MAPOROMOKO YA ARDHI WILAYA YA MOSHI YAMSHTUA MBUNGE WA JIMBO LA VUNJO ,JAMES MBATIA.

May 02, 2016
Mbunge wa Jimbo la Vunjo akisalimiana na mmoja wa waathirika wa mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni na kusababisha kufusi kilichokuwa kando ya nyumba yake kuporomoka na kuhatarisha maisha yake katika kijiji cha Iwa ,Kirua Vunjo katika wilaya ya Moshi.
Mbunge wa jimbo la Vunjo James Mbatia akizungumza jambo mara baada ya kutembelea familia ambazo nyumba zao zimeathirika na mvua zilizonyesha hivi karibuni baada ya kuangukiwa na vifusi na kunusulika vifo.
Mbunge wa jimbo la Vunjo akitizama zoezi la uondoaji wa Vifusi vilivyo poromoka kutoka na mvua zinazoendelea kunyesha.
Sehemu ya Kifusi kilichoporomoka kando ya nyumba .
Mkazi wa kijiji cha Iwa ambaye nyumba yake iliathirika na maporomoko ya udongo yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha akimuonesha maeneo yaliyoathirika kuzunguka nyumba hiyo.
Mbunge wa jimbo la Vunjo James Mbatia akitiama sehemu ya nyuma ya nyumba hiyo ambapo pia udongo umeporomoka na kuhatarisha uwepo wa nyumba hiyo katka kijiji ch Iwa wilaya ya Moshi vijijini.
Sehemu ya Udongo ulioporomoka.
Mh akitizama nyumba nyingine iliyoathirika na maporomoko hayo ya udongo yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Mbunge wa Jimbo la Vunjo ,James Mbatia akizungumza na mmoja wa wananchi katika kijiji cha Iwa  ,Kirua Vunjo katika wilaya ya Moshi ambaye nyumba yake imeathirika baada ya kuangukiwa na kifusi baada ya kuporomoka .
Mh Mbatia akitoka katika nyumba iliyoathirika na udongo ulioporomoka huku akishauri familia hizo mbili kuhama kwa muda katika nyumba zao hizo hadi pale mvua zitakapo malizika kunyesha .
Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akisalimiana na wanafunzi wakati akipita kando ya barabara iliyoathirika na maporomoko ya udongo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Mbunge Mbatia akisaidia kumbebesha udongo mmoja wa vijana waliokuwa wakijaribu kurekebisha sehemu ya barabara iliyoathirika na mvua zinazoendele kunyesha.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaksazini.

KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII,MEJA JENERALI GAUDANCE MILANZI AWASILI MKOANI KATAVI KWA AJILI YA KUFUNGA MAFUNZO YA MFUMO WA JESHI USU KWA WAHIFADHI WA SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA (TANAPA

May 02, 2016
Ndege ndogo ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) iliyombeba Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Mpanda ,Meja Jenerali Milanzi anatarajia kufunga rasmi Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na Askari waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) yaliyofanyika katika Kambi ya Mlele iliyopo Hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenrali Gaudance Milanzi akipokelewa na mwenyeji wake Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Allan Kijazi alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani mkoani Katavi kwa ajili ya shughuli ya kufunga Mafunzo hayo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Mpanda
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Mtango Mtahiko.
Mkurugeni wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) akimuongoza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudance Milanzi ,kuelekea chumba cha mapokezi cha watu mashuhuri katika uwanja wa ndege wa Mpanda mkoani Katavi.
Watendaji wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) wakiongozwa na Meneja Mawasiliano wa Shirika hilo Pascal Shelutete wakiwa katika mkoa wa Katavi kwa ajili ya shughuli ya ....

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini aliyeko mkoani Katavi.
WAMBURA-SITAKUBALI RASILIMALI ZA TAIFA HILI ZICHEZEWE

WAMBURA-SITAKUBALI RASILIMALI ZA TAIFA HILI ZICHEZEWE

May 02, 2016

a1Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Anastazia Wambura(wa pili kushoto) akipata msaada wakati akiteremka toka katika kiwanja cha shirika la utangazaji Tanzania(TBC) kulipojengwa nyumba za watumishi wa shirika hilo ambazo hazijaisha kwa zaidi ya miaka 20 sasa na kutoa maagizo ya kumalizia nyumba hizo au kuwapa Halmashauri ya Kisarawe ili wajenge Hostel za wanafunzi.(Picha na Daudi Manongi-WHUSM)
a2Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa shirika la utangazaji Tanzania(TBC) Bi.Joselin Lugola akitoa mrejesho kuhusu nyumba za shirika hilo zilizo kisarawe mkoani Pwani ikiwemo kukamilisha upatikanaji wa hati  wa eneo hilo na kuliendeleza ili watumishi wa TBC wa kisarawe walitumie kwa makazi.
a3 
Kaimu mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Bi.Nahya Mansour(wa kwanza kushoto) akimskiliza Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Anastazia Wambura(hayupo pichani) wakati akitoa maagizo juu ya nyumba za Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) zilizopo eneo la kimani Kisarawe mkoa wa  Pwani.wengine pichani ni Mkurugenzi mtendaji wilaya ya Kisarawe Bi.Mwanamvua Mrindoko(wa pili kushoto).
a4 
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Anastazia Wambura akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa shirika la utangazaji Tanzania(TBC) Bi.Joselin Lugola wakati alipofanya ziara katika nyumba za shirika hilo zilizopo kisarawe mkoani Pwani.
……………………………………………………………………………………….
Na.Daudi Manongi-WHUSM
Naibu Waziri Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura ametoa wito kwa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) kutunza Rasilimali za Taifa kwa kuwa ni pesa inayotoka na jasho la mlipa Kodi na ingeweza kutumika kwa kazi nyingine kuliko uharibifu unaofanyika katika kiwanja cha Shirika hilo kilicho eneo la kimani ambako zimejengwa nyumba za wafanyakazi wa shirika hilo waliopo kisarawe mkoa wa Pwani.
Mhe.Wambura alisema hayo wakati alipotembelea eneo la shirika hilo ili kupata mrejesho wa maagizo aliyotoa wakati alipofanya ziara ya kwanza katika eneo hilo Aprili 2011 mwaka huu na kuipatia siku saba Idara ya Miradi ya shirika hilo ikishirikiana na Halmashauri ya kisarawe kufanikisha upatikanaji wa hati miliki ya eneo hilo la makazi ya wafanyakazi wa shirika hilo.
“Taratibu za Kisarawe za upatikanaji wa hati zimekamilika na sasa wamepeleka ile Rasimu kwa kamishna wa hati kanda ya mashariki ,na maelezo tumeyaskia kwamba kulikuwa na kupishana katika uaandaaji wa hati ndo maana ikachelewa lakini kwa sasa hivi bado tunaitaji kulinda rasilimali za Taifa.Tunaitaji kuzuia uhalibifu”,Alisema Mhe Wambura.
Aidha Mhe Wambura ametoa maagizo kwa shirika hilo kuangalia uwezekano wa kuendeleza makazi hayo kwa kuwa mpaka sasa imepita miaka 20 eneo hilo halijaendelezwa na shirika hilo au kufanyiwa uwekezaji wowote au wakabidhi eneo hilo kwa halmashauri ya kisarawe ili wajenge hostel za wanafunzi na kuongeza kwamba yeye hatakubali eneo hilo lipotee kwa uharibifu kwa wananchi  kubomoa nondo na kuuza kama vyuma chakavu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) Bi.Joselin Lugola alimwahidi waziri huyo kuwa watahakikisha kwenye bajeti ya mwaka 2017/18 suala hilo linashughulikiwa  na kudai kwamba mara nyingi wanaweka pesa ya ukarabati lakini inakatwa lakini wataanza ukarabati kwa awamu kwa mikoa ya Arusha na Mwanza na makao makuu kwa hiyo hata izi za kisarawe zitakarabatiwa mara moja.
RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI MJINI DODOMA

RAIS DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI MJINI DODOMA

May 02, 2016

kib1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo Mei 2, 2016
kib2 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiendesha kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo Mei 2, 2016
kib3 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiendesha kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo Mei 2, 2016
PICHA NA IKULU

DAY ONE OF THE WORLD PRESS FREEDOM DAY 2016 COMMEMORATION IN PICTURES.

May 02, 2016
Registration in progress during the first day of the World Press Freedom Day Commemoration that is being held at Malaika Beach Hotel in Mwanza.
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DKT. ALI MOHAMED SHEIN AAPISHWA KUWA MJUMBE WA BARAZA LA MAWAZIRI

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DKT. ALI MOHAMED SHEIN AAPISHWA KUWA MJUMBE WA BARAZA LA MAWAZIRI

May 02, 2016

sg1 
Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman akimuapisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri ili aweze kushiriki na kutekeleza majukumu yake kwenye Baraza hilo huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia tukio hilo katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
sg2 sg3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya kuapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
sg4 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman mara baada ya tukio la uapisho.  PICHA NA IKULU
………………………………………………………………………………………………………………
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein leo asubuhi tarehe 02 Mei, 2016 ameapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri ili aweze kushiriki na kutekeleza majukumu yake ndani ya Baraza hilo.
Rais Shein ameapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma, tukio ambalo limeshuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Viongozi wengine walioshuhudia tukio hilo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo mchana ameongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Baraza la Mawaziri, uliopo Ofisi ya Rais TAMISEMI Mjini Dodoma.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
02 Mei, 2016
MECHI YA NDANDA VS YANGA

MECHI YA NDANDA VS YANGA

May 02, 2016

 Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Ndanda FC ya Mtwara na Young Africans umerudishwa nyuma kwa siku moja na sasa itachezwa Mei 14, 2016 badala ya Mei 15, 2016 kama ratiba ya awali inavyosomeka.
Taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema sababu za kurudisha nyuma mchezo huo Na. 218 utakaofanyika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara ni kuipa timu ya Young Africans nafasi ya kujiandaa na kusafiri kwenda nchini Angola kwenye mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Mbali ya mechi hiyo, kuna michezo miwili ambayo imesogezwa mbele kwa siku moja. Mechi hizo ni kati ya Simba na Mwadui ambayo sasa itachezwa Mei 8, 2016 badala ya Mei 7, 2016.
Sababu za mchezo huo kusogezwa mbele ni kwamba Mei 7, 2016 kutakuwa na mchezo wa kimataifa utakaozikutanisha Young Africans dhidi ya Esperanca ya Angola kuwania Kombe la Shirikisho.
Mchezo mwingine uliosogezwa mbele ni kati ya Kagera Sugar dhidi ya Azam FC ambao sasa utafanyika Mei 8, 2016 badala ya Mei 7, 2016.
Sababu za mchezo huo kusogezwa mbele ni Uwanja wa Kambarage Shinyanga. Mei 7, 2016 uwanja huo utakuwa na mchezo kati ya Stand United ya Shinyanga dhidi ya Coastal Union ya Tanga.
Kadhalika Ligi Kuu Tanzania Bara, inatarajiwa kuendelea  kesho Mei 3, 2016 kwa mchezo mmoja ambao Young Africans ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Jumatano Mei 4, 2016 Azam FC ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu ya Pwani kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Michezo hiyo itaanza saa 10.000 jioni na kurushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni ya Azam. 
KAMATI YA RUFAA YA NIDHAMU

KAMATI YA RUFAA YA NIDHAMU

May 02, 2016

wambura

Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kesho Jumanne Mei 3, 2016 saa 5:00 asubuhi itatangaza uamuzi wa rufaa nane zilizowasilishwa na kujadiliwa za viongozi, mchezaji na timu tatu zilizoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara 2015/2016.
 Kamati hiyo itatangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Mikutano wa ofisi za TFF, zilizoko kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Jumla ya rufaa nane zinazohusu timu, kocha, viongozi na mchezaji mmoja zilijadilikuwa na kamati hiyo kwa Jumapili Mei mosi, 2016 kwenye ofisi za TFF jijini.
Rufaa zilizojadiliwa kwenye kikao hicho ni za:
  1. Timu ya Geita Gold
  2. Choki Abeid ambaye ni Kocha Msaidizi wa timu ya soka ya Geita Gold FC
  3. Denis Richard Dioniz – Kipa wa Geita Gold
  4. Fatel Rhemtullah – Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora
  5. Saleh Mang’ola – Mwamuzi wa Soka wa Mkoa wa Dodoma
  6. Timu ya Soka ya Polisi Tabora
  7. JKT Oljoro Fc ya Arusha
  8. Yusufu Kitumbo – Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tabora
Wadau hao wa soka walikata rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati ya Nidhamu baada ya kamati hiyo kuwatia hatiani na kuwaadhibu kwa makosa ya kupanga matokeo ya michuano ya Ligi Daraja la Kwanza. Wakata rufaa wote walihudhuria kikao cha rufaa zao.  
Waziri Makamba awasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha

Waziri Makamba awasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha

May 02, 2016

jan1 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
jan2 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
jan3 
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akitoa ufafanuzi kuhusu wizara hiyo leo Bungeni mjini Dodoma.
jan4 
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Andrea Kigwangalla (kushoto) akiwa Bungeni leo mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Dkt. Ashatu Kijaji.
jan5 
Baadhi ya Wabunge wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
jan6Mwanafunzi wa kidato cha tatu kutoka shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini Mwanza Getrude Clement akiwa Bungeni leo mjini Dodoma kwa  mwaliko wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba ambapo Serikali imetambua na kuthamini mchango wake kwenye  utunzaji wa mazingira. Mwanafunzi huyo alihutubia viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu mabadiliko ya tabia nchi, uliofanyika New York Marekani.
jan7Mashududa walihusika katika zoezi la kuchanganya udongo wakati wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964, wakiwa Bungeni leo mjini Dodoma kwa  mwaliko wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba ambapo Serikali imetambua na kuthamini mchango wao katika kuuenzi na kuulinda Muungano wa Tanzania.
jan8Mwanafunzi wa kidato cha tatu kutoka shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini Mwanza Getrude Clement (wa pili kushoto) ambaye alihutubia viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu mabadiliko ya tabia nchi, uliofanyika New York Marekani akiwa na wanafunzi wenzake Bungeni leo mjini Dodoma.
jan10 
Naibu Spika Dkt Tulia Ackson na Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Mhe January Makamba wakiwa katika picha ya pamoja na mashuhuda waliohusika katika zoezi la kuchanganya udogo wakati wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964. Mashuhuda hao walikuja kutembelea Bunge leo Mei 2, 2016.
(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma)
………………………………………………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma.
Serikali inaendelea kusimamia mazingira na kuhakikisha mifuko ya plastiki inayotumika nchini iwe ni ile inayokidhi viwango vianvyokubalika ili kuondokana na changamoto ya kuzagaa kwa mifuko hiyo katika maeneo mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba alipokuwa akitoa hoja ya wizara yake kuidhinishiwa maombi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Makamba amesema kuwa sababu kubwa ya kusambaa kwa mifuko plastiki inatokana na mifuko hiyo kutolewa bure na hivyo kuchafua mandhari na kuziba mifereji sehemu mbalimbali hali inayosababisha athari kubwa katika mazingira.
“Asilimia kubwa kwenye mito, maziwa na fukwe za bahari imejaa mifuko ya plastiki, hali hii ni hari kwa usalama wa mazingira yetu” alisema Makamba.
Akiwasilisha hotuba yake, Waziri Makamba amesisitiza kuwa mifuko ya plastiki isiyotakiwa kutumika nchini ni ile yenye unene chini ya maikroni 50 ambayo hairuhusiwi kuzalishwa wala kuingizwa.
Kwa mujibu wa maelekezo ya bajeti ya mwaka wa fedha 2015/2016, Waziri huyo amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais imekamilisha kanuni mpya ya mifuko ya plastiki zinazorekebisha viwango vya unene unaoruhusiwa kutoka Maikroni 30 kwenda Maikroni 50.
Waziri Makamba amesema kuwa kanuni hizo tayari zimesainiwa kupitia tangazo la Serikali Na.271 la mwaka 2015 na kutolewa katika Gazeti la Serikali Julai 17, 2015 na kupewa Na. 29.
Kwa upande wake mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16 wa kidato cha tatu anayesoma shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini Mwanza Getrude Clement ambaye alihutubia viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu mabadiliko ya tabia nchi, uliofanyika New York Marekani amewahimiza Watanzania kutunza mazingira na kufauata maelekezo yanayotolewa na Serikali na wataalamu wa mazingira ili kuyatunza mazingira wanamoishi.
Getrude amesema kuwa amefarikjika kwa kuwawakilisha vijana wa Tanzania na dunia kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi ambapo mataifa 175 yalikutana kusaini makubaliano ya Paris.
Katika kuwahimiza vijana kujenga tabia ya kutunza mazingira, Getrde amewaasa vijana hasa wanafunzi kusimamia sauala la utunzaji wa mazingira wakiwa shuleni kwa kwa kujiunga na klabu mbalimbali ambapo yeye amejiunga na klabu ya “Mali Hai” iliyopo shuleni anaposoma.
Kwa upande wa Watanzania kwa ujumla kwenye utunzaji wa mazingira, Getrude amesema kuwa ni vema wajifunze kutoka mataifa mengine yanavyosimamia utunzaji wa mazingira hasa matumizi ya mifuko ya plastiki.  
Mwanafunzi huyo amekaribishwa na kutambulishwa kwa wabunge leo mjini Dodoma kwa heshima ya kuliwakilisha vema taifa wakati wa utiaji saini makubaliano ya namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki moon alimkaribisha Getrude kwa viongozi hao na kusema “Ni furaha yangu kumualika Getrude Clement ambaye pia ni mwakilishi wa vijana anayeishi Tanzania na anaziwakilisha sauti za vijana”.

MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI 2016 YAFANYIKA KITAIFA JIJINI MWANZA.

May 02, 2016

Bi.Valerie Msoka kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), akiongoza kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari kwa mwaka 2016 yanayofanyika kitaifa katika hoteli ya ufukweni ya Malaika Jijini Mwanza.
Na George Binagi
………………………………………………………………………………..
Kauli mbiu ya Maadhimisho haya mwaka huu ni “Kupata Taarifa ni Haki yako ya Msingi:Idai'”. Maadhimisho haya yanafanyika kitaifa kwa mara ya nne na yanalenga kukumbusha Umma na dunia kwa ujumla umuhimu wa vyombo vya habari kufanya kazi yake bila kuingiliwa na mtu ama chombo chochote. 
Zaidi ya wadau 250 wakihusisha waandishi wa habari wakongwe na wapya, wahariri, viongozi wa mashirika wahisani (ya kimataifa na ya hapa nchini) wawakilishi wa mihili ya nchi, wasomi wa vyuo vikuu na balozi mbalimbali wamekusanyika jijini hapa kwa maadhimisho hayo ambayo kilele chake ni kesho.
Watoa Mada katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2016 yanayofanyika Jijini Mwanza. Kilele cha Maadhimisho hayo kinafanyika kesho Mei 3,2016 ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman. Pia Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Nnauye pamoja na wageni wengine waalikwa wanatarajia kuhudhuria maadhimisho hayo.
Watoa Mada katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2016 yanayofanyika Jijini Mwanza. Kilele cha Maadhimisho hayo kinafanyika kesho Mei 3,2016 ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman. Pia Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Nnauye pamoja na wageni wengine waalikwa wanatarajia kuhudhuria maadhimisho hayo.
Usia Nkhoma Ledama ambae ni Afisa Habari kutoka UN Information Centre (Tanzania) akiwasilisha Mada katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika Kitaifa Jijini Mwanza.
Wanahabari na Wadau wa Habari wakiwa katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika Kitaifa Jijini Mwanza.
Wanahabari na Wadau wa Habari wakiwa katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika Kitaifa Jijini Mwanza.
Wanahabari na Wadau wa Habari wakiwa katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika Kitaifa Jijini Mwanza.
Wanahabari na Wadau wa Habari wakiwa katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika Kitaifa Jijini Mwanza.
Wanahabari na Wadau wa Habari wakiwa katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yanayofanyika Kitaifa Jijini Mwanza.