WAGANGA WAKUU WA HOSPITALI WILAYANI WAKUMBUSHWA KUENDELEA KUTOA ELIMU YA MFUKO WA BIMA YA AFYA

February 02, 2015


Wakurugenzi  na Waganga wakuu wa hospitali za Wilaya Mkoani Tanga,  wametakiwa kupita kila  kijiji na kitongoji kutoa elimu ya  kujiunga  na mfuko wa bima ya afya ili kuiwezesha Serikali kufikia  malengo iliyojiwekea.

 Akifungua kikao cha  kujadili mpango  wa mfuko wa Afya ya jamii na kusaini mkataba wa uhamasishaji  wa CHF kwa Wilaya  ya Lushoto na Muheza jana, Katibu Tawala  Mkoa wa Tanga,  Salim Mohammed Chima  alisema elimu ya mfuko wa afya ya jamii inahitajika na  kuwataka viongozi wenye  dhamana kuacha  kujifungia  maofisini.

 Alisema viongozi  wengi wamekuwa  wakishindwa kutekeleza wajibu wao wakiwemo watu wenye  dhamana kushindwa  kuhamasisha jamii kujiunga  na mifuko wa bima  ya afya ya jamii.  

 “Leo nawafungulia  kikao chenu wenyewe  cha kujadili na kuweka mikakati ya jamii kujiunga na mfuko  wa afya ya  jamii---baada ya hapa kila mmoja ahakikishe anatimiza wajibu  wake” alisisitiza Chima

  “Tumekuwa  tukikemea tabia ya wakuu wa  idara na viongozi wenye dhamana kujifungia maofisini na  kushindwa kutekeleza  wajibu wao kwa mujibu wa mikataba ya utumishi wa umma”  alisema

 Alisema tabia ya  viongozi kujifungia  maofisini na kuacha kutekeleza wajibu wao ataikomesha   ikiwemo utoro   pamoja  na muda wa kuingia na kutoka kazini na hivyo kutoa agizo la  kila mmoja kujua  wajibu wake katika kazi.

 Awali akizungumza  katika kikao hicho,  Mganga Mkuu wa Mkoa, Asha Mahita, alipinga vikali ukosefu wa  madawa katika  hospitali zake na kuwabebesha mzigo waganga wa hospitali za  Wilaya kwa uzembe  wa kuacha kuagizia dawa.

 Alisema malalamiko  yanayotoka kwa  wananchi juu ya ukosefu wa madawa ni uzembe wa waganga wakuu  wa hospitali na  hivyo kutoa wito kwa kila mmoja kuhakikisha kituo chake   kinakuwa na dawa za  kutosha ili kuondosha malalamiko kutoka kwa  wananchi.

 “Hakuna ukosefu  wa madawa hospitalini  na ikotokea ni waganga wakuu wa hospitali kufanya uzembe wa  kuacha  kuagizia-----dawa zipo za kutosha na hili nitalishughulikia  mimi mwenyewe”  alisema na kuongeza  

 “Tena natoa wito  kwa wananchi popote  katika Mkoa huu mgonjwa aendapo hospitali na kuelezwa kuwa  hakuna dawa  awasiliane na ofisi yangu au mimi mwenyewe nitalivalia njuga  ” alisema Mahita  

 Kwa kauli hiyo,  Mahita aliwataka  waganga wakuu wa hospitali za Wilaya  kuhakikisha vituo vyao  havipungukiwi na  madawa na kudai kuwa hakuna upungufu huo na yoyote ambaye  atafanya uzembe  atamchukulia hatua. Habari & picha na  Salim Mohammed, Mwananchi 
MJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM NA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. BILAL AONGOZA MAADHIMISHO MIAKA 38 YA CCM DAR ES SALAAM

MJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM NA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. BILAL AONGOZA MAADHIMISHO MIAKA 38 YA CCM DAR ES SALAAM

February 02, 2015

3
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Ramadhan Madabida akimkaribisha Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kuzungumza na Wananchi na Wanachama wa CCM Mkoa wa Dar es salaam kwenye maadhimisho ya miaka 38 ya CCM yajiyoadhimishwa  jana Februar 01,2015  kwenye uwanja wa Tawi la CCM kwa Mwinjuma Kinondoni Dar es salaam.
4
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia Wananchi na Wanachama wa CCM Mkoa wa Dar es salaam kwenye maadhimisho ya miaka 38 ya CCM yajiyoadhimishwa  jana Februar 01,2015  kwenye uwanja wa Tawi la CCM kwa Mwinjuma Kinondoni Dar es salaam.
2
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea CD yenye mashairi  maalum ya kukipongeza chama cha Mapinduzi CCM kwa kutimiza miaka 38 tangu kuanzishwa kwake kutoka kwa msanii Ahmad Amour Nyangany, kwenye maadhimisho ya miaka 38 ya CCM yajiyofanyika jana Februar 01,2015  kwenye uwanja wa Tawi la CCM kwa Mwinjuma Kinondoni Dar es salaam.
1
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Wananchi na Wanachama wa CCM Mkoa wa Dar es salaam alipowasili Viwanja vya Tawi la CCM kwa Mwinjuma Kinondoni Dar es salaam jana Februar 02,2015 kwa ajili ya kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 38 ya CCM.
5
Wananchi na Wanachama wa CCM Mkoa wa Dar es salaam wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipokua akiwahutubia kwenye maadhimisho ya miaka 38 ya CCM yajiyoadhimishwa  jana Februar 01,2015  kwenye uwanja wa Tawi la CCM kwa Mwinjuma Kinondoni Dar es salaam.
(Picha na OMR)

LULU: RANGI YA MTUME NIMEZALIWA NAYO

February 02, 2015
Urembo: Mrembo na mwigizaji wa filamu za kibongo, Diana Elizabeth Michael ‘Lulu’ hivi majuzi alitupia picha yake ya zamani mtandaoni (hiyo hapo juu) ikiwa kama ni “ThrowBackThursday” (TBT) yake, na kuiandikia mameno haya;

Temeke mabingwa Wa Proin Women Taifa Cup mara baada ya kuifunga Pwani katika fainali

February 02, 2015


Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo, Mh Dkt Femella Mukangara (wa pili kushoto) akiwasili katika uwanja wa Azam Complex Chamanzi wakati wa fainali ya Mashindano ya Proin Women Taifa Cup yaliyofikia Tamati leo kwa kuzikutanisha Timu za Temeke na Pwani.
Waziri wa habari utamaduni na Michezo, Mh Dkt Fenella Mukangara akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Temeke mara baada ya kuibuka washindi wa Mashindano ya Proin Women Taifa Cup ambayo yalichezwa katika Dimba la Azam huku Proin Promotions na Azam wakidhamini mashindano hayo.
Nahodha wa Timu ya Pwani akipokea Mfano wa hundi ya Shilingi Milioni Mbili ambazo ni zawadi ya Mshindi wa pili katika Mashindano ya Proin Women Taifa Cup na kuwamalizika kwa Temeke kuwa Mabingwa kwa kuifunga Pwani goli 1 kwa 0.
Nahodha wa Timu ya Ilala ambao ni washindi wa tatu akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni 1 ambayo mshindi wa tatu katika Mashindano hayo ni Ilala
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara (wa kwanza kulia) na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Jamal Malinzi wakishuhudia fainali ya Mashindano ya Proin Women Taifa Cup mechi iliyochezwa katika dimba la Azam Complex kwa kuzikutanisha timu za Pwani na Temeke na Temeke Kuibuka Bingwa wa Proin Women Taifa Cup kwa kuichapa Pwani goli 1 kwa 0.
Kikosi cha Timu ya Pwani
Kikosi cha Timu ya Temeke ambacho kimeifunga Kikosi cha Timu ya Pwani kwa goli 1 kwa 0 katika Mchezo wa Fainali ya Mashindano ya Proin Women Taifa Cup, mchezo uliomalizika kwa Temeke kuibuka mabingwa wa Proin Women Taifa Cup katika Dimba la Azam Complex
 Waziri Mukangala akisalimiana na timu ya Temeke pamoja na timu ya Pwani kabla ya Mechi ya Fainali ya Proin Women Taifa Cup kuanza katika dimba la Chamanzi Complex. Temeke iliibuka Mshindi kwa kuifunga Pwani Goli 1 kwa 0

Hatari langoni mwa timu ya Pwani
 Wakichuana vikali
Wachezaji wa timu ya temeke wakishangilia goli lililofungwa katika kipindi cha Kwanza cha Mchezo na kupelekea kudumu kwa dakika tisini na kuwapa ubingwa temeke.
 Mashabiki waliojitokeza kushuhudia mtanange huo 

MH.HAMAD RASHID AWAASA WANAFUNZI KUJIUNGA NA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF ILI KUPATA MIKOPO YA ELIMU NA MIKOPO YA KUANZIA MAISHA

February 02, 2015
Mgeni rasmi Hamad Rashid ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Wawi kupitia CUF akizunguza na wanafunzi walioudhuria kwenye siku ya Career Day iliyofanyika kwenye viwanja vya chuo cha Biashara (CBE) jijini Dar es Salaam
Rais wa Serikali ya Wanafunzi Katika Chuo cha Biashara,(CBE),Ramadhani S Kirungi akiwakaribisha wageni mbalimbali katika siku ya "CAREER DAY" iliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho Jijini Dar es salaam
Afisa wa PSPF Hadji Jamadary akiwa anafafanua na kuelezea  kuhusu na uchangiaji wa hiari wa PSS kwa wanafunzi wa Chuo Cha Biashara (CBE) jijini Dar es salaam
Maseko Kodalo Afisa wa Mfuko wa pensheni Wa PSPF akiwa anatoa maelekezo ya kujiunga na mfuko huo kwa mpango wa lazima, Mikopo ya Elimu na mikopo ya kuanzia maisha.
Mgeni rasmi Mh. Hamad Rashid ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Wawi kupitia CUF akitolewa ufafanuzi kufusu kazi za mfuko wa PSPF na Afisa wa PSPF Hadji Jamadary (wa pili kutoka Kushoto)

Mgeni rasmi Mh. Hamad Rashid ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Wawi kupitia CUF akipata ufafanuzi kutoka kwa wanafunzi wa Chuo kikuu cha biashara (CBE) wa kozi mbalimbali kuhusu kazi zao na maendeleo ya masomo yao.
Afisa wa PSPF Hadji Jamadary akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa wanafunzi waliotembelea banda la mfuko wa PSPF.
Wanafunzi wakiwa kwenye banda la Mfuko wa PSPF wakipatiwa elemu kuhusu mikopo ya kuanzia maisha na fao la elimu.
Afisa wa  mfuko wa Pesheni (PSPF)  Ahamed
Wanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE) jijini dar es Salaam wakijaza fomu za kujiunga na mfuko wa PSPF
Baadhi ya washiriki ya washiriki wa Cereer Day
Baadhi ya wanafunzi walioweza kutembelea banda la PSPF na kuweza kulimishwa juu ya fao la elimuna mikopo ya kuanzia maisha wakitizama mtandao wa Mfuko huo kwa njia ya simu
Mgeni Rasmi na PSPF wakiwa kwenye picha ya pamoja na Baadhi ya viongozi wa Chuo cha Biashara (CBE)  jijini Dar 


Mbunge wa Jimbo la Wawi kupitia CUF Mh.Hamad Rashid ameupongeza mfuko wa pensheni wa PSPF kwa kuwa wadhamini katika Career Day ya Chuo cha biashara (CBE) iliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho  siku ya ijumaa ambapo mbunge huyo aliweza kuwa mgeni rasmi wa tukio hilo na kuwapa hongera PSPF kwa kitendo cha kuweza kuwa pamoja na wanafunzi kwa ajiri ya kuwaandaa kuwa washiriki wazuri katika uchangiaji wa mafao mbalimbali na kuweza kupata mikopo ya elimu na ile ya kuanzia maishi

Rais wa Serikali ya Wanafunzi Katika Chuo cha Biashara,(CBE) Bw.Ramadhani S Kirungi amewashukuru wanafunzi wote walio weza kushiriki katika sherehe hizo kwani ni za kwanza toka chuo hicho kianze yapata miaka hamsini (50) hazijawahi fanyika lakini katika uongozi wake amepata bahati ya kuweza kuifanya siku hiyo, pia amewapongeza wanafunzi wa kozi mbalimbali walio weza kufanya maonesho katika viwanja vya chuo hicho kwaajiri ya kuwaonesha wahudhuriaji ufasaha wa masomo yao.

Pia Mfuko wa Pensheni wa  PSPF kupitia Maafisa wao walio weza kujitoa kwa ajiri ya kuwapa elimu ya jinsi na namna ya kujiunga na mfuko huo hususani katika fao la elimu na fao la kuanzia maisha ambapo ni mfuko mojawapo wenye manufaa makubwa kuliko mifuko mingine unaoweza kutoa huduma kulingana na mahitaji wa watanzania pasipo na ubaguzi wala upendeleo

Maseko Kodalo Ambaye ni Afisa wa Mfuko wa pensheni Wa PSPF yeye aliweza kutoa rai kwa wanafunzi wote na wananchi wote waweze kujiunga na mfuko huo ili kuweza kupata mafanikio, alitoa mifano michache ambayo inawezekana ukaimudu pindi unapo jiunga na mfuko huo ambapo kwa mwanafunzi alitaja kuwa unaweza kupata mikopo na kujiwekea akiba ili kuweza kukusaidia katika masomo, vilevile kuna mikopo ya kuanzia maisha  ambayo itakuwezesha kupata nyumba ambazo wamezijenga kwa ajiri ya mtanzania aweze kununua au kukopeshwa na baadae kuweza kurejesha mkopo huo wanyumba, pia aliongeza kwa kusema nyumba zote zimewekewa bima endapo tatizo lolote likitokea basi nyumba hizo zitakuwa salama .

Airtel yaja na Promosheni Mpya ya "shinda gari na Yatosha Zaidi"

February 02, 2015

Mkurugenzi wa kitengo cha Masoko wa Airtel Tanzania,Levi Nyakundi (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Airtel Tanzania,Beatrice Singano Mallya (pili kulia) wakifunua moja wa Gari aina ya Toyota IST ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Promosheni mpya ya Yatosha Zaidi ambayo itawawezesha wateja wa Airtel wanaotumia huduma ya Airtel Yatosha kujishindia zawadi ya Gari kupitia droo maalim itakayokuwa ikichezeshwa kila siku kwa muda wa miezi miwili,wateja watakaojiunga na Airtel Yatosha wataingia moja kwa moja kwenye droo ya Promosheni hiyo.
Mkurugenzi wa kitengo cha Masoko wa Airtel Tanzania,Levi Nyakundi (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Airtel Tanzania,Beatrice Singano Mallya (pili kulia) wakionyesha kipeperushi cha Promosheni hiyo iliyozinduliwa rasmi leo kwenye viwanja vya Mlimani City,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa kitengo cha Masoko wa Airtel Tanzania,Levi Nyakundi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Promosheni mpya ya Yatosha Zaidi ambayo itawawezesha wateja wa Airtel wanaotumia huduma ya Airtel Yatosha kujishindia zawadi ya Gari aina ya Toyota IST kupitia droo maalim itakayokuwa ikichezeshwa kila siku kwa muda wa miezi miwili,wateja watakaojiunga na Airtel Yatosha wataingia moja kwa moja kwenye droo ya Promosheni hiyo.Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Airtel Tanzania,Beatrice Singano Mallya.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Airtel Tanzania,Beatrice Singano Mallya akifafanua jambo wakati mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye uzinduzi wa Promosheni mpya ya Yatosha Zaidi ambayo itawawezesha wateja wa Airtel wanaotumia huduma ya Airtel Yatosha kujishindia zawadi ya Gari aina ya Toyota IST kupitia droo maalim itakayokuwa ikichezeshwa kila siku kwa muda wa miezi miwili,wateja watakaojiunga na Airtel Yatosha wataingia moja kwa moja kwenye droo ya Promosheni hiyo.
Sehemu ya Waandishi wa Habari wa vyombo mbali mbali wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Promosheni hiyo.
Sehemu ya Magari yatakayotolewa kwa washindi wa Promosheni ya Airtel Yatisha Zaidi.

Balozi wa Promosheni hiyo,Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya,Ney wa Mitego akiwa kwenye moja ya magari hayo.
Uzinduzi huo ilinogeshwa na burudani kutoka kwa vijana hawa.