RAIS KIKWETE AELEKEA NCHINI MAREKANI LEO

November 06, 2014


Rais Profesa Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe said Meck Sadik na Meneja wa Huduma za Shirika la ndege la Emirates katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere Bw.  Aboubakar Juma leo Novemba 6, 2014 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea Marekani kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake
 Rais Profesa Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na askari polisi pamoja na wafanyakazi katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kabla ya kupanda ndege ya shirika la Emirates kuelekea Marekani leo Novemba 6, 2014

RAIS AFANYA MAGEUZI: MKUU WA MKOA NA WA WILAYA TANGA WAHAMISHWA.

November 06, 2014
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewaapisha wakuu wa mikoa baada ya kufanya mabadiliko kwa wakuu wapya wanne wa Mikoa, na kuwahamisha wengine sita.
Halima Omari Dendego
Wakuu wapya wa Mikoa ni Halima Omari Dendego ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Dkt. Ibrahim Hamisi Msengi ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Amina Juma Masenza ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa na John Vianney Mongella ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa, kabla ya uteuzi wake Bi. Dendego alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Dkt. Msengi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Bi. Masenza alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela na Mongella alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa Wakuu wa Mikoa ambao watapangiwa kazi nyingine ni Kanali (Mst) Fabian Massawe wa Kagera, Dkt. Christine Ishengoma wa Iringa na Kanali Joseph Simbakalia wa Mtwara.


Luteni (Mst) Chiku A.S. Galawa
Wakuu wa Mikoa ambao wamehamishwa vituo vya kazi ni Bwana Magesa S. Mulongo ambaye anakwenda Mkoa wa Mwanza kutoka Arusha, Dkt. Rehema Nchimbi ambaye anakwenda Mkoa wa Njombe kutoka Dodoma,  Ludovick John Mwananzila anakwenda Tabora kutoka Lindi, Kepteni (Mst) Anseri Msangi anayekwenda Mkoa wa Mara kutoka Njombe na Mhandisi Everist Ndikilo ambaye anakwenda Arusha kutoka Mwanza.

Wengine waliohamishwa ni Luteni (Mst) Chiku A.S. Galawa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kutoka Tanga, Dkt. Rajab Rutengwe ambaye anakwenda Mkoa wa Tanga kutoka Katavi, Fatma Mwasa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita kutoka Tabora na Magalula S. Magalula ambaye anahamishiwa Lindi kutoka Geita.

Taarifa hiyo imesema kuwa Wakuu wa Mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya,Morogoro, Pwani, Rukwa, Shinyanga, Ruvuma, Singida na Simiyu watabakia kwenye vituo vyao vya sasa.

Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi wa Wakuu wapya wa Wilaya, kuhamisha baadhi yao na kutengua uteuzi wa baadhi.

Taarifa kamili itatolewa na Waziri Mkuu baada ya kuwa wamepangiwa vituo vya kazi.
JONAS MKUDE AZITOSA YANGA SC NA AZAM FC NA KUJIFUNGA SIMBA SC

JONAS MKUDE AZITOSA YANGA SC NA AZAM FC NA KUJIFUNGA SIMBA SC

November 06, 2014
Na Baraka Mbolembole,
Kiungo wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Jonas Mkude amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea klabu yake ya Simba. Mkude, 21 ni moja ya matinda ya kikosi cha pili cha mabingwa hao mara 19 wa kihistoria wa Tanzania Bara, amepatiwa gari aina ya Toyota GX 115, huku pia kiwango chake cha mshahara kikipanda.
Mchezaji huyo wa nafasi ya kiungo ambaye atafikisha miaka 22 Disemba 3, ni mchezaji muhimu katika timu hiyo na alikuwa akihusishwa na mpango wa kusajiliwa na klabu ya Yanga SC na Azam FC lakini kitendo cha kusaini klabu iliyomlea ni kama kumaliza mbio za timu hizo ambazo zilionesha nia ya kumuhitaji kiungo huyo wa ulinzi.
8
Habari za ndani kutoka klabu ya Simba zinadai kuwa kiungo raia wa Burundi, Pierre Kwizera anaweza kutemwa klabuni hapo baada ya kuonyesha kiwango cha chini huku akishindwa kuendana na uchezaji wa timu hiyo. Kwizera ni mzuri katika kupanga mashambulizi pekee, wakati Mkude anaweza kukaba na kuichezesha timu. Wote wawili hucheza kama viungo wa chini na ili kuendelea kuijenga timu hiyo, Simba imeona ni bora kumuongezea mshahara, na kumpatia kile alichokuwa akihitaji Mkude kwa kuwa wataendelea kupata huduma nzuri..

WATUMISHI 11 WA MORAVIAN WAKOSA MISHAHARA YA MIEZI MITATU KISA DENI LA MBEYA CITY SOMA HAPA

November 06, 2014


Na Mwandishi  wetu, Mbeya
Watumishi 11 wa Kanisa la  Moraviani Tanzania, Jimbo la Kusin Magharibi,wameshindwa kupata malipo yao ya mishahara kwa miezi mitatu baada ya klabu ya timu ya mbeya city kudaiwa kushindwa kulipa  deni la shilingi milioni 19.

Deni hilo limetokana na Timu hiyo ya  mbeya City  kutumia hostel na malazi, wakati wa maandalizi ya msimu wapili wa ligi kuu ya Vodacom 2013.

Timu hiyo, ambayo iliweza kujizolea mashabiki wengi  ukilinganisha na timu kongwe za Yanga na Simba kwa msimu uliopita, imetajwa kukwamisha baadhi ya shughuli za kanisa hilo pamoja na wafanyakazi 11 kutolipwa mishahara yao, kutokana na kushindwa kulipa kiasi hicho cha fedha kwa wakati.

Akizungumza na blog hii Meneja wa Hosteli Msaidizi, Tuntufye Mwachuga alisema kiasi hicho cha fedha ni malipo ya kipindi cha miezi miwili walichotumia uongozi wa timu hiyo, kipindi cha msimu wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwaka 2013.

“Uongozi wa klabu hii ya Mbeya City, walifika ofisini na kuingia mkataba wa wachezaji wake kuweka kambi kwenye hosteli hii  kwa malazi na chakula kilichojumuisha milo mitatu, asubuhi, mchana na jioni kwa kipindi chote cha miezi miwili watakacho kitumia na sisi kukubaliana nao,”alisema.

Alisema, baada ya makubaliano hayo timu ilikaa na kumaliza muda wake huku timu ikifanikiwa kufanya vizuri lakini cha ajabu ni pale, uongozi wa kanisa ulipoanza kufuatilia malipo  na kuanza kupigwa kalenda kitendo ambacho hatujapendezwa nacho.

“Kanisa linaidai klabu ya Mbeya City kiasi cha shilingi milioni 19, 681,000 kwa malipo ya malazi na chakula katika kipindi cha miezi miwili walichotumia wakati walipoweka kambi msimu uliopita  wa ligi kuu ya Vodacom tangu February 3 hadi April 17 mwaka 2014 ,”alisema.

Katibu wa  Mbeya City Emanuel Kimbe
Akizungumzia deni hilo, Katibu wa klabu ya Mbeya City, Emmanuel Kimbe, alikiri uwepo wa deni na kwamba tayari taratibu za malipo zinaendelea.

“Kila Taasisi inayojiendesha hudai na kudaiwa, kwa hiyo Mbeya City kama Taasisi inayojiendesha inadaiwa pia lakini tunaendelea na mchakato wa malipo,”alisema Kimbe.

Alisema, malipo hayo yameanza kufanyika tangu Alhamis na ijumaa ya wiki iliyopita hivyo aliwaomba wadai kuwa wavumilivu.

BREAKING NEWZZZZ: Beatus Kinyaia ateuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo kuu Katoliki la Dodoma.

November 06, 2014

Na  Frederic M. Gabriel wa Globu ya Jamii

Hatimaye leo baba Mtakatifu Papa Francisco amempandisha kutoka  askofu hadi kuwa askofu Mkuu askofu Beatus Kinyaiya, O.F.M. Cap (pichani) wa jimbo kuu Katoliki la Dodoma.

Askofu Beatus Kinyaiya alizaliwa Mei 9, 1957. 

Akapata daraja takatifu la Upadre katika shirika la Kimisionari la Wafranciscan Minor  tarehe 25 juni, 1989. 

Aliteuliwa kuwa askofu wa jimbo Katoliki la Mbulu tarehe 22 Aprili, 2006, nakusimikwa/ wekwa wakfu rasmi na Kardinali Polycarp Pengo  kuwa askofu wa jimbo la Mbulu tarehe 2 Julai 2006. 

 Leo tarehe 06 Novemba, 2014 ameteuliwa kuwa askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katoliki la Dodoma ambalo nalo limepandishwa hadhi na kuwa jimbo kuu. 

Atasimikwa rasmi kuanza utume wake huo mpya katika jimbo hilo mwezi wa Januari, 2015.

WANAWAKE TANGA TISHIO % 50 KWA 50

November 06, 2014

ALIYEKUWA MKUU WA MKOA TANGA LUTENI (MSTAAFU) CHIKU GHALAWA KATIKA MOJA YA VIKAO MKOANI HAPA AMBAYE KWA SASA AMEHAMISHIWA MKOA WA DODOMA

WANAWAKE Mkoani hapa wametakiwa kuwa sehemu ya kukua kwa uchumi wa Taifa, na kuunga mkono dira ya Taifa 2025, MKUKUTA na Malengo ya milenia kwa kufanya biashara na ujasiriamali wenye tija zitakaz waongezea kipato.

Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 ilianzwa kutekelezwa mwaka 2000 ili kuongoza harakati za maendeleo ya uchumi na jamii zitakazoiwezesha Tanzania kufikia hadhi ya nchi yenye kipato cha kati na kuondoana na umaskini uliokithiri.

Malengo ni kuboresha hali za maisha ya watanzania, kuwepo kwa kwa mazingira ya amani, usalama na umoja, Kujenga utawala bora, kuwepo na jamii inayoelimika vyema na inayojifunza; na Kujenga uchumi imara unaoweza kukabiliana na ushindani kutoka nchi nyingine.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Luteni (mstaafu) Chiku Ghalawa alipokuwa akifugua kampeni ya Wanawake na Uchumi kwenye ukumbi wa Naivera Compex, eneo la Bombo Mkoani hapa.

Amesema kwa muda mrefu uchumi wa nchi umeongozwa na wakulima na wafanyakazi na kwamba wakati kwa wajasiriamali na wafanyabiashara ni sasa kuwa wachangiaji wakubwa wa pato la Taifa.

Kampeni hiyo imeandaliwa na asasi isiyo ya kiserikali ya Angels Moment kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa lengo la kuwaonyesha wanawake kuwa si kila changamoto inaashiria kurudisha nyuma juhudi zao  bali ni firsa ya kusonga mbele kwa kuanzisha mpya yenye ushindani.

Awali Mkurugenzi wa Kampeni ya Wanawake na Uchumi, Mahada Erick amesema pamoja na juhudi nyingi za kumkomboa mwanamke mjasiriamali bado ameendelea kukumbana na changamoto zilezile kila siku hali inayosababisha wengine kukwepa biashara na ujasiriamali kwa kuogopa matokeo ya waliotangulia kushindwa.

Licha ya changamoto hizo Mkuu wa Mkoa wa Tanga amewatia moyo wanawake walioudhuria hafla hiyo wapatao 300 kuwa halmashauri ya Jiji la Tanga imetenga asilimia 10 ya pato lake kuwanufaisha pamoja na vijana huku akiwasisitizia wasiwaache kinababa nyuma kwani baadhi yao mkoani hapa hawajishughulishi jambo ambalo ni fedheha na kugusia maandiko yanayosema asiye fanya kazi na asile.

IGP AFANYA MABADILIKO NDANI YA JESHI LA POLISI

November 06, 2014

Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu amefanya mabadiliko ya baadhi ya makamanda wa mikoa, wakuu wa upelelezi wa mikoa, wakuu wa usalama barabarani wa mikoa pamoja na watendaji wengine wa vikosi na vitengo mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi.
Miongoni mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa mabadiliko ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa Mkoa wa Ruvuma Kamishna msaidizi mwandamizi (SACP) Deusdedit Nsimeki anayekwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara, Aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara kamishna msaidizi (ACP) Akili Mpwapwa anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma.
Wengine ni aliyekuwa Afisa Mnadhimu mkoa wa Lindi Kamishna msaidizi (ACP) Renatha Mzinga anakuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi, aliyekuwa afisa Mnadhimu Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Suzan Kaganda amehamishwa kwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora na aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora kamishna msaidizi (ACP) Peter Ouma amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi.
Zaidi ya hao wengine waliyohamishwa ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Mtwara Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Eliyakimu Masenga anakwenda kuwa Mkuu wa upelelezi kikosi cha Tazara, aliyekuwa mkuu wa upelelezi Mkoa wa Tabora Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) David Mnyambuga anakwenda kuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Ilala, na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Ilala, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Juma Bwire, anakwenda kuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Tabora.
Aidha, aliyekuwa afisa Mnadhimu mkoa wa Tabora Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) John Kauga anakuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Tabora, aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Rombo (SSP) Mrakibu mwandamizi Ralph Meela anakwenda kuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Mtwara na aliyekuwa Mkuu wa upelelezi wa kikosi cha Tazara Mrakibu wa Polisi (SP) Isack Msengi anakwenda kuwa Kaimu mkuu wa upelelezi mkoa wa Pwani.
Kwa upande wa wakuu wa Polisi wa mikoa wa Usalama Barabarani ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Ibrahim Mwamakula ambaye amehamishiwa Trafiki Kanda Maalum Dar es Salaam, aliyekuwa Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Mtwara, Mrakibu wa Polisi (SP) Awadh Haji anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Kinondoni, na Mrakibu wa Polisi (SP) Ezekiel Kiko Mgeni aliyekuwa ofisi ya RPC Temeke, anakuwa Mkuu wa Trafiki mkoa wa Temeke.
Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Lindi Mrakibu wa Polisi (SP) James Kiteleki anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Njombe, aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Ilala, Mrakibu wa Polisi (SP) Meloe Buzema anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Lindi, aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Temeke Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Prackson Kibogoyo anakwenda kuwa Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Pwani, na aliyekuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Njombe, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Chacha Nsaho Maro anakwenda kuwa Mkuu wa Trafiki Mkoa wa Ilala. Mabadiliko hayo ni ya kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi katika kuhakikisha kwamba wananchi wanaendelea kupata huduma bora ya usalama.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP Msemaji wa Jeshi la Polisi

WAZIRI MKUU AKAGUA MAGHALA YA CHAKULA KIZOTA DODOMA

WAZIRI MKUU AKAGUA MAGHALA YA CHAKULA KIZOTA DODOMA

November 06, 2014

DSC03728
* Mwekezaji wa Poland asema wataanza kujenga Januari, mwakani
 WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amekagua maghala ya kuhifadhia chakula yaliyopo Kizota nje kidogo ya mji wa Dodoma ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Alhamisi iliyopita kwamba Serikali inalenga kujenga maghala kwenye mikoa sita kupitia mkopo ambao itaupata kutoka Serikali ya Poland.
 Akizungumza na viongozi wa mkoa wa Dodoma pamoja na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) leo asubuhi (Alhamisi, Novemba 6, 2014) wakati akikagua maghala hayo, Waziri Mkuu alisema katika mkoa huo, Serikali ina nia ya kujenga maghala makubwa (SILOS) yenye uwezo wa kuhifadhi tani 100,000 za nafaka kwa wakati mmoja.
 “Tukipata maghala yenye uwezo wa kuhifadhi tani 100,000 tutakuwa na uhakika wa kuchukua na akiba ya nafaka kutoka mikoa ya jirani ya Singida, Tabora na Manyara,” alisema.
 Waziri Mkuu alifuatana na Bw. WITOLD KARCZEWSKI ambaye ni mmiliki wa kiwanda kikubwa cha kusindika nafaka nchini Poland ambacho Waziri Mkuu Pinda alikitembelea alipozuru nchi hiyo Oktoba 24, mwaka huu. Bw. KARCZEWSKI anamiliki pia kiwanda kinachotengeneza malighafi za kujengea SILOS.
 Akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Mkuu wa kituo cha NFRA Kanda ya Kati, Bw. Ruwaichi Mambali alisema kituo hicho kina maghala yenye uwezo wa kuhifadhi tani 30,000 lakini kwa sasa kina tani 69,000 ambazo kati ya hizo tani 62,000 zipo Kizota (Dodoma) na tani 7,000 ziko Manyoni (Singida).
 Alisema eneo zima la Kizota lina ukubwa ekari 33 na kwamba kuna maghala matatu yenye uwezo wa kuhifadhi tani 10,000 kila moja. “Lakini kwa sasa tumelazimika kuweka mahindi mengine na mtama hapa nje ambayo tumeyafunika kwa maturubali,” alisema.
 Kwa upande wake, Bw. KARCZEWSKI alitaka kufahamu miundombinu iliyopo kwenye ghala la Kiszota ikiwemo umabli wa kutoka barabara kuu pamoja na reli. Pia alitaka kujua eneo zima lina ukubwa kiasi gani. Na alitaka kufahamu mbinu zinazotumika hivi sasa kuhifadhi chakula kwenye ghala hilo.
 Alisema wakipata michoro ya eneo hilo (site map), atatuma wataalamu wake Januari mwakani waangalie uwezekano wa kuanza ujenzi mapema iwezekanavyo pindi mazungumzo yakikamilika.
 Alhamisi iliyopita, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwl. Julius Nyerere akitokea Oman, Waziri Mkuu alisema alikwenda Poland kutafuta msaada wa mfumo wa mkopo wenye masharti nafuu ambao utasaidia kupambana na tatizo la uhaba wa maghala  kwa ajili ya kuhifadhia nafaka.
 Alisema Serikali imelenga mikoa sita ya kuanzia ambayo ni Ruvuma, Rukwa, Njombe (pamoja na Iringa) ambako kuna uzalishaji mkubwa wa mahindi. Pia inaangalia Kanda ya Ziwa ambako mara nyingi wana uhaba wa chakula; na kwamba itaweka maghala mkoani Dodoma kwa sababu ni katikati ya nchi ili ikusanye akiba kutoka mikoa ya jirani ya Singida, Manyara na Tabora.
 “Lengo ni kupata uwezo wa kuhifadhi tani 700,000 hadi 1,000,000 na ujenzi wao siyo kama huu wa kwetu. Tumewaomba watujengee SILOS (maghala makubwa) kwa sababu zina teknolojia ya kujua kiasi gani cha nafaka kimeingia, zina unyevu kiasi gani, unaweza kuweka dawa nafaka zako, kuosha na kukausha na kisha ukasindika kwa kiwango unachotaka,” Waziri Mkuu aliwaeleza waandishi wa habari.
 Alisema uzalishaji mwaka huu umetoa ziada ya tani milioni 1.5 za nafaka na tani 800,000 za mpunga ikilinganishwa na ziada ya tani 300,000 iliyokuwepo mwaka jana. “Serikali inakabiliwa na changamoto ya kupata soko la uhakika kwa mazao ya wakulima kwa sababu tulizoea kumtumia Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) kama mnununzi mkuu na uwezo wezo wake ni tani 240,000 tu kwa mwaka,” alisema.

RAIS KIKWETE AWAAPISHA MAKATIBU WAKUU, MABALOZI,WAKUU WA MIKOA NA MAKATIBU TAWALA WAPYA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

November 06, 2014


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe Samwel William Shellukindo kuwa Balozi na Msaidi wa Rais Masuala ya Diplomasia leo Ikulu jijini Dar es salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe John Vianney Mongella kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe Halima Omary Dendengo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Dkt Ibrahim Hamisi Msangi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi leo Ikulu jijini Dar es salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha na kumpa vitendea kazi Dkt Yohana Budeba kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha na kumpa vitendea kazi Injinia Mbogo Futakamba kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha na kumpa vitendea kazi Dkt Donan Mmbando kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha na kumpa vitendea kazi Mhe Jack Mugendi Zoka kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha na kumpa vitendea kazi Mhe Charles Pallangyo kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Geita Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akumuapisha na kumpa vitendea kazi Bw, Adoh Stephen Mapunda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 6, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakiwa katika picha ya pamoja na Makatibu wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa wapya baada ya kuwaapisha Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Balozi mpya wa Tanzania Nchini Canada Mhe. Jack Mugendi Zoka , pamoja na mabalozi wengine kutoka kushoto Balozi Mbelwa Kairuki (Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Austrlia). Balozi Simba yahya (Mkurugenzi idara ya Mashariki ya Kati na Balozi Celestine Mushi, Mkurugenzi wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa.

KATIBU TAWALA CHIMA AFUNGUA KONGAMANO KUHUSU KUMUDU MATARAJIO YA WANANCHI KUHUSIANA NA UZINDUAJI WA GESI ASILIA NA MAFUTA LEO MKOANI TANGA

November 06, 2014
KATIBU TAWALA WA MKOA WA TANGA,SALUM CHIMA AKIZUNGUMZA WAKATI AKIFUNGUA KONGAMANO HILO LEO

MWENYEKITI WA MAZINGIRA NETWORK TANZANIA(MANET) JOSIAH SEVERRE AKIZUNGUMZA WAKATI WA KONGAMANO HILO
MJUMBE WA NORTHERN COALITION AMBAYE PIA NI MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MAZINGIRA MKOA WA TANGA TARUJA AKIELEZA JAMBO KWENYE KONGAMANO HILO


MKUU WA WILAYA YA MKINGA,MBONI MGAZA AKIELEZA JAMBO KWENYE KONGAMANO HILO LEO

DIWANI WA KATA YA KWALE MTINDI BAMBA AKISISITIZA JAMBO KWENYE KONGAMANO HILO

                  MWENYEKITI WA MAZINGIRA NETWORK TANZANIA(MANET) JOSIAH SEVERRE AKIZUNGUMZA WAKATI WA KONGAMANO HILO

 MJUMBE WA NORTHERN COALITION AMBAYE PIA NI MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MAZINGIRA MKOA WA TANGA TARUJA AKIELEZA JAMBO KWENYE KONGAMANO HILO
KATIBU WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA VIJIJINI NA MAZINGIRA(TARUJA)BURHAN YAKUB AKIELEZEA JAMBO KWENYE KONGAMANO HILO

REGIONAL ADMISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT ENG.AMON KYOMO AKIELEZEA JAMBO KWENYE KONGAMANO HILO LA SIKU MOJA

DAS WA WILAYA YA MKINGA,JOSEPH SURA AKIFUATILIA MADA MBALIMBALI ZILIZOKUWA ZIKIWASILISHWA

ALIYEKAA KATIKATI NI MKUU WA WILAYA YA MKINGA,MBONI MGAZA AKIANDIKA BAADHI YA DONDOO ZILIZOKUWA ZIKIWASILISHWA KWENYE KIKAO HICHO LEO
WAJUMBE WAKIPIGA PICHA YA PAMOJA LEO MARA BAADA YA KUMALIZIKA KONGAMANO HILO