NAIBU WAZIRI MPINA AMUUNGA MKONO MAKONDA KATIKA ZOEZI LA KUPANDA MITI.

NAIBU WAZIRI MPINA AMUUNGA MKONO MAKONDA KATIKA ZOEZI LA KUPANDA MITI.

September 30, 2016
luh1
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akipanda mti katika shule ya Sekondari ya Mama Salima Kikwete iliyopo Kijitonyama Jijini Dar es salaam ikiwa ni ishara ya kuunga mkono kampeni ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ya kupanda miti                       
luh2
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akiongea na wanafunzi mara baada ya kumaliza zoezi la kupanda miti katika shule ya sekondari ya Mama Salima Kikwete.                          
luh3
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh Luhaga Mpina akifafanua jambo mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mama Salima Kikwete.
……………………………………………………………..
EVELYN MKOKOI
 Kuelekea siku ya uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti jijini  Dar es salaam maarufu kama “mti wangu’, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Ameunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda katika Jitahada zake za kutunza mazingira kwa kupanda miti.
Naibu Mpina ameshiriki kwa kutangulia kupanda mti leo katika shule ya sekondani ya Salma Kikwete iliyopo kijitonyama jijini Dar es Saalam, ambapo wakala wa misitu nchini wametoa miti 600 ili kukamilisha zoezi hilo katika shule hiyo ya sekondari.
Naibu Waziri amewataka wakuu wote  wa mikoa na wilaya kuiga jitihada za Mhe. Makonda na  kuacha tabia za mazoea zilizojitokeza huko nyuma za kutoa taarifa za uwongo katika Ofisi ya Makamu wa Rais Kuwa Miti kadhaa imepandwa lakini ki uhailisia hakuna kilichofanyika.
Aidha ametoa wito kwa watendaji wa serikali wanaochakachua maaagizo ya viongozi na kusema kuwa serikali hii ipo makini hivyo kutakuwa na ufuatiliaji kwa  kila Mkoa, Wilaya na Halmashauri kwani zoezi hili la upandaji miti ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama tawala.
“Hatutavumilia kuona miti inakatwa ovyo, misitu inachomwa moto na viongozi wa serikali wakilifumbia macho suala hilo.” Alisisitiza.
Kwa Upande wake Kaimu Mkurugezi wa Wakala wa Misitu Nchini  Profesa Santos Silayo alisema, Taasisi hiyo imetoa jumla ya miche ya miti 8000 ili kukamilisha zoezi hilo katika jiji la Dar es Salaam, na kumpongeza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kuonyesha mwanzo mpya na jitihada katika jiji la Dar es Salaam kwa kupanda miti na kutunza mazingira.
Bi Jacquline Wolper Muhamasishaji wa swala la utunzaji wa mazingira na muigizaji maarufu nchini, akishiriki zoezi hilo, kwa kupanda miti amepongeza jitihada za mkuu wa Mkoa Makonda kwa kuzunguka katika mashule mbalimbali jijini kuhamasisha zoezi hilo kwa kutoa miche ya miti kadhaa.
 Rais Magufuli afunga Maadhimisho ya Miaka 52 ya JWTZ ashuhudia Zoezi la Amphibious Landing Bagamoyo

Rais Magufuli afunga Maadhimisho ya Miaka 52 ya JWTZ ashuhudia Zoezi la Amphibious Landing Bagamoyo

September 30, 2016
j1
Amiri  Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akipiga ngoma za bendi ya jeshi ya Mwenge Jazzz wana Paselepa wakati  wa kufunga Zoezi la medani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016
j2
 Amiri  Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na meza kuu wakipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa wakati wa kufunga Zoezi la medani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016
j3
 Ndege vita zikipita angani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016
j4
 Ndege vita zikipita angani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016
j5
Amiri  Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na meza kuu wakipiga makofi wakati wa Zoezi la medani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani leo Septemba 30, 2016.PICHA NA IKULU.
…………………………………………………………………………………
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 30 Septemba, 2016 amefunga maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa kushuhudia zoezi la medani liitwalo ”Amphibious Landing” lililofanyika katika Kijiji cha Baatini Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.
Zoezi hilo lililochukua muda wa wiki mbili, limeshirikisha kamandi zote tano za JWTZ  ambazo ni Nyika, Majini, Anga, Kamandi ya Makao Makuu na  Jeshi la Kujenga taifa limefanyika katika ufukwe wa bahari ya Hindi na limetekelezwa kwa mfano wa mapambano ya kivita yaliyohusisha kutua nchi kavu kutoka majini na kukomboa eneo lililotekwa.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Rais na Amiri jeshi Mkuu Dkt.John Pombe Magufuli amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange pamoja na Makamanda na Wapiganaji wote wa JWTZ walioshiriki katika zoezi hilo ambalo limefanywa kwa umakini, uhakika na weledi wa hali ya juu.
”Kwa kweli nimefurahi na nimeamini tuna wapiganaji wa kutosha katika maeneo yote, hii
mikakati na mipango iliyotumika inaonesha tuna jeshi imara na linaloaminika” amesema Dkt. Magufuli. 
Rais na Amiri Jeshi Mkuu amewahakikishia Makamanda na Wapiganaji wote wa JWTZ kuwa Serikali yake itahakikisha inaendeleza na kuongeza zaidi juhudi zilizofanywa na Marais waliopita kwa kuimarisha na kuwa na jeshi la kisasa linalotumia vifaa na teknoljia ya kisasa na pia itahakikisha maslai ya askari yanaboreshwa.
Aidha, Dkt. Magufuli ametaka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuimarishwa zaidi na kujielekeza
katika uzalishaji mali ikiwemo uwekezaji katika viwanda.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ambaye pamoja na kuipongeza  JWTZ amesema miaka 52 tangu kuanzishwa kwa Jeshi hilo Watanzania wanashuhudia jeshi lao likiwa imara na makini zaidi kwa ajili ya kulinda nchi.
Nae Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange amemshukuru Rais na Amiri Jeshi
Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake na nia yake ya kuliimarisha Jeshi na kuboresha maslai ya Makamanda na Wapiganaji na ameongeza kuwa anajivunia kuwa kiongozi  wa Jeshi hilo.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Viongozi wengine wakiwemo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar Abdulhamid Yahaya Mzee.
Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli, amemuagiza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kuwapa ajira za JWTZ askari mgambo wote walioshiriki zoezi la Amphibious Landing, Gerson Msigwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU Dar es Salaam

BRITISH COUNCIL WAZINDUA UTAFITI WA SAUTI ZA VIJANA JIJINI ARUSHA

September 30, 2016

Mkuu wa wilaya ya Arusha,Mh.Gabriel Daqarro akizindua kitabu cha utafiti wa Sauti ya Kijana nchini Tanzania uliofanywa na taasisi ya British Council kupitia ufadhili wa Shirika la misaada la serikali ya Uingereza  la DFID kuwezesha sauti za vijana kuwafikia watunga sera na watoa maamuzi nchini,kulia ni Meneja Mradi wa British Council Tanzania,Elizabeth Nkanda.

Mkuu wa wilaya ya Arusha,Mh.Gabriel Daqarro akizindua kitabu cha utafiti wa Sauti ya Kijana nchini Tanzania uliofanywa na taasisi ya British Council kupitia ufadhili wa Shirika la misaada la serikali ya Uingereza  la DFID kuwezesha sauti za vijana kuwafikia watunga sera na watoa maamuzi nchini.

Mtaalamu wa sera za ufugaji, Carolyn Kandusi akiongoza shughuli nzima iliyofanyika jijini Arusha.

Mkurugenzi wa Miradi wa taasisi ya British Council Tanzania,Nesia Mahenge akizungumza katika kongamano la Vijana.

Mkurugenzi wa Miradi wa taasisi ya British Council Tanzania,Nesia Mahenge akizungumza katika kongamano la Vijana.

Vijana kutoka taasisi mbalimbali na vyuo Vikuu katika mkoa wa Arusha na Kilimanjaro wakifatilia kwa makini namna ya kutumia fursa mbalimbali kujiajiri na kuanzisha miradi wakati wa uzinduzi huo.

Vijana kutoka taasisi mbalimbali na vyuo Vikuu katika mkoa wa Arusha na Kilimanjaro wakifatilia kwa makini namna ya kutumia fursa mbalimbali kujiajiri na kuanzisha miradi wakati wa uzinduzi huo.

Mtaalamu wa masuala ya Mitaji,Baraka Megiroo akiwapa mbinu vijana wenzake namna ya kutumia fursa zinazojitokeza kujikwamua kiuchumi.
Mtaalamu wa masuala ya kijamii,Hadija Hassan akizungumza na vijana umuhimu wa kujiamini na kuzikabili changamoto mbalimbali,kushoto ni Mtaalamu mwenzake Gladys Mmari na Mary Bird
Vijana kutoka taasisi mbalimbali na vyuo Vikuu katika mkoa wa Arusha na Kilimanjaro wakifatilia kwa makini namna ya kutumia fursa mbalimbali kujiajiri na kuanzisha miradi wakati wa uzinduzi huo.

TAASISI YA ADLG YABAINISHA SABABU ZA KUWEPO MAENDELEO DUNI KWENYE BAADHI YA VIJIJI VYENYE WAWEKEZAJI WA MADINI NCHINI.

September 30, 2016
Taasisi ya Demokrasia na Utawala bora nchini ADLG, imebainisha kwamba kukosekana kwa uwajibikaji miongoni mwa baadhi ya viongozi, kunasababisha maendeleo duni kwenye baadhi ya maeneo/vijiji yenye wawekezaji ikiwemo migodi.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Jimmy Luhende, ameyasema hayo leo kwenye mdahalo wa kila mwezi unaoendeshwa na taasisi hiyo kujadili masuala mbalimbali yanayohusu rasilimali asilia ikiwemo madini, gesi na mafuta.

Amesema katika tafiti zilizofanywa na taasisi hiyo katika vijiji mbalimbali vinavyozungukwa na migodi katika mikoa ya kanda ya ziwa, wamebaini kukosekana kwa huduma muhimu za kijamii ikiwemo zahanati, shule, miundombinu bora ya barabara pamoja na maji safi na salama.

Amesema taasisi hiyo imeanzisha midahalo mbalimbali inayowahusisha wananchi pamoja na viongozi katika vijiji 147 vya mikoa minne ya kanda ya ziwa yenye uwekezaji wa madini ili kuwajengea uwezo wananchi kutumia uwekezaji ulio kwenye maeneo yao kurahishisha maendeleo.

Afisa Miradi (Sheria na Mikataba) kutoka taasisi ya ADLG, Carolina Tizeba, amesema katika tafiti zilizofanywa na taasisi hiyo kwenye Vijiji vinne vya Nyenze, Ikonongo, Songwa na Maganzo katika Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, umebaini kuwepo kwa ushiriki mdogo wa wananchi pamoja na uwajibikaji wa viongozi wao katika masuala ya uwekezaji wa madini jambo ambalo linasababisha kushindwa kufuatilia manufaa ya uwekezaji katika vijiji vyao na hivyo kuchangia kuwepo kwa huduma duni za kijamii katika vijiji hivyo ambavyo kuna wawekezaji wa madini.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Jimmy Luhende, akizungumza jambo kwenye mdahalo huo uliofanyika Isamilo Jijini Mwanza.
Nicholaus Ngelea ambaye ni Afisa Miradi ADLD, akiwasilisha mada kwenye mdahalo huo uliofanyika Isamilo Jijini Mwanza.
Carolina Tizeba ambaye ni Afisa Miradi (Sheria na Mikataba) ADLG, akiwasilisha taarifa ya utafiti uliofanywa na taasisi hiyo kwenye vijiji vinavyozungukwa na migodi mkoani Shinyanga.
Washiriki mbalimbali wakiwemo Wanahabari, Taasisi za Utawala bora, wachumi, wanamazingira na watafiti mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.
Washiriki mbalimbali wakiwemo Wanahabari, Taasisi za Utawala bora, wachumi, wanamazingira na watafiti mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.
Mshiriki akichangia mada
Mshiriki akichangia mada
Washiriki mbalimbali wakiwemo Wanahabari, Taasisi za Utawala bora, wachumi, wanamazingira na watafiti mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.
Washiriki mbalimbali wakiwemo Wanahabari, Taasisi za Utawala bora, wachumi, wanamazingira na watafiti mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.
Washiriki wa mdahalo huo
Washiriki mbalimbali wakiwemo Wanahabari, Taasisi za Utawala bora, wachumi, wanamazingira na watafiti mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.
Washiriki mbalimbali wakiwemo Wanahabari, Taasisi za Utawala bora, wachumi, wanamazingira na watafiti mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.
Washiriki mbalimbali wakiwemo Wanahabari, Taasisi za Utawala bora, wachumi, wanamazingira na watafiti mbalimbali wakiwa kwenye mdahalo huo.
Bonyeza HAPA Kwa Mdahalo uliopita. Imeandaliwa na BMG.

WAREMBO 30 MISS TANZANIA WATINGA KAMBINI LEO, WAPEWA SOMO LA AWALI NA MISS TANZANIA WA SASA

September 30, 2016
Baadhi ya Washiriki watakaowania Taji la Miss Tanzania 2016 wakiwa katika picha pamoja muda mfupi baada ya kuwasili kambini. Jumla ya Washiriki 30 kutoka kanda mbalimbali nchini wameingia Kambini leo Septemba 30, 2016 tayari kwa maandalizi ya Shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi ujao.
Mrembo anaeshikilia Taji la Miss Tanzania kwa sasa, Lilian Kamazima akizungumza na Warembo alipokutana nao leo Septemba 30, 2016 kwenye Hoteli ya Regency, Jijini Dar es salaam. ambapo jumla ya Washiriki 30 wameingia kambini leo tayari kwa maandalizi ya Shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi ujao.


Baadhi ya Washiriki wa Miss Tanzania 2016 wakimsikiliza kwa makini Mrembo anaeshikilia Taji la Miss Tanzania kwa sasa, Lilian Kamazim.
 Warembo wakifanyiwa Usaili na viongozi wa Miss Tanzania.
-- Othman Michuzi Editorial Director & Chief Photographer CELL: +255 713 775869 /+255 789 103610 WEB: issamichuzi.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com michuzijr.blogspot.com EMAIL: othmanmichuzi@gmail.com Dar Es Salaam. Tanzania.

BENKI KUU YA TANZANIA YASEMA PATO LA TAIFA LIMEONGEZEKA KWA ASILIMIA 7.9

September 30, 2016
 Kaimu Meneja Kitengo cha Mahusiano kwa Umma wa BoT, Victoria Msima, akimkaribisha  Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu (wa pili kushoto), kuzungumza na wanahabari kuhusu ukuaji wa pato la taifa kwa robo na nusu mwaka 2015 Dar es Salaam leo.
 Taswira ya meza kuu katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Kaimu Meneja Kitengo cha Mahusiano kwa Umma, Victoria Msima,Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mabenki,  Kenedy Nyoni, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Beno Ndulu na Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti wa Sera za Kiuchumi, David Kwimbere.
 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandshi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa ya ukuaji wa pato la taifa kwa robo na nusu ya mwaka 2016. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mabenki,  Kenedy Nyoni.
 Wapiga picha wakiwa kazini.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mwanahabari Samuel kutoka kituo cha Televisheni ya ESTV akiuza swali


Na Dotto Mwaibale

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesema ukuaji wa pato la Taifa umeongezeka kwa asilimia 7.9 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 5.8 kwa kipindi kama hicho mwaka 2015.

Hayo yamebainishwa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu Dar es Salaam leo asubuhi wakati akizungumza na wanahabari kuhusu ukuaji wa pato la Taifa kwa robo na nusu mwaka 2016.

Profesa Ndulu alisema shughuli za kiuchumi zilizokua kwa kasi ya juu zaidi katika kipindi hicho ni usafirishaji na uhifadhi wa mizigo ikiwa ni asilimia 30.6, uchimbaji wa madini kwa asilimia 20.5, mawasiliano na habari asilimia 12.6 na sekta ya fedha na bima kwa asilimia 12.5.

Alisema ukuaji wa sekta ya uchukuzi na uhifadhi wa mizigo umetokana na kuongezekea kwa usafirishaji wa abiria kwa njia ya barabara na gesi asilia ambao umekua kwa zaidi ya nusu ukilinganisha na robo ya pili ya mwaka 2015 kwa asilimia 9.4.

"Kwa upande mwingine, ukuaji wa sekta ya uchimbaji wa madini na gesi umechangiwa zaidi na kuongezeka kwa uzalishaji wa gesi ambao umekua kutoka mmSFt3.7,793 kwa mwaka 2015 mpaka mmSFt3 11,267 kwa mwaka 2016" alisema Ndulu

Profesa Ndulu alitaja sekta nyingine ambayo imefanya vizuri ililinganishwa na kipindi kama hicho kwa mwaka 2015 kuwa ni sekta ya kilimo ambayo imekua kwa asilimia 3.2 kwa robo ya pili ya mwaka 2016 wakati mwaka jana ilishuka kwa asilimia 1.9.

Aidha sekta ya fedha na bima imekua kwa asilimia 12.5 kwa robo ya pili ya mwaka 2016 ikilinganishwa na asilimia 10.0 kwa robo ya pili ya mwaka 2015.

Akizungumzia ukuaji wa pato la Taifa alisema katika nusu ya mwaka 2016 yaani Januari hadi Juni 2o16 kasi ya ukuaji wa pato la taifa imeongezeka na kufikia asilimia 6.7 ikilinganishwa na asilimia 5.7 kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2015.


Mashindano ya Tigo Igombe Marathon kulindima jumapili hii

September 30, 2016
Meneja  Mauzo wa Tigo mkoani Tabora, Bright Kisanga(kushoto) akiongea na wanahabari jana wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Igombe marathon yatayofanyika jumapili mkoani Tabora. Wengine ni Amon Mkoga Mratibu wa mashindano na katibu wa chama cha riadhaa mkoani Tabora, SalumTaradadi. Kampuni ya Tigo ndio mdhamini mkuu wa mashindano hayo.





Mratibu wa mashindano ya Igombe Marathon, Amon Mkoga(katikati) akionesha kombe na medali kwa washindi wa Igombe marathon kwa wanahabari wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo jana,Wengine pichani kushoto Meneja Mauzo wa Tigo mkoani Tabora, Bright Kisanga na katibu wa chama cha riadha  mkoani humo Salum Taradadi.



Mratibu wa mashindano ya Igombe Marathon, Amon Mkoga(katikati) akiongea na wanahabari wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo jana,Wengine pichani kushoto Meneja Mauzo wa Tigo mkoani Tabora, Bright Kisanga na katibu wa chama cha riadha  mkoani humo Salum Taradadi.



Msanii akicheza na Nyoka wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Igombe marathon




28 Septemba 2016 Tabora, Kampuni ya simu za mkononi Tigo Tanzania  ikishirikiana na kampuni ya Chief promotions imetangaza rasmi kwamba  tarehe 02/10/216  kampuni ya Chief Promotions imendaa mbio za kila mwaka kwa jina la Tigo Igombe Marathon.
Bright Kisanga ambaye ni Meneja Mauzo kutoka Tigo mkoani Tabora, alielezea kwamba, “lengo kuu la mbio hizi ni kusaidia vijana wenye vipaji vya riadha  kupitia  mchezo huo kuwa ajira yao kamili na pili kuwatangaza kitaifa na kimataifa, na Tigo ndio mdhamini mkuu, ambapo tumedhamini mbio hizi kwa 50m/-”
Lakini mbio hizi za KM 21 kwa wote,KM 5 za kujifurahisha na Mita 10 kwa watoto,Mita 10 kwa kinamama vilevile hutumika kuamsha ari ya wanajamii kutatuwa changamoto zao haswa za kimaendeleo.
Akiongea na waandishi habari, Meneja Mkuu wa Chief Promotions, Amon Mkoga alisema, “Kwa mwaka huu kundi litakalofaidika ni wasichana wa mashuleni kwa kushirikiana na wafadhili wa mbio hizi tumeamua kutoa Pad kwa wanafunzi kwa ajili ya kujinga kipindi cha hedhi, kama tunavyofahamu ingawa kumekuwepo kwa juhudi mbalimbali za kuinua elimu lakini bado mtoto wakike ana vikwazo vingi kimojawapo kushindwa kuhudhuria shule kipindi cha hedhi hii itasaidia kwa kiasi fulani kufikia malengo hayo.
“Mwaka huu marafiki wa Igombe Marathon watatoa misaada mbalimbali katika Hospitali ya Kitete kwa nia ya kuwa pamoja na wanajamii haswa katika kusukuma gurudumu la maendeleo.” Alieleza Mkoga
Mbio hizi zitaanzi uwanja wa Ali hassani mwinyi kuanzia saa 12 asubuhi na kuzunguka katika viunga vya Tabora mjini na baadae kumalizikia uwanjani hapo.
Mbio hizi zimedhaminiwa na kampuni ya simu ya Tigo,Umoja wa Ulaya(EU),Tabora Hotel,Coca Cola,TBL na HQ .

Mgeni rasmi:Tunategemea atakuwa  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye
photo