HAKIKISHENI MWANACHAMA WA PSSSF ASIONDOKE OFISINI KWETU HAJARIDHIKA: CPA. KASHIMBA

October 06, 2023

NA K-VIS BLOG, DAR ES SALAA.

MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), CPA. Hosea Kashimba, amewataka watumishi wa Mfuko huo kuhakikisha kwamba mwanachama anapofika ofisini kuhudumiwa asiondoke hajaridhika.

Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, Oktoba 6, 2023 kwenye kilele cha maadhimisho wa Wiki ya Huduma kwa Wateja, alipokuwa akizungumza na watumishi wa PSSSF ofisi ya Kanda ya Kinondoni.

“Ombi langu kwenu, ule utaratibu mwanachama akiwa na tatizo anaambiwa andika barua, hatuuhitaji hapa, hizo ni taratibu za kizamani, tutatue matatizo ya wanachama wetu haraka.” Alisema.

Alisema ukigundua kuna tatizo, litatue, ukimwambia mwanachama aandike barua unamshawishi alalamike, tuhakikishe tatizo lisiwe upande wetu, huo ndio mtizamo wetu na hata kama litakuwa upande wa pili tujitahidi kulifuatilia sisi wenyewe na kulitatua, alisisitiza CPA. Kashimba.

Alisema watumishi wa PSSSF, popote walipo nchini, wahakikishe hakuna tatizo la mwanachama linalala halijatatuliwa.

Kuhusu uboreshaji wa utoaji huduma, CPA. Kashimba amewahakikishia wanachama azma ya Mfuko ni kuhakikisha wanatumia mifumo ya TEHAMA kupunguza kuonana na wanachama.

"Niwaambie wateja wetu kuanzia Juni mwakani, tumedhamiria kupunguza kuonana na wanachama, tunataka uwasilishaji madai unafanyika online, kuyachakata online, mwanachama akutane na fedha yake benki na hilo tayari tumelianza," alisema na kuongeza...nia hapa ni kumuondolea mwanachama gharama za kufuata huduma kwenye ofisiz etu, kuokoa muda, lakini pia kupunguza matumizi ya karatasi, na kwa vile karatasi ni miti, tutakuwa tumeokoa mazingira na hivyo kuisaidia Serikali katika kutunza mazingira yetu." Alifafanua.

Aidha, CPA.  Kashimba, amepongeza ushirikiano baina ya taasi yake na zile za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

Wiki ya Huduma kwa wateja ni tukio la kimataifa ambalo linaangazia umuhimu wa huduma kwa wateja na watu wanaotoa huduma kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kwa watoa huduma na wateja na kauli mbiu ya mwaka huu ni TEAM SERVICE “Ushirikiano kwa Huduma Bora.”

“Team service ni ushirikiano wa kutoa huduma, tunapokuwa kama timu inasaidia kujibu hoja za wanachama wetu, vizuri na kwa haraka, ndio maana tumekuwa na watu wa NIDA , ambao wametusaidia sana kutatua changamoto za vitambulisho vya taifa kwa wanachama wetu takriban 36 hivi.” Alisema.

Alisema, “Wanachama wetu hawa wamehudumiwa wakiwa hapa na hawakuhitaji kwenda ofisi za NIDA.” Alisema

Hata wenzetu wa NSSF, ushirikiano tulio nao ni kama timu moja, jambo likiwa kwetu, lakini linahitaji uingiliaji wa NSSF, tunaweza kuliona, kwa hiyo ujumbe wa mwaka huu unatafsiri ushirikiano huu wa kitaasisi.” Alisema CPA. Kashimba.

Alisema ushirikiano kama huu umekuwepo hata kwenye maonesho mbalimbali kama vile Sabasaba, Nane nane na kwingineko, ambapo Mifuko ya PSSSF na NSSF wamekuwa wakikaa pamoja ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wateja wao.

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba, akizungumza kwenye hafla hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba (kulia), akimkabidhi cheti cha shukrani (Appreciation), Afisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Wilaya ya Knondoni, Bi. Zuwena Abdallah, kwa ushirikiano walioutoa wakati wa wiki ya huduma kwa wateja, 2023. Kushoto ni  Mkurigenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa PSSS, Bw. Mbaruku Magawa, na Meneja wa Kanda wa PSSSF Kinondoni, Bi. Ritha Ngalo.

CPA. Kashimba (wakwanza kushoto) kwa karibu akiwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji PSSSF, Bw. Mbaruku Magawa (wapili kushoto), akichukua maoni ya mwanachama
Mkurugenzi wa Uendeshaji PSSSF, Bw. Mbaruku Magawa, akizungumza kwenye hafla hiyo.

Meneja wa Kanda wa PSSSF Kinondoni, Bi. Ritha Ngalo (kushoto), akimuhudumia mteja (mwanachama) wa PSSSF.

CPA. Kashimba akipitishwa kwenye eneo la NSSF ambao nao waliungana na PSSSF kuhudumia wanachama.

NSSF TANGA WAMSHUKURU RAIS DKT SAMIA ANAVYOPAMBANIA NCHI KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI MIKUBWA YA KIMKAKATI

October 06, 2023

 

MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Tanga Nuhu Ramadhani Mbaga akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja
MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Tanga Nuhu Ramadhani Mbaga akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja
AFISA Mkuu wa Idara ya Matekelezo wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakari Mshangama akifuatilia kwa umakini matukio mbalimbali wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya wateja 
MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Tanga Nuhu Ramadhani Mbaga katikati akikata keki na waajiri wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja
MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Tanga Nuhu Ramadhani Mbaga akimlisha cheki mmoja wa waajiri wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja
MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Tanga Nuhu Ramadhani Mbaga akimlisha keki mwandishi wa habari wa Chanel Ten Raya Kipingu wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja
MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Tanga Nuhu Ramadhani Mbaga akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa mfuko huo wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja



Na Oscar Assenga,TANGA.

MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Tanga Nuhu Ramadhani Mbaga amshukukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa jinsi anavyopambania nchi katika kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati nchini na hivyo kuongeza chachu kwao kutokana na  kuongeza wigo wa waajiriwa wapya

Mbaga aliyasema hayo wakati wa kilele cha kuhitimisha wiki ya huduma kwa wateja iliyokwenda sambamba na kuwakabidhi vyeti waajiri wakubwa katika mkoa huo Pepee ,Tanga Cement ,Maweni kwa kutambua mchango wao katika uchangiaji katika mfuko huo

Alisema utekelezaji wa miradi hiyo imewawezesha kuongeza wigo wa makusanyo kwa mkoa wa Tanga na hivyo kupanua wigo mpana wa kuongeza makusanyo katika mfuko huo kutokana na waajiri kuongezeka.

“Leo tupo kwenye kilele cha Kufunga siku ya huduma kwa wateja tunawashukuru bodi ya wadhamani ya NSSF Mkurugenzi mkuu na watumishi katika kuadhimisha wiki ya wateja lakini pia tunamshukukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa jinsi anavyopambania nchi katika kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati nchini na hivyo kuongeza chachu kwao kwa kuongeza waajiriwa wapya

Meneja huyo alisema ili kutoa huduma nzuri kwa wanachama lazima waajiri wawe wamelipa michango yao kwa wakati huku akitoa wito kwa waajiri wanaodaiwa michango na mfuko huo ikiwemo waliongia makubaliano nao kulipa michango yao kwa wakati kwa mujibu wa sheria.

Ambapo alisema michango hiyo inatakiwa kuwasilishwa mwezi moja baada ya kulipa mishahara ya wafanyakazi wao ili nao kama mfuko waweza kusimamia na kutoa huduma nzuri kwa wanachama huku akieleza kwa sasa wanaweza kulipa ndani ya siku moja wanachama wao na hivyo kupelekea furaha kwa wanachama kwa sababu wanafanyaa kazi kutoka na miongozi na sheria na taratibu.

Akizungumzia suala la rushwa ,Meneja huyo alisema jambo hilo ni adaui wa haki mtu hatakiwa kupokea rushwa wala kudai rushwa ikiwemo kutoa wito kwa wafanyakazi wenzake kufanya kazi kwa waledi pasipo kudai mtu chochote.

Alisema rushwa ina madhara makubwa kwa mfuko na ni adui wa haki na inaharibu sifa nzuri ya mfuko huo ambao umejengeka kwa muda mrefu halikadhalika serikali chini ya Rais Dkt Samia Suluhu inapinga rushwa kwa vitendo.

Alisema nao wanaunga mkono juhudi hizo za Serikali kwa kupinga na kukemea masuala ya rushwa kwenye mfuko huo huku akitoa wito kwa wananchi kutumia mifumo yao iliyopo katika kuandikisha wanachama wengi zaidi pamoja na akuchangia kwa hiari ili kuweza kuongeza wigo wa kinga ya hifadhi ya jamii kwa wananchi.

Kilele cha maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja kwa mwaka huu kimebeba kauli mbiu isemavyo “Ushirikiano kwa huduma Bora”

MAADHIMISHO YA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA: PSSSF YAGAWA MICHE KWA WATEJA WAKE MBEYA

October 06, 2023

NA K-VIS BLOG, MBEYA

MAADHIMISHO ya wiki ya Huduma kwa Wateja yamefikia kilele leo Oktoba 6, 2023 ambapo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, wametumia maadhimisho hayo kwa kujumuika pamoja watumishi na wateja (wanachama) na kisha wateja kupewa zawadi ya miche wakapande na kuitunza.

Kimsingi wiki ya Huduma kwa Wateja ni tukio la kimataifa ambalo linaangazia umuhimu wa huduma kwa wateja na watu wanaotoa huduma kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kwa watoa huduma na wateja.

Kauli mbiu ya mwaka huu ya maadhimisho hayo inatamka “Ushirikiano kwa Huduma Bora.” ikilenga kuhamasisha ushirikiano baina ya watumishi (watoa huduma) wenyewe, lakini pia ushirikiano na wateja ili hatimaye kila upande ufurahie HUDUMA BORA.

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Utumishi na Utawala wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Paul Kijazi, aliwaongoza watumishi wa Mfuko huo Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, yenye makao yake makuu jijini Mbeya, kutoa huduma kwa wateja sanjari na kuwapatia zawadi za miche, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Mfuko wa PSSSF, kuunga mkono juhudi za serikali za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza na wateja (wanachama) wa PSSSF waliofika kwenye ofisi za PSSSF jijini humo, ili kupata huduma, Bw. Kijazi alisema, Mfuko unawathamini sana na katika maboresho makubwa ya utoaji huduma, mtumishi anayekaribia kustaafu sasa atawasilisha madai kupitia mtandao.

Pia, PSSSF imewarahisishia wastaafu wake kujihakiki kupitia simu janja (Smart phones).

“Mstaafu akishajihakiki kwa alama za vidole (biometric) hatalazimika tena kuja ofisini kujihakiki, na badala yake atatumia simu janja (smart phone) kujihakiki akiwa mahala popote.” Alifafanua Bw. Kijazi.

Miongoni mwa huduma ambazo Bw. Kijazi alishirikiana na watumishi kuwahudumia wateja (wanachama) ni pamoja na huduma za Uhakiki, huduma za taarifa za michango, lakini pia kusikilzia changamoto kutoka kwa wateja na kupokea maoni kwa nia ya kuboresha zaidi utoaji huduma.

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Utumishi na Utawala wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumisjhi wa Umma (PSSSF), Bw. Paul Kijazi, (kushoto), akimhudumia mteja kwenye ofisi za Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,  Jijini Mbeya, wakati wa kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja (Customer Service Week) Oktoba 6, 2023.

Meneja wa PSSSF Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bw. Ramadhan Mgaya (kulia), akimkabidhi zawadi ya mche wa Parachichi, mmoja wa wateja wa PSSSF kwenye ofisi za Kanda jijini Mbeya,  Oktoba 6, 2023.

Mteja akihudumiwa huku akiwa na mche aliozawadiwa na Mfuko.

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Mfuko wa Pensheni PSSSF Paul Kijazi, (kulia) akimkabidhi mche wa Parachichi, mmoja wa wateja wa Mfuko huo, Kanda Nyanda za Juu Kusini, kwenye kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja, katika ofisi za Kanda zilizopo Jijini Mbeya.

Bw. Kijazi (kulia) akimuhakiki mteja (mwanachama) kupitia mashine maalum (Biometric)
Katika kujenga upendo na ushirikiano baina ya Mfuko na wateja (wanachama) Bw. Kijazi akiwapatia keki wateja waliofika PSSF Ofisi ya Mbeya Oktoba 6, 2023.
Katika kujenga upendo na ushirikiano baina ya Mfuko na wateja (wanachama) Bw. Kijazi akiwapatia keki wateja waliofika PSSF Ofisi ya Mbeya Oktoba 6, 2023.
Bw. Kijazi na watumishi wengine wa PSSSF Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, wakiwa katika picha ya pamoja na wateja wa Mfuko.

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Utumishi na Utawala wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumisjhi wa Umma (PSSSF), Bw. Paul Kijazi, (wapili kushoto), akimhudumia mteja kwenye ofisi za Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,  Jijini Mbeya, wakati wa kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja (Customer Service Week) Oktoba 6, 2023.

Wateja wa PSSSF, wakiwa na zawadi zao za miche ya Parachichi waliyopewa baada ya kuhudumiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja jijini Mbeya Oktoba 6, 2023.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Utumishi na Utawala wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumisjhi wa Umma (PSSSF), Bw. Paul Kijazi, (kushoto), akimsikilzia Meneja wa PSSSF Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bw. Ramadhan Mgaya wakai w ahafla hiyo.
Bw. Kijazi na viongozi wengine wa PSSSF, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wateja wa PSSSF, baada ya kuhudumiwa na kupatiwa zawadi ya miche ya Parachichi.

 Bw. Kijazi (katikati) na Meneja wa Kanda, Bw. Mgaya wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wengine wa Mfuko.