TEA KUENDELEA KUJENGA MABWENI YA WASICHANA

May 27, 2016

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Yombo, Christina Kasyupa wakati wa hafla ya kukabidhiwa vifaa vya kujihifadhi wanawake vilivyotolewa na Benki ya CRDB kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo. Kushoto ni Ofisa wa TEA, Happines Tandari, Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sophia Hassad na Mwalimu Emily Salumu. 
(Picha na Francis Dande) 
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Yombo wakiimbo nyimbo katika hafla hiyo. 
 Ofisa wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Happines Tandari akizungumza kaba la makabidhiano ya vifaa hivyo.
Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sophia Hassad (kushoto),
akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Yombo, Christina Kasyupa (katikati)
na mwalimu Salumu sehemu ya msaada wa vifaa vya kujihifadhia wanawake ‘taulo za
kike’ vilivotolewa na Benki ya CRDB kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania kwa ajili
ya wanafunzi wa shule hiyo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sophia Hassad (kushoto), akimkabidhi mwanafunzi wa Shule
ya Msingi Yombo, Monica Singano sehemu ya msaada wa vifaa vya kujihifadhia wanawake ‘taulo za kike’ vilivotolewa na Benki ya CRDB kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Christina Kasyupa. 
Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sophia Hassad (kushoto), akimkabidhi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Yombo, Sabina Yona, sehemu ya msaada wa vifaa vya kujihifadhia wanawake ‘taulo za kike’ vilivotolewa na
Benki ya CRDB kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Christina Kasyupa.
Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Sophia Hassad (kushoto), akimkabidhi mwanafunzi wa Shule
ya Msingi Yombo, Amina Abdalah, sehemu ya msaada wa vifaa vya kujihifadhia wanawake ‘taulo za kike’ vilivotolewa na Benki ya CRDB kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwalimu Emily Salumu.

Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje wafunguliwa jijini Dar

May 27, 2016

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akimkaribisha Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga kwenye mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika Mei 27, Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere. 
Mhe. Waziri Mahiga akiwahutubia watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara. Katika hotuba yake aliwaasa watumishi kuwa waadilifu, kufanyanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuhakikisha shughuli za kidiplomasia zinafanyika kwa tija ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Sera ya Mambo ya Nje inatekelezwa na kuifanya Tanzania kuendelea kupaa katika medani za kimataifa. 
Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akitoa taarifa ya utangulizi ya mkutano kwa Mhe. Waziri, Viongozi wa TUGHE-Taifa pamoja na wafanyakazi waliohudhuria Mkutano huo hawapo pichani. Pia alitumia fursa hiyo kumkaribisha Mhe. Waziri ili aweze kufanya ufunguzi wa Mkutano ambapo tukio hilo liliambatana na utoaji wa zawadi za wafanyakazi bora wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Sehemu ya Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba 
Sehemu nyingine ya Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba.
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Abdallah Kilima akitoa neno la shukrani kwa Waziri Mahiga kwa niaba ya Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Pamoja na kuahidi kufanyia kazi nasaha zilizotolewa, Balozi Kilima alimpongeza Waziri Mahiga kwa kuwa kiongozi bora na wa mfano wa kuigwa na Watumishi wote katika utendaji wa kazi. 
Mjumbe kutoka TUGHE-Taifa, Bw. Arcado Nchinga pia alizungumza na Watumishi wa Wizara ambapo aliwahimiza kuendelea kufanya kazi kwa juhudi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanaiwakilisha nchi vizuri katika mataifa mengine.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika mashariki, Bw. Nigel Msangi akitoa taarifa ya wafanyakazi bora wa Wizara wa mwaka 2015/2016 kwa Waziri Mahiga ambao walitunukiwa zawadi katika mkutano huo.
Afisa Habari katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Ally Kondo ndiye aliyeibuka Mfanyakazi Bora na Hodari wa iliyokuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Pichani akipongezwa na Mhe. Waziri Mahiga.
Afisa TEHAMA katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw.Salum M. Nalolah ndiye aliyeibuka Mfanyakazi Bora na Hodari wa iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Pichani akipongezwa na Mhe. Waziri Mahiga.
Picha ya pamoja ya Mhe. Waziri na Wafanyakazi bora wa Idara zote za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Picha ya pamoja Mhe. Waziri Mahiga na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUJIRUSHA KUTOKA KWENYE MNARA WA SIMU JIJINI MWANZA

May 27, 2016
Kijana Mmoja (picha) Jijini Mwanza amenusurika kifo baada ya kujirusha kutoka katikati ya mnara wa simu.
Na BMG
Tukio hilo limetokea hii leo na kuvuta watu wengi waliofika kumshuhudia kijana huo ambae amepanda katika mnara huo tangu majira ya asubuhi na kukatalia mnarani hadi majira ya saa sita mchana.

Mashuhuda wa tukio hilo ambao pia ni marafiki wa karibu na kijana huyo, wamesema huenda kijana huyo amefikia maamuzi hayo kutokana na ugumu wa maisha ambao amekuwa akiulalamikia huku wengine wakisema ni kutokana na kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo gundi ambayo amekuwa akiyatumia.

Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa jeshi la uokoaji na zima moto mkoani Mwanza, mmoja wa maafisa wa uokoaji Mussa Kaboni, amsetoa rai kwa makampuni yenye minara ya simu kuimarisha ulinzi katika minara hiyo ili kuondoa hatari inayoweza kujitokeza kutoka kwa raia wasio wema.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walionekana kuchukizwa na kitendo cha kijana huyo na kusikika wakifoka kwa hasira na makelele ya hali ya juu "rukaa, ruka sasa, jirushe kama wewe ni mwanaume" hali ambayo ilikuwa ikimuongezea morari kijana huyo na hivyo kujirusha kweli kutoka katikati ya mnara huo.


Baada ya kijana huyo kujirusha kutoka katikati ya mnara hadi chini, alipoteza fahamu na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure kwa ajili ya huduma ya kwanza.
Waziri Profesa Makame Atembelea daraja la Nyerere na Kituo cha kupimia mafuta yaingiayo nchini kuona Maendeleo

Waziri Profesa Makame Atembelea daraja la Nyerere na Kituo cha kupimia mafuta yaingiayo nchini kuona Maendeleo

May 27, 2016
p1 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na wawakilishi wa kampuni ya Mabey Bridge kutoka Marekani(hawapo pichani) na wadau wengine wa Ujenzi leo kuhusu mpango wa kujenga fly overs takribani tatu katika jiji la Dar es salaamu kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika jiji.
p2 
Katibu mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga akifafanua jambo kuhusu mpango wa ujenzi wa kujenga fly overs katika jiji la Dar es salaamu kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika jiji hilo kushoto ni muakilishi kutoka Kampuni ya Kimarekani ya Mabey Bridge Bw. Darren Keep na kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.
p3 
Msimamizi Mkuu wa Daraja la Nyerere Bw. Gerald Sondo akieleza jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu maendeleo ya Daraja pamoja na changamoto wanazozikabili, katika Ziara ya kushtukiza iliyofanya na Waziri huyo leo jijini Dar es salaamu.
p4
p5 p6Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo  kutoka kwa Fundi mitambo Bw. Simon Dotto  kuhusu maendeleo ya ukarabati wa mtambo wa kupima mafuta kutoka kwenye meli kabla ya kuingia kwenye matanki ambao uliharibika hivi karibu kutokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali.
p7 p8 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo  kutoka kwa mmoja wa wahudumu wa kivuko cha Mv Magogoni kuhusu utaratibu wa ukatishaji tiketi katika kivuko hicho leo jijini Dar es Salaam.
p9 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo na changamoto mbalimbali kutoka kwa abiria wanaotumia kivuko cha Mv Magogoni leo jijini Dar es Salaam.
(Picha zote na Beatrice Lyimo)
SERIKALI YANUNUA VIFAA VYA KUPIMA UBORA WA MAJENGO BILA KUYAHARIBU

SERIKALI YANUNUA VIFAA VYA KUPIMA UBORA WA MAJENGO BILA KUYAHARIBU

May 27, 2016

1 
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Bw. Elius Mwakalinga akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari kuhusu kutekelezwa kwa mpango wa Serikali wa kuhakikisha kuwa watumishi wa umma wanapata makazi bora ambapo wakala huo unajenga nyumba 10,000 ili kutimiza azma hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Milki  Bw. Baltazar Kimangano na kushoto ni Mkurugenzi wa Ushauri Bw. Edwin Nnunduma.
2 
Mhandisi  Ujenzi kitengo cha Upimaji  na Ukaguzi Majengo  toka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)  wakwanza kulia Bi Khadija Salum  akionesha kwa waandishi wa Habari sehemu ya vifaa vilivyonunuliwa na wakala huo kwa ajili ya kupima ubora wa majengo yaliyokwisha jengwa na yale yanayoendelea kujengwa ili kuhakikisha kuwa Serikali inakuwa na majengo yenye ubora kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa.
( Picha   na Habari na Frank Mvungi ).
………………………………………………………………………………………………….
Frank Mvungi-Maelezo
Serikali kupitia wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imenunua vifaa vya kupima Ubora wa Majengo bila kuyaharibu (Non destructive Testing equipments) .
Hayo yamesemwa Leo Jijini Dar es salaam na Mtendaji Mkuu waTBA  Bw. Elius Mwakalinga wakati wa mkutano na vyombo vya Habari uliolenga kutoa taarifa ya utekelezaji wa  miradi mbalimbali  ya ujenzi inayotekelezwa na wakala huo.
Akifafanua Mwakalinga amesema kuwa wakala huo umenunua vifaa vya kisasa ili kuwezesha ukaguzi wa ubora wa Majengo ya Serikali ili kuwa na majengo yenye Ubora unaotakiwa.
“Lengo la kununua vifaa hivi ni kuhakikisha kuwa majengo yote ya Serikali yanakuwa na ubora kwa kuwa tutayapima yaliyopo na yale yanayojengwa ili tuweze kuchukua hatua pale inapodi” alisisitiza Mwakalinga.
Akieleza umuhimu wa vifaa hivyo Mwakalinga amesema kuwa  hakutakuwa na wasiwasi tena kuhusu uwezekano wa wakandarasi kudanganya wakati wa ujenzi.
Aidha vifaa hivyo vitawezesha Wakala kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika majengo ya Serikali ili kubaini hali ya ubora wa majengo hayo ambapo gharama ndogo za ada ya ushauri zitatozwa kwa Taasisi husika.
Vifaa hivi ni kama Rebund hammer inayotumika kupima uimara wa zege iliyokauka, cover meter kwa ajili ya kupima ukubwa wa nondo na umbali uliowekwa.
Akitaja vifaa vingine Mwakalinga amesema kuwa ni “Utrasonic system/testing device” kwa ajili ya kupima muonekano wa ndani ya zege iliyokauka.
Mbali ya jukumu la kuhakiki ubora wa majengo ya Serikali, Wakala umeendelea na mpango wa ujenzi wa nyumba zinazouzwa kwa gharama nafuu kwa watumishi wa umma ambapo mpango wa wakala huo ni kujenga nyumba elfu kumi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

BUNGE LAENDELEA NA KIKAO CHAKE MJINI DODOMA LEO

May 27, 2016

 Baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza cha maswali na majibu na uchangiaji wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi leo mjini Dodoma.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Anthony Peter Mavunde ambaye akiwasalimia kwa furaha wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Dodoma leo kwenye viwanja vya Bunge.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Ajira na Vijana Mhe. Anthony Peter Mavunde akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi -VETA mkoa wa Dodoma nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
 Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) George Masaju (katikati) akizungumza na viongozi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) waliolitembelea Bunge mjini Dodoma.
 akiwasisitiza jambo viongozi wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) alipokutana nao nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo.
 Waziri wa Elimu,Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako (kushoto) akimweleza jambo Rais wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) Bw. Frank Nkya (kulia) nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma
 Waziri wa Elimu,Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako (kulia)akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angella Kairuki (kushoto) nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
 Waziri wa Elimu,Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na
wanafunzi wa Chuo cha Ufundi -VETA mkoa wa Dodoma nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.PICHA/Aron Msigwa-MAELEZO.
RAIS DKT. JOHN MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA NNE DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE

RAIS DKT. JOHN MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA NNE DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE

May 27, 2016

jk1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.
jk2 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.
jk3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na  Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete wakifurahia jambo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
jk5 jk6 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na  Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete wakifurahia jambo mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU
WAZIRI MKUU MH. KASSIM MAJALIWA AKAGUA MRADI WA MABASI YA MWENDOKASI DART LEO

WAZIRI MKUU MH. KASSIM MAJALIWA AKAGUA MRADI WA MABASI YA MWENDOKASI DART LEO

May 27, 2016

1 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza na mwanafunzi Amina Abdallah wa darasa la sita katika shule ya msingi ya Ukombozi jijini Dar es salaam ambaye amepanda basi la Mwendo Kasi Ajentina na kushuka Manzese, Waziri Mkuu Majaliwa ametumia usafiri wa DART leo kutoka Feri kwenda Kimara Mwisho wakati alipokagua miundombinu ya usafiri huo ili kujionea mafanikio na changamoto mbalimbali zinazojitokeza mara baada ya mradi huo kuanza mwezi mmoja sasa ili ziweze kurekebishwa na kuuboresha zaidi.
Usafiri DART  umekuwa  mkombozi kwa wasafiri wengi wa jiji la Dar es salaam wakati wanapotoka majumbani mwao na kuelekea kazini na kurejea majumbani mwao,Katikati ni Bw. David Mwaibula aliyekuwa Mwenyekiti Mamlaka ya Usafiri wa Daladala Dar es salaam (DRTLA) zamani  aliyeambatana na Waziri Mkuu kukagua mradi huo leo.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
2 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akifurahia jambo wakati Mkurugenzi wa DART Bw. David Mgwasa akisamimiana na Bw. David Mwaibula aliyekuwa Mwenyekiti Mamlaka ya Usafiri wa Daladala Dar es salaam (DRTLA) zamani  aliyeambatana na Waziri Mkuu kukagua mradi huo leo.
3 
Baadhi ya abiria wakisafiri pamoja na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa kwenye basi la DART.
4 
Moja ya Basi likiwa katika ruti yake kutoka Kimara kuelekea Posta.
5 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akikagua kituo cha Kimara Mwisho mara baada ya kuwasili kituoni hapo
6 7 
Moja ya basi la Mwendo kasi likipakia abiria katika kituo cha Kimara Mwisho leo.
10 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza na mwanafunziambaye jina lake halikufahamika mara moja wakati alipofika kwenye kituo cha mabasi ya Mwendo kasi Kimara Mwisho leo.
11 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akiuliza swali kwa mmoja wa wafanyakazi wanaokatisha tiketi katika vituo hivyo wakati alipokagua miundombinu ya DART leo.
12 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akiangalia utendaji kazi unavyoendelea ikiwa ni pamoja na kubaini changamoto zinazojitokeza.
13 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akikaua kituo cha Kimara Mwisho.
14 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akifurahia jambo na Mkurugenzi wa DART Bw. David Mgwasa katikati ni Mzee David Mwaibula.
8 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua miundombinu hiyo leo kulia ni Mzee David Mwaibula na katikati ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamanda Mohamed Mpinga.
9