KAMATI YA KUWAHOJI WAOMBA HIFADHI (NEC) YAANZA KAZI KAMBI YA WAKIMBIZI NYARUGUSU, KIGOMA

KAMATI YA KUWAHOJI WAOMBA HIFADHI (NEC) YAANZA KAZI KAMBI YA WAKIMBIZI NYARUGUSU, KIGOMA

August 24, 2014
PIX 1-KAMATI SELECTED
Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Kuhoji Waomba Hifadhi (NEC), Faraja Nchimbi (katikati-meza kuu) akiwa na wajumbe wa Kamati hiyo wakati walipokuwa wanawahoji waomba hifadhi (hawapo pichani) katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, iliyopo Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma. Waombaji hao wanatoka nchi mbalimbali ambapo wengi wao ni Wakongo. Zaidi ya waomba hifadhi 300 wanahojiwa na Kamati hiyo ambayo inaongozwa na Taasisi nane za Serikali ambazo ni Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP), Idara ya Wakimbizi, Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Kiongozi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Inspekta Jererali wa Polisi, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji na Shirika la Kimataifa ya Kuhudumia Wakimbizi ambao ni waangalizi wa tukio hilo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

PIX 2 -KAMATI SLECTED
Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Kuhoji Waomba Hifadhi (NEC), Faraja Nchimbi (watatu kushoto), Katibu wa Kamati hiyo, Philo Nombo (watatu kulia) ambaye anamwakilisha Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati hiyo baada ya kuwahoji waomba hifadhi katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, iliyopo Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma. Waombaji hao wanatoka nchi mbalimbali ambapo wengi wao wanatoka nchini Kongo. Zaidi ya waomba hifadhi 300 wanaendelea kuhojiwa na Kamati hiyo ambayo inaongozwa na Taasisi nane za Serikali ambazo ni Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP), Idara ya Wakimbizi, Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Waziri Kiongozi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Inspekta Jererali wa Polisi, Kamishna Mkuu wa Uhamiaji na Shirika la Kimataifa ya Kuhudumia Wakimbizi ambao ni waangalizi wa tukio hilo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

ZAHANATI YA MAJENGO YAPATA CHUMBA CHA UPASUAJI MDOGO NA KUZINDULIWA NA MWENGE HVI KARIBUNI.

August 24, 2014

Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kilindi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Muhingo Rweyamamu(mwenye 'track suit') akikabidhi Mwenge wa uhuru kwa Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe Majjid Mwanga.
Mwenge wa uhuru mwaka 2014 umeweka jiwe la msingi katika chumba cha upasuaji mdogo kilichojengwa katika zahanati ya Majengo iliyopo kata ya Manundu mjini Korogwe.

Akisoma taarifa ya mradi kabla ya kuwekewa  jiwe la msingi na Mkimbiza Mwenge kitaifa Rachel Kassanda, Mganga Mkuu wa halmashauri ya mji Korogwe Dkt Jerry Mwakanyamale alisema kuwa mradi huo ulioanza kujengwa mwaka 2013 kwa fedha za bajeti ya CDG na MMAM mpaka sasa umegharimu jumla ya Tsh.21,048,410/-
Aliongeza kuwa mwaka wa fedha 2012/2013 mradi huo ulitengewa jumla ya Tsh.34,147,000 zikiwa ni CDG Tsh.24,100,000/- ambapo Tsh .18,000,000/- zimeshaletwa na Serikali wakati MMAM ilitengwa Tsh 10,047,000 na fedha zote zimeshatolewa.
Dkt Mwakanyamale alifafanua mpaka sasa ujenzi huo ili kukamilika  umebakisha vyumba 2 vya kubadilishia nguo kabla ya kuingia chumba cha upasuaji,vyoo viwili na korido la kusubiria wagonjwa wakiwa 'theatre'
Wakizungumza na Mwandishiwa habari  katika mahojiano maalumu baadhi ya Wananchi waliohudhuria uwekaji wa jiwe la msingi katika zahanati hiyo, walisema kuwa wanaishukuru sana Serikali kwa kuzidi kuwasogezea huduma za afya jirani na makazi yao na kuongeza kuwa wana imani  chumba hicho cha upasuaji mdogo kitakuwa msaada mkubwa kwao katika masuala ya afya.
"Hii 'theatre' itatusaidia sana hasa ukizingatia kuwa Korogwe imekuwa ikikumbwa na ajali nyingi za barabarani kwa kuwa ni njia kuu ya miji mikuu ya Tanzania,hivyo itaipunguzia mzigo Magunga".Alisema Asha Hassan mkazi wa Manundu.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa wilaya ya Korogwe Dkt Rashid Said alisema kuwa chumba hicho cha upasuaji mdogo kitaisaidia sana wilaya yake kwani kitapunguza msongamano katika hospitali ya  Magunga kwa kuwa wagonjwa wengi  wa upasuaji mdogo,kufungwa na kusafishwa vidonda,walioumia katika ajali wataweza kupata huduma  katika 'thearter' hiyo ya zahanati  ya Majengo pindi itakapokamilika tofauti na sasa ambapo Magunga huhudumia wagonjwa wote na hivyo kuwa na mzigo mkubwa sana hasa zinapotokea ajali za barabarani. 
Baadhi ya viongozi wa wilaya ya Korogwe wakisikiliza taarifa ya mradi mbele ya jengo la chumba cha upsuaji mdogo katika zahanati ya Majengo mara baada ya Mwenge wa uhuru kuwasili kattika zahanati hiyo

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Majjid Mwanga akimkaribisha kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Rachel Kassanda wilayani Korogwe (Kilole),akitokea wilaya ya Kilindi.

MAMA SALMA KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA JAJI MSTAAFU LEWIS MAKAME, TANGA

August 24, 2014

 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimfariji Mama Mary Mbaga Makame, mjane wa Marehemu Jaji Lewis Mhina Makame mara baada ya kuwasili kijijini Tongwe, wilayani Muheza  kwa ajili ya mazishi tarehe 23.8.2014.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimfariji Mama Mary Mbaga Makame, mjane wa Marehemu Jaji Lewis Mhina Makame mara baada ya kuwasili kijijini Tongwe, wilayani Muheza  kwa ajili ya mazishi tarehe 23.8.2014.
DIAMOND ATANGAZA NDOA YAKE NA WEMA RASMI ASEMA UWANJA WA TAIFA UTUMIKA ILI MASHABIKI WAKE WOTE WAHUDHURIE

DIAMOND ATANGAZA NDOA YAKE NA WEMA RASMI ASEMA UWANJA WA TAIFA UTUMIKA ILI MASHABIKI WAKE WOTE WAHUDHURIE

August 24, 2014


Diamond na Wema wamekuwa katika mahusiano ya muda mrefu, wakiachana na kurudiana.
Diamond na Wema wamekuwa katika mahusiano ya muda mrefu, wakiachana na kurudiana.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platinumz ametangaza ndoa na mchumba wake wa muda mrefu Wema Sepetu anayosema itafungwa hivi karibuni. Msanii huyo ghali zaidi nchini kwa sasa, ametamka hayo alipozungumza na Mwanaspoti nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam juzi Jumatano. Alisema kuna mambo mengi yaliyomchelewesha kufikia hatua hiyo, ikiwamo maandalizi kwani amepanga mashabiki wake wahudhurie harusi hiyo.
“Ndoa ni kitu cha heri na baraka, lakini kitu kinachofanya kidogo mambo yachelewe ni kwamba sisi au mimi ni mtu ninayefahamika, kwa hiyo hata ndoa yangu watu wengi wanatamani waihudhurie,” alisema Diamond.
Pia amesisitiza kwamba ndoa si jambo la masihara kwani ni tendo la kiimani na ndio maana amekuwa makini katika mipango yake.
“Nataka kila kitu kishuhudiwe na mashabiki, ninaweza hata kuifanyia Uwanja wa Taifa,” aliongeza.
“Unajua nilishindwa kufanya mambo haya haraka kwa sababu wengi nadhani wangeamini kwamba ninafanya hivyo ili kutafuta umaarufu zaidi, tunataka tufanye kiusahihi yasije tokea mambo kama ya Instagram tunataka tuje kuwa mfano wa kuigwa.”
Alipoulizwa tarehe ya ndoa hiyo Diamond alisema: “Nilishasema ni hivi karibuni, unajua siku zote vitu vya kheri waswahili wanasema lazima uvifiche, hata Mwenyezi Mungu naye anasema anampenda mtu aliye na siri, lazima vitu vingine uvifiche ili vipate kufanikiwa.
Wakati mwingine kunakuwa na husda, hasidi kwa hiyo ukiviweka wazi sana vinaweza kutofanikiwa.”
Taarifa kwamba Diamond hataoa zilisambaa na kudaiwa kumchefua mchumba wake Wema Sepetu ambapo katika mahojiano mkali huyo wa wimbo ‘Mdogo Mdogo’
“Kwanza sikuwahi kusema siwezi kuoa, nilishtushwa na gazeti hilo, nilisikitika kwa kweli na iliniuma sana, lakini nikaona nikijibu nitaonekana kwamba sina adabu, kwa sababu siku zote anayeanza huwa haonekani lakini anayemaliza.
Pia siwezi kubishana na vyombo vya habari, mwisho wa siku ni watu haohao nitawategemea wanifanyie kazi zangu,” alisema.
Hata hivyo Diamond alisema mchumba wake anaumizwa na vichwa vya habari ambavyo vimekuwa mwiba kwake.
“Hata hivyo magazeti yetu tumeshayazoea jinsi yanavyoandika, wakati mwingine inakuwa kama chachandu au kufurahisha baraza,” aliongeza.
Kuhusu taarifa kwamba ameachana na mchumba wake huyo, alisema: “Hatuna tatizo watu wengi wanasema tumeachana, lakini hatujaachana na hatuwezi kujibishana.
“Sijui nikujibu nini kwa sababu kila nitakachokujibu utaona namsifia kwa sababu yule ni mchumba wangu”
Na Mwanaspoti.