazwa, ili kuhakikisha wanahabari
wanaburudika ambapo pia kuwa kuwa na benki maalum ambayo itatumnbuiza
siku za tamasha.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa TASWA
Arusha, Jamila Omar alitoa wito kwa wanahabari wote na familia zao
kujitokeza katika tamasha hili ambalo hufanyika kila mwaka mkoani
Arusha.
Alisema kauli mbio ya tamasha hilo, ambalo
linaendama na maadhimisho ya kumbukumbu ya mwalimu nyerere ni michezo ni
ajira, michezo ni kazi tufanye kazi kwa bidii kuunga mkono jitihada za
serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda.
Mratibu
wa Tamasha hilo, Andrea Ngobole alizitaja timu ambazo zitashiriki kuwa
ni TASWA Dar es Salaam, Triple A,RadioSunrise , chuo cha uandishi habari
cha Arusha(AJTC)timu ya Arusha One Fm, TASWA Arusha,Radio ORS ya
Manyara ,NSSF na timu ya Wazee Klabu.
KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAKULA LAFANA MKOANI GEITA
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akizungumza wakati wa kongamano katika maadhimisho ya siku ya Chakula ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita wakifatilia kwa makini mada mbalimbali zikiwasilishwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akizungumza
wakati wa kongamano katika maadhimisho ya siku ya Chakula ambayo Kitaifa
yanafanyika Mkoani Geita.
Mchambuzi na mshauri wa sera katika Wizara
ya kilimo Ndg Revelian Ngaiza Akiwasilisha mada kuhusu mchango wa sera za kilimo
katika mageuzi ya uchumi wa viwanda wakati wa kongamano la maadhimisho ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Meneja wa Muendelezo wa wakulima wadogo TADB Ndg Joseph Mabula Akiwasilisha
mada kuhusu Mikopo nafuu kwa mapinduzi ya kilimo na viwanda wakati wa kongamano la maadhimisho
ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Afisa uendeshaji Mwandamizi Utoaji Mikopo na kudai madeni Kutoka Mfuko wa Pembejeo Ndg Joshua Kalab akiwasilisha mada kuhusu Mchango wa mfuko wa pembejeo
katika kuongeza uzalishaji wa chakula, kupambana na njaa na kupunguza umasikini
hususani vijijini wakati wa kongamano la maadhimisho
ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano serikalini kutoka Wizara ya Kilimo Ndg Issa Sabuni akichangia mada wakati wa kongamano la maadhimisho
ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Katibu wa Chama cha Biashara Tanzania Mkoa wa Kagera (TWCC) Bi Paskazia Sebastian akichangia mada wakati wa kongamano la maadhimisho
ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Afisa Mfawidhi kutoka Taasisi ya udhibiti wa mbegu TOSCI Mkoa wa Mwanza Ndg Ngura Joseph Akiwasilisha
mada kuhusu Mchango wa mbegu bora katika usalama wa chakula wakati wa kongamano la maadhimisho
ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
Afisa Kilimo Mkuu kutoka Wizara ya kilimo Bi Mwanaid Kiya Akiwasilisha
mada kuhusu Sumu kuvu kwenye mahindi: Madhara katika sekta ya kilimo, Biashara na afya ya binadamu wakati wa kongamano la maadhimisho
ya siku ya Chakula Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika Mkoani Geita.
BONANZA LA MICHEZO JIJINI TANGA LAHUDHURIWA NA MAMIA YA WAKAZI WA JIJI HILO
Wananchi wa mkoa wa Tanga wakishuhudia uhondo wa michezo mbalimbali katika bonanza hilo
Wachezaji wa timu ya mpira wa pete ya chuo cha Utumishi Mkoani Tanga wakitoka uwanjani mara baada ya mechi yao kumalizika |
Wachezaji wa timu ya Maveterani ya Tanga Middle Age wakipasha kabla ya kuwavaa wapinzani wao Kilombero Veterani ambapo Tanga Middle Age walishinda kwa bao 1-0 |
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kulia akitoa elimu kwa mkazi wa Jiji la Tanga aliyetembelea banda lao waliloweka kwenye bonanza hilo kwa lengo la kuhamasisha jamii kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na matibabu
Wachezaji wa timu za maveterani wakichuana katika Bonanza hilo ambalo lilikuwa la aina yake kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani Mjini Tanga ambalo liliandaliwa na kituo cha Radio cha Jijini Tanga (TK)
Mashabiki wa michezo wakifuatilia kwa umakini bonanza hilo
Afisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Denis Kapinga akitolea ufafanuzi baadhi ya huduma wanazozitoa wakati wa bonanza hilo
Mamy Mohamed ambaye ni Meneja wa Kituo cha Radio cha TK FM ya Jijini Tanga akitoa utaratibu wa zawadi kwa washindi mara baada ya kumalizika bonanza hilo
Mkurugenzi wa Radio TK ya Jijini Tanga,Saidi Othumani kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel
Ally Choki mzee wa Farasi kulia akiwa na Luiza Mbutu kwenye jukwaa wakitumbuiza katika Bonanza la Michezo ambao liliandaliwa na Radio TK FM ya Jijini Tanga
Wasanii wanaounda Bendi ya Twanga Pepeta wakitumbuiza Jukwaani
Wasanii wanaounda Bendi ya Twanga Pepeta wakitumbuiza Jukwaani
Baadhi ya washiriki waliojitokeza katika bonanza hilo wakipiga picha ya pamoja
RAIS DKT MAGUFULI AONGOZA SHEREHE ZA KUZIMA MWENYE, NYERERE DAY NA WIKI YA VIJANA ZANZIBAR LEO
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikvishwa
skafu baada ya kuwasili kuongoza sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa
uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana katika uwanja wa
Amaan mjini Zanzibar leo Oktoba 14, 2017
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana
na mwakilishi wa familia ya Mwalimu, Mhe. Makongoro Nyerere wakati
akiwasili kwenye sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa uhuru,
Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana katika uwanja wa Amaan
mjini Zanzibar leo Oktoba 14, 2017.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa
Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
wakiteta jambo wakati wa sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa uhuru,
Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana katika uwanja wa Amaan
mjini Zanzibar leo Oktoba 14, 2017.
Vijana
wa Halaiki wakitumbuiza kwenye sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa
uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana katika uwanja wa
Amaan mjini Zanzibar leo Oktoba 14, 2017.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea
Mwenge wa uhuru wakati wa sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa
uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana katika uwanja wa
Amaan mjini Zanzibar leo Oktoba 14, 2017.
Subscribe to:
Posts (Atom)