TAARIFA KUTOKA SIMBA KUHUSU MLINDA MLANGO SAID MOHAMED

August 28, 2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Klabu ya Simba inapenda kuwajulisha wanachama na mashabiki wake kuwa,Golikipa wake wa kimataifa,Said Mohamed Nduda amepata matatizo ya goti ambayo yamempelekea kueleka India kwa ajili ya matibabu.

Nduda aliumia mazoezini wakati timu ikijiandaa kuelekea mchezo dhidi ya Yanga wiki ilipita,Matibabu hayo yatamuweka mchezaji huyo nnje kati ya wiki nne hadi sita kabla ya kujiunga tena na wenzake kwa ajili ya mazoezi na anatarajiwa kuondoka nchini mwishoni mwa wiki hii.

Klabu pia inayofuraha ,kuwaambia kuwa wachezaji wake John Bocco na Haruna Niyonzima ,ambaye alipata majeraha madogo juzi wameshaanza mazoezi na wenzao hii leo.

Huku pia Shomari Kapombe ambaye ni majeruhi wa muda mrefu naye anatarajiwa kuanza mazoezi siku chache zijazo baada ya madaktari kuthibitisha uzima wa afya yake.

Mwisho,Klabu inaufahamisha umma wa watanzania kupitia vyombo vya habari kuwa taarifa zote rasmi za klabu ya Simba zitakuwa zikitolewa katika mfumo na barua hii(Heading paper)

Pia Klabu inawaomba washabiki wake kote nchini kuendelea kuiunga mkono timu yao ili iendelee kufanya vizuri kwenye ligi kuu iliyoaanza wikiendi iliyopita.

Imetolewa na Mkuu wa Habari na Mawasiliano

Haji.S.Manara
SIMBA NGUVU MOJA

YALIYOJIRI KWENYE UZINDUZI WA MFUKO WA ELIMU WILAYANI IKUNGI

August 28, 2017
BMG Habari, Pamoja Daima!
Jumamosi iliyopita, Agost 19,2017 Wilaya ya Ikungi mkoani Singida ilizindua rasmi “Mfuko wa Elimu Ikungi” ulioanzishwa wilayani humo kwa lengo la kusaidia utatuzi wa kero za elimu ikiwemo uhaba wa maabara, madarasa, vyoo pamoja na nyumba za waalimu.

Katika uzinduzi huo, pia zilifanyika shughuli kadhaa ikiwemo uzinduzi wa ligi ya soka ya “Ikungi Elimu Cup 2017” yenye lengo la kuhamasisha wananchi pamoja na wadau mbalimbali kuchangia Mfuko wa Elimu Ikungi, uzinduzi wa zoezi la ufyatuaji wa matofali ambapo kila Kata wilayani Ikungi imeazimia kufyatua matofali elfu kumi.

Karibu kwa dakika chache kutazama yaliyojiri kwenye uzinduzi huo ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi ambaye aliwakilishwa na Katibu Tawala mkoani humo Dkt.Angeline Lutambi huku mwenyeji wake akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi na mlezi wa Mfuko wa Elimu Ikungi, Mhe.Miraji Jumanne Mtaturu. Tazama video hapo chini. Attachments area Preview YouTube video UZINDUZI WA MFUKO WA ELIMU WILAYANI IKUNGI

HIZI NDIO MECHI KUBWA ZA WATANI WA JADI BARANI AFRIKA

August 28, 2017
Na Jumia Travel Tanzania

Miongoni mwa matukio yanayosisimua zaidi kwenye mchezo wa soka ni mipambano ya watani wa jadi. Katika nchi nyingi barani Afrika ukiwauliza kwa harakaharaka mashabiki wengi wa soka ni mechi zipi huwa wanazisubiria sana utawasikia wanakutajia michezo kama vile Real Madrid na Barcelona, Manchester United na Manchester City, Inter Milan na AC Milan, Liverpool na Manchester United, Chelsea na Arsenal au Bayern Munich na Borussia Dortmund.
Kutokana na umaarufu wa soka la nchi za Ulaya imekuwa ni rahisi kwa mechi zao kufuatiliwa kwa urahisi ukilinganisha na huku Afrika. Lakini hiyo haimaanishi kwamba bara la Afrika nalo halina michezo ya namna hiyo ambayo ikiwa inakaribia homa miongoni mwa mashabiki huwa juu kuliko kawaida.

Ukweli ni kwamba mechi za namna ya mifano iliyotajwa hapo juu zipo na zimekuwa zikichezwa kwa miaka mingi tu.kw au pengine inawezekana ukawa unazisikia tu lakini haujui umuhimu uliopo pindi zinapokutana. Jumia Travel imekukusanyia orodha ya mechi kali za mpira wa miguu ambazo timu zikikutana kunakuwa ni patashika, presha na vimbwanga vya kila aina.  
Orlando Pirates dhidi ya Kaizer Chiefs (Afrika ya Kusini) -  Soweto derby. Kama yalivyo mapambano mengine ya watani wa jadi, mchezo huu ni zaidi ya mpira wa miguu kwani ni uhasama hasa. Mchezo ambao umpewa jina la ‘Soweto derby’ huzikutanisha timu za Orlando Pirates na Kaizer Chiefs mara kadhaa ndani ya mwaka katika jiji la Johannesburg. Uhasama wa timu hizi mbili unakuja kutokana na kuwa zote zinatokea sehemu moja. Kaizer Chiefs ilianzishwa na aliyekuwa mmojawapo wa wachezaji wa Orlando Pirates, Kaizer Motaung.
   
Wydad Casablanca dhidi ya Raja Casablanca (Morocco) - Casablanca derby. Hakuna ubishi kwamba nchi za Afrika ya Kaskazini zimebarikiwa kuwa na vipaji lukuki vya mpira wa miguu ambapo mpaka hivi sasa vinaliwakilisha vema bara hili sehemu mbalimbali duniani. Katika mji wa Casablanca kwenye nyakati tofauti za mwaka kunakuwa na mchezo mkali ambao huzikutanisha timu za Wydad Casablanca na Raja Casablanca ambao pia hujulikana kama ‘Casablanca derby’. Mchezo wa watani wa jadi hawa mara nyingi hupigwa katika uwanja wa Mohammed V Stadium ambapo licha ya kuonyesha nani ni fundi wa kusakata kandanda lakini pia ni juu ya nani ni bora katika anga za kuliwakilisha jiji na nchi kwa ujumla.  
Al Ahly dhidi ya Zamalek (Misri) - Cairo derby. Linapokuja suala la mchezo wa soka basi mashabiki wa timu za Al Ahly dhidi ya Zamalek ni nambari moja kwa kuzishangilia timu zao. Mojawapo ya mitanange mikali kabisa ya soka ambayo hutawaliwa na presha na msisimko mkubwa ni pindi timu hizi zinapokutana ambao pia umepewa jina la ‘Cairo derby.’ Inapofikia siku ya mechi hii hali ya hewa ya jiji zima la Cairo hubadilika kutokana na homa ya mchezo huo. Mbali na kuwa ushindani huwa ni wa kisoka lakini kwa upande mwingine ni wa kisiasa zaidi.
    
Club Africain dhidi ya Espérance Sportive de Tunis (Tunisia) - Tunis derby. Katika jiji la Tunis kwenye ratiba tofauti za mchezo wa soka huzikutanisha timu mbili zinazowakilisha jiji hilo za Club Africain na Espérance Sportive de Tunis. Ushindani mkubwa katika mchezo huu umekuwa na historia tofauti ambapo hapo awali ulihusishwa na matabaka kama vile ilisemekana timu ya Espérance ilikuwa ikimilikiwa na serikali na tabaka la juu la watu wa mji wa Tunisia huku Club Africain ikimilikiwa na watu maarufu wa matabaka tofauti. Lakini hiyo imebadilika na ikawezekana kutokuwa na ukweli ndani yake kwani unaweza kukuta watu wa familia moja wanashabikia hizo kwa wakati mmoja.
  
Simba S.C. dhidi ya Young Africans S.C. (Tanzania) - Dar es Salaam au Kariakoo derby. Tukiachana na umaarufu wa mchezo wa mpira wa miguu katika nchi za Afrika ya Kuskazini pia katika kalenda za soka barani Afrika huwa inapigwa mechi kali sana kwenye ukanda wa Afrika ya Mashariki baina ya timu za Simba na Young Africans au Yanga ambazo zote hutokea jiji la Dar es Salaam. Mbali na timu hizo kukutana katika michezo kadhaa ya ligi kuu pia kuna michezo mingine ni pamoja na ngao ya jamii, kombe la shirikisho la mpira wa miguu, kombe la mapinduzi ne mingineyo. 
Kama ni mgeni kwenye jiji la Dar es Salaam basi ikifika siku ya mchezo huo utajua homa ya watani wa jadi wa timu hizo mtaani kwani utawatambua mashabiki wa timu hizo kwa mbwembwe, tambo na shamrashamra kwa kuvalia jezi za rangi nyekundu na nyeupe (Simba) huku Yanga ni (kijani na njano). 

Uhasama wa timu hizo ambazo zinatokea katika eneo moja la Kariakoo si tu kuhusu mpira bali ni heshima juu ya nani ni mfalme na bingwa wa kusakata kandanda nchini Tanzania na kuliwakilisha taifa kwenye anga za kimataifa. Mchezo baina ya timu hizi mbili huwa unapigwa kwenye uwanja wa taifa ambao unao uwezo wa kukusanya mashabiki takribani 60,000.
USM Alger dhidi ya MC Alger (Aljeria). Mchezo huu wa watani wa jadi kama ilivyo mingine huzitenganisha familia na majirani na wakati mwingine huisha kwa ugomvi na vurugu baina ya mashabiki wa pande mbili. Uhasama baina timu ya hizi mbili unahusishwa kwa kiasi kikubwa na historia ya nchi hiyo wakati wa harakati za kudai uhuru. Katika sehemu mbalimbali za nchi ya Aljeria mchezo baina ya timu hizi mbili hubakia kuwa ni tukio la kitaifa kutokana na kuzungumziwa na kupewa nafasi kubwa kwenye vyomo tofauti vya habari.

TP Mazembe dhidi ya FC Lupopo (R.D Congo). Jina la TP Mazembe sio geni miongoni mwa mashabiki wengi wa soka nchini Tanzania kutokana na wachezaji wa hapa nyumbani Mbwana Samata ambaye alifanikiwa kujitwalia taji la mchezo bora wa ndani wa Afrika na Thomas Ulimwengu kuchezea pale. Katika jiji la Lubumbushi kila mwaka kunakuwa na tukio kubwa la mchezo wa soka ambalo huwakutanisha watani wa jadi kati ya TP Mazembe na FC Lupopo.

Gor Mahia dhidi ya AFC Leopards (Kenya) - Nairobi au Mashemeji derby. Shamrashamra na tambo za mashabiki wa mchezo wa mpira miguu katika mitaa mbalimbali ya jiji la Nairobi huonekana wazi pindi timu za Gor Mahia na AFC Leopards zinapokutana. Mchezo huu ambao una historia ya muda mrefu kwenye soka nchini Kenya huchukuliwa kama ni siku kubwa ambapo mashabiki licha ya kuonyesha uhasama mkubwa lakini ni sherehe, likizo na huchukuliwa kama siku maalum.
Asec Mimosas dhidi ya Africa Sport Abidjan (Ivory Coast) - Abidjan derby. Miongoni mwa tukio baya kutokea pindi timu hizi mahasimu zinazotokea katika jiji la Abidjan nchini Ivory Coast ni mwaka 2001 ambapo vurugu zilitokea ambapo mtu mmoja alifariki huku 30 wakijeruhiwa. Timu ya Asec Mimosas inajivunia kwa kutoa vipaji vikubwa kabisa vya soka nchini humo na duniani wakiwemo Kolo Toure, Didier Drogba na Gervinho.

Al-Merreikh dhidi ya Al-Hilal (Sudani). Uhasama wa timu hizi mbili zinazotokea kwenye jiji la Omdurman nchini Sudan ambapo mnamo mwaka 1934 timu ya Al-Merreikh iliifunga Al-Hilal kwa mabao 2 bila ya majibu ambapo kulikuwa hakuna uwanja enzi hizo. Uhasama baina ya timu hizo mbili pia huchochewa kwa kiasi kikubwa na idadi ya wachezaji kila timu iliyo nayo kwenye kikosi cha timu ya taifa.      
Ipo michezo mingine mingi tu ya watani wa jadi kwenye soka lakini hiyo ndiyo mikubwa ambayo inasubiriwa na kuangaliwa zaidi. Jumia Travel inaamini kwamba sasa utakuwa umeijua na utaanza kuifuatilia kwani kuna burudani nyingi ulikuwa ukiikosa kwa kutoifuatilia. Mechi hizo kutokupewa nafasi kubwa na vyombo vya habari tofauti barani Afrika kama ilivyo kwa ile ya Ulaya haimaanishi kwamba haina ushindani mkubwa.

NMB Holds a Business Executive Network Meeting for Top end Business and Corporate Customers in Dar es Salaam

NMB Holds a Business Executive Network Meeting for Top end Business and Corporate Customers in Dar es Salaam

August 28, 2017
 
The NMB Bank’s Managing Director - Ms Ineke Bussemaker making opening remarks at the Executive Network event organized by NMB Bank in Dar es Salaam over the weekend. Over 150 high end customers attended the event where they also benefited from TAX training organized by Pricewaterhousecoopers. 
NMB Bank Managing director, Ms Ineke Bussemaker exchages views with Checknoctras Limited Head of Operations Mr Balraj Bhatt (left) and Head of Finance for the same company at the Executive Network event organized by NMB Bank in Dar es Salaam over the weekend. Over 150 high end customers attended the event where they also benefited from TAX training organized by Pricewaterhousecoopers.[/caption]   NMB Bank Plc has today organized a customer networking meeting with its top end Business Customers and Corporates. The meeting attracted over 150 customers from Dar es Salaam. The discussion of the meeting focused on ways to improve business and the impact of the 2017/2018 budget for businesses relationship between the bank and its customers. The NMB Business Executive Network is organized in large commercial cities of Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Morogoro, Mbeya, Mtwara, Kilimanjaro and soon to launch in Dodoma. The NMB Managing Director – Ineke Bussemaker, said that the aim of holding such meetings is to strengthen business relations with its top end business and corporate customers. “NMB is committed in ensuring that customers get the best service while the bank supports to their business growth. The bank has done major improvements and innovations to suit the need of customers. Private Banking and the launch of business centers in big cities are among the improvements,” said Ineke. Ms Bussemaker further said “the improvements done by the bank so far will help to bring services more closely to this segment of customers. They will not only get the best services but also acquire financial, regulatory, business and forex information in order to become and remain competitive.” She further said after the banks successfully implemented the business clubs which targeted Micro, Small and Medium Enterprises (MSME), the bank decided to start the business executive network to bring in the large business customers.     
NMB Bank Managing Director - Ms Ineke Bussemaker exchages views stockholders at the Business Executive Network event organised by NMB Bank in Dar es Salaam over the weekend. Over 150 high end customers attended the event where they also benefited from TAX training organized by Pricewaterhousecoopers.

WATAALAMU WAAINISHA UMUHIMU WA KUIPITIA UPYA SERA YA MAENDELEO YA VIWANDA ENDELEVU (SIDP 1996-2020) IENDANE NA WAKATI

August 28, 2017

WATAALAMU na wanazuoni wamekubaliana haja ya kupitia mpango wa maendeleo endelevu wa viwanda, SIDP (1996-2020), ili kwenda na wakati kwa kubadili kilimo na kuiweka nchi katika njia bora ya kufikia uchumi wa viwanda.
Kauli hiyo imetamkwa kwa namna tofauti na wataalamu hao ambao wamekutana jijini hapa kuangalia uhusiano uliopo kati ya viwanda, mabadiliko ya tabia nchi na kilimo; na ni namna gani sera ya viwanda inaweza kupitiwa upya kuakisi mahusiano haya.
Warsha hiyo iliyoandaliwa na ESRF na CUTS International imelenga katika kuelezea umuhimu wa kuangalia  mahusiano ya sera ya maendeleo ya viwanda na mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na biashara.
Wakijadili mada mbalimbali zilizowasilishwa katika semina hiyo iliyofanyika ESRF, wataalam hao walitambua umuhimu  wa pekee wa kupitia upya sera hiyo ili iweze kuonesha muunganiko fasaha uliopo kati ya viwanda, kilimo na biashara; na hatua/mikakati ipi iwepo kukinga adhma hii ya viwanda dhidi ya athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Wamesema kwamba kwa kuunganisha sera ya maendeleo endelevu ya viwanda na uchakataji wa bidhaa za kilimo na kilimo chenyewe kunaleta mwanya wa kuweka msingi imara katika mchakato wa maendeleo na hasa viwanda. Pia, kwa kuwa na sera madhubuti, nchi itaweza kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika sekta ya Viwanda, hususani viwanda vinavyotegemea maligafi za sekta ya kilimo.
Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida wakati wa mkutano wa awamu ya pili ya kuangalia Tabia nchi, Uboreshaji kilimo, na mahusiano yake na biashara kwa jumuiya ya Afrika Mashariki (PACT EAC2), uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo ilikubalika haja ya kuwa na mikakati ya utetezi kwa kuangalia tafiti zitakazofanywa juu ya kinachojiri katika maendeleo kwa kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula na biashara. Zaidi ya yote, pia wadau waliona kuna haja kubwa ya kuwa na tafiti itayoweza kuonesha ni kwa kiasi gani sera ya SIDP (1996-2020) imeweza kuchangia katika ukuaji wa viwanda Tanzania, na changamato zipi imekumbana nazo ambazo zinapaswa kutatuliwa na kuanishwa wakati wa mapitio ya sera hii.
Akiwasilisha hoja yake ndugu Solomon Baregu, Mtafiti wa ESRF na Meneja wa Mradi wa PACT EAC 2, amesema kwa kuangalia hali halisi ya sasa ipo haja kwa wataalamu kutambua changamoto zinazojitokeza katika maendeleo endelevu ya viwanda na kukiangalia kilimo kama msingi wa uimarishaji wa viwanda.
Aidha alisema kwamba kwa kuangalia hali ya sasa ipo haja kubwa ya kubadili kilimo cha Tanzania ili kuboresha maisha ya wananchi na kuimarisha viwanda kwa kuvipatia mali ghafi ya kutosha na yenye ubora.
Alisema ni vyema kuelewa uhusiano uliopo katika sera za maendeleo ya viwanda na kilimo ili kuwa na mpango mahsusi wa utetezi kwa lengo la kuimarisha viwanda.
Katika mkutano huo washiriki pia walipitia mambo mbalimbali na hatua zinazochukuliwa kupitia sera ya mpango wa maendeleo wa viwanda unaomalizika 2020.