Waziri Nape aongeza hamasa mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga

Waziri Nape aongeza hamasa mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga

February 20, 2016

NNA2
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (kushoto)walipokutana katika mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Afrika na Simba Sports Club katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.(Picha na: Frank Shija,WHUSM)
NNA3
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na mashabiki wa mpira wa miguu wakati wa mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Afrika na Simba Sports Club katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.
NNA4
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na mashabiki wa mpira wa miguu wakati wa mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga Afrika na Simba Sports Club katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.
NNA5
Mabeki wa Timu ya Simba wakiokoa mpira wa hatari katika lango lao wakati wa mechi dhidi ya Yanga iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam.Mechi hiyo imeisha kwa wenyeji Yanga Afrika kuibuka kidedea kwa mabao 2:0.
NNA7
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba akishangilia mara baada ya Donald Ngoma kuiandikia Yanga bao la kwanza mnamo Dakika ya 38 ya mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam. Hadi dakika 90 zinayoyoma Simba SC ililala kwa mabao 2 : 0.
NNA8
Mbunge wa Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Mhe. Venance Mwamoto akifuatilia mchezo kati ya Yanga Afrika na Simba SC uliofanyika katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam. Hadi dakika 90 zinayoyoma Simba SC ililala kwa mabao 2 : 0.
NNA9
Mashabiki wa Timu ya Simba SC wakifuatilia mchezo kati yao na Yanga Afrika uliofanyika katika Uwanja wa Taifa leo jijini Dar es Salaam. Hadi dakika 90 zinayoyoma Simba SC ililala kwa mabao 2 : 0.
YANGA YAIBURUZA SIMBA MAGOLI 2-0 UWANJA WA TAIFA LEO, YAPAA KILELENI MWA LIGI

YANGA YAIBURUZA SIMBA MAGOLI 2-0 UWANJA WA TAIFA LEO, YAPAA KILELENI MWA LIGI

February 20, 2016

ya1
Wachezaji wa timu ya Yanga wakishangilia mara baada ya kufuga goli la pili katika mchezo wao wa ligi kuu kati yao na timu ya Simba zote za jijini Dar es salaam kwenye uwanja wa Taifa mjijini Dar es salaam, katika mchezo huo Yanga imeibuka na magoli 2 huku simba ikiangikia pua kwa kutoka uwanjani bila goli. 
ya4
Mchezaji wa timu ya Simba ya jijini Dar es salaam akitapatapa kuutafuta mpira katikati ya wachezaji wa Yanga wakati wa mchezo wao uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
ya5
Mashabiki wa timu ya Yanga wakishangilia kwa nguvu mara baada ya timu yao kuibuka na ushindi mnono wa magoli 2-1 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.
……………………………………………………………………………………………………………………..
YANGA leo imeendeleza umwamba kwa Simba katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu baada ya kuinyuka kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo wa duru la kwanza baina ya timu hizo kwenye uwanja huohuo Septemba mwaka jana, Yanga ilishinda kwa idadi kama hiyo ya mabao.

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI MHANDISI NGONYANI ATEMBELEA BANDARI YA TANGA.

February 20, 2016
PRO wa Mamlaka ya Bandari TPA Tanga,Moni Jafuru akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa wilaya ya Tanga,Abdulla Lutavi kulia ili amkaribishe  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani wa kwanza kushoto aliyefanya ziara ya kutembelea Bandari hiyo.

Kaimu Mkuu wa Bandari ya Tanga,Capt Andrew Matilya akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja baina yao na
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani kushoto  ambaye alitembelea bandari hiyo kuona namna inayofanya kazi zake
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani kushoto akizungumza na viongozi wa mamlaka ya Bandrai Mkoani Tanga wakati alipfanya ziara yake kulia kwake ni
Kaimu Mkuu wa Bandari ya Tanga,Capt Andrew Matilya



PRO wa Mamlaka ya Bandari TPA Tanga,Moni Jafuru akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa wilaya ya Tanga,Abdulla Lutavi kulia ili amkaribishe  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani wa kwanza kushoto aliyefanya ziara ya kutembelea Bandari hiyo
 







Kaimu Mkuu wa Bandari ya Tanga,Capt Andrew Matilya kushoto akimuonyesha baadhi ya maeneo yanayotumika kupakulia mizigo nangani  Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani wa kwanza kulia alipofanya ziara ya kuitembelea Bandari hiyo.


Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano katikati  Eng. Edwin Ngonyani akisisitiza jambo wakati alipofanya ziara ya kuitembelea Bandari ya Tanga kushoto ni Kaimu Meneja wa Bandari ya TangaKaimu Mkuu wa Bandari ya Tanga,Capt Andrew Matilya

Kaimu Mkuu wa Bandari ya Tanga,Capt Andrew Matilya katikati akiwa na Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano katikati  Eng. Edwin Ngonyani wakitembelea Bandari ya Tanga .

 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katikati  Eng. Edwin Ngonyani kwenye shuti akimsikiliza Kaimu Mkuu wa Bandari ya Tanga,Capt Andrew Matilya kushoto akimuelezea namna wanavyofanya kazi kulia ni Moni Jafuri ambaye ni PRO wa Bandari ya Tanga wakati alipofanya ziara ya kuitembelea
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani kwenye shuti katikati akitembelea bandari ya Tanga kushoto kwake ni Kaimu Mkuu wa Bandari ya Tanga,Capt Andrew Matilya


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akitazama matishari yaliyonununuliwa na Mamlaka ya Bandari Mkoani Tanga yanayotumika kwa ajili ya ukuaji wa mizigo.
Yanga yaendeleza ubabe kwa Simba, yaichapa goli mbili kwa bila

Yanga yaendeleza ubabe kwa Simba, yaichapa goli mbili kwa bila

February 20, 2016



Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) imeendelea leo jumamosi kwa michezo mitano huku mchezo ulivuta hisia za mashabiki wengi wa soka ukiwa ni pambano la watani wa jadi Yanga na Simba.
Katika mchezo huo ambao Yanga ilikuwa wenyeji umemalizika kwa Yanga kuendeleza ubabe kwa  watani zao Simba baada ya kuwafunga goli mbili kwa bila na huku ikikumbukwa kuwa mchezo wa mzunguko wa kwanza Yanga iliibuka na ushindi sawa na ushindi wa leo.
Mchezo ulianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu huku Simba ikionekana kujisahau kwa kucheza faulo nyingi karibu na maeneo ya lango lao nao Yanga wakionekana kuwa wajanja kwa kutengeneza ukuta imara ambao washambuliaji wa Simba walishindwa kuupita.
Katika dakika ya 25, beki wa Simba, Abdi Banda alionyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi wa mchezo huo, Jonesia Rukyaa baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kumchezea faulo mshambualiji wa Yanga, Donald Ngoma.
Dakika 10 mbele baada ya Banda kuonyeshwa kadi nyekundu, Yanga ilifanikiwa kupata goli kupitia kwa Donald Ngoma baada ya beki Hassan Kessy kurudisha mpira ambao hakuupiga kwa kasi kwa golikipa wa Simba, Angban na ndipo Ngoma alipouwahi kasha kumpiga chenga golikipa na kufunga goli ambalo lilidumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili mpira kilianza kwa timu zote kufanya mashambulizi ya kushtukiza na kurudi kulinda lango lao na katika dakika ya 72, Amissi Tambwe aliiandikia Yanga goli la pili nala ushindi ambalo lilidumu hadi mwamuzi, Jonesia Rukyaa anapiliza filimbi ya kumaliza mchezo huo.
Katika mchezo huo timu zote zilifanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji ili kuona kama wanaweza kubadili hali ya mchezo ambapo kwa Simba walimtoa Mwinyikazimoto, Hamisi Kiiza na Ibrahim Hijib na nafasi zao kuchukuliwa na Nova Lufunga, Danny Lyanga na Brian Majwega.
Yanga wao walifanya mabadiliko kwa kumtoa Haruna Niyonzima na Deus Kaseke na nafasi kuchukuliwa na Simon Msuva na Godfrey Mwashiuya.
Vikosi:
Yanga: Barthez, Abdul, Bossou, Twite, Mgwali, Ngonyani, Kaseke, Kamusoko, Tambwe, Ngoma na Niyonzima.
Simba: Angban, Kessy, Tshabalala, Juuko, Banda, Majavi, Mkude, Kazimoto, Kiiza, Hijib na Ndemla.
MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO MAALUM WA WANARUKWA NA KATAVI

MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO MAALUM WA WANARUKWA NA KATAVI

February 20, 2016

sm1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Februari 20, 2016 kufungua mkutano Malum wa Wanarukwa na Katavi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
sm2
Waziri Mkuu, Kasim Majlaliwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda wakifurahia ngoma baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Februari 20, 2016 kufungua mkutano Malum wa Wanarukwa na Katavi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
sm3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wakitazama badhi ya magari ambayo baba wa taifa , Mwalimu Julius Nyerere aliyatumia kwenye miaka ya 1950 na 1960 baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Februari 20, 2016 kufungua mkutano Malum wa Wanarukwa na Katavi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
sm4
 Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akizungumza katika mkutano Maalum wa Wanarukwa na Katavi uliofunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam Februari 20, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
sm5
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akifungua   mkutano Maalum wa Wanarukwa na Katavi  kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam Februari 20, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
sm6
 Baadhi ya wananchi wa Mikoa ya Katavi na Rukwa wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majliwa wakati alipofungua  mkutano maalum wa  Wanarukwa na Katavi  kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam Februari 20, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
sm7
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akionyesha Tuzo Maalum aliyotuzwa na  Wanarukwa na Katavi katika mkutano wao maalum uliofunguliwa na Waziri Mkuu,  Kassim Majalwa kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam Februari 20, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

OFISI YA MBUNGE WA VITI MAALUMU (CHADEMA) MKOANI MWANZA KUZINDULIWA RASMI HII LEO.

February 20, 2016
Viongozi mbalimbali wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ngazi ya Mkoa na Taifa hii leo wanatarajia kuzindua Rasmi Ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema) iliyopo Mtaa wa Ghana, Kata ya Nyamanoro Jimboni Ilemela.

Uzinduzi huo utaambana na shughuli mbalimbali ikiwemo kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure. Pichani juu ni Secretary wa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema).
Pichani ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoani Mwanza (Chadema), Susan Maseke.
Kushoto ni Ofisi ya Katibu  (Mwenye Miwani) wa Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema) na Kulia ni Ofisi ya Katibu wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA).
Jengo la Ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoani Mwanza (Chadema), Susan Maseke ambayo inatarajiwa kuzinduliwa Rasmi hii leo. Ofisi hii iko GreenView, Mtaa wa Ghana Kata ya Nyamanoro, Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG
DKT.KIGWANGALLA AFANYA KIKAO CHA PILI NA KIKOSI KAZI CHA KUBORESHA HUDUMA ZA MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF)

DKT.KIGWANGALLA AFANYA KIKAO CHA PILI NA KIKOSI KAZI CHA KUBORESHA HUDUMA ZA MFUKO WA AFYA YA JAMII (CHF)

February 20, 2016
kamati 2 kigwangalla
Baadhi ya wajumbe wa kikosi kazi hicho wakiendelea na majumu yao.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla amekutana kwa mara ya pili na kikosi kazi cha watu 24 ambacho kitakuwa na kazi ya kutengeneza mpango mkakati wa kuwezesha kuboresha Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).
Mkutano unaoendelea katika ukumbi wa Wizara hiyo ya Afya, leo Februari 20th, 2016 unachambua mambo mbalimbali ya kuweza kuyafanyia maboresho na ya kimkakati ilikuweza kufikia malengo ya Mfuko huo wa Afya ya Jamii (CHF).
Katika Mkutano huo, Dkt. Kigwangalla ni mwenyekiti wa kikosi kazi hicho ambapo kwa ujumla na wajumbe hao wapo kupanga mikakati thabiti.
Baadhi ya Wajumbe wa kikosi kazi hicho wanaoshiriki kikao ni pamoja na Prof. Angwara Kiwara, Prof. Phares Mujinja, Dkt. Francis Frederick, Dkt. Heri Marwa, Dkt. Deogratius Pisa, Dkt. Amos Kahwa, Irene Kiria, Semkae Kilonzo, Gemini Mtei, Dkt. Jehovaness Aikaeli na Obey Assey.
Wengine ni Mathias Kabunduguru, Dkt. Dereck Chitama, Prof. Flora Kessy, Florence Mwanri, Athuman Rehani, Maximillian Mapunda, Bedason Shallanda, Daniel Ngowi, Beng' Issa, Edwin Mikongoti, Hussein Sengu, Dkt. Beatus Leon na Dkt. Pastory Sekule.
imeandaliwa na Andrew Chale,modewjiblog
kamat66
Mkutano huo ukiendelea.
kamati 78Baadhi ya wajumbe wa kikosi kazi hicho wakimsikiliza Naibu Waaziri wa Afya Dkt.Kigwangalla (Hayupo pichani) wakati wa mkutano huo unaoendelea Wizarani hapo.
kamati 8
kamatii
kamati 3
Naibu Waziri Dkt.Kigwangalla ambaye ni Mwenyekiti wa kikosi kazi hicho (kulia) akiwa pamoja na baadhi ya wajumbe hao. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog).

Wingi wa vizuizi wawakera wafanyabiashara wa mazao ya misitu.

February 20, 2016
Na.Ahmad Mmow,Lindi.
Wingi wa vizuizi vya ukaguzi barabarani umetajwa kusababisha rushwa na usumbufu kwa wafanyabiashara wanaosafarisha mazao ya misitu.
Hayo yalielezwa jana na wafanyabiashara wa mbao na magogo kwenye warsha ya wafanya biashara wa mbao na magogo wa uwanda wa Selous hadi Ruvuma, iliyofanyika jana katika manispaa ya Lindi.

Wakizungumza kwenye warsha hiyo iliyoandaliwa na mashirika ya kiraia ya Jumuiko la Maliasili Tanzania(TNRF), Mtandao wa Kijamii wa Usimamizi wa Misitu(MJUMITA) uhifadhi, usimamizi na maendeleo ya mpingo(MCDI) kupitia kampeni ya mama misitu inayofadhiliwa na serikali ya Finland kupitia ofisi za WWF zilizopo nchini, walisema vizuizi hivyo vinasababisha rushwa, usumbufu na kuwapotezea muda.

Frank Nganyanyuka alisema wingi wavizuizi unasababisha wafanyabiashara hao kupoteza muda mwingi barabarani.

Alisema kutoka Nachingwea hadi Dar-es-Salaam kuna vizuizi takribani 19, ambavyo vinasababisha wachelewe barabarani
"Wastani kila eneo lenye kizuizi tunatumia saa moja, maana yake siku mzima inakwisha kwa ajili ya kusimama, vizuizi vipunguzwe havinafaida zaidi ya kuchochea rushwa tu," alisema Nganyuka.

Mfanyabiashara Mikidadi Kinogeandanga wa Lindi, alisema licha ya kuchelewa lakini pia maofisa waliopo katika vizuizi hivyo niwasumbufu na hawaziamini nyaraka ziliandikwa na maofisa wenzao wa kule zilikotoka mbao na bidhaa nyingine za misitu. Alihoji nisababu gani zinazosababisha wasiwaamini wenzao ambao wanadhamana na mamlaka kama yao.

Alibainisha ili kuepuka kuchelewa wanajikuta wanarahisha usumbufu kwa kutoa chochote, kwa madai bila kufanya hivyo wanasumbuliwa hata kama hawakiuki, sheria, taratibu na kanuni.
"Malendego, Jaribu, Kimanzichana sijui wapi, niusumbufu tupu, lakini yote hayo nikutaka rushwa tu," alisema Kinogeandanga.

Ali Kinunga anayefanyia biashara yake wilayani Kilwa, licha kuyalalamikia wingi wa vizuizi alilaumu serikali kutowashirikisha wafanyabiasha wa mazao ya misitu ili kupata maoni yao kabla ya kupitisha sheria ambazo baadhi yake siyo rafiki na zinawaumiza.

Alitolea mfano mabadiliko ya tozo mbalimbali ambayo yamekuwa yakiwaumiza. Kwamadai kuwa wanaotengeneza kanuni na sheria hawajui matatizo na vikwazo wanavyokutanavyo wafanyabiashara. Badala yake wamekuwa wakitoa maagizo tu. 

Naye Bakili Kilete anayefanyia biashara yake katika wilaya hiyo ya Kilwa, alisema sheria zinazohusu misitu siyo rafiki kwa wafanyabiashara ikiwamo na uwepo wa vizuizi vingi visivyo natija kwa serikali na wafanyabiashara.
"Usumbufu na wingi watozo unasababisha tutafute njia nyingine ili tupate faida, maana kwa sheria zilizopo kama utataka utii na kutekeleza huwezi kufanyabiashara hii," alisema Kilete.

Akijibu malalamiko ya wafanyabiashara hao, mratibu wa usimamizi shirikishi wa misitu nchini, Joseph Kigula, alisema sababu ya kuwepo vizuizi vingi ni kwasababu baadhi ya wafanyabiashara sio waaminifu.

Akibainisha kuwa wafanyabiashara wangekuwa waaminifu kusingekuwa na sababu ya kuwa na vizuizi vingi.
Fungwa S.Kilozo Founder of Lindiyetu.com & Kickzacelebrity.blogspot.com P.o.Box 285, Lindi, Tanzania Mob.+255787572019 OR +255713572019 Email: fkilozo@gmail.com or lindiyetu@gmail.com

UNUNUZI WA GARI LA HALMASHAURI YA NACHINGWEA UTATA MTUPU

February 20, 2016
Na.Ahmad Mmow, Lindi-Nachingwea.
Ununuzi wa gari lenye namba usajili DFPA 1695, Landcruiser mali ya Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, mwanzo mwanzo mwa wiki iliyopita ilizua mvutano baina ya madiwani na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Mhandisi, Jackson Masaka.
Landcruiser
Wakizungumza kwenye mkutano wa pili cha baraza la madiwani kwa mwaka wa fedha 2015/2016 Madiwani hao walisema walikuwa na mashaka katika ununuzi wa gari hiyo, kutokana na mabadiliko ya mara kwa mara ya fedha zilizotumika kununulia gari hiyo na bila kuwashirikisha.

Diwani wa kata ya Mkutokuyana, Sada Makota, alisema mchakato wa ununuzi wa gari hiyo umegubikwa na utata, kwa madai kuwa fedha ambazo awali zilitengwa kwa ununuzi wa gari hiyo ni shilingi 84 milioni, wakati zilizoidhinishwa kwenye bajeti ni shilingi milioni 120.00 tu, hata hivyo ilionekana ilinunuliwa kwa shilingi 124.76 milioni.

Alisema licha ya ongezeko hilo, lakini pia taarifa haikuonesha fedha za nyongeza zilitoka wapi na kwaidhini ya nani.

Diwani wa kata ya Lionja, Joachim Mnungu, alisema mkurugenzi alikuwa na kila sababu ya kuwajulisha madiwani kila hatua iliyohusu mchakato wa ununuzi, ikiwamo mabadiliko ya mara kwa mara ya bei.

Alisema fedha zilizokatengwa kwa ajili ya ununuzi ni shilingi 84 milioni. Hata hivyo kabla ya gari hiyo kuletwa, bei ilipanda na kufikia shilingi 96 milioni.

Kama hiyo haitoshi, baada ya kuletwa waliambiwa imenunuliwa kwa shilingi 124.76 milioni.
"Gari imekuja na namba za usajili za gari za misaada (DFPA) tena mtumba, wakala wa manunuzi gani anaweza kuleta gari yenye namba za usajili wa magari ya misaada," alisema na kuhoji Mnungu.

Mkurugenzi mtendaji, Mhandisi Masaka akijibu hoja za madiwani hao, alisema ingawa yeye alikuwa hajahamia katika Halmashauri hii, wakati mambo hayo yanafanyika.

Lakini taarifa zinaonesha mchakato ulikwenda sawa bila kukiuka taratibu, kanuni na sheria. Kwani ununuzi ulifanywa na wakala wa manunuzi wa serikali(GPSA) na kwamba shilingi 4 milioni ziliongezeka kutokana na gharama ya kusafirisha gari hiyo ambayo gharama yake halisi ni shilingi 115milioni.
"Hizo shilingi 95.4 milioni zilirejeshwa na GPSA baada yakuonekana hazitoshi kununua gari iliyokuwa inatakiwa, ilibidi ziongezwe fedha" gharama ya gari ni shilingi 115, kusafirisha ni dola 4,354 sawa na shilingi 9milioni," alifafanunua Mhandisi Masaka.

Alisema kiasi kilichongezeka kilitoka kwenye akaunti ya utawala. Nakwamba kiasi kilichoongezeka(shilingi 4milioni) kiliweza kutolewa bila kupata idhini ya madiwani kwani sheria inampa mkurugenzi uwezo huo.

Akibainisha kuwa gari hiyo siyo ya msaada bali walilazimika kuchukua kabla ya taratibu kukamilika baada ya kupewa maelezo na GPSA kuwa wanaweza kusubiri hadi taratibu za usajili zikamilike au waipokee na wakati wowote wakachukue namba za usajili.
"GPSA walitoa maelekezo kama tunaweza kusubiri au tupokee gari hiyo, ili baadae ikakachukuliwe baada ya taratibu zote kukamilika ikiwa ni pamoja na namba za usajili," alibainisha Masaka.

Hatahivyo majibu hayo hayakuwaridhisha. Diwani wa kata ya Ugawaji, ambaye pia ni mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Ahmad Makoroganya, alisema hakubaliani na majibu hayo kwani hadi baraza la madiwani la Halmashauri hiyo linavunjwa mwaka jana, mchakato wote kuhusu ununuzi wa gari hiyo ulikuwa umekamilika, ulibaki ufuatiliaji tu.

Hivyo maelezo yaliyotolewa na mkurugenzi ilibidi waelezwe kipindi cha mchakato wa ununuzi.

Madai ya madiwani hao yaliungwa mkono na mkuu wa wilaya hii ya Nachingwea, Pololeti Mgema, ambae alisema wataalamu walishindwa kuonesha thamani ya dola kwa shilingi ya Tanzania kwenye mabadiliko hayo ya bei ambayo yalikuwa yanafanyika.

Aliwashauri madiwani hao waendelee kuhoji ili wapate maelezo yanayojitosheleza kwenye mkutano au waunde kamati ya uchunguzi, ambayo pamoja namambo mengine ichunguze uhalali wa gari hiyo kubandikwa namba za usajili wa magari yanayotolewa kwa msaada na wahisani.

Mvutano ulikwisha baada ya madiwani hao kukubaliana kujadili suala hilo kwenye kikao cha kamati ya madiwani, baada ya baraza hilo kujigeuza nakuwa kamati.MWISHO.
Fungwa S.Kilozo Founder of Lindiyetu.com & Kickzacelebrity.blogspot.com P.o.Box 285, Lindi, Tanzania Mob.+255787572019 OR +255713572019 Email: fkilozo@gmail.com or lindiyetu@gmail.com