VIJANA WAHIMIZWA KUJISHUGHULISHA KULETA TIJA

VIJANA WAHIMIZWA KUJISHUGHULISHA KULETA TIJA

October 12, 2016
TABIA ya vijana kutojishughulisha katika miradi mbalimbali yenye tija kumeeelezwa kuwa moja ya vyanzo vya kudorora kwa uchumi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama katika ufunguzi wa kongamano la kitaifa la vijana lililofanyika katika ukumbi wa shule ya msingi Allience Mjini Bariadi.

Alisema kumeanza kujitokeza hali ambapo vijana nchini kutokupenda kujishughulisha katika miradi mbalimbali ya kiuchumi na hivyo kushindwa kuondokana na umaskini na pia kuchangia katika pato la taifa.

Alisema kuwa vijana wanaongoza kwa idadi kubwa lakini wanashindwa kujishughulisha kuhakikisha wanapata maendeleo ambayo yanaweza kulisaidia taifa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida (kushoto) akisalimiana na mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama (kulia) alipowasili katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi kufungua kongamano la vijana.

Mhagama alisema katika Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Mkoa wa Simiyu, kuratibiwa na Taasisi ya utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kwamba kuna fursa nyingi lakini vijana wanakuwa wagumu kuzichangamkia na matokeo yake kubaki wakiilalamika serikali kuwa haiwajali.

Alibainisha kuwa serikali itaendelea kusaidia makundi ya vijana yanaoonesha nia ya kujiendeleza

Aidha alifafanua kuwa itawaongezea mtaji wa shilingi milioni 30 kwa kikundi cha vijana cwalioanzisha kiwanda Maziwa cha Meatu pamoja na kile cha Chaki kutokana na jitihada zao walizofanya na matunda kuonekana.

Awali kabla ya kumkaribisha mgeni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alisema lengo la serikali mkoani hapa ni kuhakikisha linainua pato la mkoa na kuchangia katika pato la taifa kwa kuwawezesha vijana wake kutengeneza bidhaa zinazotokana na malighafi zinazozalishwa mkoani hapa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama na Naibu wake Mh. Anthony Mavunde wakisalimiana na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na ESRF mara baada ya kuwasili kwenye kongamano la kitaifa la vijana lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

Alisema zaidi kwamba wanalengo la kuhakikisha mkoa unaingia katika tano bora ya uchangiaji wa pato la taifa.

Amehimiza viongozi kuwasaidia vijana kuwaongoza, kuwaelekeza na amewataka vijana kuwa na uthubutu na kuungana kwa pamoja.

Pamoja na harakati za kiuchumi vijana wametakiwa kuwa na mwendo wenye maadili mema ili kuendelea kuwa na afya bora na kukwepa magonjwa yanatokanayo na ukosefu wa maadili.

Amesistiza kuwa kauli mbiu waliyoanzisha ya “Bidhaa moja,wilaya moja” itumike ipasavyo ili kufanikisha maendeleo yao na ya wilaya.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la vijana Simiyu lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida alisema ushiriki wa vijana katika viwanda vidogovidogo kunaweza kukuza uchumi kutokana na viwanda hivyo kutoa ajira na pia kutengeneza mnyororo wa thamani katika mazao ya wakulima ambako vijana ndiko wanakotarajiwa kuonesha ushujaa wao.

Hata hivyo alisema ukuaji wa uchumi kwa sasa bado ni changamoto kwa wananchi wanaoishi vijijini kutokana na baadhi ya huduma kutowafikia kwani asilimia 7 inayopanda kiuchumi huwa haitafsiriki kufikia makundi yote ya kijamii .

“Tumekuwa tukiendesha tafiti nyingi lakini tunaona kipato chetu kinaendelea kushuka hasa katika wananchi wanaoishi vijijini hivyo kuwepo kwa viwanda kutaweza kuwainua kiuchumi wananchi kutokana na bidhaa zao ghafi kuuzwa katika viwanda”Alisema Dk. Kida.

Nao wafadhili wa Kongamano hilo UNDP wamesema wametenga fedha kwa ajili ya kuwasaidia vijana katika programu zao za maendeleo.

Sehemu ya wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Waziri Mhagama.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza machache awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama kufungua kongamano la kitaifa la vijana lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.
Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico akitoa salamu kwa vijana kutoka visiwani Zanzibari kwenye kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.
Meza kuu mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama, Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico (wa tatu kulia), Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dk.Titus Kamani ( wa pili kulia), Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida (kushoto), Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Anthony Mavunde (wa pili kushoto) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (wa tatu kushoto).

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya kuondoa Umaskini wa Wizara ya Fedha na Mpiango, Mudith Cheyo (kulia) na Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango, Maduka Kessy wakifuatilia hotuba mbalimbali wakati wa kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida akiwasilisha mada ya mageuzi ya kiuchumi yanayohitajika kuboresha maisha ya vijana pamoja na hali ya uchumi nchini kwa makundi ya vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini walioshiriki kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.
Bw. Abdallah Hassan (kushoto) na John Kajiba wa ESRF wakifuatilia jambo kwenye kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo UNDP, Amon Manyama akizungumzia mchango wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN/UNDP) katika Maendeleo Endelevu ya Vijana wakati wa kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA KIWANDA CHA MAZIWA MEATU SIMIYU

October 12, 2016
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akikata utepe kabla ya kuzindua kiwanda cha kusindika maziwa wilayani Meatu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, akiweka jiwe la uzinduzi katika kiwanda cha kusindika Maziwa wilaya ya Meatu, Mkoani Simiyu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, akipewa maelezo na vijana wa kikundi cha Meatu Milk wanaojishughulisha na usindikaji wa maziwa kabla ya kuweka jiwe la uzinduzi katika kiwanda cha kusindika Maziwa Meatu.
: Naibu Waziri wa kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde akizungumza na Vijana na wananchi wa Meatu baada ya  Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama  kufungua kiwanda cha maziwa Meatu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Vijana na wananchi wa Meatu wakati wa ufunguzi wa  kiwanda cha maziwa Meatu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi zawadi ya maziwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka mara baada ya kuzindua kiwanda cha maziwa Meatu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mhe. Pius Machungwa akipokea zawadi ya  maziwa kutoka kwa Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama mara baada ya kufungua kiwanda cha maziwa Meatu.
Baadhi ya viongozi wa Wilaya Meatu, mkoa wa Simiyu na viongozi wa kitaifa wakicheza muziki ishara ya kufurahia uzinduzi wa Kiwanda cha Maziwa wilayani Meatu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (waliokaa) wa nne) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Maswa, Mkoa wa Simiyu, na Vijana wa Meatu Milk.

Na Stella Kalinga

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amefungua kiwanda cha kusindika maziwa kinachoendeshwa na  kikundi cha Vijana wa Meatu kilichopo wilayani humo Mkoa wa Simiyu.

Akizungumza na Vijana hao wanaosindika maziwa ya Meatu (MEATU MILK), Waziri Mhagama amewataka kuutunza mradi huo ili uwe mradi mkubwa wa kuwaingizia mapato wao na Serikali kwa ujumla. 

Mhagama amesema kwa kadri mradi huo utakavyokuwa mkubwa ndivyo wafugaji wa Wilaya ya Meatu na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla watakavyonufaika kwa kupata soko la uhakika la maziwa.

Aidha, Waziri huyo amewataka Viongozi wote wa wilaya kuunga mkono juhudi zilizofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka za kuwatengenezea  vijana mazingira mazuri ya kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo yao, ikiwa ni pamoja na kushughulikia upatikanaji wa mitaji na mafunzo ya kuwajengea uwezo.

Wakati huo huo Waziri Mhagama ameahidi  kuwa Ofisi yake itatoa mkopo wa shilingi 30,000,000 kwa lengo la kuwasaidia vijana hao kuongeza uzalishaji ili kupanua soko la maziwa yao ndani na nje ya Mkoa.

“Mhe. Mkuu wa Mkoa Ofisi ya Waziri Mkuu itawapa mkopo vijana wa “Meatu Milk”ili wapanue uzalishaji; Wizara yangu itatoa mikopo kwa vijana walio tayari kutekeleza ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda vidogo vidogo vitakavyowasaidia kuwapa ajira na kujikwamua kwenye umaskini” alisema Mhagama.

Akizungumza na wananchi wa wilaya ya Meatu kabla ya kumkaribisha Waziri Mhagama Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Mkoa huo umejipanga kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa kutumia malighafi zinazopatikana hapa nchini.

“Tumejichagua kuwa pacha wa Mhe. Rais katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa Vitendo na tumedhamiria kuwa miongoni mwa mikoa mitano inayofanya vizuri katika uchumi”, alisema Mtaka.

Akiwasilisha taarifa ya mradi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu  kwa Mhe. Waziri, kiongozi wa kikundi cha Meatu Milk Lightness Benedicto amesema Halmashauri imewapa mtaji na kuwajengea uwezo kwenye teknolojia za usindikaji, ufungishaji wa bidhaa za maziwa pamoja na elimu ya ujasiriamali.


Naye Mbunge wa Jimbo la Meatu, Mhe. Salum Mbuzi ameahidi kuwaongezea mtaji wa shilingi 5,000,000 vijana hao pamoja na kuwasaidia kukutafuta soko la uhakika kwa maziwa watakayosindika.

Mradi wa kiwanda cha kusindika maziwa Meatu wenye vijna 18 hadi sasa umegharimu jumla ya shilingi 34,903,000 kati ya hizo shilingi 10,000,000 ni michango ya wanachama kutoka kwenye gawio la fedha za mkopo uliotolewa na Wizara yenye dhamana na vijana,shilingi 24,903,000 ni mkopo kutoka kwenye 5% ya mapato ya ndani ya Halmashauri. 

Kampuni ya Tigo yasherehekea wiki ya huduma pamoja na wateja wake katika hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam.

October 12, 2016


  Meneja wa Mifumo ya Kibiashara na Mawasiliano wa Tigo Halima Kasoro (kulia)akizungumza na wateja walioalikwa katika chakula cha usiku katika hotel ya Double Tree jijini Dar es Salaam, kushoto kwake ni Meneja wa Ubora wa huduma kwa Wateja Tigo, Mwangaza Matotola na meneja huduma kwa wateja Charles Gardner.

  Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata, akipunga mkno kuwasalimu wateja wa Tigo walioalikwa chakula cha jioni katika kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja.

  Msanii Elias Barnabas (Barnaba) akiburudisha kwa kuimba na kucheza pamoja na wageni waalikwa.

Wateja wa Tigo wakisikiliza kwa makini.

 Meneja Rasilmali watu wa Kampuni ya Tigo, Catherine Olaka akimpongeza mwangalizi wa duka la Manzese Glory kwa kupata zawadi ya mfanyakazi bora

Meneja wa Ubora wa huduma kwa Wateja Tigo, Mwangaza Matotola akiwaongoza wateja kupata chakula cha jioni.

CHUMI AENDELEA KUTAFUTA WADAU WA KUISAIDIA SHULE YA MSINGI MAKALALA

October 12, 2016


Mkurugenzi wa TEA Joel Laurent katikati akiangalia darasa la Tehama Computer ambazo baadhi zilitolewa kama msaada na TEA kwa shule hiyo.

na fredy mgunda,Iringa. 
MBUNGE wa jimbo la mafinga mjini cosato chumi amewataka wananchi kuendelea kujituma kufanya kazi wakati akitafuta ufumbumzi wa kero na changamoto mbalimbali za jimbo hilo jimpya.

Aliyasema hayo alipokutana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bw Joel Laurent katika Shule ya makalala yenye mahitaji maalumu huku lengo likiwa ni kumuonyesha mkurugenzi huyo jinsi hali ilivyombaya ya kitaalum na mazingira yalivyo magumu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

“Ninajitahidi kufanya kila kinachowezekana ili mradi kutatua changamoto za wananchi wa jimbo la mafinga na kuleta maendeleo kadili ninavyoweza” alisema chumi 

 Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elim Tanzania Bw Joel Laurent alisema kuwa atatuma timu yake ya wataalam kwa ajili ya kufanya tathimini ya mahitaji ya miundombinu katika Shule ya Msingi Mchanganyiko ya Makalala iliyopo Mafinga.

Bw Laurent aliyasema hayo siku Alhamis alipoitembelea Shule hiyo kufuatia ombi la Mbunge wa Mafinga Mjini.

Mkurugenzi huyo alisema kwamba TEA pamoja na mambo mengine Ina wajibu wa kusaidia miundombinu na vifaa saidizi vya kufundishia na kujifunzia na kwamba Mwaka huu wataelekeza nguvu katika Shule za mahitaji maalum kama Makalala na kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule za kawaida.

Shule hiyo yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 48 wa bweni wenye ulemavu wa akili, wenye ualbno na wenye uono hafifu inakaribiwa na uhaba wa Bweni ambapo kwa Sasa wanafunzi wanalazimika kulala mpaka watoto Sita katika baadhi ya vyumba.

Naye mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Williamu alisema kuwa anaishukuru TEA kwa kuitikia wito wa kuitembele shule hiyo yenye mahitaji maalumu na kuomba serikali kuwapa ushirikiano kutatua changamoto za shule ya makalala sambamba na kuwaomba wada wengine kuendelea kuisadia shule hiyo.

Wiki  iliyopita TEA ilitoa msaada wa vifaa visaidizi vya kusomea katika shule ya Ilboru sambamba na kukabidhi fimbo nyeupe mkoani Mbeya.
NAIBU WAZIRI MPINA AIADHIBU MANISPAA YA MJI WA TABORA

NAIBU WAZIRI MPINA AIADHIBU MANISPAA YA MJI WA TABORA

October 12, 2016

ga1
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazngira Mhe. Luhaga Mpina akiongea na maafisa na waaandishi wa habari alotangulizana nao katika DAMPO la mji wa Tabora na kushangazwa na hali halisi ya DAMPO hiyo na taarifa ya mazingira aliyopewa na mkoa kuhusu usafi wa mazingira wa mji wa Tabora
ga2
Bw. Benjamini Dotto Afisa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC (katikati) akieleza kitaalam nini kifanyike katika DAMPO la Mji wa Tabora kabla ya manispaa kuwasilisha mpango mkakati kuhusu dampo la mji huo. (Picha na Evelyn Mkokoi)
…………………………………………………………
EVELYN MKOKOI-TABORA
Kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina ameipa adhabu Halmashauri ya Maispaa ya Mji wa Tabora kwa kuitoza faini ya shilingi Milioni kumi na mbili na kutakiwa kulipa faini hiyo kwa muda wa wiki mbili, kwa kile kilichodaiwa ni kutokutii mamlaka za juu na kusema uwongo kuhusu hali ya usafi wa maingira ya mji wa Tabora.
Alipokoukuwa katika siku ya Pili ya ziara yake mkoani Tabora baada ya kupata taarifa ya hali ya mazingira ya mkoa huo, Na kuambiwa kuwa ni ya kuridhisha na kuwa DAMPO la mji huo ambalo siyo rasmi,lipo katika hali ya kuridhisha ndipo alipoamua kjutembelea DAMPO hilo na kujioea hali ya uchafu isiyovumilika kwa taka ngumu na hatarishi, kutomwagwa katika eneo husika na kuzagaaa barababarani.
Aidha kufuatia malalamiko ya wakazi wa mji huo, Mpina halikadhalika aliktembelea soko ya mji wa Tabora na kushuhudia Dampo katikati ya soko hilo lenye taka mbichi zenye harufu kali ambayo huweza kuhatarisha maisha ya watumiaji wa soko hilo kwa kupata magonjwa ya mlipuko kama kipindu pindu.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora Bw. Bosco Nduguru alisema ofisi yake ilikuwa na mpango wa kuhamishia soko hilo sehemu nyingine na kukubali changamoto zilijitokeza sokoni hapo na kuzifanyia kazi wakati mwenyekiti wa soko hilo bwana Bakari Mpumila alieleza kuwa kuhamishwa kwa soko hilo hakuwezi kuwa suluhisho la kudumu kutatua changamoto za usafi wa mazingira kwani dampo linalotumika katikati ya soko hilo limekuwa ni kero iliyoshindikana toka kwa uongozi uliopita na Kumshukuru Naibu Waziri Mpina kwa ziara yake kwani ana imani kuwa sasa kero hiyo imeshatapatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Pamoja na kulipa faini hiyo manispaa pia inatakiwa kuondosha taka hizo a kumwaga kifisi cha molamu katika eneo hilo na kurekebisha mazingira ya choo sokoni hapo.

WAZIRI LUKUVI. HAKUNA MAKAZI HOLELA YATAKAYOBOMOLEWA JIJINI MWANZA.

October 12, 2016
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Willium Lukuvi, akizungumza na wakazi wa Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza, alipofanya ziara Jijini Mwanza hii leo.

Waziri ameziagiza halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, kuhakikisha zinakamilisha zoezi la upimaji na urasimishaji makazi yaliyojengwa kiholela hadi ifikapo june 30 mwakani.
Na BMG
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Willium Lukuvi, akizungumza na wakazi wa Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza, alipofanya ziara Jijini Mwanza hii leo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Willium Lukuvi, akimkabidhi hati ya umiliki wa ardhi na makazi mmoja wa wakazi wa Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza ambaye makazi yake yamerasimishwa kutoka makazi holela baada ya zoezi la upimaji kufanyika.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Willium Lukuvi, akimkabidhi hati ya umiliki wa ardhi na makazi mmoja wa wakazi wa Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza ambaye makazi yake yamerasimishwa kutoka makazi holela baada ya zoezi la upimaji kufanyika.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Willium Lukuvi, akizungumza na watendaji mbalimbali Jijini Mwanza (Ilemela na Nyamagana).
Baadhi ya Watendaji na Madiwani wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza
Baadhi ya Watendaji na Madiwani Jijini Mwanza
Pia Waziri Lukuzi amempandisha cheo aliyekuwa Afisa Mipango na Maendeleo ya Jiji la Mwanza, Deogratius Kalimerize, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mipango Miji na Vijijini Kanda ya Ziwa. 

Ni baada ya kuridhishwa na kazi yake ya usimamiaji na uandaaji wa Mpango Kabambe wa Jiji la Mwanza wa mwaka 2015-3015 ambao umelenga kulifanya Jiji la Mwanza kuwa kitovu cha kiuchumi na biashara katika nchi za maziwa makuu.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, akizungumza kwenye mkutano huo baina ya waziri Lukuvi na watendaji mbalimbali wa Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.
Watendaji na wananchi wa Kata ya Buhongwa wakimsikiliza waziri Lukuvi (hayupo pichani).
**********************
Na George Binagi-GB Pazzo
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi, ameziagiza halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, kuhakikisha zinakamilisha zoezi la upimaji na urasimishaji makazi yaliyojengwa kiholela hadi ifikapo june 30 mwakani.

Waziri Lukuvi ametoa agizo hilo hii leo Jijini Mwanza alikofanya ziara ya kujionea utekelezaji wa urasimishaji makazi yaliyoendelezwa kiholela Jijini Mwanza ambapo amebainisha kwamba Serikali haina mpango wa kuwavunjia wananchi makazi yaliyojengwa kiholela na badala yake imeandaa mpango huo ili kutambua makazi hayo na kuwapatia wananchi hati miliki ya makazi yao.

Aidha amewatahadharisha wananchi kwamba, mpango wa kurasimisha makazi yaliyojengwa kiholela hautayahusisha makazi yaliyojengwa kwenye maeneo hatarishi ikiwemo kwenye mabonde, miinuko, mafuriko pamoja na hifadhi za barabara.

Baadhi ya wananchi Jijini Mwanza ambao makazi yao yamerasimishwa na kupewa hati ya umiliki, wameipongeza serikali kwa hatua hiyo ambapo wameomba kasi ya zoezi hilo kuongezeka ili wananchi zaidi ya elfu 35 ambao makazi yao hayajapimwa, yaweze kupimwa na kupatia hati za umiliki kwa wakati kama Waziri Lukuvi alivyoagiza.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amemuhakikishia Waziri Lukuvi kwamba hadi kufikia mwezi Januari mwaka ujao, zoezi la kupima makazi yaliyojengwa kiholela na kuyarasimisha katika Jiji la Mwanza na Maspaa ya Ilemela, litakuwa limekamilika.
MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI ATOA TAARIFA YA MATEMBEZI YA HIYARI NA UCHANGIAJI DAMU

MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI ATOA TAARIFA YA MATEMBEZI YA HIYARI NA UCHANGIAJI DAMU

October 12, 2016
ku1 ku2
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed akitoa tarifa kwa wandishi wa habari kuhusu matembezi ya hiyari na zoezi la kuchangia Damu kwa Mkoa Mjini Magharibi yatayofanyika tarehe 16/10/2016.  
ku3
Sehemu ya wandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud alipokuwa akitoa tarifa kuhusu matembezi ya hiyari na zoezi la kuchangia Damu kwa Mkoa Mjini Magharibi.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar
MJI WA DODOMA LAZIMA UPANGWE – WAZIRI MKUU

MJI WA DODOMA LAZIMA UPANGWE – WAZIRI MKUU

October 12, 2016
mold1
Waziri Mkuu Kassim Majiliwa amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Molard Tanzania Bwana Abeid Abdallah ambaye kampuni yake inajishughulisha na ujenzi wa nyumba za kisasa kwa gharama nafuu Waziri mkuu ameikaribibisha kampuni hiyo kujenga nyumba za watumishi Mkoani Dodoma mazungumzo hayo yamefanyika ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam
mold2
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Molard Bwana Abeid Abdallah akimuonyesha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baadhi ya picha na michoro ya nyumba za kisasa na zabei nafuu zinazo weza kujengwa Dodoma Picha na ofisi ya Waziri Mkuu 
………………………………………………………
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameikaribisha kampuni ya ujenzi ya Moladi Tanzania ielekeze nguvu zake Dodoma ambako kuna mahitaji makubwa ya nyumba za watumishi.
“Natambua kuwa mnatumia teknolojia ya kisasa na ujenzi wa nyumba zenu unachukua siku chache sana. Ninawaencourage mje Dodoma ambako kuanzia Machi mwakani, watumishi wengi wataanza kuhamia huko,” amesema.
Waziri Mkuu ametoa wito huo leo mchana (Jumatano, Oktoba 12, 2016) wakati akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw. Abeid Abdallah ambaye alifika ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam na kumuonyesha ramani ya nyumba za watumishi ambazo wanazitumia.
Waziri Mkuu amesema Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) ina maeneo ambayo imeyatenga rasmi kwa ajili ya viwanja vya makazi na anaamini katika muda wa miezi miwili wanaweza kujenga nyumba za kutosha watumishi wanaotarajiwa kuhamia katika awamu ya pili.
“Nimeangalia michoro yenu, nyumba za vyumba vitatu vya kulala zina hadhi ya kukaa hata wakurugenzi; na watumishi wa kawaida wanaweza kumudu zile za vyumba viwili vya kulala… ninawatia moyo mwende haraka Dodoma na wale ambao wako serious wataleta maombi yao mara moja,” amesema.
Waziri Mkuu amesema amefarijika kuona kuwa size ya ramani zao inatosha kwenye kiwanja cha ukubwa wa mita za mraba 550 ambacho ni high density na watumishi wengi wanaweza kumudu kuvinunua.
Kwa upande wake, Mkurugenzi huyo, Bw. Abdalla amemweleza Waziri Mkuu kwamba nyumba ya ukubwa wa vyumba vitatu vya kulala, yenye sebule, jiko, stoo na choo inatosha eneo la mita za mraba 94 tu.
“Kati ya vyumba hivyo vitatu, kimoja ni master, pia kuna sebule, chumba cha kulia na kibaraza. Hii inaanzia shilingi milioni 35 hadi milioni 41 kutegemea na aina ya vifaa unavyoweka kwenye umaliziaji. Lakini tukiongeza na servant quarter utalazimika kulipia shilingi milioni 7 ambapo unapata vyumba viwili na choo na bafu ndani,” amesema.
“Kimsingi, ni lazima tutaweka madirisha, milango, vyoo, masinki ya bafuni na jikoni, tiles (na mtu anaruhusiwa kuchagua za China, Italy au Spain),” ameongeza.
Akifafanua kuhusu nyumba yenye vyumba viwili vya kulala, Bw. Abdalla amesema nayo pia ina sebule, jiko, stoo na choo kimoja na inatosha eneo la mita za mraba 54. Amesema nyumba hizo zinaanzia sh. milioni 20 hadi 25 kutegemeana na aina ya vifaa vinavyowekwa kwenye umaliziaji.
Amesema ujenzi wa nyumba moja unachukua wiki sita na kama viwanja viko eneo moja au jirani, wanaokoa muda wa siku tatu hadi tano kwa kila nyumba. “Tunajenga ukuta kwa kumwaga theluji isiyochanganywa na kokoto ambayo ni mchanganyiko wa saruji, mchanga na kemikali. Inakauka baada ya saa saba na ukuta wetu ni imara mara nne zaidi ya ukuta uliojengwa na tofali la zege.”
Teknolojia yetu inawezesha ukuta wa nyumba nzima kukamilika ndani ya siku sita, nyumba zetu zinastahimili matetemeko, vimbunga na ujenzi wake unapunguza gharama za ujenzi kwa asilimia 40.
Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa nyumba hizo, Bw. Abdalla amesema wana mikataba na mabenki kwa hiyo wanaweza kujenga nyumba na kuziuza mara moja lakini pia wananchi wanaweza kuingia mikataba na mabenki na kulipia kidogo kidogo katika muda maalum (mortgage).

TABATA KIMANGA JIJINI DAR ES SALAAM WAOMBA KUONDOLEWA TAKATAKA BARABARANI

October 12, 2016
 Mchuuzi wa mbogamboga akipita karibu na takataka zilizoachwa bila ya kuondolewa jirani na kituo cha daladala cha Tabata Kimanga mwisho Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam.
 Takataka zikiwa kando ya barabara.
Mwendesha bodaboda akizikwepa takataka zilizoachwa bila ya kuondolewa jirani na stendi ya daladala ya Tabataaa Kimanga mwisho jijini Dar es Salaam.

Na Dotto Mwaibale

WANANCHI wa Tabata Kimanga Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wameomba kuondolewa kwa takataka zilizotelekezwa katika maeneo mbalimbali na mkandarasi aliyepewa tenda ya kuziondoa.

Akizungumza na mtandao wa www. habari za jamii.com Dar es Salaam juzi mkazi wa eneo hilo, Mfaume Wakwetu alisema katika maeneo mengi ya Tabata Kimanga kunatakataka nyingi zimerundikwa kando ya barabara bila kuondolewa na wahusika.

"Takataka nyingi zimerundikwa katika eneo la stendi ya mabasi hapa Tabata Kimanga na kuwa kero kubwa kwa watumiaji wa stendi hiyo na wapita njia" alisema Mfaume.

Aliongeza kuwa takataka zilitolewa majumbani huwekwa katika madampo madogo yaliyoanzishwa kandio ya barabara lakini mkandarasi aliyepewa tenda hiyo hushindwa kufika kwa wakati kuziondoa hivyo kuwa kero kwao.

Aliongeza kuwa kutokana na takataka hizo kuachwa kwa muda mrefu bila kuondolewa husambaa hadi kwenye mifereji ya maji taka ambayouziba na kusababisha maji kushindwa kupita na kutoa hahrufu kali na kusababisha mafuriko mvua zinaponyesha.