JK AHANI MSIBA WA MUHIDIN MAALIM GURUMO JIONI HII

April 15, 2014
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh83yxs5YBE6ywVoEHC_XHtAq9KSUOsJbMK4KQWVB8xtcSWrywKRvti140hM0wqlcUWl09vgxorbMWMy8sB0b5FxfZT0WBGp0LxT1S2KKkNuz7xYQChadXyF-zkmPxwe9HK2FTkLNaeoIdB/s1600/g1.jpg
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa marehemu Muhidin Maalim Gurumo (mwenye shuka nyeupe) na wanafamilia alipokwenda kuhani msimba huo Ubungo Makuburi jioni ya leo April 15, 2014, siku ambayo marehemu alizikwa kijijini kwao Masaki, Kisarawe, Mkoa wa Pwani.
Marehemu Gurumo, aliyefariki dunia juzi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matatizo ya moyo, atakumbukwa kama Baba wa Muziki wa dansi nchini akianzia miaka ya 1960 na bendi mbalimbali ikiwemo NUTA Jazz na kumalizia na Msondo Ngoma kabla ya kustaafu muziki mwaka jana.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhgLa9VAzVwjIVsRFkexzAUZbEA1_r4tbGv4xpOPwoQu0J5zFCmcAKlBQIIFNMH4HqCYuoVW-XxDCmjESpVO21rbk7dIkMUEvH959l5qFJodlmT66FKkrgzpYYGrJXqKoTux4ey-TlIPm7R/s1600/g5.jpg
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pole Bw. Abdallah Muhidin Gurumo, mtoto wa marehemu Muhidin Maalim Gurumo na wanafamilia alipokwenda kuhani msimba huo Ubungo Makuburi jioni ya leo April 15, 2014,

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjm-9Vb9Qc-cFwJr1r9dNrt3RS9jQoi05YfnRE9fIb4AzyQ5JqOk2jl7t0OgtvVQ8wbYhazZvPXf7-0X7TWfxPy8xpftHdOspd65RnHJ-PNnp1uC_qsLnZLGhijqWj7D5gObdKO3Mw1El8x/s1600/g6.jpg
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Bw. Omar Muhidin Maalim Gurumo na wanafamilia alipokwenda kuhani msimba huo Ubungo Makuburi jioni ya leo April 15, 2014.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhvOAwozK36psQwEaFI2wpUV3Z-U7Iiiff0GPg4cLm-RqX-PqXGhSZ7iMbAGwtkw9g796sf9l9AyDoGk-trHNqq6dT6G-DjyPZ2GkHd9R5oDWIF1w5fbwlnrSTVqF3jUN0gUl8vvr6ZrBuW/s1600/g3.jpg
Sehemu ya waombolezaji
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh_aZf9cSF9JtzCW_7Bq6G8njbaOLXob094RftTIOpkyIIE81TE9hFUZP2851Z-K4UX2BUlSyMaWwTo7nAi47LPJR_xAoboYQEKAc2vei6IngLTCgwfNMsJSl5cNlcffO1C8jaZuzEFIK95/s1600/g7.jpg
 Mmoja wa wana familia Bw. Salim Zagar akitoa taarifa fupi ya msiba pamoja na mazishi kwa Mhe Rais
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEitPOfOjeAdDJcx2p-GimlC0odpZBdgSJrCsBPR9GvMa3ah4xTQQ7VXKYUTDXF0LASEdz5I07UC91jHMLZyuUBEsBLRpn7WjWN1mIoZSSSWA_ZqmmxJqHucYkBb96hnLS4WvAkAujSb7Mew/s1600/g8.jpg
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa dansi Bwana Brighton akimshukuru Rais Kikwete kwa kwenda kutoa pole ya msiba huo
CREDIT: MICUZI WEB

WASOMI NA WANASIASA WA 'BBC- BORN BEFORE COMPUTER' MNAWAFUNDISHA NINI VIJANA WA DOT COM???, NANI ANASEMA HAKUNA HATI ZA MUUNGANO!!!!

April 15, 2014


 Waasisi wa Muungano wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (kushoto) na Hayati, Abeid Aman Karume (kulia waliokaa) wakisaini nyaraka muhinchi za Hati za Muungano mwaka 1964 (mada ya historia).
******************************
''WASOMI NA WANASIASA WAKONGWE NINYI NDIYO HASA TEGEMEO LA KWELI KWA VIJANA WA KIZAZI KIPYA KWA KUMBUKUMBU MLIZONAZO KUHUSU SUALA ZIMA LA TANGANYIKA NA ZANZIBAR, BADALA YAKE MNAWALISHA SUMU VIJANA ILI KUAMINI KILE MNACHOKIELEZA MBELE YA JAMII, MNAHISI NINI KITATOKEA IWAPO VIJANA WA DOT COM WAKIAMINI MNACHOKIPIGIA DEBE???? BADALA YA KUUELEZA UMMA UKWELI  NA KUJENGA HOJA  YA HAJA ILI MUWEZE KUELEWEKA''. 

Rais Julius Kambarage Nyerere, akichanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar, huku akishuhudiwa na Rais wa Zanzibar, Abeid Aman Karume, (wa tatu kushoto) na Mhe. Rashind Mfaume Kawawa (wa kwanza kulia) wakati wa sherehe za kwanza za Muungano zilizofanyika Tarehe 26 APRIL, 1964. 
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (kushoto) na  Sheikh Abeid
Amani Karume (kulia) wakibadilishana Hati za Muungano wa Tanganyika na
 Zanzibar mwezi Aprili, 1964.
Walioshiriki katika tukio la kuchanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 24 Aprili, 1964 wakiwa katika viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam wakati wa halfa fupi ya sherehe za miaka 48 ya Muungano tarehe 26 Aprili, 2012. Kutoka kushoto ni Bi.  Khadija Abasi Rashid, Bw. Elisaeli Mrema, Bw. Hassan Omari Mzee na Bi. Sifael Mushi.

Rais Julius K. Nyerere (katikati), Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar Mhe. Abeid Amani Karume wakukagua gwaride wakati wa maadhimisho ya sherehe za Muungano zilizofanyika Zanzibar mwaka 1966.
*********************************************
TAMKO LA SERIKALI KUHUSU HATI ZA MUUNGANO

TAREHE 14 APRILI, 2014 __________________________________________________    
Siku 12 zijazo tutasherehekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kuzaliwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wamezaliwa watu ndani ya Muungano huu na wengine wana wajukuu.    

Inasikitisha sana kuwa leo, miaka 50 baadaye ipo dhana potofu inayojengwa kuwa Muungano huu si halali kwa vile hakuna Hati ya Muungano (Articles of the Union).    
Waasisi wa Taifa letu ambao tarehe 22 Aprili, 1964 kule Zanzibar walitia saini Hati hiyo, mbele ya mashuhuda, nao wameonekana kama walichokifanya kilikuwa kiini macho, na kwa hiyo kwamba waliongoza Taifa jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa msingi wa kiini macho hicho kwa miaka yote hadi Mwenyezi Mungu alipowaita.    

Mambo yote mawili yametusononesha sana sisi Serikalini, na bila shaka yamewasononesha wananchi wanaoipenda nchi yao, wanaowapenda Waasisi wa Taifa letu na kuuenzi Muungano wao.    

Madai ya kuonyeshwa Hati ya Muungano yalianza siku nyingi lakini hatukuweza kuamini hali itafikiwa ilipofikia, ambapo wapo watu wanathubutu kudai na kuapa kuwa Hati hiyo haipo.    

Ukweli ni kuwa hati hiyo ipo, ilikuwepo siku zote. 

Hata hivyo, lazima tukubaliane kuwa zipo Hati fulani ambazo ni kiini cha uwepo wetu kama Taifa huru, Jamhuri huru na Muungano huru, ambazo tunazihifadhi kama mboni ya jicho. 

Hati hizo ni pamoja na Hati ya Uhuru wa Tanganyika ya mwaka 1961, Hati ya Tanganyika kuwa Jamhuri mwaka 1962, na Hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ya mwaka 1964. 

Hati za aina hii zinahifadhiwa maeneo maalum ambayo ni salama ili zisipotee wala kuharibika. Kwa kawaida hatuzitoi, tunazifungua ili kuzihifadhi kwa namna yoyote ile.    Lakini sasa maneno yanakua mengi, tuhuma zimekuwa nyingi, dhihaka zimekuwa nyingi, kiasi cha wananchi kuanza kutiwa mashaka iwapo kweli Hati ya Muungano ipo au la.    

Hivyo, kwa maagizo na ridhaa ya Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninaleta mbele yenu Hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyotiwa saini Zanzibar na waasisi wetu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Aman Karume, ili muione na kuwahakikishia Watanzania kuwa yanayosemwa kuwa hakuna Hati hiyo si kweli. 

Hati hiyo ipo tangu wakati huo, imetunzwa vizuri na waliotutangulia, tumeirithi, na tutaendelea kuihifadhi.    Na, tukiombwa kufanya hivyo na Mwenyekiti wa Bunge Maalum nina uhakika Rais ataridhia ipelekwe huko ili kuondoa mjadala wa kama Hati ipo au la.    

Isitoshe, tufanye utaratibu wa kuweka nakala kwenye Makumbusho ya Taifa ili kila atakayetaka kuiona katika miaka mingine 50 ijayo na kuzidi aione.    

Mwisho, narejea kusema kuwa kwa upande wa Serikali tunasikitishwa na kufadhaishwa sana na tuhuma nzito kwamba labda waasisi wetu hawakuwa makini au walitufanyia kiini macho. Hatukutarajia wawepo Watanzania wenzetu, wafikie hapo.    Ni jambo zito. Vile vile hatukutarajia kuwa Serikali itatuhumiwa kuwa haikuwa makini kuhifadhi waliosaini waasisi wetu.   

 Matumaini yetu ni kuwa baada ya leo tutaendelea na mambo ya msingi kwa mustakabali, umoja na uimara wa Taifa letu badala ya kuchochea hisia kuwa Muungano wetu hauna msingi imara wa kisheria.   Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, DAR ES SALAAM.   14 Aprili, 2014

*MAMA SALMA AZINDUA RASMI UCHUNGUZI WA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI WILAYA YA BAHI - MKOANI DODOMA.

April 15, 2014


 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mkuu wa Wilaya ya Bahi Ndugu Betty Mkwasa mara baada ya kuwasili mjini Bahi kushiriki mkwenye sherehe ya uzinduzi wa uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete akiwapungia wanafunzi na wananchi wa Bahi waliohudhuria sherehe ya uzinduzi wa saratani ya shingo ya kizazi mjini hapo.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mganga wa Macho wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Frank Magupa, wakati alipotembelea maonesho ya kitabibu yaliyofanyika sambamba na upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake wa wilayani Bahi.
 Mamia ya wananchi wa Bahi wakisikiliza hotuba mbalimbali zilizokuwa zinatolewa na viongozi wa wakati wa sherehe ya uzinduzi wa upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi iliyofanyika huko Bahi, Mkoani Dodoma
 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.Kebwe Staphen Kebwe akitoa salamu hotuba kwa niaba ya wizara ya Afya wakati wa uzinduzi wa upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi huko wilayani Bahi.

*MJUMBE WA BUNGE MAALUM APONGEZWA NA WENZAKE KWA KUONYESHA MSIMAMO WAKE NA KUTETEA WANAWAKE BUNGENI

April 15, 2014


 Keki Maalum iliyoandikwa kumpongeza Bi Asha, ambayo imeandaliwa na baadhi ya Wajumbe Wanawake wa Bunge Maalum la Katiba kumpongeza Mjumbe wa Bunge hilo Mh. Asha Bakari Makame kwa umahiri wake wa kupinga udhalilishaji wa kijinsia ndani ya Bunge hilo na kuwa na msimamo.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Asha Bakari Makame akikata Keki Maalum kuashiria uzinduzi wa hafla fupi ya kupongezwa kwake kutokana na msimamo wake ndani ya Bunge Maalum la Katiba linaloendelea Mjini Dodoma. Kushoto kwake ni Waziri wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Maendeleo ya Vijana wanawake na Watoto Mh. Zainab Omar Mohammed.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Asha Bakari akimlisha Keki Mjumbe mwenzake wa Bunge hilo Mh. Zainab Omar Mohammed kwenye hafla fupi ya kupongezwa kwake.
 Munge wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Waride Bakari Jabu akitoa neno la shukrani kwenye hafla fupi ya Kupongezwa Mjumbe mwenzake Mh. Asha Bakari Makame kwa Msimamo wake ndani ya Bunge hilo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mh. Asha Bakari Makame akitoa shukrani zake kwenye hafla fupi ya Kupongezwa kutokana na kutetea jinsia ya Wanawake ndani ya Bunge la Katiba

TAMBWE ATAKA KUONGEZA BAO SIKU YA YANGA

April 15, 2014


Mshambuliaji nyota wa Simba, Amissi Tambwe amesema anataka kufunga angalau bao moja katika mechi dhidi ya Yanga, Jumamosi.

Tambwe amesema kwa kuwa wamekosa ubingwa na nafasi ya pili, anaamini mashabiki wao watakuwa na furaha kubwa kuwaona wanashinda mechi hiyo.
“Pia ningependa kufunga bao moja au zaidi kutokana na mchezo utakavyokuwa.
“Napenda kuwafunga Yanga, lakini napenda kuona timu yangu ya Simba inashinda mechi hiyo ya watani,” alisema Tambwe.
Tambwe anaongoza listi ya wafungaji bora akiwa na idadi ya mabao 19.
Idadi hiyo tayari imevuka ile ya mfungaji bora msimu uliopita, Kipre Tchetche raia wa Ivory Coast.

Mechi hiyo ya Jumamosi itakuwa ni funga dimba Ligi Kuu Bara huku Yanga ikiwa na uhakika wa kushina nafasi ya pili, wakati watani wao wanagombea kubaki katika nafasi ya nne.

HIVI NIDVYO ILIVYOKUWA ZIARA RAIS KIKWETE MKOANI TANGA HIVI KARIBUNI AZINDUA MRADI WA MAJI MKATA, AGAWA MADUME BORA YA NG'OMBE HANDENI

April 15, 2014


Chipukizi wa Mkoa wa Tanga wakimkaribisha kwa maua Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika tarafa ya Mkata, wilayani Handeni mkoa wa Tanga, Rais Kikwete yupo Mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi 
 -Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Msomela wakatia  a lipokwenda kukabidhi madume bora ya ng’ombe kwa wafugaji jana.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua baadhi ya madume bora ya ng’ombe na kasha kuwakabidhi baadhi ya wafugaji katika kijiji cha Msomela wilayni Handeni jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mmoja wa wafugaji mwenye asili ya kimasai bwana Shayo Lahoda aliyegawiwa dume bora la ng’ombe katika kijiji cha Msomela wilayani handeni jana
 .Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizindua Bwawa la Maji la Mkata wiklayni Handeni jana
 .Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na ngoma za utamaduni baada ya kuzindua Bwawa la Maji la Mkata wiklayni Handeni jana
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Bwawa la maji la Mkata muda mfupi baada ya kulizindua huko Mkata wilayani Handeni Mkoa wa Tanga jana asubuhi.Rais Kikwete yupo Mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo. 
Picha na Freddy Maro wa Ikulu

“POSHO YA WABUNGE WAPEWE WAATHIRIKA WA MAFURIKO”… MWANDOSYA.

“POSHO YA WABUNGE WAPEWE WAATHIRIKA WA MAFURIKO”… MWANDOSYA.

April 15, 2014
MJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba, Profesa Mark Mwandosya ameomba Bunge Maalumu la Katiba, kukata posho ya siku moja ya wajumbe wote wa Bunge hilo ili kuwapa pole waathirika wa mafuriko nchini, ikiwa ni pamoja na viongozi waliopata ajali ya helikopta.

Profesa Mwandosya alitoa pendekezo hilo kwa Bunge, baada ya Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta kutoa taarifa ya maendeleo ya afya za viongozi waliopata ajali ya helikopta jijini Dar es Salaam wakati wakitathimini maafa ya mafuriko hayo.

Alisema wanaendelea vizuri. Baada ya taarifa hiyo, Profesa Mwandosya aliomba mwongozo wa Mwenyekiti na kutoa pendekezo hilo la kutaka Bunge kukata posho ya siku moja ya wajumbe wote kutoa pole kwa waathirika wa mafuriko hayo.

Akijibu mwongozo huo, Sitta alisema kwa vile suala hilo lilikuwa halijajadiliwa na Kamati ya Uongozi ya Bunge, isingekuwa rahisi kwake kukubaliana au kukataa pendekezo hilo na hivyo alisema ataliwasilisha kwenye Kamati hiyo kupata uamuzi.

Katika hatua nyingine, Sitta amesema mjumbe yeyote wa Bunge hilo ambaye ataona hatendi haki katika uendeshaji wa Bunge hilo kuwasilisha malalamiko yake kwa Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge.

Aliyasema hayo bungeni mjini hapa jana wakati akijibu mwongozo wa Mjumbe wa Bunge hilo, Dk Hamisi Kigwangala aliyemtuhumu Sitta kuwa anafanya upendeleo katika uendeshaji wa bunge hilo kwa kuwapendelea wajumbe walio wachache.

Kigwangala alisema kwa vile Sitta alimpa nafasi maalumu Msemaji wa walio wachache wa Kamati Namba Nne, Tundu Lissu kutoa ufafanuzi baada ya kukatika matangazo ya TBC 1 Jumamosi, yeye pia anastahili kupewa nafasi hiyo kwa vile matangazo yalikatika akiwasilisha maoni ya Kamati hiyo.

Akijibu mwongozo huo, Sitta alisema alimwagiza Katibu wa Bunge kufuatilia. “Baadaye Katibu wa Bunge alinitaarifu kuwa baada ya kuwasiliana na watu wa TBC 1 na walipofuatilia namna matangazo hayo yalivyokuwa yakirushwa hawajabaini kama kuna mahali yalikatika wakati Dk Kigwangala akizungumza, hivyo hoja yake ikakosa nguvu,” alisema Sitta.
SENTESI KUMI NA MBILI ALIZOZITA KATIKA BUNGE LA KATIBA MH,JOSEPH MBILINYI "SUGU"

SENTESI KUMI NA MBILI ALIZOZITA KATIKA BUNGE LA KATIBA MH,JOSEPH MBILINYI "SUGU"

April 15, 2014
Screen Shot 2014-04-15 at 12.24.52 PMWajumbe mbalimbali kwenye bunge la katiba wameendelea kuwasha vipaza sauti vyao kuchangia, kutoa ya moyoni kwa kujadili sura ya kwanza na ya sita huku ishu ya serikali mbili au tatu ikizimiliki headlines zaidi.

Zifuatazo ni kauli za mjumbe Mh. Joseph Mbilinyi ambae pia ni mbunge wa Mbeya mjini April 15 2014
1. ‘Wabunge Wakristo hii ni kwaresma, ni kipindi cha toba… mnatumia kipindi hiki kufanya unafiki mbele ya Wananchi mtakuja kuhukumiwa siku itakapofika, wameharibu mchakato wakati tumeshatumia mabilioni mengi ya hela’
2. ‘Ukarabati tu wa jengo la bunge hili ili sisi tukae zimetumika BILIONI 8.2 alafu leo kwa sababu ya hotuba moja tu ya Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wote wamegeuka, wanaharibu kabisa tunashindwa kufanya mambo ya maana, wanaacha kupanga mkakati wa hoja wanapanga mkakati wa kuzomea, wameishiwa mikakati mpaka wanazomea kimkakati’
3. ‘Unakutana na mbunge tena Waziri kama rafiki yangu Mwigulu Nchemba tunataniana ananiita mzee wa Maandamano mi namuita mzee wa kuteka, ananiambia wewe Sugu sijui unataka serikali tatu sijui vipi na vipi, namwambia kwani hutaki kabisa Tanganyika anasema mi nataka Tanganyika ila nataka serikali moja, sasa kama mnataka serikali moja kwa nini uibuke kwenye hoja ya serikali mbili?
4. ‘Kuna watu ambao wanajadili vitu ambavyo hawaviamini na havipo kwenye mioyo yao na hao watu wanadhamana kwenye uongozi wa taifa hili na hii ni hatari’
Screen Shot 2014-04-15 at 1.04.32 PM5. ‘Tuko kwenye nafasi nzuri sana ya kujadili hili swala, tulijadili wakati tunaheshimiana kuliko siku tuje kulazimisha mabadiliko ambayo hatukuyapanga, tusifikie sehemu Wazanzibari hao wanaosemwa elfu sitini ndio waingie barabarani na jeshi’
6. ‘Mwenyekiti alikuja hapa akatutisha oooh sijui serikali tatu jeshi, Mwanajeshi atakuja atachukua nchi… Mwenyekiti mwenyewe alikua ni Mwanajeshi akavua uniform, Nyerere aliposema vueni uniform akavua na leo ni rais, kuna ubaya gani Mwanajeshi akitawala kama ana akili? hakuna ubaya, wanajeshi ni ndugu zetu’
7. ‘Hakuna tatizo lolote siku Mwanajeshi akija kuwa Rais kwa sababu tunae Mwanajeshi Rais Kikwete na anaendelea tu, asiweke vikwazo kwa Wanajeshi wengine ambao watakua na tija kwa taifa hili’
8. ‘Wanasema serikali tatu gharama, hivi kama gharama inaongezeka alafu tija inaongezeka kuna tatizo gani? ukifanya biashara rejareja ukitaka kuwa mkubwa ni lazima uongeze mtaji, kama huu mfumo wa serikali mbili umeshindwa kutuondolea matatizo mwengine anasema Znz wana hiki wana kile, mbona hamsemi kama mpaka umeme tunawalipia?? lakini sisi huku tunalia’
Screen Shot 2014-04-15 at 1.07.07 PM9. ‘Tuna serikali mbili na hakuna aliesimama hapa akasema serikali mbili gharama zake zipi, Wizara ngapi hapa zinapanga  majengo kila siku yanatolewa furniture? serikali tatu gharama against what? against tija? against maendeleo? against kwenda mbele?
10. ‘Sababu akili yenu ni fedha ndio maana mnaangalia faida kwamba ni fedha tu, hamuangalii faida nyingine za kijamii ambazo zitaleta tija kwa taifa hili’
11. ‘Kuna hawa ndugu zangu viongozi wa dini, tunasema hivi mara nyingi viongozi wa dini wamekosea walipochagua kuwa upande wa dola dhidi ya matakwa ya nchi, hii imetokea mfano ni Padri wa Rwanda, leo hii yukwapi? kwa hiyo viongozi wa dini wawe makini wanavyoangazia haya maswala’
12. ‘Mungu ibariki Tanganyika, Mungu ibariki Zanzibar , Mungu bariki mchakato huu wa shirikisho la Zanzibar na Tanganyika, acheni kutupiga mkwara eti tutagawana mbao… ni heri kugawana mbao kuliko kwenda kuzinguana huko mbele ya safari’
 CHANZO  http://www.babamzazi.com

TEMBO WA HIFADHI YA RUAHA KUFUNGIWA VIFAA MAALUM VYA KUWALINDA DHIDI YA UJANGILI

April 15, 2014
Tembo wakivinjari hifadhi ya Taifa ya Ruaha
Viongozi wa makundi ya tembo kati ya 20 na 30 waiishio kwenye ikolojia ya Ruaha wanatarajiwa kufungwa vifaa maalumu kwa ajili ya kufuatilia nyendo zao ikiwa ni mkakati wa kuwalinda dhidi ya ujangili.
Ikolojia ya Ruaha inayojumuisha Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (RUNAPA) ndio yenye tembo wengi kuliko eneo jingine kwa Tanzania kwa sasa hivyo zinahitajika juhudi za pamoja katika kuwalinda tembo hao.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mratibu wa Mratibu wa Mradi wa Kuboresha Mtandao wa Maeneo ya Hifadhi Kusini mwa Tanzania (SPANEST), Godwel Ole Meing'aki alisema eneo hilo lina tembo wanaofikia 20,090 ambao ni wengine kuliko eneo jingine.
Mpango huo utakaotumia teknolojia ya kisasa ya mawasiliano ya setilaiti ya utambuzi wa jiografia ya maeneo (GPS) na kompyuta utatekelezwa kupitia SPANEST ikiwa ni mkakati wa kuimarisha ulinzi dhidi ya majangili.
"Kwa kawaida tembo huongozwa na jike mkubwa ambaye anajua njia na kuelekeza kundi zima na ndio watakaofungwa vifaa hivyo. Zoezi hili linahitaji gharama kubwa kwa kuwa litahusisha wataalamu wengi" alisema.
Alisema awali Selous ndio iliyokuwa ikiongoza kwa kuwa na makundi makubwa ya tembo hapo awali lakini kutokana na zoezi la kuhesabu lililofanyika mwaka jana kwa ufadhili wa mradi huo imebainika kuwa Ruaha inaongoza.
"Kwa mujibu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyama Tanzania (TAWIRI) ambao waliendesha zoezi la kujua idadi ya tembo eneo la Ruaha ni tembo 20,090 waliopo idadi ambayo huenda miaka michache iliyopita ilikuwa zaidi ya 30,000", alisema.
Alisema tembo hao watafungwa 'Color' ambazo zitakuwa na vifaa maalumu vitakavyokuwa vikionesha mahali walipo kwa nyakati tofauti.
Alisema sambamba na kufanya zoezi hilo Shirika la Maendeleo la Kimataifa (UNDP) kupitia SPANEST litaimarisha mfumo wa mawasiliano kwenye hifadhi hizo ili iwe rahisi kwa askari, kituo na kituo kuweza kuwasiliana kwa urahisi.
Mwenyekiti wa Mpango wa Matumizi Bora ya Maliasili Idodi na Pawaga (MBOMIPA), unaojumuisha vijiji vyote vinavyozunguka RUNAPA, Philip Mkumbata alisema mpango huo ni mzuri na utasaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti ujangili hasa dhidi ya tembo.

DKT. MAGUFULI AWANYIMA LIKIZO YA PASAKA WAKANDARASI MPAKA BARABARA ZILIZOHARIBIWA NA MAFURIKO ZIKAMILIKE

April 15, 2014

WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, amewataka wahandisi wote nchini kutokwenda likizo kwa ajili ya Sikukuu ya Pasaka hadi miundombinu iliyoharibiwa na mvua itakapokamilika kukarabatiwa.
Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana wakati wa kuiaga na kuizindua Bodi mpya ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa).
Alisema kutokana na kuharibika kwa miundombinu mbalimbali nchini hakuna haja ya mhandisi kwenda likizo hata akiwa katika hali ngumu.
“Watanzania wanategemea miundombinu ya barabara na madaraja katika kupitisha mizigo na vyakula pamoja na shughuli za maendeleo, hivyo kazi hii inapaswa kufanyika na kukamilika haraka,” alisema.
Alisema kunahitajika nguvu za ziada katika kutekeleza hilo, ndiyo maana ameamua kukatisha likizo za wahandisi ili kufanikisha hilo.
“Nafanya ziara za ukaguzi katika maeneo yote yaliyoathrika na nikibaini kuna mhandisi kaenda likizo basi afungashe virago vyake huko huko na asirudi tena,” alisema.
Alitaja baadhi ya madaraja yaliyoanza kukamiliki na kutumika kuwa ni Daraja la Lindi linaloungana na Kongowe, Daraja la Mpiji Magohe na Bagamoyo ambalo hadi sasa limekamika katika tuta kiasi cha mita 75 pamoja na Daraja la Ruvu ambalo linatumika upande mmoja.
Mbali na hayo, aliitaka Bodi mpya ya Temesa kuwa makini katika shughuli zake, kwani ni miongoni mwa wahusika wakubwa pia wanaowajibika katika utekelezaji wa  miundombinu nchini.

UKAWA WAUMBULIWA SERIKALI YAONYESHA HATI YA MUUNGANO

April 15, 2014



 
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiowaonesha waandishi wa habari hati halisi ya Muungano ikulu jijini Dar es Salaam jana  jioni(picha na Freddy Maro)
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgMw5SWt7pMW1WRqlvhxuQsrM1O6rptkdQjpZwMxsLPah3eT6nHekle9qbov_pMJ7_PemOWmouxrVpDGWObpIi1cBs0udGADRdiFauPD3x9FnsjdqSxyYYYPnz9dMrCxQTYH485PqNN9SdI/s1600/D92A5133.jpg

MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA (TCAA) WAKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM.

April 15, 2014


Inspekta  Mwanadamizi  Idara ya udhibiti Maswala ya Anga,Mutesigwa Mango ,akifafanua jambo  kuhusiana na ajira za Maarubani  na wahudumu wa ndege  hapa nchini  wakati wa mkutano na wahariri wa vyombo vya habari uliohusu  kanuni na taratibu za Mamlaka hiyo,Mkuatano huo ulifanyika katika hoteli ya Peacoco  jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Fadhili Manongi .Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Udhibiti  Masuala ya Anga Julius Kamhabwa.
Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakiwa katika mkutano  uliofanyika jijini Dar es Salaam ulioandaliwa na Mamlaka ya Usafiri  wa Anga Tanzania  ambao ulilenga kuwapa elimu juu ya shughuli zinazofanywa na mamlaka hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene akifafanua  jambo  wakati alipohudhuria mkutano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga ulioandaliwa mahususi kwa Wahariri wa Vyaombo vya habari  jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia  wanaomsikiliza ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Fadhili Manongi  ,  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Udhibiti Masuala ya Anga, Julius Kamhabwa.
Picha na albart jackson