WAZIRI KAIRUKI AZINDUZA MAFUNZO UONGOZI KWA MAOFISA WA POLISI

WAZIRI KAIRUKI AZINDUZA MAFUNZO UONGOZI KWA MAOFISA WA POLISI

April 22, 2017
unnamed
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala bora Mhe.Angelah Kairuki akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Mafunzo ya Uongozi kwa Maofisa wa wa Jeshi la Polisi Mjini Dodoma.Mafunzo hayo yanaendeshwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini Finland.Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi Balozi Simba Yahaya
A
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Mafunzo ya Uongozi kwa Maofisa wa Jeshi la Polisi Mjini Dodoma.Mafunzo hayo yanaendeshwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini Finland.Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala bora Mhe.Angelah Kairuki na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja.
A 1
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala bora Mhe.Angelah Kairuki akizindua Programu ya Mafunzo ya Uongozi kwa Maofisa wa wa Jeshi la Polisi Mjini Dodoma yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini Finland.Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu na kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja.
 
A 2
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala bora Mhe.Angelah Kairuki (katikati), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu wakionyesha Vitabu vyenye Programu ya Mafunzo ya Uongozi kwa Maofisa wa Jeshi la Polisi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini Finland mjini Dodoma leo.Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo Maofisa wa Polisi katika Uongozi.
 
A 3
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala bora Mhe.Angelah Kairuki, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba na Viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na  Maofisa wa Jeshi la Polisi waliopo katika Mafunzo ya Uongozi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini Finland.Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo Maofisa wa Polisi katika Uongozi ambapo baada ya kuhitimu watatunukiwa “Post-Graduate Diploma in Leadership”
 
A 4
Baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Polisi waliopo katika Mafunzo ya Uongozi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini Finland.Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo Maofisa wa Polisi katika Uongozi ambapo baada ya kuhitimu watatunukiwa “Post-Graduate Diploma in Leadership”.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFANYA MAZUNGUMZO NA KAMISHNA MKUU WA TRA

April 22, 2017
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) Bw. Charles Kichere (kushoto) aliyemtembelea leo ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Charles Kichere (kushoto)ambaye aliongozana na Mkurugenzi wa Elimu ya Mlipa Kodi TRA Bw. Richard Kayombo (kushoto), Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Afisa Mahusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato (TRA)Tanzania Bi. Mariamu Mwayela mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Charles Kichere.
                                              …………………………………………………..

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amemwagiza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere ahakikishe anaweka utaratibu wa kukutana na wafanyabiashara mara kwa mara kama njia ya kujadili na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara hao.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere kuhusu namna bora ya kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara nchini kama hatua ya kuongeza kasi ya ukusanyaji wa kodi wa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Makamu wa Rais ameonyesha kusikitishwa na baadhi ya Maafisa wa TRA kuwanyanyasa wafanyabiashara na wengine kuwabambikizia kodi kubwa hali ambayo inazua malalamiko mengi kutoka kwa wafanyabiashara hao jambo ambalo amesema ni muhimu likatafutiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.
Amesisitiza kuwa ni muhimu kama TRA itafanya mabadiliko yeyote ya ulipaji wa kodi ikawafahamisha wafanyabiashara hao mapema ili kuondoa usumbufu mkubwa unaoweza kutokea katika ulipaji wa kodi pindi wanapoagiza bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi.
Makamu wa Rais amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha ulipaji wa kodi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa unafanyika kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu na sio kuwakandamiza Watanzania kwa kuwalipiza kodi mara mbili jambo ambalo amesema halifai hata kidogo.
Makamu wa Rais amemtaka Kamishna wa TRA kukomesha mara Moja tabia ya baadhi ya Maafisa wa mamlaka hiyo kutoa lugha chafu na kuudhi kwa wafanyabiashara bali watumie lugha nzuri ili kuhamasisha wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiyari bila kulazimishwa na mtu.
Makamu wa Rais pia ameipongeza TRA kwa kazi kubwa inayoifanya katika ukusanyaji wa mapato na amewapa moyo wa kuongeza bidii katika ukusanyaji wa kodi hizo ambazo Serikali inatumia katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali nchini.
Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa TRA nchini Charles Kichere amemuahidi Makamu wa Rais kuwa atafanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha malalamiko mbalimbali yanayotolewa na Wafanyabiashara yanapata ufumbuzi haraka iwezekanavyo.
Kamishna Kichere amesisitiza kuwa kwa baadhi ya maafisa wa Mamlaka hiyo wanaokiuka maadili ya kazi ataendelea kuwachukulia hatua stahiki ili kurejesha nidhamu katika utendaji wa kazi na ukusanyaji wa mapato.

MKUU WA MKOA WA TANGA AKOLEZA VITA YA MADAWA YA KULEVYA

April 22, 2017

 MKUU wa Mkoa wa Tanga, Martin Shighela, amesema vita ya madawaya kulevya inaendelea hivyo kuviagiza vikosi vya ulinzi na usalama kuhakikisha inawakamata vinara wa wasafirishaji na wauzaji.
Akizungumza katika hafla ya fupi ya makabidhiano ya jengo la Afya ya Akili Hospitali ya Rufaa ya Bombo lililokarabatiwa na Kituo cha Tanga International Comperence Centre (TICC), Shighela alisema vita ya madawa itakuwa endelevu.
Alisema vijana wengi wamekuwa wakiathirika na matumizi ya madawa ya kulevya na Taifa kukosa nguvu kazi ya kuleta maendeleo na kuviagiza vyombo vya  ulinzi na usalama kuhakikisha Tanga hakuna njia ya upitishaji.
“Kuna wagonjwa wa akili kutokana na maumbile yao lakini kuna wagonjwa wengine wa akili wa kujitakia ambao sababu zake ni matumizi ya madawa ya kulevya” alisema Shighela na kuongeza
“Ili kuwaokoa vijana wetu na kupunguza nguvu kazi naviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuongeza nguvu ya mapambano ya madawa ya kulevya” alisema
Kwa upande wake Balozi wa Norway hapa nchini, Hanne-Marie Karstand, amewataka watumishi wa hospitali ya Bombo kulitunza jengo hilo kama ilivyo matumizi yake.
Alisema Serikali ya Norway itaisaidia Tanzania katika Nyanja mbalimbali za kijamii ikiwemo Afya, elimu,  Mazingira pamoja na wagonjwa wa Afya ya  Akili.
“Niuombe uongozi wa hospitali ya Bombo kulitunza jengo hili kwa kutumika matumizi yake kama ilivyokusudiwa, Norway itaisaidia Tanzania kila ambapo kunahitajika msaada” alisema
Nae Mganga Mkuu wa Mkoa, Asha Mahita, alisema awali wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosa uwezo wa kuwasafirisha wagonjwa kwenda vituo vinavyotoa huduma za Afya ya akili.
Aliwataka wafadhili wengine kuiga mfano wa Norway kuisadia hospitali hiyo kutokana na changamoto ambazo imekuwa ikabiliana nazo.






Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shighela (katikati), Balozi wa Norway wa kwanza kulia, Hanne-Marie Karstand na Mganga Mkuu wa Mkoa, Asha Mahita (kushoto) wakifungua jengo la Afya ya Akili hospitali ya Rufaa ya Bombo lililokarabatiwa na kituo cha Tanga International Comperence Centre Tanga

Habari kwa hisani ya blog ya kijamii ya tangakumekucha 0655 902929
DIAMONDPLUTNAMZ AZINDUA PAFYUM YAKE AINA YA (CHIBU), YAINGIA RASMI KWENYE SOKO, KUPATIKANA MADUKA YOTE YA GSM

DIAMONDPLUTNAMZ AZINDUA PAFYUM YAKE AINA YA (CHIBU), YAINGIA RASMI KWENYE SOKO, KUPATIKANA MADUKA YOTE YA GSM

April 22, 2017
9
Mwanamuziki Naseeb Abdul aka Diamond Plutnamz akiwasili kwenye maduka makubwa ya GSM Mall Barabara ya Nyerere leo tayari kwa kuzindua Pafyum yake inayoitwa (CHIBU), Diamond akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo amesema ameamua kuingia kwenye soko la kutengeneza pafyum zenye nembo yake CHIBU ili kusaidia serikali katika suala zima la kutatua changamoto ya uhaba wa ajira nchini.
Ameongeza kwamba kuanza kutengenezwa na kuuzwa kwa pafyum hizo kutaongeza ajira kwa vijana wengi lakini pia kutasaidia kukuza uchumi wa nchi kupitia kodi zitakazotozwa kutokana na bidhaa hiyo ambayo wanaume na wanawake wote wanaweza kuitumia, Pafyum ya CHIBU itapatikana katika maduka yote ya GSM na itauzwa bei ya rejareja kiasi cha shilingi 105.000 kwa moja.
Katika mkakati mwingine wa soko Meneja wa Msanii huyo Bw. Salaam Mendes amesema wako katika mazungumzo na mashirika kadhaa likiwemo shirika la ndege la Kenya Airways kwa ajili ya kuitangaza bidhaa hiyo na kuifikisha kwenye soko la kimataifa ikiwa ni pamoja na kuuzwa katika maduka makubwa kwenye viwanja vya ndege katika nchi mbalimbali ambako ndege za shirika hilo zinafika
11
Mwanamuziki Naseeb Abdul aka Diamond Plutnamz akizungumza na waandishi wa habari wakati akizindua Pafyum hiyo kulia ni Mmoja wa Mameneja wake Babu Tale.
12
Mmoja wa mameneja wa Diamond Plutnamz akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa bidhaa hiyo.
13
Mwanamuziki Naseeb Abdul aka Diamond Plutnamz akionyesha Pafyum ya CHIBU ambayo ndiyo kwanza imeingia sokoni.
14 15
Meneja wa Diamond Plutnamz Bw. Salaam Medes akizungumza mara baada ya kuzindua pafyum hiyo kwenye duka kubwa la GSM Mall barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam leo.
16
Mwanamuziki Naseeb Abdul aka Diamond Plutnamz akionyesha chupa ya pafyum ya CHIBU aliyoizindua leo jijini Dar es salaam.
17
Mwanamuziki Naseeb Abdul aka Diamond Plutnamz akimkabidhi chupa ya Pafyum Aisha Azori mteja wake wa kwanza aliyenunua bidhaa hiyo kwenye maduka ya GSM Mall jijini Dae salaam.
18
Bw. Salaam Mendes akitaja bei ya pafyum hiyo kwa waandishi wa habari mara baada ya kuizindua rasmi leo jijini Dar es salaam.

NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA NISHATI NA MADINI, DKT. JULIANA PALLANGYO ATEMBELEA MIRADI YA TANESCO KINYEREZI

April 22, 2017


NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt, Juliana Palangyo, (pichani anayezungumza), ametembelea miradi ya kuzalisha umeme wa  Gesi Asilia ya upanuzi wa Kinyerezi I pamoja na ule wa Kinyerezi II.
Akizungumza katika ziara yake ya kukagua miradi hiyo, Dkt Pallangyo ameridhishwa sana na jitihada zinazofanywa na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO),  katika kuhakikisha Miradi hiyo inakamilika kwa wakati, ambapo mpaka sasa ujenzi wa mradi wa kinyerezi II umefikia asilimia 53%.
“Niwapongeze sana TANESCO kwa jitihada kubwa mnazozifanya katika kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa wakati, ambapo mmewezesha Majenereta 8 yenye jumla ya Megawati (MW) 240 mpaka sasa yameshafika, hii  ni hatua nyingine kubwa sana ,hivyo  kupitia Mradi huu wa kinyerezi nina amini Tanzania ya Viwanda inawezekana”.
Akielezea maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Kinyerezi II, Meneja wa Kituo hicho Mhandisi Steven Manda alisema kuwa kituo hicho kinaendelea vizuri na ujenzi katika kuhakikisha kinakamilika Desemba 2018, ambapo mpaka sasa ukamilifui wa Mradi huo unategemea Kinyerezi I kutokana na Baadhi ya mitambo kuingiliana hasa mitambo ya mfumo wa upozaji  maji  ambao utaunganishwa na mtambo wa Kinyerezi I.
Naye Kaimu meneja wa Kituo cha Kinyerezi I Mhandisi Lucas Busunge amesema kuwa Mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 150, Umeongezewa uwezo wa kuzalisha Megawati zingine 185 ikiwa ni Awamu ya pili ya upanuzi wa Mradi huo.

Kwa ujumla miradi yote miwili itakapokamilika, jumla ya Megawati 575MW za umeme utokanao na Gesi Asilia, zitazalishwa na kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa na hivyo zitasaidia kuongeza upatikanaji wa Umeme wa Uhakika na kuwezesha wananchi wengi kupata  huduma ya umeme na kufikia malengo ya Serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda kwa kuhakikisha Umeme unatumika kama njia moja wapo ya kuleta maendeleo ya wananchi na kuinua  vipato  vyao binafsi na Taifa kwa ujumla. Naibu waziri Pallangyo alifanya ziara hiyo Aprili 20, 2017.

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt, Juliana Palangyo akiongea na wanahabari alipotembelea miradi ya kuzalisha umeme wa  Gesi Asilia ya upanuzi wa Kinyerezi I pamoja na ule wa Kinyerezi II.





Mafundi wakiendelea na kazi katika moja ya jengo lilopo katika mradi wa kufua umeme wa gesi asili megawati 240 wa Kinyerezi I ambapo unafanyiwa upanuzi.



Naibu katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Pallangyo (wa pili kutoka kushoto) akiambatana na viongozi wa TANESCO alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Miradi ya Umeme Kinyerezi I&II.  Kushoto kwake ni kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Bi.Joyce Ngahyoma akifuatiwa na Kaimu Meneja Uhusiano Bw. Yasini Didas Slayo Kulia pamoja na Meneja Mradi wa Kinyerezi II, Mhandisi Stephen Manda, (Kushoto)

Waziri Mpina akutana na Taasisi za kusimamia Kemikali nchini

April 22, 2017

Bw. Justine Ngaile Mkurugenzi wa Kinga na Mionzi kutoka Tume ya Atomiki akiwasilisha mada kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Luhaga Mpina. Waziri Mpini alikutana na Taasisi zinazohusika na usimamizi wa kemikali kujadilili mkakati wa pamoja wa kusimamia kemikali nchini.
Baadhi ya wataalamu kutoka Taasisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mamlaka ya Chakula na Dawa na Tume ya Nguvu za Atomiki wakifuatilia majadiliano na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina (hayupo pichani), kikao kazi hicho kimefanyika katika Ofisi ya Makamu wa Rais Dodoma.
Na Lulu Mussa
Dodoma

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, hii leo amekutana na taasisi zizohusika na uratibu na usimamizi wa kemikali hapa nchini.
Akiongea na Taasisi hizo, Waziri Mpina amewaagiza watendaji hao kudhibiti na kusimamia kemikali hatarishi nchini ikiwa ni pamoja na kuratibu usafirishaji, usambazaji na matumizi ya kemikali hizo hapa nchini kwa namna bora zaidi.
Waziri Mpina amezitaka taasisi hizo kutoa taarifa za utendaji wa kazi kila robo ya mwaka kwa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimizi wa Mazingira kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira kifungu namba 170. “Nawaagiza kuwasilisha takwimu za kemikali zinazozalishwa nchini, zinazoagizwa au kusafirishwa nje ya nchi, pamoja na kuainisha viwanda vinavyozalisha kemikali vilivyosajiliwa na maghala yaliyosajiliwa kuhifadhi kemikali hizo” alisisitiza Mpina.
Katika kikao hicho Waziri Mpina pia ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini ndani ya miezi miwili kuandaa muongozo na kuupitisha katika hatua zote wa namna bora ya kuteketeza taka hatarishi bila kuathiri mazingira.
Aidha Waziri Mpina ameagiza kuandaliwa kwa andiko litakalobainisha umuhimu wa kuteketeza taka hatarishi. “Kama taifa ni lazima tuwe na “dedicated Incinerator” kubwa kutekeza taka hizo hatarishi kwa kuzingatia taka zinazozalishwa hapa nchini” Mpina alisisitiza.
Katika hatua nyingine, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini, Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania, Tume ya Nguvu za Atomiki, Taasisi ya Utafiti ya Viuatilifu katika Kanda za Kitropiki, Mamlaka ya Chakula na Dawa, OSHA na Mkemia Mkuu wa Serikali kwa pamoja wametakiwa kuanda Hati ya Makubaliano ya kuratibu utekelezaji wa majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuhuisha Sheria zao na kuleta mapendekezo Serikali ya vifungu vya kufanyiwa marekebisho.
Taasisi alizokutana nazo ni pamoja na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC), Taasisi ya Nguvu za Atomiki, Mamlaka ya Chakula na Dawa na Mkemia Mkuu wa Serikali.