Mgombea
Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (aliesimama kulia) akizungumza
machache wakati alipofika kuhani msiba wa Mtoto wa Mzee Mashaka Athuman
mkazi wa kijiji cha Rupungwi,Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la
Chalinze jana Machi 17,2014.
Mgombea
Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akipokea moja ya kati ya mbili ya Kadi
za Chadema kutoka kwa aliekuwa Mwanachama wa Chadema,Mrisho Issa mkazi
wa Kijiji cha Msata,ndani ya Jimbo la Chalinze.Mwingine alierudisha kadi
ni Kassim Msakamali (hayupo pichani).