March 01, 2014

CCM WAKONGA NYOYO ZA WATU WA KALENGA: MKUTANO WA UFUNGUZI WA KAMPENI ZA UBUNGE ,JIMBO LA KALENGA

Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Godfrey William Mgimwa akibebwa Juu na Wanachama/wapenzi wa CCM mara baada ya Kuwasili Viwanja Vya Stendi-kata ya Ifunda.
Mapokezi Mazito yakiendelea ya Naibu Katibu Mkuu CCM-Bara na Kijana Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga Ndugu Godfrey William Mgimwa kwenye uwanja wa Stedi-Kata ya Ifakara hii leo wakati wa Mkutano wa Ufunguzi wa Kampeni za Ubunge Jimbo la Kalenga.
 
Mh:Naibu Katibu Mkuu CCM-Bara akisaini Kitabu akiwa na Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga Ndugu Godfrey William Mgimwa mara baada ya kuwasili Viwanja Vya Stendi Kata ya Ifunda.

YANGA YAICHAPA 1-0 AL AHLY, CANNAVARO SHUJAA

March 01, 2014
Na Mahnmoud Zubeiry, Dar es Salaam
BAO pekee la Nahodha Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’ jioni hii limeipa ushindi wa 1-0 Yanga SC katika mchezo wa kwanza wa kuwania kucheza Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika, dhidi ya Al Ahly ya Misri Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Cannavaro alifunga bao hilo dakika ya 87 akimalizia kona maridadi ya winga Simon Msuva kutoka wingi ya kulia.
Kona hiyo ilitokana na kipa Sherif Ekram Ahmed kupangua shuti kali la mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi. 
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Heileyesus Bazeze aliyesaidiwa na Kindie Mussie Tdedesse Shawangiza  wote kutoka Ethiopia, hadi mapumziko milango ilikuwa migumu.
Shujaa; Beki Nadir Haroub 'Cannavaro' akipongezwa na wenzake Emmanuel Okwi na SImon Msuva baada ya kufunga bao pekee jioni dhidi ya Al Ahly  
Yanga SC ndiyo waliotawala zaidi mchezo na kutengeneza nafasi kadhaa nzuri za kufunga, lakini wakakosa umakini katika kumalizia.
March 01, 2014


*KINACHOENDELEA KUTOKA UWANJA WA TAIFA, MECHI BADO MASHABIKI WA SIMBA WARUDIA KUNG'OA VITI
 VURUGU UWANJANI, Mashabiki wa Simba waking'oa viti na kuwarushia mashabiki wa Yanga, kabla ya mchezo wa Klabu Bingwa Afrika kati ya Yanga na Al-Ahly unaotarajia kuanza muda mchache ujao. 
Vurugu hizo zimeanza baada ya mashabiki wa Yanga kuamua kuzunguka uwanja huo na kusogea hadi eneo la mashabiki wa Simba huku wakishangilia jambo ambalo liliwaudhi mashabiki wa simba ambao waliamua kuanza kurusha chupa za maji na wengine kung'oa viti na kuwarushia mashabiki wa Yanga.
 Mashabiki wa Simba wakirusha viti kuwashambulia mashabiki wa Yanga.
 Wakiendelea kung'oa viti na kurusha
 Mashabiki wa Yanga wakifurahia huku wakionyesha bango lenye idadi ya mabao.

DC DENDEGO AMKABIDHI ZAWADI MFANYAKAZI BORA MWEZI WA KWANZA HOTEL YA TANGA BEACH

March 01, 2014
Kushoto ni Mfanyakazi bora wa mwezi wa kwanza katika hotel ya Tanga Beach Resort jijini Tanga kutoka kitengo cha Upishi akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Tanga,Halima Dendego kwenye halfa ya kuwapongeza wafanyakazi bora iliyofanyika kwenye ukumbi wa La Crande La Casachika mwishoni mwa wiki

WABUNGE WAWALIPUA BONGO MOVIES WASEMA NI OMBA OMBA BALAA, SOMA WALICHOFUNGUKA WABUNGE HAPA

March 01, 2014

SKENDO nzito ya Bongo Muvi imeibuliwa na baadhi ya wabunge waliopo mjini Dodoma kufuatia kuwalipua wasanii wake kuwa, ni ombaomba balaa, Risasi Jumamosi lina mkanda mzima.

Kwa mujibu wa wabunge hao ambao walitaka majina yao yasitiriwe kwa sasa, baadhi ya wasanii hao ambao wengi ni mastaa wamekuwa wakiwazukia na kuwapiga mizinga jambo linalowashangaza hasa wakizingatia kuwa, wapiga mizinga hao wana majina makubwa na huonekana wakitembelea magari ya kifahari.


“Hivi nyie mapaparazi, mnashindwa kabisa kukomesha hii tabia ya mastaa wa Bongo Muvi? Hawa jamaa ni ombaomba sana.


“Wamekuwa wakitupiga mizinga sana. Tunawashangaa maana wengine wana majina makubwa, wanatembelea magari ya kifahari lakini bado wanaomba pesa ndogo,” alisema mbunge mmoja ambaye anatoka kwenye moja ya majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam.
March 01, 2014
Sifa ya wanaume anaowapenda Wema Sepetu.

MINGONI mwa mastar wa Tanzania wenye ushawishi mkubwa ni pamoja na Wema Sepetu ambaye pia aliwahi kuwa Miss Tanzania 2006 ambaye kwa sasa anaendesha kampuni yake binafsi iitwayo Endless Fame inayojishughulisha zaidi na utengenezaji wa Filamu mbalimbali.

March 01, 2014

Wananchi wa Wakijitokeza katika Zoezi la Uandikishaji wa Vitambulisho vya Taifa

Wananchi wa maeneo ya Mtoni wakijitikeza katika zoezi la Uandikishaji wa Vitambulisho vya Taifa, katika viwanja vya Skuli ya Mto Pepo Wilaya ya Magharibi Unguja.zoezi hilo linafanyika kwa nchi nzima kuandikishwa Wananchi ili kuweza kupata Vitambulisho hivyo
          Wananchi wa kiwa katika viwanja vya Skuli ya Mto Pepo wakijiandikisha Vitambulisho vya Taifa.
Afisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Tanzania akitaja majina ya Wananchi waliokuwa tayari wameshafanyiwa usaili na kufuata hatua nyengine ya upigaji picha.
                     Mwananchi akikamilisha taratibu za usajili kwa ajili ya Kitambulisho cha Taifa.
March 01, 2014

MSICHANA ALIYEONGOZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2013,AFUNGUKA MENGI FUATILIA HAPA

 
Tovuti ya Times Fm imefanya mahojiano ‘exclusively’ na Robina Nicholaus, msichana aliyeshika nafasi ya kwanza/ aliyeongoza kitaifa (Tanzania One) kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2013.
Robina, mwenyeji wa wilaya ya Bunda mkoa wa Mara ambaye alikuwa anasoma katika shule ya wasichana ya Marian, akiwa na ndoto ya kuwa daktari wa watoto amejibu maswali kumi muhimu na majibu yake yanaweza kuchukuliwa kama mfano wa kuigwa kwa wanafunzi walioko shuleni ambao wanakumbwa na changamoto kadhaa, na wazazi wanaowapeleka watoto wao shule.
March 01, 2014
Ajali imehusisha gari ya abiria aina ya hiace inayofanya safari zake kati ya Mweka na moshi mjini  na landcruiser VX iliyokuwa  imewabeba  wanafunzi wa chuo cha usimamizi na uhifadhi wa wanyama pori Mweka kilichopo Mweka, Moshi vijijini. 
March 01, 2014

TWIGA STARS YAAGA RASMI MASHINDANO YA AFRIKA BAADA KUTOKA SARE YA 1-1 NYUMBANI









TIMU ya Taifa ya Wanawake(Twiga Stars) imetolewa katika mashindano ya raundi ya kwanza kuwania kufuzu fainali za Mataifa Afrika kwa wanawake baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Shepolopolo ya Zambia katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam. 

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa nchini Zambia Twiga Stars ilifungwa mchezo huo kwa mabao 2-1 hivyo imetolewa kwa jumla ya mabao  3-2.