Walk for Kagera yachangisha shilingi bilioni 1.5

Walk for Kagera yachangisha shilingi bilioni 1.5

September 17, 2016
mbd1
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi akizungumza wakati wa kufungua rasmi Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera “Walk For Kagera” leo Jijjini Dar es Salaam. Matembezi hayo ya kilomita tano yalianzia katika viwanja vya Bwalo la Maofisa wa Polisi Osterbay ambapo jumla ya shilingi 1,502,680,000/= zilichangwa.
mbd2
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Agustine Mahiga akizungumza na washiriki wa Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera “Walk For Kagera” leo Jijini Dar es Salaam. Matembezi hayo ya kilomita tano yalianzia katika viwanja vya Bwalo la Maofisa wa Polisi Osterbay ambapo jumla ya shilingi 1,502,680,000/= zilichangwa.
mbd4
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi akishiriki mazoezi ya viungo kabla ya kuanza Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera “Walk For Kagera” leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kutoka kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Agustine Mahiga, Mwenyekiti wa Wabunge kutoka Kagera, Profesa Anna Tibaijuka na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
mbd5
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akizungumza katika hafla ya kuchangia wahanga wa Tetemeko lililotokea mkoani Kagera  iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu leo Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo iliyotanguliwa na Matembezi ya Hisani ambapo kiasi cha shilingi 1,502,680,000/= kilipatikana.
mbd6
Naibu Waziri wa Nchi, OWM –Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Abdallah Posi akizungumza katika hafla ya kuchangia wahanga wa Tetemeko lililotokea mkoani Kagera  iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu leo Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo iliyotanguliwa na Matembezi ya Hisania ambapo kiasi cha shilingi 1,502,680,000/= kilipatikana.
mbd7
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi akimkabidhi cheti cha utambuzi wa mchango wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki katika kufanikisha Matembezi ya hisani ya “Walk for Kagera” Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Dkt. Aziz Mlima leo Jijini Dar es Salaam.
mbd8
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi akishiriki Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera “Walk For Kagera” leo Jijini Dar es Salaam. Katika matembezi hayo kiasi cha shilingi 1,502,680,000/= kimepatikana.
mbd9
Baadhi ya washiriki wa  hafla ya kuchangia wahanga wa Tetemeko lililotokea mkoani Kagera  iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu wakifuatilia mtukio katika hafla hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ilitanguliwa na Matembezi ya Hisani ambapo kiasi cha shilingi 1,502,680,000/= zilipatikana.
mbd11 mbd13
Wawakilishi wa Jumuiya ya Wabohora nchini  wakimkabidhi Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera kwa Rasi wakati wa Matembezi ya hisani yalioyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
mbd14
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF Bw. William Erio na Afisa Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele wakimkabidhi Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya kusaidia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera wakati wa Matembezi ya hisani yalioyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kutoka kushoto ni Waziri wa Mmbo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Agustine Mahiga.
mbd15
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi akimkabidhi cheti cha utambuzi wa mchango wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashari katika kufanikisha Matembezi ya hisani ya “ Walk for Kagera” Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Busemaker akipokea cheti kwa ajili ya kutambua udhamini wa Benki hiyo katika kufanyikisha matembezi ya hisani kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko la Kagera leo Jijini Dar es Salaam.
mbd16
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi akiagana na baadhi ya washiriki wa Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera “Walk For Kagera” leo Jijjini Dar es Salaam. Matembezi hayo ya kilomita tano yalianzia katika viwanja vya Bwalo la Maofisa wa Polisi Osterbay ambapo jumla ya shilingi 1,502,680,000/= zimechangwa.
……………………………………………………………………………..
Na: Frank Shija, MAELEZO
TAKRIBANI shilingi bilioni 1.5 zimechangwa kufuatia matembezi ya hisani yaliyopewa jina la “Walk for Kagera” yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la  kusaidia wahanga  wa Tetemeko la Ardhi lililotokea tarehe 10 septemba mwaka huu  mjini Bukoba Mkoani Kagera.
Akizungumza mara baada ya matembezi hayo Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe Ally Hassan Mwinyi  aliwashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza na kushiriki matembezi hayo ya hisani.
“Nawapongeza sana wadau wote mlioshiriki katika matembezi haya, mmeonyesha mshikamano mkubwa kwa umoja wenu mmeweza kuchangisha jumla ya shilingi 1,502,680,000 hii inatia faraja sana muendelee na moyo huo” Alisema Mzee Mwinyi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Kagera kuwa Serikali inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha wahanga wa tetemeko hilo wanapatiwa huduma stahiki na kwa wakati.
Balozi Kijazi aliongeza kuwa kutokana na kuguswa na tatizo hilo Serikali pamoja na Taasisi zake imetoa msaada wake ambao unakadiriwa kuwa zaidi ya shilingi bilioni moja ikiwa ni kuthamini utu wa wahanga.
“Najua kuna athari kubwa imetokea kutokana na tetemeko hili, sisi kama Serikali tunafanya kila jitihada kuhakikisha wahanga wote wanapata misaada na kurejesha huduma zote katika hali yake” Alisema Balozi Kijazi.
Awali akisoma maelezo ya tathmini ya athari za tetemeko hilo Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Abdallah Posi amesema kuwa hadi kufikia tarehe 16 idadi ya vifo ni 17, nyumba zilizoanguka zimefikia 840 huku zilizoharibika zikiwa ni 1264 na majengo 44 mali ya Taasisi za umma yameharibika.
Kwa upande wake Kiongozi wa Mabalozi nchi, Balozi wa Zimbabwe ametoa pole kwa wahanga wa tukio hilo na kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania pale panapo hitaji msaada wao.
Matembezi hayo ya hisani kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia wahanga wa tetemeko la Ardhi yaliandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu.
MKUU WA WILAYA YA ILALA AONGOZA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUCHANGIA MAAFA YA TETEMEKO BUKOBA

MKUU WA WILAYA YA ILALA AONGOZA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUCHANGIA MAAFA YA TETEMEKO BUKOBA

September 17, 2016
1
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akipokea kiasi cha shilingi milioni zaidi ya milioni 6 kutoka kwa mmoja wa wafanyabiashara wa Kariakoo Bw. Deo Senya  wakati Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo (JWK) walipofanya Harambee ya kuchangia wahanga wa Tetemeko la Ardhi kule Bukoba mkoani Kagera ambapo Mkuu wa wilaya hiyo aliongoza harambee hiyo, Kuliani ni Katibu Tawala wa wilaya ya Ilala Bw. Edward Mpogolo na katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanya Biashara Kariakoo Bw.Philimin Lomano Chonde.
Katika harambee hiyo jumla ya shilingi milioni 13,708,000/= fedha taslimu zilikusanywa na vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 31564800/= jumla ya michango kwa ujumla ni shilingi milioni 45,672,800/= harambee hiyo leo ilikuwa inazinduliwa rasmi na michango inaendelea mpaka siku ya jumamosi ijayo ambapo ndiyo harambee hiyo itafungwa rasmi na wafanyabiashara mbalimbali wametakiwakuendelea kuchangia kwa kupitia jumuiya yao ya wafanyabiashara mpaka siku ya jumamosi.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
2
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akipokeamsaada wa viatu kutoka kwa wafanyabiashara wa kikundi cha Raha Square wafanyabiashara ambao wametoa mchango ubwa sana wa fedha na vitu mbalimbali katika harambee hiyo.
3
Wafanyabiashara wa Raha Square Kariakoo wakikabidhi mcahngo wao wa fedha kwa mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema.
4
Raha Square wakikabidhi Magodoro , Nguo, Vikoi , Mashuka na vitu vingine mbalimbali katika harambee hiyo.
5 6
Wakikabidhi Suti na vitengi pamoja na mashuka katika harambee hiyo.
7
Mkuu wa wilaya ya Ilala akipiga picha ya pamoja na viongozi  wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo mara baada ya harambee hiyo.
8 9
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akiwahutubia wafanyabiashara na wananchi mbalimbali waliohudhuria katika harambee hiyo.
10
Mfanyabiashara Mohammed Abdallah Nofa akizungumza mara baada ya kukabidhi mchango wake wa shilingi 500.000  kwa Mkuu wa wilaya Ilala Mh. Sophia Mjema wa pili kutoka kulia . katika picha kulia ni Edward Mpogolo Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala na Kushoto ni Katibu wa JWK Bw. Abdallah Mwinyi
11
Wafanyabiashara kutoka Raha Square wakikusanya michango yao ya fedha taslimu na vifaa mbalimbali kabla ya kuvikabidhi leo.
12
Kiongozi wa Wafanyabiashara wauza Simu za mkononi Bw.Stanley Mwakipesile akizungumza machache mara baada ya kukabidhi mchango wao zaidi shilingi milioni 1.500.000 kwa mkuu wa wilaya ya Ilala katika Harambee hiyo.
MREMBO LAURA KWAI ATWAA TAJI LA TTCL MISS HIGHER LEARNING INSTITUTIONS 2016.

MREMBO LAURA KWAI ATWAA TAJI LA TTCL MISS HIGHER LEARNING INSTITUTIONS 2016.

September 17, 2016


 Mshindi wa Taji la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Laura Kwai akipunga mkono kwa mashabiki wa ulimbwende mara baada ya kutangazwa kutwaa taji hilo jana katika Ukumbi wa King Solomoni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mshindi wa pili wa taji la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Evelyn Andrew pamoja na mshindi wa tatu wa taji la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Clara Nyaki (kulia). Shindano hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL). Mshindi wa Taji la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Laura Kwai akipunga mkono kwa mashabiki wa ulimbwende mara baada ya kutangazwa kutwaa taji hilo jana katika Ukumbi wa King Solomoni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mshindi wa pili wa taji la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Evelyn Andrew pamoja na mshindi wa tatu wa taji la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Clara Nyaki (kulia). Shindano hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL). Mshindi wa taji la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2015 (kushoto) akimvisha Mshindi mpya wa Taji la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Laura Kwai (aliyeketi) mara baada ya kutangazwa kutwaa taji hilo. Hellen George a.k.a 'Ruby' akitumbuiza kwenye shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 jana katika Ukumbi wa King Solomoni jijini Dar es Salaam. Shindano hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL). Meneja Masoko wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Beda Kinunda (kushoto) akimtangaza mshiriki Glory Gidion kuwa balozi wa TTCL kutoka katika shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016. Mshiriki huyo atasaini mkataba wa kufanya kazi na TTCL kutangaza huduma na bidhaa za kampuni hiyo. Baadhi ya maofisa wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL) na wadhamini wakuu wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakifuatilia matukio anuai katika mchuano huo wa walimbwende wasomi kutoka vyuo mbalimbali nchini jana jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa TTCL (kulia) ambao ni wadhamini wakuu wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakiwasajili kupata laini baadhi ya wapenzi wa ulimbwende waliovutiwa na huduma za kampuni hiyo katika mchuano huo wa walimbwende wasomi kutoka vyuo mbalimbali nchini jana. Baadhi ya maofisa wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL) na wadhamini wakuu wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakifuatilia matukio anuai katika mchuano huo wa walimbwende wasomi kutoka vyuo mbalimbali nchini jana jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wafanyakazi wa TTCL (kulia) ambao ni wadhamini wakuu wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakiwasajili kupata laini baadhi ya wapenzi wa ulimbwende waliovutiwa na huduma za kampuni hiyo katika mchuano huo wa walimbwende wasomi kutoka vyuo mbalimbali nchini jana. Baadhi ya wafanyakazi wa TTCL (kulia) ambao ni wadhamini wakuu wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakiwasajili kupata laini baadhi ya wapenzi wa ulimbwende waliovutiwa na huduma za kampuni hiyo katika mchuano huo wa walimbwende wasomi kutoka vyuo mbalimbali nchini jana. Sehemu ya wadau na wapenzi wa masuala ya urembo wakiwa katika mapozi ya picha kwenye Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 jana.

DAVID KAFULILA AONGOZA MAAFALI YA DARASA LA SABA KATIKA SHULE YA GOSHEN NURSERY AND PRIMARY SCHOOL BUNJU JIJINI DAR

September 17, 2016

 Mwanafunzi Eugene Kephasi, akimvika skafu, aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ambaye alikuwa  mgeni rasmi katika maafali ya saba ya darasa la saba katika Shule ya Goshen Nursery and Primary School  Bunju jijini Dar es Salaam leo mchana.
 David Kafulila akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Shule hiyo, Nipael Mrutu wakati akipewa historia fupi ya shule hiyo kutoka kwa Mkuu wa Shule hiyo, Felister Mrutu (hayupo pichani).
 Kafulila (katikati) na viongozi wa shule hiyo wakielekea meza kuu tayari kwa maafali hayo. Kutoka kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Felister Mrutu, Mkurugenzi wa Shule, Nipael Mrutu, Lupi Kiyabo na Mchungaji Elisifa Kephasi.
 Wanafunzi wakiwa tayari kwa gwaride.
 Wanafunzi wa darasa la saba wakiwa kwenye maafali yao.
 Mkuu wa shule hiyo, Felister Mrutu (kushoto), akimuongoza mgeni rasmi David Kafulila wakati wa kukagua shule hiyo.
 Skauti akionesha namna ya kupika katika kambi yao waliyoiweka katika shule hiyo kunogesha maafali hayo.
 Magari yanayotoa huduma za usafiri kwa wanafunzi yakiwa shuleni hapo
 walimu wakiwa kwenye maafali hayo.
 Wahitimu wa darasa la saba wakiimba wimbo wa shule.
 Wanafunzi wa darasa la tatu wakiimba kwenye maafali hayo.
 Wanafunzi wakiimba wimbo wa kuwaaga darasa la saba.
 Majadiliano meza kuu na mgeni rasmi. Kulia ni Mchungaji Elisifa Kephasi na Mkurugenzi wa Shule hiyo, Nipael Mrutu.
 wanafunzi wa darasa la pili wakitoa burudani.
 Hapa ni furaha tupu kwa wanafunzi wa darasa la pili baada ya kutoa burudani.



 Sarakasi zikifanyika katika maafali hayo.
 Wageni waalikwa, wazazi na walezi wa watoto hao wakijumuika na watoto wao kwenye maafali hayo.
 Sarakasi zikiendelea.
 Hapa ni Karate kwa kwenda mbele "madogo wapo vizuri sana katika mchezo huo baada ya kupata mafunzo kutoka kwa Kamanda Mduma wa Skauti"
Skauti wakionesha namna ya kumuokoa mtu aliyepoteza fahamu ambaye yupo kwenye eneo la kikwazo kumfikia. Hapa muokoaji akipita chini ya moto kwenda kumchukua mgonjwa.

Na Dotto Mwaibale

MBUNGE wa zamani wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila amesema urithi pekee wa watoto ni elimu na sio mali kama ilivyozoeleka.

Kafuli ametoa kauli hiyo katika maafali ya saba ya darasa la saba katika Shule ya Goshen Nursery and Primary School Dar es Salaam leo mchana.

"Napenda kuwaomba wazazi na walezi kuendelea kuwapa elimu watoto wenu kwani ndio msingi wa maisha yao badala ya kuwarithisha magari, nyumba na vitu vingine vya thamani" alisema Kafulila,

Kafulila ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maafali hayo alitoa shukurani zake kwa uongozi mzima wa shule hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwaandaa wanafunzi hao ambao watakuja kuwa wataalamu na viongozi wa baadae.

Mkuu wa Shule hiyo, Felister Mrutu alisema shule yao imekuwa ikipokea wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali bila ya kujali dini wala uraia na inazingatia maadili jambo linalowavutia watu wengi kuwapeleka watoto wao wakiwemo wa kutoka nje ya nchi.

Katika maafali hayo wanafunzi wa shule hiyo walionesha burudani mbalimbali kama kuimba, gwaride, sarakasi, karate na michezo mingine ya ukakamavu waliyofundishwa na vijana kutoka chama cha Skauti Tanzania.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)