MASAUNI AKAGUA VIPENYO VYA MPAKA WA KASUMULU UNAOTENGANISHA NCHI YA TANZANIA NA MALAWI

January 23, 2017


 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipokea salamu za heshima baada ya kuwasili kituo cha Uhamiaji Kasumulu, kinachosimamia masuala ya uingiaji na utokaji nchini kwa wananchi wa Nchi za Tanzania na Malawi. Kulia ni Afisa Uhamiaji Mfawidhi wa kituo hicho, Kamishna Msaidizi Taniel Magwaza. Naibu Waziri yupo wilayani Kyela kwa ziara ya kikazi. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto),  akikagua hati ya kusafiria ya mwananchi kutoka nchi ya Malawi, Miston Chikankheni aliyekuwa anaingia  nchini katika Kituo cha Uhamiaji Kasumulu, wilayani Kyela mkoa wa Mbeya. Naibu Waziri yupo wilayani Kyela kwa ziara ya kikazi. 
 Mrakibu Mwandamizi wa Idara ya Uhamiaji, Gragiza John  akijibu maswali aliyoulizwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto) ,baada ya kutembelea moja ya vipenyo vinavyopitisha wahamiaji haramu kutoka Malawi katika mpaka wa Kasumulu. Naibu Waziri ameiagiza  idara hiyo wakishirikiana na Jeshi la Polisi kudhibiti njia hizo ili kuzuia uingiaji wa wahamiaji hao, wakati wa ziara ya kikazi wilayani Kyela.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,akumuuliza swali, Mrakibu Mwandamizi wa Idara ya Uhamiaji, Gragiza John(kulia)  wakati wa ziara yake ya kikazi ya ukaguzi wa vipenyo vinavyotumiwa na wahamiaji haramu mpakani Kasumulu kuingia nchini wakitokea Malawi. Naibu Waziri yupo wilayani Kyela kwa ziara ya kikazi. 
 Mkuu wa Idara ya Uhamiaji jijini Mbeya, Kamishna Msaidizi, Asumsio Achachaa, akizungumza na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) baada ya kutembelea mpaka waKasumulu unaotenganisha nchi za  Tanzania na Malawi wilayani Kyela. Mlima unaoonekana nyuma upo nchini Malawi. Naibu Waziri yupo wilayani Kyela kwa ziara ya kikazi. 
Afisa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Lenny Mkola, akijibu swali lililoulizwa na  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni linalohusiana na mapato  kwenye mpaka wa Kasumulu unaotenganisha nchi za Tanzania na Malawi. Naibu Waziri yupo wilayani Kyela kwa ziara ya kikazi. 

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI- WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

TTCL YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MAABARA KWA SHULE ZA SEKONDARI TABORA VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI SABA

January 23, 2017



Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Aggrey Mwanry akipokea msaada wa vifaa hivyo vya maabara ya Sayansi kutoka kwa Meneja wa TTCL tawi la Tabora Bw.James Mlaguzi,vifaa hivyo vinathamani ya shilingi milioni saba.

Meneja wa TTCL tawi la Tabora Bw.James Mlaguzi akisoma taarifa fupi ya kukabidhi msaada huo wa vifaa vya maabara vilivyogharimu jumla ya shilingi milioni saba.
Meneja wa TTCL tawi la Tabora Bw.James Mlaguzi akikabidhi taarifa aliyoisoma wakati wa kukabidhi vifaa hivyo vya maabara ya Sayansi kwa Shule za Sekondari kwa Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Aggrey Mwanry.
Baadhi ya maafisa wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule za Sekondari ya Tabora Wavulana na Wasichana nje ya Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tabora baada ya hafla fupi ya TTCL kukabidhi msaada wa vifaa vya Maabara ya Sayansi kwa Shule za Sekondari za mkoa wa Tabora.


Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Tabora Wasichana wakiwa wamebeba masanduku ya vifaa vya maabara vilivyotolewa msaada na Kampuni ya Simu Tanzania TTCL

Baadhi ya maafisa wa TTCL wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya maabara ya sayansi vilivyokabidhiwa na Kampuni hiyo ya simu Tanzania.

MAMA JANETH MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKE WA RAIS WA UTURUKI

January 23, 2017


 Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan akimueleza jambo Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli Ikulu Leo Jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akimkaribisha Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan Ofisini Kwake Leo Jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan wakifurahi na kinamama waliowalaki wakati anawasilini ofisini kwa Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli.
 Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan baada ya kusaini kitabu cha wageni Ofisini Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan.

  Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan akiongea na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli ambapo amemuahidi kuendelea kushirikiana katika kuwasaidia watoto na wanawake.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akimshukuru Mke wa Rais wa Uturuki Mama Emine Erdogan kwa kufanya ziara nchini pamoja na makubaliano ya kushirikiana katika kuiendeleza jamii leo Jijini Dar es Salaam.

KAMATI YA TAIFA YA MATUMIZI YA BIOTEKNOLOJIA SALAMA YARIDHISHWA NA UTAFITI WA MAHINDI KATIKA KITUO CHA MAKUTUPORA MKOANI DODOMA

January 23, 2017

Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia (NBC), waandishi wa habari na watafiti wakielekea ukumbuni walipowasili Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Kanda ya Kati Makutupora mkoani Dodoma leo asubuhi kuangalia shamba la majaribio la mahindi yaliyotokana na teknolojia ya uhandisi jeni (GMO)
 Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Hussein Mansour akizungumza katika mkutano huo wakati akiwakaribisha wajumbe wa NBC katika kituo hicho cha utafiti wa kilimo cha Makutupora cha mkoani Dodoma.
Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya (kkushoto), akitoa maelezo mafupi kwa wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia (NBC), kabla ya kuingia katika shamba la majaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni (GMO) chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo.
Waandishi wa habari, Lucy Ngowi wa gazeti la Habari Leo (kushoto), Dotto Mwaibale wa Jambo Leo (katikati) na Fatma Abdu wa Daily News wakijadiliana jambo katika shamba hilo la majaribio.
Mwonekano wa shamba hilo.
Mjumbe wa Kamati hiyo, Mhandisi Kissina kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, akiangalia hindi lililotokana na teknolojia hiyo.
Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya (kulia), akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia (NBC), kuhusu matumizi ya Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) walipotembelea shamba la majaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni (GMO) chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo.
Meneja wa shamba hilo, Bakar Mohamed akielezea kuhusu 
shamba hilo.

Safari ya kuelekea kuangalia shimo la kuchomea uchafu mbalimbali baada ya kufanya utafiti ikiendelea.
Wajumbe wa kamati hiyo na watafiti wa kilimo wakiangalia shimo la kuchomea uchafu mbalimbali baada ya kufanya utafiti huo.
Wajumbe wa kamati hiyo na watafiti wa kilimo wakiangalia shimo la kuchomea uchafu mbalimbali baada ya kufanya utafiti huo.
Mlinzi wa shamba hilo, Mbisi Masinga akiwa kazini.
Watafiti wa Kilimo na Wajumbe wa Kamati ya NBC wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya shamba hilo.


Na Dotto Mwaibale, Dodoma

KAMATI ya Taifa ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia (NBC) imeridhishwa na  matumizi ya Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) yenye lengo la kuwakwamua wakulima nchini.

Wajumbe wa kamati hiyo wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari wakati walipotembelea shamba la majaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni (GMO) chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo walisema hatua iliyofikiwa na watafiti hao ni kubwa hivyo haipaswi kuachwa ikapotea bure. 

Elisa Moses kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe ambaye ni mjumbe wa NBC alisema teknolojia hii ya bioteknolojia ni nzuri na inaonesha uhalisia halisi na inaweza kusaidia changamoto za ukosefu wa chakula iliyopo nchi.

"Binafsi nimefurahi kujionea hali halisi ya teknolojia hii hasa ninapoyaona mahindi haya ya GMO yalivyomakubwa kwani ni muhimu sana katika kukabiliana na ukame uliopo sehemu kubwa nchini" alisema Moses.

Mjumbe mwingine wa kamati hiyo kutoka Chemba ya Wanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo, Magdalene Mkocha alisema wamefurahi kuona jambo walilolipitisha linafanyiwa kazi vizuri na linaleta matumaini makubwa kutokana na matokeo ya jaribio hilo.

Alisema wadau wa sekta binafsi wanasubiri kwa hamu kuhusu matokeo hayo baada ya kuthibitishwa na takwimu za kisayansi kwani kwa kuangalia kwa macho mahindi yanaonekana ni bora zaidi.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Kanda ya Kati Dodoma, Sebastian Kandira alisema hapo awali tafiti hizo zilikuwa hazifikishwi kwa wakulima ndio maana zilikuwa hazieleweki vizuri lakini hivi sasa wameanza kuzielewa kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo Kanda ya Kati, Leon Mroso alisema wakati wanaanza majaribio hayo kulikuwa na changamoto nyingi kutokana na wadau kutokuwa na uelewa hasa kwa mahindi yaliyobadilishwa vinasaba kikubwa ni mshukuru Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba  kwa kufika katika shamba hili la majaribio ambalo tulipanda mahindi Oktoba 5, mwaka jana na kutupa faraja kuwa kuna kila sababu ya kuharakisha matumizi ya teknolojia hiyo ili iweze kutumika kama zinazofanya nchi zingine zinazofanya tafiti za namna hiyo. 

MBUNGE WA TANGA AWATAKA MADEREVA KUACHA KUENDESHA MWENDOKASI .

January 23, 2017
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku (pichani )amewataka  madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda jijini Tanga kuacha kuendesha mwendokasi kwani maisha ya watu yanapotea kwa sababu yao.

Sambamba na hilo amewataka kuondokana na tabia ya kupakia abiria zaidi ya mmoja wanapokuwa barabarani maarufu kama mshikaki kwani jambo hilo ni hatari kwa mustakabali wa maisha yao wanapokuwa njiani.

Mbunge huyo alitoa wito huo juzi wakati akizungumza na madereva wa pikipiki Kata ya Kirare Jijini Tanga ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuwatembelea wananchi na kuangalia changamoto zinazowakabilia kasha kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi.

Aliwataka pia kutii sheria za usalama kwa kuvaa kofia ngumu na kuacha kuwa na mbwembwe wanapokuwa barabarani jambo ambalo linaweza kusababisha ajali zinazoweza kugharimu maisha ya watu.

“Lakini pia madereva wa bodaboda hakisheni mnakuwa nadhifu kwa wateja wenu pendeni kazi ikiwemo kuacha kuvaa malapa badala yake wavae viatu vya ngazi “Alisema mbunge huyo.

Hatua ya mbunge hiyo inatokana na kuwepo kwa malalamiko kwa baadhi ya waendesha bodaboda hao kuwa wamekuwa wakikamatwa na askari wa usalama barabarani wanapokuwa kwenye shughuli zao jambo ambalo linasababisha kushindwa kufikia malengo yao.

Bakari Juma ambaye ni mwendesha bodaboda eneo hilo alisema kuwa wamekuwa wakikumbana na wakati mgumu katika kufanya shughuli hizo kutokana na kukamatwa mara kwa mara na kutakiwa kutoa faini.

Naye Zuberi Omari alimuomba mbunge huyo kuangalia namna ya kuwasaidia waendesha bodaboda hao ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha chama cha kukopa na kuweka akiba (Saccos) yao ambayo inaweza kuwa mkombozi.

Alisema hivi sasa baadhi ya watu mbalimbali wamekuwa wakianzishya vikundi mbalimbali vikiwemo vya kukopa na kuweka fedha hivyo nasi tungeweza kupata fursa hiyo ingeweza kutusaidia kukabiliana na ugumu wa maisha.

Akizungumzia suala hilo, Mbunge Mussa alisema lazima wahakikisha wanaheshimu sheria za usalama barabara kwa kuacha kuendesha mwendokasi ikiwemo kuwa na leseni za kufanya shughuli hizo ili kuweza kuzifanya kwa usalama zaidi bila kuwepo kwa usumbufu.

Mussa aliwataka pia kuacha kutumia mtindi wa kupakia abiria zaidi ya uwezo wanaakiwa kuwapakia wanaopokuwa kwenye shughuli hizo maarufa kama mshikaki kwani madhara yake ni makubwa sana kwa usalama wao na abiria hao kwani wanaweza kukumbana na ajali ikiwemo kugharimu maisha yao.

 “Leo hii ukiangalia wapo watu ambao wanaendesha vyombo vya moto kama vile bodaboda hawavai elementi lakini wanapakia abiria mishikaki sasa hawa wanakuwa na hatari kubwa kwa usalama barabarani hivyo niwatake muache suala hilo “Alisema.