MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI ZA UCHANGIAJI WA UJENZI BWENI LA MWANACHUO WA KIKE KATIKA CHUO KIKUU CHA MZUMBE

June 18, 2016

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia katika Siku ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Uzinduzi wa Kampeni za Uchangiaji wa Ujenzi wa Bweni la Wanachuo wa Kike.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia katika Siku ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Uzinduzi wa Kampeni za Uchangiaji wa Ujenzi wa Bweni la Wanachuo wa Kike ambapo aliwashi mabinti kuzingatia masomo kwanza kabla ya kuingia kwenye mambo mengi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua rasmi kampeni za uchangiaji wa ujenzi wa bweni la wanachuo wa Kike.
 Wanafunzi wa Chuo Cha Mzumbe wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye Siku ya Wahitimu wa Chuo Kikuuu cha Mzumbe na uzinduzi wa kampeni za uchangiaji wa ujenzi wa bweni la wanachuo wa kike.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Bernadetha Msigwa mwanafunzi wa chuo cha Mzumbe ambaye amepoteza uwezo wake wa kuona na anasubiri kwenda nje kwa matibabu.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea kitabu chenye orodha ya majina ya wanachuo waliohitimu katika chuo cha Mzumbe
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Msanii maarufu wa kuigiza sauti za Viongozi anayejulikana kwa jina la JK Komedian
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbali mbali wakati wa sherehe ya Siku ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Uzinduzi wa Kampeni za Uchangiaji wa Ujenzi wa Bweni la Wanachuo wa Kike Kampasi Kuu mjini Morogoro, Waliokaa kutoka kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako na Mkuu wa Chuo cha Mzumbe,Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Barnabas Samatta, kulia ni Mkuu wa mkoa wa Moro Mhe. Steven Kebwe na Rais wa Baraza la la Masajili,chuo kikuuu Mzumbe Bw. Ludovick Utouh

NAIBU SPIKA AKUTANA NA UJUMBE WA WABUNGE KUTOKA BUNGE LA CHINA

June 18, 2016

 Naibu Spika Dkt Tulia Ackson akisalimiana na Kiongozi wa Msafara wa Ujumbe wa Wabunge wa Kamati ya Mambo ya  Nje kutoka Bunge la China ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe  Zhang Haiyang wakati alipofanya mazungumzo na Kamati hiyo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
 Naibu Spika Dkt Tulia Ackson akizungumza na Ujumbe wa Wabunge wa Kamati ya Mambo ya  Nje kutoka Bunge la China  kushoto  ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe  Zhang Haiyang ambaye pia ni Kiongozi wa
Msafara huo.
 Kiongozi wa Msafara wa Ujumbe wa Wabunge wa Kamati ya Mambo ya  Nje kutoka Bunge la China ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe  Zhang Haiyang (katikati) akisanini Kitabu cha Wageni alipomtembelea Naibu Spika Dkt Tulia Ackson ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma.
 Kiongozi wa Msafara Ujumbe wa Wabunge wa Kamati ya Mambo ya  Nje kutoka Bunge la China ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe  Zhang Haiyang  akimkabidhi Naibu Spika Dkt Tulia Ackson zawadi mara baada ya kuzungumza nae ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma.
Naibu Spika Dkt Tulia Ackson akiangalia zawadi aliyopewa na  na Kiongozi wa Msafara Ujumbe wa Wabunge wa Kamati ya Mambo ya  Nje kutoka Bunge la China ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe  Zhang Haiyang
mara baada ya kuzungumza nao ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma.
(Picha na Ofisi ya Bunge)
Wanachama wa Chama cha waajiri wafanya ziara ya mafunzo TBL

Wanachama wa Chama cha waajiri wafanya ziara ya mafunzo TBL

June 18, 2016

JE1 
Meneja usalama ,afya na mazingira wa TBL Group Renatus Nyanda,akitoa mafunzo kwa wanachama wa Chama cha waajiri Tanzania( ATE) wakati walipokwenda kujifunza mambo mbalimbali yanayohusiana na usalama sehemu za kazi kwenye kiwanda cha  TBL Ilala jijini Dar es Salaam.
JE2Wanachama wa Chama Cha Waajiri Tanzania(ATE) wakimsikiliza kwa makini mtaalam wa upishi wa TBL Group  Castor Masawe, kuhusiana na  uzalishaji wa bia unavyofanyika.
JE3Wanachama wa Chama cha Waajiri (ATE) wakipewa maelekezo na Meneja usalama ,afya na mazingira wa TBL Group Renatus Nyanda wakati walipotembelea chumba cha maabara cha TBL Ilala jijini Dar es Salaam
JE4Wanachama wa Chama cha Waajiri (ATE) wakipewa maelekezo na Meneja usalama ,afya na mazingira wa TBL Group Renatus Nyanda wakati walipotembelea chumba cha maabara cha TBL Ilala jijini Dar es Salaam
JE5 
Baadhi ya wanachama cha Waajiri Nchini (ATE) wakiangalia vikombe vya tuzo mbalimbali ambavyo TBL Group ilishinda
………………………………………………………………………………………………
Kutokana na kampuni  ya TBL Group kuonyesha mafanikio ya kuwa mwekezaji bora nchini na mchango wake kutambuliwa na taasisi mbalimbali kwa kuitunukia tuzo ,imekuwa kivutio kikubwa kwa taasisi zinazotaka kupata mafanikio  kwa kutembelea viwanda vyake kwa ajili ya kupata mafunzo na uzoefu na kujua siri ya mafanikio.
Wanachama wa Chama cha Waajiri nchini (ATE) wamefanya ziara katika kiwanda cha TBL cha Ilala ambako wamepatiwa mafunzo ya usalama kazini ikiwemo kuona uzalishaji unavyofanyika kiwandani hapo.
Meneja Usalama,Afya na Mazingira wa TBL Group,Renatus Nyanda aliwapatia somo la kanuni za usalama zinazotekelezwa na kampuni hiyo ambazo zinalenga kulinda usalama wa wafanyakazi wanapokuwa kazini na nje ya kazi ikiwemo wageni mbalimbali wanaofika kiwandani hapo.
Wanachama hao walifurahishwa na mafunzo hao ikiwemo mkakati wa  kampuni hiyo kuendelea kufanya uwekezaji unaozingatia utunzaji wa mazingira,kuchangia kuendeleza uchumi wa taifa,kupunguza tatizo la ajira na kubadilisha maisha ya jamii kuwa bora.

MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI AKABIDHI VYAKULA VYA FUTARI KWA VITUO VINNE VYA KULEA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM

June 18, 2016

 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akikabidhi sehemu ya vyakula hivyo kwa Mwenyekiti wa Kituo cha Charambe Islamic Center Dkt. Haruni Kondo aliyepokea kwa niaba ya vikundi vigine vinne. Mke wa Rais amekabidhi mchele kilo 500, sukari kilo 500 na tende kilo 28, tukio hilo limefanyika katika ofisi ya Mke wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Khalifa wa Zawiyatul lqadiria, Abas Hamdan watatu kutoka kulia akiongoza dua ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na viongozi wengine wakuu wa serikali mara baada ya tukio la kukabidhi vyakula hivyo. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Mke wa Waziri mkuu Mama Marry Majaliwa pamoja na viongozi mbalimbali vya vikundi vya kulea watoto yatima na watu waishio kwenye mazingira magumu.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa na  mke wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa vikundi vya kulea watoto yatima na watu waishio kwenye mazingira magumu. Tukio hilo limefanyika katika Ofisi za Mke wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Mama Mlezi wa Kituo cha Charambe Islamic Center Asile Zahali mara baada ya kukamilika zoezi la utoaji wa vyakula mbalimbali kwa vituo vinne vya kulea watoto na watu waishio kwenye mazingira magumu. 
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa na mke wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa akizungumza na viongozi mbalimbali wa vituo hivyo kabla ya kuwakabidhi vyakula hivyo katika Ofisi yake Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

MKE wa Rais Mama Janeth Magufuli amekabidhi chakula kwa ajili ya futari wakati huu wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa vituo vinne vya kulea watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu Jijini Dar es salaam.

Vyakula hivyo vimekabidhiwa leo tarehe 18 Juni, 2016 katika ofisi ya Mke wa Rais Ikulu Jijini Dar es salaam vimejumuisha Mchele kilogramu 500, Sukari kilogram 500 na Tende kilogramu 28.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vyakula hivyo, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli aliyeongozana na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa amewatakia heri Waislamu wote katika mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuwasihi waendelee kuliombea Taifa amani na utulivu.

 (“Tunawatakia mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, katika kipindi hiki tunawaomba mzidi kuiombea nchi yetu amani, viongozi wetu wa nchi na watanzania wote kwa ujumla, nchi ikiwa na amani ndio mambo mengi mazuri yanaweza kufanyika”)

Kwa niaba ya vituo vilivyopatiwa vyakula hivyo, Mwenyekiti wa Kituo cha Charambe Islamic Center Dkt. Haruni Kondo amemshukuru Mke wa Rais kwa kutoa vyakula hivyo na ameeleza kuwa kitendo hicho kinaonesha mshikamano na ushirikiano walionao watanzania wote bila kujali tofauti ya dini, kabila wala maeneo wanayotoka.

 (“Kwa hiyo ndugu zangu mna imani ya kikristo lakini mnatambua waislamu ni ndugu zenu, wote tunajenga nyumba moja, mshikamano ndio tunu tuliyoachiwa na Baba yetu wa Taifa, leo mmeguswa kuona wenzenu tunafanya ibada na nyinyi mmeingia kwenye ibada, sasa ibada ya kutoa ni ibada kubwa sana, sio nchi nyingi katika Afrika zinafanya kitendo hiki, watu hawaelewi, ni nchi chache sana ambazo imani moja inaunga mkono imani nyingine, lakini sisi waislamu tunalitambua hili hata toka kipindi ambacho mtume wetu SWA anapigana kusimika dini hii kwa waumini alipata nusura kwa wakristo”)  

Vituo vilivyokabidhiwa vyakula hivyo ni Charambe Islamic Center, Tasofe Lqadiria, Nur Twarigatu Lqadiria na Zawiyatul Lqadiria.

MFUKO WA PENSHENI WA PPF WAANDAA FUTARI KWA WAFANYAZI WAKE DAR ES SALAAM

June 18, 2016

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (kushoto) akiongozana na mgeni Ramsi Kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA, Sheikh Ali Hamis, wakati alipofika kwenye Hoteli ya City Garden jijini Dar es Salaam jana Juni 17, 2016 kwa ajili ya kumwakilisha Mufti  Mkuu wa Tanzania katika Hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mfuko huo. Picha na Mafoto Blog
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (katikati) mgeni Ramsi Kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA, Sheikh Ali Hamis, wakiwaongoza wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, kuchukua Futari wakati wa hafla Futari iliyoandaliwa na Mfuko huo katika Hoteli ya City Garden jijini Dar es Salaam jana Juni 17, 2016.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakijisevia futari wakati wa hafla hiyo kwenye Hoteli ya City Garden jana

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akizungumza na wafanyakazi wa mfuko wake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na mfuko huo  kwenye Hoteli ya City Garden jijini Dar es Salaam, jana Juni 18, 2016. Kushoto ni mgeni rasmi, Sheikh Ali Hamis. 
 Mgeni rasmi Sheikh Ali Hamis, akizungumza na wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF,(hawapo pichani)  wakati wa hafla ya Futari iliyoandaliwa na mfuko huo  kwenye Hoteli ya City Garden jijini Dar es Salaam, jana Juni 17, 2016. Katikati ni Mkurugenzi mkuu wa Mfuko huo, William Erio.
*********************************************
Na Mwandishi Wetu, Dar
JAMII imetakiwa kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwani mfuko huo ni faraja kwa Watanzania na unaofanya mambo makubwa kwa lengo la kuwasaidia wananchi.
Wito huo umetolewa na mwakilishi wa Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Ali Hamis wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na uongozi wa mfuko huo kwa wafanyakazi wake.
Alisema kuna faida kubwa kwa wananchi kujiunga na mfuko huo kwani watafaidika na mafao mbalimbali yanayotolewa na PPF.
Aidha Sheikh Hamis alisema kuwa ipo haja kwa watendaji wa mfuko huo kuendelea kuwaelimisha wananchi ili waendelee kujiunga na PPF.
Alifurahishwa na namna uongozi wa mfuko huo ulivyoandaa hafla ya futari hiyo maalum kwa kuwafuturisha wafanyakazi wake na kwamba hilo ni jambo jema kwani wafanyakazi wanafahamiana na kubadilishana mawazo.
Sheikh Hamis aliitaka jamii kuwaenzi waasisi wa taifa hili kwa kuendelea kudumisha Amani na umoja kwani wamefanya jambo jema la kuwafanya wananchi wote kuwa kitu kimoja bila kujali dini wala kabila.
Kwa mujibu wa Sheikh Hamis,  PPF ni aina ya mfuko unaowawezesha wananchi kujikomboa.
Hivyo ameuomba uongozi wa mfuko huo uendelee na jitihada za kuwafikia wananchi kwenye maeneo mbalimbali hapa nchi na hasa maeneo ya vijijini.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa PPF, William Erio aliwashukuru wafanyakazi kwa kushiriki futari hiyo,ambayo imekuwa ikiandaliwa kika mwaka na kuwashirikisha wafanyakazi wake wote.
Naye mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi TUICO aliushukuru uongozi wa mfuko huo kwa kuwaandalia futari hiyo.
Futari hiyo ilihudhuriwa na wafanyakazi wa PPF kutoka makao makuu, kanda za Ilala, Temeke na Kinondoni.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko huo wakiwa makini kumsikiliza mgeni rasmi katika hafla hiyo, Sheikh, Ali Hamis, wakati wa hafla hiyo. 
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko huo wakiwa makini kumsikiliza mgeni rasmi katika hafla hiyo, Sheikh, Ali Hamis, wakati wa hafla hiyo. 
 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, Tawi la Tuico, akiwashukuru wafanyakazi wa mfuko huo kwa kushiriki kikamilifu katika hafla hiyo.
 Sheikh Mohamed Ali, kutoka Baraza Kuu la Waislam Tanzania BAKWATA, akiomba dua baada ya kumalizika kwa hafla hiyo. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko huo wakiwa makini kumsikiliza mgeni rasmi katika hafla hiyo, Sheikh, Ali Hamis, wakati wa hafla hiyo. 
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakijisevia futari wakati wa hafla hiyo kwenye Hoteli ya City Garden jana
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakijisevia futari wakati wa hafla hiyo kwenye Hoteli ya City Garden jana
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakijisevia futari wakati wa hafla hiyo kwenye Hoteli ya City Garden jana
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakijisevia futari wakati wa hafla hiyo kwenye Hoteli ya City Garden jana
 Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni PPF, wakifuturu katika hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mfuko huo jana Juni 17, 2016 kwenye Hoteli ya City Garden, jijini Dar es Salaam. 