February 10, 2014
February 10, 2014

PINDA AKUTANA NA BALOZI WA ISRAEl

IMG_1007Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na Balozi wa Israel nchini,  Mhe. Gil  Haskel, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

BALOZI WETU MPYA MTEULE WA MALASYIA DR. AZIZ PONERY ALIPOTEMBELEA TUME YA MIPANGO HAPA BONGO LIVE!!

February 10, 2014

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MJUMBE WA EU, NA SHIRIKA LA GLOBAL VOLUNTEERS LA MAREKANI LEO IKULU

February 10, 2014
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ujumbe toka Umoja wa Ulaya (EU) kutoka kwa Mkurugenzi wa EU pembe ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ambaye pia ni mjumbe maalumu wa EU kwenye nchi za ukanda wa Maziwa Makuu, Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 10, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na  Mkurugenzi wa EU pembe ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ambaye pia ni mjumbe maalumu wa EU kwenye nchi za ukanda wa Maziwa Makuu, Bw. Koen Vervaeke (kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa EU nchini Tanzania Balozi  Filiberto Ceriani Sebregondi, bada ya kukutana nao  Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 10, 2014.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea  ujumbe toka Umoja wa Ulaya (EU) ukiongozwa na  Mkurugenzi wa EU pembe ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ambaye pia ni mjumbe maalumu wa EU kwenye nchi za ukanda wa Maziwa Makuu Bw. Koen Vervaeke, Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 10, 2014. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bw. Burham Philbrook wa Shirika la Global Volunteers la Minnestota, Marekani, akishuhudiwa na Askofu Dkt. Owdenburg M. Mdegella wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Iringa walipomtembelea na kufanya naye mazungumzo  Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 10, 2014.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jarida toka kwa  Bw. Burham Philbrook wa Shirika la Global Volunteers la Minnestota, Marekani, akishuhudiwa na Askofu Dkt. Owdenburg M. Mdegella wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Iringa walipomtembelea na kufanya naye mazungumzo  Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 10, 2014. PICHA NA IKULU
February 10, 2014

SEKRETARIETI YA BUNGE LA KATIBA KUKABIDHIWA UKUMBI BAADA YA KUKAMILIKA KWA MAREKEBISHO KUELEKEA BUNGE LA KATIBA

 Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa na wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge, wakati walipofika kukagua ukumbi huo baada ya kukamilika kwa marekebisho ya ukumbi huo kuelekea Bunge la Katiba, linalotarajia kuanza Feb 18, mwaka huu.
 Muonekano wa Ndani ya ukumbi huo baada ya kazi ya uwekaji viti kukamilika
 Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda, (katikati) Naibu Spika Mhe. Job Ndugai (kushoto), Katibu wa Bunge (Wa pili Kulia) na Mhe. Hamadi Rashid Mohamed Kulia wakiangalia baadhi ya maboresho yaliyofanywa katika Ukumbi wa Bunge kwa ajili ya Bunge la Katiba.
Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda pamoja na wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi walioshiriki kuukarabati ukumbi wa Bunge kwa ajiri ya matumizi ya Bunge la Katiba.
Picha kwa hisani ya Bunge
February 10, 2014

*KOCHA MSAIDIZI WA STARS MARSH ASUBIRI VIPIMO VYA MWISHO

Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Sylvester Marsh (Pichani kushoto) ambaye amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) anasubiri vipimo vya mwisho ili aweze kuanza matibabu.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtoa kocha huyo nyumbani kwake jijini Mwanza na kumleta Dar es Salaam kwa lengo la kuhakikisha anapata matibabu zaidi na kwa uangalizi wa karibu.

Tayari majibu ya kipimo cha kwanza yameshapatikana, hivyo yanasubiriwa majibu ya kipimo kingine ili aweze kuanza rasmi matibabu, lengo likiwa ni kubaini kitaalamu ugonjwa unaomsumbua.

*KUWASILISHA MAJINA YA MABINGWA WA MIKOA MACHI 30

Vyama vya Mpira wa Miguu vya mikoa vimetakiwa kuwasilisha majina ya mabingwa wao kufikia Machi 30 mwaka huu kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL).

Timu zote zitakazofuzu kucheza RCL zinaruhusiwa kusajili wachezaji wapya wasiozidi watano kutoka ndani ya mkoa kwa kufanya taratibu za uhamisho. Kamati imesisitiza kuwa usajili wa RCL ni uleule uliotumika kwenye Ligi ya Mkoa.

Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana Februari 6 mwaka huu imekataa ombi la Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) kuongeza timu za Ligi ya Mkoa kutoka 20 hadi 24.

Ikiwa chini ya Mwenyekiti wake Geofrey Nyange, Kamati hiyo imesema kwa mujibu wa Kanuni ya Ligi ya Mkoa, ligi hiyo inatakiwa kuwa na timu kati ya 16 na 20, hivyo vyama vya mpira wa miguu vya mikoa vinatakiwa kuendesha ligi kwa kufuata kanuni.

Kamati hiyo imeongeza kuwa hata kama ingekubalia ombi la MZFA kiutaratibu lisingewezekana kwa vile kanuni hufanyiwa marekebisho baada ya msimu kumalizika, wakati ombi hilo limewasilishwa katikati ya msimu.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

February 10, 2014
Release No. 022
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Februari 10, 2014

WATANO KANEMBWA JKT WAFUNGIWA MECHI TATU
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewafungia mechi tatu wachezaji watano kati ya tisa wa timu ya Kanembwa JKT waliolalamikiwa na Sekretarieti kwa kumpiga mwamuzi kwenye mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) iliyochezwa Novemba 2 mwaka jana.

Wachezaji hao ni Bariki Abdul, Mrisho Musa, Nkuba Clement, Nteze Raymond na Philo Ndonde. Wachezaji ambao hawakutiwa hatiani kutokana na ushahidi dhidi yao kutojitosheleza ni Abdallah Mgonja, Mbeke Mbeke, Ntilakigwa Hussein na Uhuru Mwambungu.

Mechi hiyo dhidi ya Stand United iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga ilivunjwa na refa Peter Mujaya dakika ya 87 kutokana na kupigwa na wachezaji hao baada ya kuamuru ipigwe penalti dhidi ya timu yao.

Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Ibara ya 49 (1)(b) ya Kanuni za Nidhamu za TFF baada ya kupitia vielelezo vilivyowasilishwa na Sekretarieti ya TFF ambavyo ni ripoti ya refa, ripoti ya kamishna wa mechi hiyo na video iliyoonesha tukio hilo.

Pia kabla ya kutoa adhabu baada ya kusikiliza utetezi kutoka kwa walalamikiwa ambao ni wachezaji hao na timu yenyewe ya Kanembwa JKT. Nayo Kanembwa JKT imetiwa hatiani na kupigwa faini ya sh. milioni ambayo inatakiwa kuilipa kabla ya kucheza mechi inayofuata.

Kamati hiyo iliyokutana jana (Februari 9 mwaka huu) chini ya Mwenyekiti wake Tarimba Abbas, kwanza imelaani kitendo cha wachezaji wa timu hiyo kumzonga refa, kwani vitendo vya aina hiyo ndiyo vichocheo vya vurugu viwanjani.

Lakini pia imempongeza nahodha wa Kanembwa JKT, Mbeke Mbeke kwa kuwa mstari wa mbele kuwazuia wachezaji wenzake waliokuwa wakimpiga refa wa mchezo huo.
Vilevile Kamati hiyo imesema aliyesababisha matatizo hayo ni refa Mujaya, na ingawa ilikuwa na uwezo wa kumchukulia hatua lakini haikufanya hivyo kwa vile hakukuwa na mlalamikaji na tayari Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilishamwadhibu.

MAJINA YA MABINGWA WA MIKOA MACHI 30
Vyama vya Mpira wa Miguu vya mikoa vimetakiwa kuwasilisha majina ya mabingwa wao kufikia Machi 30 mwaka huu kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL).

Timu zote zitakazofuzu kucheza RCL zinaruhusiwa kusajili wachezaji wapya wasiozidi watano kutoka ndani ya mkoa kwa kufanya taratibu za uhamisho. Kamati imesisitiza kuwa usajili wa RCL ni uleule uliotumika kwenye Ligi ya Mkoa.

Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana Februari 6 mwaka huu imekataa ombi la Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) kuongeza timu za Ligi ya Mkoa kutoka 20 hadi 24.

Ikiwa chini ya Mwenyekiti wake Geofrey Nyange, Kamati hiyo imesema kwa mujibu wa Kanuni ya Ligi ya Mkoa, ligi hiyo inatakiwa kuwa na timu kati ya 16 na 20, hivyo vyama vya mpira wa miguu vya mikoa vinatakiwa kuendesha ligi kwa kufuata kanuni.

Kamati hiyo imeongeza kuwa hata kama ingekubalia ombi la MZFA kiutaratibu lisingewezekana kwa vile kanuni hufanyiwa marekebisho baada ya msimu kumalizika, wakati ombi hilo limewasilishwa katikati ya msimu.

KOCHA MARSH ASUBIRI VIPIMO VYA MWISHO
Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Sylvester Marsh ambaye amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) anasubiri vipimo vya mwisho ili aweze kuanza matibabu.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtoa kocha huyo nyumbani kwake jijini Mwanza na kumleta Dar es Salaam kwa lengo la kuhakikisha anapata matibabu zaidi na kwa uangalizi wa karibu.

Tayari majibu ya kipimo cha kwanza yameshapatikana, hivyo yanasubiriwa majibu ya kipimo kingine ili aweze kuanza rasmi matibabu, lengo likiwa ni kubaini kitaalamu ugonjwa unaomsumbua.

KIKOSI CHA TWIGA STARS KUAGWA FEB 12
Timu ya Twiga Stars itaagwa rasmi Jumatano (Februari 12 mwaka huu) tayari kwa safari ya Lusaka, Zambia kwa ajili ya mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) ambayo fainali zake zitafanyika Oktoba mwaka huu nchini Namibia.

Msafara wa timu hiyo itakayoondoka kwa ndege ya Fastjet utaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Ahmed Idd Mgoyi.

Hafla ya kuwaaga wachezaji wa timu hiyo itafanyika saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF. Timu hiyo itaondoka Februari 13 mwaka huu alfajiri tayari kwa mechi hiyo itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Rwanda.

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)