TANZANIA YAPOKEA MSAADA WA TRIONI MOJA KUTOKA GLOBAL FUND KUSAIDIA TB,UKIMWI NA MALARIA

January 29, 2018

 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Makamu wa Rais (Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora (kulia), na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamisi Shaaban, wakisaini hati za makabidhiano ya sh. trioni moja zilizotolewa na Shirika la Global Fund kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kusaidia mapambano ya Ukimwi, TB na Malaria katika hafla iliyofanyika Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam leo. Wengine waliosimama katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  na viongozi wengine kutoka Global Fund.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk. Mpoki Ulisubisya, akizungumza katika hafla hiyo.

Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania, Frederic Clavier, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mnufaika wa Global Fund, Joan akielezea jinsi alivyo nufaika na shirika hilo.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaishi na VVU-Ukimwi, Mwinuka Juastine, akizungumza.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamisi Shaaban (kulia), akimkabidhi hati ya makabidhiano Mwakilishi wa Global Fund Tanzania, Linden Morrison.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Makamu wa Rais (Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora, akizungumza.
Taswira ya ukumbi wa mkutano katika uzinduzi huo.


Na Dotto Mwaibale

SHIRIKA la Kimataifa la Global Fund limetoa shilingi trioni moja kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya mapambano ya magonjwa ya ukimwi, malaria na kifua kikuu kwa mwaka 2018-2020. 

Akizungumza katika hafla ya kutiliana saini makabidhiano ya fedha hizo baina ya mfuko huo na serikali Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema fedha hizo ni muhimu sana kwa nchi yetu.

Alisema fedha hizo zitaelekezwa katika kupambana na magonjwa hayo ambapo kwa ugonjwa wa ukimwi zimetolewa sh.bilioni 769, TB sh. bilioni 67 wakati malaria sh.bilioni 320.

Alisema fedha hizo zitatumika kikamilifu kwa lengo lililokusudiwa na zitasimamiwa  na Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Afya na Mashirika Yasiyo ya kiserikali.

Alisema katika masuala ya ukimwi zitatumika kwa ajili ya vipimo, dawa za kurefusha maisha na kufubaza virusi kwa wagonjwa wa ukimwi na katika ugonjwa wa malaria fedha hizo zitatumika kwa ajili ya vipimo na matibabu pamoja na kununua vyandarua.


"Kwa upande wa wagonjwa wa TB ni asilimia 40 tu ndio waliofika kwenye vituo vya afya na kuthibitika kuwa na maambukizi na wamepatiwa matibabu lakini tunataka hadi ifikapo mwaka 2020 tunataka asilimia 70 ya watanzania watakaogundulika kuwa na maambukizi wajulikane na wapatiwe matibabu" alisema Ummy.

Ummy aliongeza kuwa kati ya wagonjwa 100 wenye maambukizi ya TB wagonjwa 90 waliothibitika kuwa na maambukizi walitibiwa na kupona kabisa.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amewataka Katibu Mkuu wa Wizara yake, Tamisemi na Ofisi ya Rais kuhakikisha wanazisimamia vizuri fedha hizo ili kupata matokeo mazuri waliyo yakusudia.

Mratibu wa Watu Wanaotumia Dawa za Kulevya Tanzania (TANPUD), Happy Assan alisema mradi huo utawasaidia sana na kuhakikisha hawataathirika ukizingatia kuwa fedha hizo zitawafikia walengwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaishi na VVU-Ukimwi, Mwinuka Juastine alisema mradi Global Fund imewasaidia waathirika 900,000 kwa kuwapa dawa za kupunguza makali ya ukimwi ARV na kufubaza virusi vya ugonjwa huo.



Regards Tone Multimedia Company Limited Sinza B, Kwa Remi Kijitonyama P.O Box 32529 Dar es salaam Tanzania Tel +255 22 2772919 Fax +255 22 2772892 E-Mail blogzamikoa@live.com Facebook: www.facebook.com/blogszamikoa WeB: www.blogszamikoa.co.tz 1458109219454_logo_blog_za_mikoi.png

MAWAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO WA TANZANIA NA RWANDA WAJADILI UJENZI WA RELI YA ISAKA- KIGALI

January 29, 2018
 Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ofisi ya Waziri wa Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Mkutano kuhusu upatikanaji wa Fedha za mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kuanzia Isaka Shinyanga  hadi Kigali nchini Rwanda.
 Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia), Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe.  Gatete Claver (kushoto) na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Eugene Kayihura (kulia) wakiwa katika majadiliano ya pamoja kabla ya kuanza kwa mkutano kuhusu namna ya kupata fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda.
 Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (wa pili kushoto) na Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe.  Gatete Claver (wa pili kulia) ukiendelea kuhusu upatikanaji wa fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe.  Gatete Claver (wa pili kulia) akizungumza jambo wakati wa mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) kuhusu upatikanaji wa fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe.  Gatete Claver (kushoto) na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (kulia) wakiondoka baada ya kumalizika kwa mkutano kuhusu upatikanaji wa fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda Jijini Dar es Salaam.
 Ujumbe kutoka Wizara ya Fedha na Mipango ukiongozwa na Waziri Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) na kutoka Rwanda ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe.  Gatete Claver (wa pili kulia) wakifurahia jambo baada ya kumalizika kwa Mkutano kati yao Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Tanzania Bw. Doto James (kulia) na mwenzake wa Rwanda Bw. Caleb Rwaunganza wakisaini maagizo kutoka kwa Mawaziri wa Wizara hizo mbili kuhusu hatua za upatikanaji wa fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Tanzania Bw. Doto James (kulia) na mwenzake wa Rwanda Bw. Caleb Rwaunganza wakibadilishana taarifa walizosaini za maagizo kutoka kwa Mawaziri wa Wizara hizo mbili kuhusu hatua za upatikanaji wa Fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)
Benny Mwaipaja, WFM
Mawaziri wa Fedha na Mipango wa  Tanzania na Rwanda wamekutana  Jijini Dar es Salaam kujadili namna ya kupata fedha za Ujenzi wa Reli yenye Kiwango cha Kimataifa (SGR) kutoka Isaka Shinyanga hadi Kigali Rwanda ikiwa ni mwendelezo wa mikutano kuhusu suala hilo iliyoanza kuanzia Januari 20, 2018.
Katika Mkutano huo wamejadili kuhusu njia ambayo inaweza kuwa rahisi kupata fedha ikiwemo ya kutumia Sekta binafsi, Serikali kukopa au kumweka mwekezaji ambapo wamekubaliana kupitia upya taarifa zilizo wasilishwa mezani za pande hizo mbili  na kufanya maboresho na pia kuzungumza na Benki ya Dunia (WB), Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa pamoja ili wakati wa kikao kijacho waweze kujadili suala hilo kwa kuangalia vigezo na masharti ya kupata fedha.
Kikao hicho ambacho ni cha watalamu kimewakutanisha Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Waziri kutoka Rwanda Mhe. Gatete Claver pamoja na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura na Makatibu wakuu wa wizara hizo na wajumbe wengine.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Tanzania Bw. Doto James na mwenzake wa Rwanda Bw. Caleb Rwaungaza, wamesaini maagizo hayo ya Mawaziri kwa ajili ya utekelezaji.
Ikumbukwe kuwa mapema mwezi huu Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais wa Rwanda Paul Kagame walikubaliana kutekeleza mradi huo wa ujenzi wa Reli kutoka Isaka Shinyanga hadi Kigali Rwanda na wakatoa maagizo ya kuanza utekelezaji kwa kuangalia namna ya kupata fedha za mradi huo.

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI MTEULE DKT. WILBROD SLAA PIA AKUTANA NA MAAFISA WAKUU WA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WANAOTARAJIWA KUSTAAFU.

January 29, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa kabla ya kuzungumza na wanahabaari Ikulu jijini Dar es Salaam.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.
 
  Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa akizungumza na Wanahabari mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari mara baada ya kufanya mazungumzo na Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari mara baada ya kufanya mazungumzo na Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa Ikulu jijini Dar es Salaam.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo kabla hajaanza kuwatambulisha Maafisa Wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (hawaonekani pichani) ambao wanatarajia kustaafu.
 Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo ambaye aliambatana na Maafisa Wakuu (sita)  wa
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ambao wanatarajiwa kustaafu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo pamoja na Maafisa Wakuu (sita) wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania  wanaotarajiwa kustaafu ambao ni Mnadhimu
Mkuu wa Jeshi la Ulinzi wa Tanzania Luteni Jenerali James Mwakibolwa wanne kutoka (kulia), Meja Jenerali Michael Isamuhyo watatu kutoka
(kulia) Brigedia Jenerali Aron Robert Lukyaa wapili kutoka (kulia),
Kanali Peter Samuel Sameji wa kwanza (kulia).  Wengine katika picha ni
Brigedia Jenerali William Ephraim Kivuyo wapili kutoka kushoto na
Brigedia Jenerali Elizaphani Lutende Marembo.
PICHA NA IKULU

BASI LA KAMPUNI YA TAHMED LAUNGUA MOTO LIKIWA SAFARINI

January 29, 2018

 NA MWANDISHI WETU,HANDENI.
BASI la kampuni ya Tahmed lililokuwa linafanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Arusha limewaka moto na kuungua katika eneo la Kitumbi Kata ya Kabuku wilayani Handeni mkoani Tanga likiwa njiani huku akibiria wakinusufika baada ya kuwahi kutoka nje.
Kamanda wa Polisi mkoani Tanga,Edward Bukombe aliuambia Mtandao wa Tanga Raha kuwa  tukio hilo lilitokea leo saa nne na dakika arobaini na tano likiwa linaelekea mkoani Arusha.
Alilitaja gari hilo lenye namba za usajili T.483 DFL lilikuwa likiendeshwa na Bakari Saidi (30) likiwa na abiria sita lilipofika eneo hilo ndipo lilipowaka moto kutokana na hilifau za kiufundi .
Alisema wakati basi hilo likianza kuwaka moto abiria waliokuwepo ndani waliwahi kutoka na kujinusuru na kifo huku wakiliacha likiendelea kuungua moto .
Hata hivyo Kamanda huyo alisema chanzo cha ajali hiyo bado wanafuatilia ili kuweza kubaini moto huo ulisababishwa na nini.
“Labda nisema taarifa ya kuungua moto na kuwaka basi hilo ni kweli kwa sasa tunafanya uchunguzi kwa lengo la kubaini nini chanzo chake “Alisema.
Mwisho.

MADARASA YA NYASI, TEMBE, UDONGO YASITUMIKE KATIKA SHULE ZOTE NCHINI, WAZIRI JAFO

January 29, 2018
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafoakifungua mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakugenzi wa Halmashauri yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa ushirikiano wa Taasisi ya Uongozi yanayofanyika kwa siku Tano Mjini Dodoma.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Josephat Kandege
akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI kufungua mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri.
 Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Prof. Joseph Semboja akiwasilisha taarifa ya Utangulizi wakati wa mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri
 Mkuuwa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Joseph Mkirikiti akitoa neno la Shukrani wakati  baada ya Waziri wa Nchi TAMISEMI Mhe. Jafo kufungua mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(Aliyekaa Mbele) katika Picha ya Pamoja na viongozi wengine walioshiriki kwenye Ufunguzi wa mafunzo hayo na Wah.Wakuu wa Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri za Wilaya ya Kilwa.
Mkuu wa Wilaya ya Londido Mhe. Daniel Chongolo (kulia) akifurahia jambo na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe wakati wa mafunzo ya Uongozi.

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafoamewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi ambao kwenye maeneo yao bado kuna wanafunzi wanasomea katika madarasa ya Tembe ama yalioezekwa Nyasi au kujengwa kwa Udongo kuhakikisha wanaacha mara moja kutumia madarsa hayo na kujenga madarasa bora.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya nne ya Uongozi wa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi yanayotolewa kupitia ofisi ya Rais Tamisemi kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi yenye lengo la kujenga uwezo wa viongozi kuweza kutawala kwa ufanisi.

“Viongozi wangu nataka Mkakusanye mapato ya ndani kwa nguvu zote na Fedha hizo mzitumie kwenye miradi ya maendeleo na kwa wale ambao mpaka leo wanafunzi wanasomea kwenye mazingira duni hawana madarasa bora watoto wanasomea kwenye madarsa ya Tembe, mengine yameezekwa kwa Nyasi nahitaji muelekeze Nguvu katika ujenzi wa madarasa bora na hayo ya Tembe yotoweke kabisa; Mjenge madarasa ambayo wanafunzi watajiskia fahari kusoma”Alisema Waziri Jafo.

Waziri Jafo hakusita kuwakumbusha Viongozi  kuhusu Usimamizi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Afya 212 vinavyoendelea kujengwa hivi sasa katika ameneo
yote yote Nchini.

Niwapongezebaadhi ya Wakurugenzi ambao mpaka sasa wamefanya kazi nzuri sana ya Usimamizi wa ujenzi wa Miundombinu hiyo ya Afya wameshakamilisha ujenzi
na wamejenga mpaka Njia za kutembelea(Walk Way) katika vituo hivyo na nataka mpaka Tarehe 30 April 2018 Kila Halmashauri iliyopokea Fedha za ujenzi wa Miundombinu ya Afya iwe imekamilika.

WaziriJafo alitumia nafasi hiyo pia kuwakumbusha viongozi mara wapatapo mafunzo haya kuheshimu  mipaka yao ya kazi, kuboresha mahusiano kazini, kutunza Siri za Serikali na kusimamia Maadili katika maeneo ya kazi.

Awali akizungumza katika Ufunguzi wa  Mafunzo ya Uongozi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja
amesema kuwa mafunzo haya yanakamilisha mtiririko wa mafunzo yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Mhe. Majaliwa K. Majaliwa miezi nane iliyopita na baada ya mafunzo haya yanayoanza leo tutakuwa tumewafikia   Viongozi 324.

Prof.Semboja aliongeza kuwa Lengo la mafunzo haya ni yale yale ambayo ambayo yamelengwa tangu Kikao cha Mwanzo cha Mafunzo haya ambayo ni kuimarisha uwezo wa kufanya maamuzi wa Kimkakati  kwa kuzingatia mahitaji ya jamii
kwa manufaa mapana ya sasa nay a baade ya Jamii Tunayoihudumia.

Sambamba na hilo Mkutano huu pia unalenga kuongeza uwezo wa Viongozi wetu katika kuongoza watu na rasillimali zingine zilizoko kwenye maeneo yetu ili kwa pamoja tuweze kufikia malengo ya pamoja.

Alisisitizakuwa Mafunzo haya yatajielekeza katika Kuimarisha Sifa Binafsi za Viongozi  kwa sababu Viongozi ndio wanaowasimamia wananchi katika kiLA Eneo hivyo ni lazima kila kiongozi aweze kujitenegenezea Sifa binafsi ili akubalike na kuhesimika katika Jamii husika.

“Sifa hizi binafsi tunazozizungumzia ni Ushawishi, Kuaminika, Uadilifu, mtenda Haki, Muumini wa Utawala bora na Utawala wa Sheria na zaidi kuwa mchahapa kazi na awe na weledi wa hali ya juu sasa haya yote yatafundishwa kupitia mafunzo haya ya namna gani Kiongozi anaweza Kujijengea Sifa Binafsi katika Jamii tunazoziongoza.

Akitoa Neno la Shukrani kwa niaba ya viongozi walioshiriki katika Mafunzo haya Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Joseph Mkirikiti ameshukuru OR-TAMISEMI na Taasisi ya Uongozi kwa kuandaa mafunzo haya na zaidi ameahidi Umakini wa washiriki kwa siku zote za mafunzo.

Mafunzo haya ya awamu ya Nne na ya mwisho kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa imegususa Viongozi kutoka katika Mikoa ya
Mtwara, Lindi, Pwani, Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

DK. KIGWANGALLA AWATAKA WALIOVAMIA KIWANJA CHA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO KILICHOPO NJIRO, JIJINI ARUSHA KUJIANDAA KISAIKOLOJIA

January 29, 2018

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akipata maelezo ya eneo la kiwanja chenye hati namba 4091 kilichopo Njiro Jijini Arusha ambacho kimevamiwa na watu mbalimbali na kuanzishwa makazi yenye kaya 82 ndani ya eneo hilo kutoka Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Dk. Fredy Manongi (katikati). Eneo hilo ni mali ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na hati halisi ya eneo hilo ipo kwa jinala Bodi ya Utalii Tanzania. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua eneo la kiwanja chenye hati namba 4091 kilichopo Njiro Jijini Arusha ambacho kimevamiwa na watu mbalimbali na kuanzishwa makazi yenye kaya 82. Eneo hilo ni mali ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na hati halisi ya eneo hilo ipo kwa jinala Bodi ya Utalii Tanzania.
  Meneja wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Egidius Mweyunge (kulia) akimuongoza Waziri Kigwangalla kukagua eneo hilo.
Dk. Kigwangalla akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukagua eneo hilo.

MKAZI WA JIJI LA MWANZA AJISHINDIA MILIONI 40 ZA TATUMZUKA

January 29, 2018
 Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ilemela,Khadija Nyembo akimkabidhi mfano wa hundi  mkazi wa Buswelu,Ilemela,jijini Mwanza, Gibson Gratian Erasms,aliyejishindia kitita cha shilingi milioni 40 kwenye mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka uliofanyika jumapili iliyopita (Jackpot ya Jumapili).
 Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ilemela,Khadija Nyembo akiwa katika picha ya pamoja na Mkazi wa Buswelu,Ilemela,jijini Mwanza, Gibson Gratian Erasms,aliyejishindia kitita cha shilingi milioni 40 kwenye mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka uliofanyika jumapili iliyopita (Jackpot ya Jumapili),sambamba na baadhi ya viongozi wa Ofisi ya Wilaya na pamoja na ndugu wa mshindi huyo.

-- Ahmad Issa Michuzi Editorial Director P.O BOX 9033, DAR ES SALAAM. issamichuzi.blogspot.com www.michuzijr.blogspot.com othmanmichuzi.blogspot.com Phone:0713 422 313/ 0783 422 313 Tanzania- East Africa.