KIKAO CHA BODI YA BARABARA CHAFANYIKA MKOANI KILIMANJARO.

February 11, 2016
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Amosi Makala akizungumza wakati wa kikao cha bodi ya barabara kilichoketi katika ukumbi wa ofisi ya RC .
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho ambacho hutangulia kabla ya kikao cha Ushauri cha Mkoa (RCC).
Waziri wa Maliasili na Utalii ,Pro Jumanne Mghembe ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mwanga akichangia hoja katika kikao hicho.
Mkuu wa wilaya ya Mwanga ,Shaibu Ndemanga akifuatilia michango iliyokuwa ikitolewa katika kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Rombo ,Lembris Kipuyo akifutilia michango ya hho .oja mbalimbali katika kikao hic
Mkuu wa Wilaya ya Moshi Novatus Makunga akifuatilia michango katika kikao hicho.
Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Kilimanjaro,Mwita Rubirya akizungumza wakati wa kikao cha Bodi ya barabara .
Mkuu wa Wilaya ya Same,Herman Kapufi akifuatilia michango katika kikao hicho.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akifuatilia michango katika kikao hicho.
Mkuu wa wilaya ya Siha,Dkt Charles Mlingwa akifuatilia michango katika kikao hicho.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Same ,Christopher Ilila akichangia katika kikao hicho.
Mkuu wa wilaya ya Same ,Herman Kapufi akichangia katika kikao hicho.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akichangia katika kikao hicho.
Mkuu wa wilaya ya Siha,Dkt Charles Mlingwa akichangia katika kikao hicho.
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi, Exaud Mamuya akichangia katika kikao hicho.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII PROF,JUMANNE MAGHEMBE AKUTANA NA WADAU WA UTALII MKOA WA KILIMANJARO.

February 11, 2016
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akizungumza na Wadau wa Utalii mkoa wa Kilimanjaro alipokutana nao katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.
Baadhi ya Wadau wa Utalii wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii (hayupo pichani) alipokutana nao.
Waziri Maghembe akiwaeleza wamiliki wa kampuni zinazofanya shughuli za Utalii katika hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ambapo aliwaeleza mambo mbali mbali yanayochangia kushusha pato la taifa .Miongoni mwa mambo aliyozungumza ni pamoja na kampuni za Utalii kutumia njia za Panya kupndisha wageni,Wapagazi kufa Mlima Kilimanjaro kutokana na baridi kali kwa kukosa mavazi maalumu ya baridi,Uchafu Mlima Kilimanjaro,Wageni kupatiwa huduma duni ,na mapunjo ya mishahara kwa wapagazi.
Mhifadhi Mkuu mpya wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Betrita Loibooki akiwa katika kikao hicho ambapo alitamburishwa rasmi akichukua nafasi ya Erastus Lufunguro aliyehamishiwa Makao Makuu, Mhifadhi Loibooki alikuwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Arusha (ANAPA).
Baadhi ya wamiliki wa kampuni za Utalii wakiwa katika mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Amosi Makala akizungumza wakati wa kikao hicho.
Aliyekuwa Mhifadhi Utalii katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, (KINAPA) Eva Mallya ambaye kwa sasa amehamishiwa Hifadhi ya Taifa ya Manyara akiteta jambo na Mhifadhi mkuu mpya wa KINAPA,Betrita Loibooki.
Katibu wa Chama cha Waongoza Watalii mkoa wa Kilimanjaro (KGA) James Mong'ateko akiwasilisha malalamiko ya wapagazi mbele ya Waziri wa Maliasili na Utalii .(hayupo pichani)
Waziri Maghembe na Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Allan Kijazi wakimsikiliza kwa makini katibu wa Chama cha Waongoza watalii mkoa wa Kilimanjaro (KGA) James Mong'ateko (hayupo pichani ) alipokuwa akieleza changamoto.
Mkurugenzi Mkuu Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Utalii na Wadauu wa Utalii kilichofanyika mkoani Kilimanjaro.
Katibu wa KGA,James Mong'ateko akikabidhi kwa Waziri Maghembe taarifa iliyohusu Changamoto mbalimbali wanazopata katika shughuli za kupanda Mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya Wadau wa Utalii katika kikao hicho.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii  Kanda ya Kaskazini.
DK. KIGWANGALLA ASEMA ATAENDELEA KUMSAIDIA RAIS MAGUFULI KUTUMBUA MAJIPU YANAYOKWAMISHA UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA AFYA

DK. KIGWANGALLA ASEMA ATAENDELEA KUMSAIDIA RAIS MAGUFULI KUTUMBUA MAJIPU YANAYOKWAMISHA UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA AFYA

February 11, 2016
kigwa111

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dk. Hamisi Kigwangalla (aliyekaa) akiwa katika ibada maalum ya kuombea wagonjwa duniani iliyofanyika leo katika Hospitali ya Ndala,Nzega Mkoani Tabora. Wengine kulia ni Rudrovic Mwananzila na kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Jacqueline Liana.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dk. Hamisi Kigwangalla amesema kwamba wao kama viongozi wataendelea kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli kutumbua majibu yanayokwamisha kutokupatikana kwa huduma bora za afya, bila kuogopa wala kumwonea mtu kwa ajili ya maslahi ya taifa.
Aidha Dkt. Kigwangalla alisema watafanya hivyo kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu ili kuhakikisha kila mtu anatimiza wajibu ipasavyo.
Dk.Kigwangalla ameyasema hayo leo 11 Februari wakati wa maadhimisho ya 24 ya ibada maalum ya kuwaombea wagonjwa Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika katika jimbo kuu la Tabora na baadae kwenye Hospitali ya Ndala, iliyopo Kata ya Ndala, Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora.
“Tutaendelea kutumbua majibu bila ya kmwonea mtu kwa kuwa tunafanya hivyo kwa kuangalia sheria, kanuni na taratibu. Haiwezekani mtu akaiba dawa ambazo zinawasaidia wananchi masikini, halafu sisi tukamwaangalia tu,” alisema Dkt.Kigwangalla.
Alisema majipu hayo yatatumbuliwa kwa watendaji ambao watakaozembea, wasio waadilifu na wasiowajibika katika sekta hiyo ya afya.
Aliongeza kwamba Serikali ya Awamu ya Tano itakuwa inafanya kazi kwa kuwafuata wananchi hususani wanyonge (masikini) mahali walipo ili kuhakikisha baada ya miaka kumi ijayo Tanzania itakuwa na maendeleo ya kiwango cha juu.
Naibu Waziri huyo aliwaomba viongozi wa dini kuendelea kuwaombea kwa kuwa kazi ya kutumbua majibu si rahisi.
Aliuomba uongozi wa hospitali hiyo kuboresha mfumo wa ukusanyaji mapato kwa kutumia njia ya ki-elekroniki kwa sababu umeonyesha matokeo chanya katika hospitali nyinigine.
Akizungumzia kuhusu suala la upungufu wa bajeti, Dkt. Kigwangalla alisema ni vema viongozi hao wadini, asasi za kijamii na taasisi zisizo za kiserikali zinazotoa huduma za afya kutafuta vyanzo mbadala vya kuongeza fedha za kuboresha huduma hizo, kwa kuwa si sekta hiyo pekee yenye changamoto hiyo.
Pia vipaumbele vya shughuli mbalimbali za kuwaletea maendeleo wananchi viko vingi, wakati rasimali fedha haitoshelezi.
Aliwataka uongozi wa hospitali hiyo na nyinginezo za mashirika ya hiari kuwasilisha taarifa za (data cleaning) UTUMISHI ikiwa ni pamoja na kuorodhesha watumishi wanaotakiwa kuondolewa kwenye malipo ya mshahara ili waweze kupatiwa kibali cha kuajiri kwani bila kufanya hivyo kibali hakitaweza kutolewa.
Dkt. Kigwangalla aliongeza kwamba hivi sasa wizara yake iko katika mchakato wa kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma za matibabu za kwa kutumia mifuko ya bima ya afya.
Maadhimisho hayo ni ya kila mwaka ya siku 11 Februari, Wakristo wote wanafanya sala maalum ya kuwaombea wagonjwa wanaosumbuka na maradhi na kuwaombea wapone haraka huku wakiyapokea mateso hayo na kuyaunganisha na mateso ya kristo na kanisa lake hii ni pamoja na kuwaombea ndugu wa wagonjwa katika kuwasaidia wagonjwa wao wakati wa kuwauguza.
Maadhimisho hayo yanaenda sambamba pamoja na kuwahudumia na kutoa misasada mbalimbali.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ludocivk Mwananzila aliwataka Watanzania kuwa na tabia ya kuwatembelea wagonjwa na wafungwa ili waweze kupata faraja.
Kihistoria, Hospitali hiyo ya Ndala, ilianza miaka ya 1930 kama Zahanati ndogo chini ya Masista Wamissionary wa Afrika (Missionary of Our Lady of Afrika-White Sisters) katika jimbo kuu hilo la Tabora
Mwaka 1963 ilikuja kuwa Hospitali kamili huku ikianza na vitanda 115 na wauguzi 15 na daktari mmoja, hata hivyo hadi sasa ina jumla ya vitanda 152, wafanyakaz 125 huku wakiweza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje wapatao 38,917 na wagonjwa wa kulazwa 8,428.
Hospitali hiyo baadae ikapandishwa ngazi ya Hospitali huku ikiwa na vitanda 152 huku ikiwa na madaktari mbalimbali.
Wakitoa shukrani zao ni pamoja na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya kwa kuweza kushirikiana bega kwa bega ikiwemo kutoa ruzuku kwa baadhi ya watumishi, posho za watumishi, vitanda vulivyohainishwa, madawa, mafunzo ya watumishi, na mambo mbalimbali.

kigwa3333Dk. Kigwangalla akitoa zawadi kwa mmoja wa akina mama waliokuwa kwenye wodi ya wazazi katika Hospitali ya Ndala, iliyopo Kata ya Ndala, Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora.

KIGWA1Baadhi ya wananchi wakiwa katika tukio hilo. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog-Nzega.)

PROF. MBARAWA AKAGUA CHUO CHA MABAHARIA (DMI)

PROF. MBARAWA AKAGUA CHUO CHA MABAHARIA (DMI)

February 11, 2016


mb1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Chuo cha Mabaharia cha Dar es Salaam (DMI) Eng. Yassin Songoro katika ziara yake ya kukagua Chuo hicho jijini Dar es Salaam.
mb2
Mkuu wa Chuo cha Mabaharia cha Dar es Salaam (DMI) Eng. Yassin Songoro (katikati) akimuongoza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa kukagua madarasa ya Chuo hicho.
mb3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akikagua dira ya kuongozea meli (compass) katika moja ya darasa la Chuo hicho. Kulia ni Mkuu wa Chuo cha DMI Eng. Yassin Songoro.
mb4
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (mwenye tai) akikagua mitambo ya kuongozea meli katika moja ya madarasa ya chuo cha DMI wakati wa ziara yake chuoni hapo.
DKT. KIGWANGALLA ASEMA WATAENDELEA KUMSAIDIA RAIS KUTUMBUA MAJIPU

DKT. KIGWANGALLA ASEMA WATAENDELEA KUMSAIDIA RAIS KUTUMBUA MAJIPU

February 11, 2016


JA6
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kigwangalla,(kulia) akiwa kati,ka ibada maalum ya maadhimisho ya   24 ya kuwaombea wagonjwa duniani ambayo kitaifa yamefanyika leo mkoani humo, katika wilaya hiyo.Kulia niMkuu wa Mkoa wa Tabora, Ludovick Mwananzila na Kwanza mbele Naibu Askofu wa Jimbo Kuu la Kanisa la Katoliki la Tabora .
JA3
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kigwangalla,(kulia) akiwa katika ibada maalum ya maadhimisho ya   24 ya kuwaombea wagonjwa duniani ambayo kitaifa yamefanyika leo mkoani humo, katika wilaya hiyo.Kulia niMkuu wa Mkoa wa Tabora, Ludovick Mwananzila na Kwanza mbele na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nzega Jaquiline Liana
JA4
Baadhi ya mapadre wakiwa katika ibada maalum ya  maadhimisho ya   24 ya kuwaombea wagonjwa duniani ambayo kitaifa yamefanyika leo mkoani humo, katika wilaya hiyo.
JA5
ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ludovick Mwananzila akitoa zawadi kwa mgonjwa aliyelazwa katika Hospitali ya Ndala, wilayani Nzega mkoani Tabora mara kushiriki ibada maalum maadhimisho ya   24 ya kuwaombea wagonjwa duniani ambayo kitaifa yamefanyika leo mkoani humo, katika wilaya hiyo.
………………………………………………………………………………………………………………………………………….
NA MAGRETH KINABO –MAELEZO
 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dk. Hamisi Kigwangalla amesema kwamba wao kama viongozi wataendelea kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli kutumbua majibu yanayokwamisha kutokupatikana kwa huduma bora za afya ,bila kuogopa wala kumwonea mtu kwa ajili ya maslahi ya  taifa.
Aidha  Dkt. Kigwangalla alisema  watafanya hivyo kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu ili kuhakikisha kila mtu anatimiza wajibu ipasavyo.
Dk.Kigwangalla ameyasema hayo  leo 11 Februari wakati wa maadhimisho ya 24 ya ibada maalum ya kuwaombea  wagonjwa Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika katika jimbo Kuu la Tabora  na baadae kwenye Hospitali ya Ndala, iliyopo Kata ya Ndala, Wilaya ya Nzega, Mkoani Tabora.
“ Tutaendelea kutumbua majibu bila ya kmwonea mtu kwa kuwa tunafanya hivyo kwa kuangalia sheria, kanuni na taratibu. Haiwezekani mtu akaiba dawa ambazo zinawasaidia wananchi masikini, halafu sisi tukamwaangalia tu,” alisema Dkt.Kigwangalla.
Alisema majipu hayo yatatumbuliwa kwa watendaji ambao watakaozembea, wasio waadili na wasiowajibika katika sekta hiyo ya afya.
Aliongeza kwamba Serikali ya Awamu ya Tano itakuwa inafanya kazi kwa kuwafuata wananchi hususan wanyonge (masikini) mahali walipo ili kuhakikisha baada ya miaka kumi ijayo Tanzania itakuwa na maendeleo ya kiwango cha juu.
Naibu Waziri huyo aliwaomba viongozi wa dini kuendelea kuwaombea kwa kuwa kazi ya kutumbua majibu si rahisi.
Aliuomba uongozi wa hospitali hiyo kuboresha mfumo wa ukusanyaji mapato kwa kutumia elekroniki kwa sababu umeonyesha matokeo chanya katika hospitali nyinigine.
Akizungumzia kuhusu suala la upungufu wa bajeti,Dkt. Kigwangalla alisema ni vema viongozi hao wadini, asasi za kijamii na taasisi zisizoza kiserikali zinazotoa huduma za afya kutafuta vyanzo mbadala vya kuongeza fedha za kuboresha huduma hizo, kwa kuwa si sekta hiyo pekee yenye changamoto hiyo.
Pia vipaumbele vya shughuli mbalimbali za kuwaletea maendeleo wananchi viko vingi, wakati rasimali fedha haitoshelezi.
Aliwataka uongozi wa hospitali hiyo na nyinginezo za mashirika ya hiari kuwasilisha taarifa za (data cleaning) UTUMISHI ikiwa ni pamoja na kuorodhesha watumishi wanaotakiwa kuondolewa kwenye malipo ya mshahara ili waweze kupatiwa kibali cha kuajiri kwani bila kufanya hivyo kibali hakitaweza kutolewa.
 
Dkt. Kigwangalla aliongeza kwamba hivi sasa wizara yake iko katika mchakato wa kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma za matibabu za  kwa kutumia mifuko ya bima ya afya. Hivyo Februari 20,mwaka huu
Maadhimisho hayo ni ya kila mwaka ya siku 11 Februari, Wakristo wote wanafanya sala maalum ya kuwaombea wagonjwa wanaosumbuka na maradhi na  kuwaombea wapone haraka huku wakiyapokea mateso hayo na kuyaunganisha na mateso ya kristo na kanisa lake hii ni pamoja na kuwaombea ndugu wa wagonjwa katika kuwasaidia wagonjwa wao wakati wa kuwauguza.
Maadhjimisho hayo yanaenda sambamba pamoja na kuwahudumia na kutoamisasada mabalimbali.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ludocivk Mwananzila aliwataka Watanzania kuwa na tabia ya kuwatembelea wagonjwa na wafungwa ili waweze kupata faraja.
Kihistoria, Hospitali hiyo ya Ndala, ilianza miaka ya 1930 kama Zahanati ndogo chini ya Masista Wamissionary wa Afrika (Missionary of Our Lady of Afrika-White Sisters) katika jimbo kuu hilo la Tabora
Mwaka 1963 ilikuja kuwa Hospitali kamili huku ikianza na vitanda 115 na wauguzi 15 na daktari mmoja, hata hivyo hadi sasa ina jumla ya vitanda 152, wafanyakaz 125 huku wakiweza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje wapatao 38,917 na wagonjwa wa kulazwa 8,428.
Hospitali hiyona baadae ikapandishwa ngazi ya Hospitali huku ikiwa na vitanda 152 huku ikiwa na madaktari mbalimbali.
Wakitoa shukrani zao ni pamoja na serikali ya Tanzania kupitia wizara ya afya kwa kuweza kushirikiana bega kwa bega ikiwemo kutoa ruzuku kwa baadhi ya watumishi, posho za watumishi, vitanda vulivyohainishwa, madawa, mafunzo ya watumishi, na mambo mbalimbali

DK. MAGUFULI AMTUMIA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MKUU WA MKOA WA TANGA KUFUATIA AJALI VIFO VYA WATU 11

February 11, 2016


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu Rais Muungano na Mazingira Atembelea Ujenzi wa Mtaro Uwanja wa Mnazi Mmoja na Jangombe Eneo Ilikozama Nyumba.

February 11, 2016

Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akitembelea Ujenzi wa Mradi wa Mtaro katika Uwanja wa Mpira Mnazi Mmoja akiwa katika ziara zake Zanzibar kutembelea Miradi ya Mazingira inayosimamiwa na Muungano.akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Mhe Hamad Yussuf Masauni. 
Kijicho cha Kampuni ya Ujenzi Mtaro huo kikiwa kazini katika uchimbaji wa mtaro huo nyambu ya pili pwani ya kizingo Zanzibar. 
Makalbi ya mtaro wa kupitishia maji kutoka katika viwanja vya mpira mnazi mmoja yakitandikwa, na kulia ni mabomba ya mtaro huo ya zamani yaliokuwa yakitoa huduma hiyo ya kupitisha maji kutoka katika uwanja huo. 
Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe.Luhaga Mpina akiangalia ujenzi huo wakati wa ziara yake kutembelea miradi huo. 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina akimsikiliza Mhandisi wa Baraza la Manispa Zanzibar Ndg Mzee Khamis Juma akitowa maelezo ya kitaalumu ya Ujenzi wa Mtaro wa maji machafu wakati wa mvua kunyesha