BENKI YA CRDB YAKABIDHI TIKETI ZA NDEGE KWA WASHINDI WA KAMPENI YA ‘SHINDA NA TEMBOCARD’

July 24, 2016

 
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB,
Tully Mwambapa (katikati), akifafanua jambo wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi
ya tiketi ya ndege ya kwenda Dubai kwa mshindi wa kampeni ya ‘Shinda na
TemboCard’, Juliana Utamwa (kushoto) katika hafla iliyofanyika makao makuu ya
benki hiyo jijini Dar es Salaama, mwishoni mwa wiki. Kulia ni Dorisia Nanage
ambaye ni ndugu yake atakayeambatana naye.
 
 
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kulia), akimkabidhi tiketi ya ndege ya kwenda Dubai mshindi wa kampeni ya ‘Shinda na TemboCard’, Juliana Utamwa katika hafla
iliyofanyika jijini Dar es Salaa.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB,
Tully Mwambapa (kushoto), akimkabidhi tiketi ya ndege ya kwenda Dubai, Dorisia Nanage
ambaye ataambatana na mshindi wa kwanza, Juliana Utamwa.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika makao makuu ya benki ya CRDB.
Wafanyakazi wa benki ya CRDB wakishuhudia tukio hilo.
 
 Mshindi wa Kampeni ya ‘Shinda na TemboCard’, Juliana Utamwa akizungumza
mara baada ya kukabidhiwa tiketi ya ndege ya kwenda Dubai na Mkurugenzi
wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki
ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto), katika hafla ya makabidhiano ya
zawadi kwa washindi wa kampeni hiyo iliyofanyika makao makuu ya benki
hiyo jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Maofisa wa benki ya CRDB wakishuhudia tukio la kukabidhi tiketi kwa washindi wa Kampeni ya ‘Shinda na TemboCard’
Maofisa wa benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
Ntahakikisha Serikali inahamia Dodoma :Rais Magufuli

Ntahakikisha Serikali inahamia Dodoma :Rais Magufuli

July 24, 2016

magMwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Rais Dk. Jakaya Kikwete akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM uliofanyika mjini Dodoma baada ya kuchaguliwa kwa kupigiwa kura za kishindo leo, kulia anayecheka ni Mwenyekiti mstaafu wa CCM Mzee Benjamin Williamo Mkapa..
………………………………………………………………………………………………………
Na. Immaculate Makilika- Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  amesema katika kipindi cha uongozi wake atahakikisha Serikali inahamishia makazi yake mjini Dodoma.
Amesema hayo leo, wakati alipokuwa  akihutibia wajumbe  wa Chama cha Mapinduzi(CCM) katika Mkutano Mkuu Maalumu  wa  Chama hicho uliofanyika  mjini Dodoma mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti.
“Nitahakikisha katika awamu ya uongozi wangu, Serikali inahamia Dodoma, najua viongozi wengine wote nao watanifata, kwa kuwa sasa miundombinu ya Dodoma inaweza kukidhi mahitaji yote” alisema Rais Magufuli.
Rais Magufuli aliendelea kusema kuwa katika kipindi cha miezi nane ya uongozi wake chini ya Serikali ya Awamu ya Tano  ameweza kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuanza kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Akiongelea maeneo ya utekelezaji katika kipindi chake Dkt. Magufuli alisema kuwa mpaka sasa Serikali imefanikiwa kusimamia suala la utoaji wa elimu bure kwa shule za Msingi na Sekondari nchini na kuwezesha udahili kuongezeka zaidi tofauti na miaka iliyopita.
Aidha Dkt. Magufuli alisema kuwa Serikali yake pia imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika ukusanyaji wa mapato ya serikali hali itakayosaidia kuimarisha utoaji wa huduma muhimu za jamii.
Aidha, Serikali ya Awamu ya Tano imeagiza  ndege mbili mpya zinazotarajiwa kuwasili nchini Septemba mwaka huu,
Rais Dkt. Magufuli aliongeza kuwa Serikali yake kwa kushirikiana na Serikali ya Uganda wamefanikiwa kujenga bomba la kusafirisha mafuta kutoka Hoima katika ziwa Alberti nchini Uganda kwenda bandari ya Tanga ambapo mafuta hayo yatasafirishwa sehemu mbalimbali duniani na bombahilo  litazalisha zaidi ya ajira 20,000.
Vile vile, Rais Magufuli alisema kuwa Serikali yake imeweza kurudisha nidhamu ya kazi kwa watumishi wa umma  na kuweza kuondoa watumishi hewa waliokuwa na waliokuwa wamefikia 12,500,na  kuongeza kuwa kwa mwaka huu Serikali imetenga fedha za matumizi jumla ya shilingi trilioni 29.5, ambapo asilimia 40 ya fedha hizo zitapelekwa katika kutekeleza  shughuli za maendeleo.
Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ulihudhuriwa na wajumbe zaidi 2,000  ulimpitisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mshindi na Mwenyekiti wa Chama hicho kwa kura 2398  kati ya kura 2398 zilizopigwa ikiwa ni sawa na asilimia 100.
Rais Magufuli anakuwa  Mwenyekiti wa awamu ya Tano baada ya  kupokea uongozi huo kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama hicho anayemaliza muda wake Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka 10.

NAIBU WAZIRI MALIASILI NA UTALII, ENG. RAMO MAKANI ATEKELEZA AHADI YA SERIKALI ALIYOITOA BUNGENI YA KUTEMBELEA ENEO LA MGOGORO WA HIFADHI YA SAYAKA

July 24, 2016

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa pili kulia) akikagua eneo la mpaka katika Msitu wa Hifadhi wa Sayaka katika Kijiji cha Bugatu, Wilayani Magu, Mkoa wa Mwanza hivi karibuni. Anayeongoza utambuzi wa mpaka huo ni Afisa Misitu na Nyuki TFS Wilaya ya Magu, Ayoub Mikae (wa tatu kulia). Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Magu, Boniventure Kiswaga.  Eng. Makani aliahidi kwa niaba ya Serikali kupitiwa upya maeneo yoye ya Hifadhi yenye migogoro nchini kwa ajili ya kutafutiwa suluhu ya kudumu. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (wa sita kushoto) akiwa na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Magu na baadhi ya Wananchi wa vijiji vinavyozunguka Hifadhi ya Msitu wa Sayaka wakikagua mpaka wa hifadhi hiyo hivi karibuni. Kinachoonekana mbele yao ni Kigingi cha mpaka kinachodaiwa kusogezwa mbele na wananchi wa maeneo hayo kwa ajili ya kumega eneo la Hifadhi. 
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kulia) akizungumza na wananchi wa vijiji vinavyozunguka Hifadhi ya Msitu wa Sayaka katika Kijiji cha Bugatu Wilayani Magu Mkoani Mwanza hivi karibuni. Aliahidi kwa niaba ya Serikali kupitiwa upya maeneo yoye ya Hifadhi yenye migogoro nchini na
kutafutiwa suluhu ya kudumu. 
Naibu Waziri Maliasili , Eng. Ramo Makani (kulia) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Bugatu, Wilaya ya Magu, Mkoani Mwanza hivi karibuni wakati akikagua ramani ya Hifadhi ya Msitu wa Sayaka kubaini maeneo ya mpaka yenye mgogoro. Eng. Makani aliahidi kwa niaba ya Serikali kupitiwa upya maeneo yoye ya Hifadhi yenye migogoro nchini kwa ajili ya kutafutiwa suluhu ya kudumu
Mbunge wa Jimbo la Magu, Boniventure Kiswaga (kulia) akizungumza na wananchi wa Jimbo lake katika Kijiji
cha Bugatu Wilayani Magu hivi karibuni.
Mwananchi wa Kijiji cha Salama kilichopo kandokando ya Hifadhi ya Msitu wa Sayaka Wilayani Magu, Charles Kassandiga (kushoto) akitoa ombi kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho la kupatiwa maeneo ya kulima na kufuga kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kulia). Eng. Makani aliahidi kwa niaba ya Serikali kupitiwa upya maeneo yoye ya Hifadhi yenye migogoro nchini na kutafutiwa suluhu ya kudumu. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kushoto) akiongoza kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama cha Wilaya ya Magu alipotembelea Wilayani humo hivi karibuni kuona eneo la mgogoro katika Hifadhi ya Msitu wa Sayaka ambapo aliahidi kwa niaba ya Serikali kupitiwa upya maeneo yoye ya Hifadhi yenye migogoro nchini na kutafutiwa suluhu ya kudumu.
 
NA HAMZA TEMBA – WMU
_____________________________________
Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeahidi kupitia upya maeneo yote ya Hifadhi
nchini yenye migogoro ya ardhi kwa ajili ya kuyatafutia suluhu ya kudumu kwa
kutumia mbinu shirikishi.
 
Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Eng. Ramo Makani wakati akizungumza na
Wananchi wa vijiji vinavyozunguka Hifadhi ya Msitu wa Sayaka katika Kijiji cha
Busega Wilayani Magu Mkoani Mwanza.
 
Eng. Makani alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano imekusudia kubadilisha mfumo wa utendaji
Serikali ambapo kwenye utatuzi wa migogoro iliyopo kwenye maeneo ya hifadhi
nchini itatatuliwa kwa kuwashirikisha wananchi wa maeneo husika na kuweka
kumbukumbu sahihi za makubaliano kufikia suluhu ya kudumu.
 
“Maeneo yote yenye migogoro tunaenda kuyapitia upya, tukija kwenye utatuzi tutawashirikisha
wananchi kupitia Serikali zao za Vijiji ambazo wajumbe wake watahusika kwenye
makubaliano kwa kuzingatia umuhimu na faida za Uhifadhi lakini huku
tukihakikisha tunajibu kero zinazowakabili” Aliesema Eng. Makani.
 
Aliongeza kuwa wakati wa kutatua migogoro hiyo yataainishwa maeneo kwa ajili ya shughuli za ufugaji
na kilimo kuepusha muingiliano kati ya wakulima na wafugaji pamoja na kuepusha
uvamizi kwenye maeneo ya Hifadhi yaliyoainishwa, utaratibu huo utazingatia sheria,
kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali ya Serikali.
 
Awali akizungumzia mgogoro wa Hifadhi ya Msitu wa Sayaka, Eng. Makani alisema kuwa, uamuzi
wa kufika katika eneo hilo la mgogoro ni kuona uhalisia kabla ya kuchukuliwa
hatua za kumaliza mgogoro huo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Serikali
aliyoitoa bungeni hivi karibuni kwa Mbunge wa Jimbo la Magu, Boniventure
Kiswaga.
 
Katika mgogoro huo wananchi wa vijiji vinavyozunguka Hifadhi hiyo walitoa malalamiko yao kwa
Naibu Waziri Makani kuwa maofisa wa TFS wamekuwa wakisogeza vigingi vya mpaka
wa eneo hilo kumega maeneo ya vijiji bila kuwashirikisha. “Sio kwamba tunapinga
Uhifadhi, lakini tunauliza kwanini vigingi vinahama kila mwaka kusogelea maeneo
yetu” Alihoji Mwanyekiti wa Kijiji cha Bugatu, Charles Kusenza.
 
Akijibu malalamiko hayo Afisa Misitu na Nyuki wa TFS Wilaya ya Magu, Ayoub Mikae
alisema kuwa, kilichokuwa kinafanyika sio kusogeza vigingi bali na kuimarisha
vigingi vilivyokuwepo ambapo utambuzi wake ulifanyika kitaalam kwa kutumia GPS.
Aliongeza kuwa baadhi ya wananchi wasio waadilifu walidaiwa kusogeza vigingi
vya mpaka wa Hifadhi hiyo ili wapate eneo la kulima jambo lililoleta taswira
tofauti wakati wa kufanya marekebisho sahihi kwa kutumia mtambo wa GPS uliosaidia
kubaini mpaka asilia.
 
Ayoub alisema kuwa sababu ya kuanzishwa kwa Hifadhi ya Msitu Sayaka ilikuwa ni kuhifadhi uoto
wa asili, kutunza vyanzo vya maji na kuhifadhi samaki wa Ziwa Victoria kwa kuwa
mto uliopo katika hifadhi hiyo unapeleka maji Ziwa Victoria.
 
Baada ya kusikiliza hoja mbalimbali za wananchi wa vijiji vinavyozunguka Hifadhi hiyo katika
mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Bugatu, Eng. Makani alisema kuwa tatizo
kubwa aliloliona katika mgogoro huo ni changamoto za Uhifadhi ikiwemo uelewa
hafifu wa baadhi ya wananchi juu ya umuhimu wa uhifadhi, ushirikishwaji hafifu wa
wananchi kwenye uwekaji wa vigingi na baadhi ya wananchi kuchanganya vigingi
vya hifadhi ya maji na hifadhi ya Msitu, changamoto ambazo alisema zitazingatiwa
kwa kina wakati wa utatuzi wa mgogoro huo.
 
Alisema kuwa “Tunahitaji uhifadhi endelevu, peke yetu bila wananchi hatuwezi, tunahitaji uhifadhi
rafiki, tukiwa na uelewa wa pamoja juu ya umuhimu wa uhifadhi na tukajibu kero
zenu mtatusaidia kulinda na kuhifadhi Maliasili zetu”. 
Kwa upande wa Wananchi wa vijiji vinavyozunguka hifadhi hiyo waliopewa fursa ya kuchangia na kuuliza
maswali kwenye mkutano huo walipaza sauti zao kuiomba Serikali kupitia Naibu Waziri huyo kuwasaidia maeneo ya kufuga na kulima kutokana na ufinyu wa maeneo uliosababishwa na ongezeko kubwa la watu. Naibu Waziri Makani Aliahidi kwa niaba ya Serikali kupitiwa upya maeneo yoye ya Hifadhi nchini yenye
migogoro na kuyatafutiwa suluhu ya kudumu kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali ya Serikali.