Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola awasili Mjini London

March 12, 2015

Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mhe. Bernard Membe na ujumbe wake kwenye mazungumzo ya kikazi na Mhe. James Duddridge, Waziri wa Masuala ya Afrika wa Uingereza mara baada ya kuwasili London Jumatano tarehe 11/03/2015.


Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mhe. Bernard Membe mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege Jijini London na kupokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe. Peter Kallaghe na Naibu Mkuu Mkuu wa Ubalozi Msafiri Marwa (wa pili kushoto) na Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy.
Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Mhe. Bernard Membe akiwa na Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola Mhe. Kamalesh Sharma kabla ya kuanza kikao cha faragha.

Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mhe. Bernard Membe na ujumbe wake wakiwa kwenye kikao cha kazi na Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola Mhe. Kamalesh Sharma Jumatano tarehe 11/03/2015.
Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Mhe. Bernard Membe akiwa na Waziri wa Masuala ya Afrika wa Uingereza Mhe. James Duddridge baada ya kuwasili Jijini London kwa ajili ya kikao cha kazi cha Jumuiya ya Madola tarehe 11-12 Machi 2015.

KAMATI YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA(LAAC) YATEMBELEA SKIMU YA UMWAGILIAJI YA MANGORA WILAYANI KARATU

March 12, 2015

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa,(LAAC) ikitembelea kukagua mradi wa umwagiliaji wa Skimu ya Mang'ora wilayani Karatu.
Baadhi ya Mashamba ya Vitunguu katika skimu ya umwagiliaji ya Mang'ora.
Watoto wakiwa wamebeba mazao wakitoka katika moja ya mashamba yaliyoko katika skimu hiyo.
Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa,Azza Hamad akiongozwa kuvuka katika mfereji wa maji katika Skimu ya Umwagiliaji ya Mang'ora wilayani Hai.
Mtoto akivusha mifugo yake katika mfereji wa maji ulioko katika skimu ya umwagiliaji ya Mang'ora.
Mfereji wa maji uliojengwa katika skimu ya Mang'ora kwa fedha za serikali ambao hata hivyo hautumiki. 
Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa,Azza Hamad akitizama mfereji wa maji katika skimu ya Maji ya Mang'ora iliyojengwa kwa fedha za serikali ambao hata hivyo hautumiki.
Mifereji ya maji ambayo imekuwa ikitumika kupeleka maji kwenye mashamba licha ya uwepo wa mfereji uliojengwa katika eneo hilo ambao hata hivyo hautumiki.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa wakiwa na wakulima wanao tumia maji katika skimu ya umwagiliaji ya Mang'ora iliyopo wilayani Karatu.
Katibu wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Dickson Bisire akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya kamati hiyo iliyofanyika wilayani Karatu.
Baadhi ya Madiwani wa Halamashauri ya wilaya ya Karatu wakiwa katika kikao hicho.
Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa wakiwa katika kikao hicho cha mwisho.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu akiwa na Mwenyekiti wa Halamashauri ya wilaya ya Karatu Lazaro Titus wakimsikiliza mwenyekiti wa Kamati hiyo wakati akitoa maazimio ya Kamati hoyo mara baada ya kumaliza ziara hiyo.
Mwenyekiti wa LAAC,Azza Hamad akitoa maazimio ya kamati mara baada ya ziara.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Karatau Lazaro Titus akizungumza jambo wakati wa kikao cha majumuisho cha kamati ya LAAC kilichofanyika katika Hotel ya Flamingo mjini Karatau. 
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Kampuni ya Push Mobile Media yazindua huduma ya kurahisha mawasiliano

Kampuni ya Push Mobile Media yazindua huduma ya kurahisha mawasiliano

March 12, 2015

 2
Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya Push Mobile Media Limited, Ezekiel Mukundi (Kulia) akielezea umuhimu wa  huduma  ya “online bulk Messaging’ kwa sekta mbalimbali. Kushoto ni Daniel Buchafwe ambaye ni Mkuu wa Idara ya Ufundi.
1
Mkurugenzi Mtendaji wa Push Mobile Media, Freddie Manento akifafanua jambo kuhusiana na huduma ya ‘Online Bulk Messaging’ inavyofanya kazi. Huduma hiyo itamwezesha mtumiaji kutuma ujumbe mmoja kwa watu wengi na katika muda muafaka.
……………………………………….
Na Mwandishi wetu
Kampuni inayoongoza kwa huduma ya teknolojia ya mawasiliano, Push Mobile Media imezindua huduma ya ujumbe kwa njia ya mtandao wa internet ijulikanyo kwa jina la “Bulk Messaging” kwa lengo la kumwenzesha mtumiaji kufikisha ujumbe mmoja kwa watu wengi na katika muda muafaka.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Push Mobile Media, Freddie Manento alisema kuwa huduma hiyo itamwezesha mtumiaji kufikisha ujumbe muhimu kwa gharama nafuu ikiwa katika sekta mbalimbali na kwa mtu binafsi.
Manento alisema kuwa lengo kubwa ya kuanzisha huduma hiyo ni kuwawezesha wafanyabiashara na sekta nyingine kufanya mawasiliano ya haraka zaidi na kujitangaza.
“Kama ni mfanyabiashara, utaweza kujitangaza pia kwani wateja watapata taarifa muhimu utakazo wapa kwa muda muafaka na wao kuutumia katika maendeleo ya biashara zao,” alisema Manento.
“Ili kupata huduma hiyo, unatakiwa kujiunga kupitia mtandao wetu,  www.pushgw.com  na kufungua akaunti yako,” alisema Manento.
Alisema kuwa makampuni au taasisi yanaweza kutumia huduma hii kuwapa taarifa wafanyakazi, wateja wao kuhusiana na biashara na taarifa nyingine.
“Kwa watu binafsi, unaweza kutumia huduma hii kutoa taarifa za shughuli mbalimbali ikiwa pamoja na harusi na hata kwa waandishi wa habari wanaweza kutumia taarifa hii kwa lengo la kuwasiliana na wahariri wao kwa kile wanachokifanya katika sekta hiyo,” alisema.
Mkuu wa Idara ya Mauzo na Masoko wa Push Mobile Media Limited Ezekiel Mukundi alisema kuwa huduma hiyo ni rahisi kwani mtumiaji anaweza kutuma ujumbe kwa kiasi cha sh 16 kwa kutegemea na ukubwa wa ‘bando’ analotaka.
Alisema kuwa kwa upande wa sekta ya afya, huduma hii inawezwa kutumiwa na madaktari kuwakumbusha wagonjwa kuhusiana na siku ya kupata matibabu.
“Unachotakiwa kufanya ni kujiunga  na huduma hii kwa njia ya mtandao na kuweka namba za simu ya mkononi kwa watu wanaotakiwa kupata taarifa na kutuma, watapata kwa haraka zaidi na kwa muda unaofaa,” alisema Mukundi.
Ziara ya Waziri Mahenge Wilayani Chunya Mkoani Mbeya

Ziara ya Waziri Mahenge Wilayani Chunya Mkoani Mbeya

March 12, 2015

1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Mheshimiwa Binilith Mahenge akisiliza jambo kutoka kwa Mwenyeji wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bwana Abas Kandoro kabla ya kuanza Ziara yake ya siku mbili Mkoani humo jana. (Picha na OMR)
002
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Mh. Binilith Mahenge (katikati), wakijadili jambo na Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mh. Deodatus Kinawito (kushoto) pamoja na Diwani wa Kata ya Mkugani ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Mh. Bosco Mwanginde (kulia) wakati wa Ziara ya Waziri Mahenge Wilayani humo jana.
004
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Mh. Binilith Mahenge, akionesha Bwawa linalotumika kuhifadhi Maji-taka yenye Sumu kutoka kwenye Mgodi wa Sunshine uliopo Wilayani Chunya Mkoani Mbeya jana, huku akiwataka Wawekezaji wa Mgodi huo kuboresha Bwawa hilo ili kukidhi Kanuni za Mazingira za Tanzania . 
005
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Injinia Binilith Mahenge akisaini Kitabu cha Mahudhurio ya Wageni mbele ya Mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bwana Abas Kandoro, kabla ya kuanza ziara yake Mkoani humo jana .
1111
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Injinia Binilith Mahenge (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi Msaidizi wa Machimbo ya Dhahabu katika Mgodi wa Sunshine uliopo Wilayani Chunya, Bwana Andy Wu (kulia), katika ziara ya Mazingira Mgodini humo jana na wakati katika picha ni Diwani wa Kata ya Mkugani ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chunya, Mh. Bosco Mwanginde.