WAHANGA WA MAFURIKO,UKAME WAPATIWA MBEGU YA MTAMA .
NA FATNA MFALINGUNDI,KOROGWE.
Halmashauri ya wilaya ya Korogwe imetoa kilo
500 za mbegu ya mtama kwa Wananchi wake walioathiriwa na mafuriko na ukame katika
msimu huu wa kilimo ili kukabiliana na njaa kwa kuwa zao hilo linahimili ukame na hivyo
kuwahakikishia usalama wa chakula kwa
mwaka huu.
Akikabidhi
mbegu hizo juzi katika kijiji cha Mapangoni
kata ya Kerenge kilichoathiriwa na
mafuriko, Afisa Kilimo wa wilaya Kakulu Lugembe aliwaambia viongozi na wakulima
wa kijiji hicho kuwa halmashauri imetoa mbegu hiyo ili kuwakinga na upungufu wa
chakula unaoweza kutokea kutokana na mahindi
yao kusombwa na maji yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha mwishoni mwa
wiki.