TANGA UWASA KUKABIDHI VIFAA VYA UJENZI WA MADARASA KWA SHULE YA SEKONDARI MISALAI NA ZIRAI AMANI MUHEZA

March 17, 2015

MKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA JIJINI TANGA(TANGA UWASAMHANDISI JOSHUA MGEYEKWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU WIKI YA MAJI LEO

              
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu maadhimisho ya wiki ya maji

                       NA MWANDISHI WETU,TANGA.
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa)inatarajia kukabidhi vifaa vya ujenzi wa madarasa kwa shule ya sekondari za Misalai na Zirai zilizopo Tarafa ya Amani wilayani Muheza vyenye thamani ya milioni 1,110,00.

KUSHOTO NI KAIMU MENEJA WA HUDUMA KWA WATEJA WA MAMLAKA HIYO,ROGERS MACHAKU NA KULIA NI KAIMU AFISA MAHUSIANO WA MAMLAKA HIYO RAMADHANI NYAMBUKA WAKIFUATILIA KIKAO HICHO CHA WAANDISHI WA HABARI NA MKURUGENZI WA MAMLAKA HIYO

Vifaa hivyo ni kwa kutambua mchano wao mkubwa katika kuhifadhi chanzo cha maji cha Mto Zigi ambapo ili kuwa na Maendeleo endelevu kwa Muheza na Tanga ili kuhakikisha maji yanapatikana kwa muda wote kwa kutunza mazingira.


Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu maadhimisho ya wiki ya maji ambapo amesema kuwa mamlaka hiyo itamkabidhi Vifaa Mkuu wa wilaya ya Muheza,Esterina Kilasi ili avikabidhi kwa wahusika.



WAANDISHI WA HABARI WAKIFUATILIA MKUTANO HUO BAINA YAO NA MKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA JIJINI TANGA(TANGA UWASA),MHANDISI JOSHUA MGEYEKWA LEO
Alisema kuwa kuelekea maadhimisho hayo watafanya mikutano ya hadhara kwa kata sita za Jiji la Tanga ili kueleza shughuli wanazozifanya wateja wao na wajibu kwao ikiwemo kuwafafanulia haki zao kama wateja pamoja na kupata maoni yao katika kuboresha huduma wanazozitoa.

Aidha alisema kuwa katika wiki hiyo watazindua rasmi jengo jipya la huduma kwa wateja katika eneo la Pongwe ikiwa ni pamoja na kuzindua huduma ya malipo ya Ankara za maji kwa Tigo Pesa ambapo inatarajiwa kuzinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Said Magalula.

Ameongeza kuwa sambamba na hilo wataendesha dawati maalumu katika ofisi kuu swahili kwa lengo la kuwahudumia wateja wenye madeni sugu pamoja na kuwapa njia rahisi ya kulipia madeni yao na wale watakaolipa watasamehewa ada ya kutejesha maji katika kipindi cha Machi 16 mwaka 22 mwaka huu.

JAMII INAPASWA KUWEKEZA KATIKA SAYANSI NA TEKNOLOJIA-BALOZI SEFUE

March 17, 2015
                                           Na May-Zuhura Simba

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema kuwa ili jamii iweze kukua kwa kasi na kupata maendeleo haina budi kuwekeza katika sayansi na teknolojia.

Aliongea hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa warsha ya kupitia marejeo ya mfumo wa Taifa wa sayansi,teknolojia na ubunifu ulioandaliwa na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

“ubunifu katika sayansi na teknolojia ni kitu muhimu katika kupata uvumbuzi wa vitu mbalimbali muhimu vinavyoleta maendelao kwa jamii husika hivyo kuna umuhimu wa kuwafungia wanasayansi katika atamizi ili kupata matokeo mazuri ya utafiti” alisema Balozi Sefue.

Aidha aliongeza kuwa nchi kama Korea na Singapore waliwekeza katika sayansi,technologia na ubunifu na hivyo kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo kwa jamii zao.

Vilevile alisisitiza kuwa ubunifu ukisimamiwa dhabiti utasaidia katika kuleta mageuzi kwenye sekta muhimu ikiwemo elimu, afya,biashara,kilimo na miundombinu na hivyo kutatua matatizo ya kijamii.

“Mfano mzuri ni Max malipo ambalo ni zao la vijana wa kitanzania waliokuwa wamewekwa katika atamizi na kuleta uvumbuzi huu kwa kutumia sayansi na teknolojia ” alisema Balozi Sefue.

Aidha aliwataka wadau mbalimbali wa maendeleo,makampuni binafsi, na serikali kushirikiana kwa pamoja kufungua vituo atamizi zitakavyosaidia vijana kuvumbua teknolojia mbalimbali.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na wajumbe wa warsha wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo ya ubunifu wa sera ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia iliyoandaliwa na Wizara ya Mawasilano,Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa warsha ya ubunifu wa sera ya Taifa katika Sayansi na Teknolojia Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(katika) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Prof. Patrick Makungu(kushoto), na Naibu Katibu Mkuu wa Hiyo John Mngodo,warsha hito iliandaliwa iliandaliwa na Wizara ya Mawasilano,Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia John Mngodo akiwasalimia wajumbe wa warsha ya kupitia marejeo ya mfumo wa Taifa wa sayansi,teknolojia na ubunifu ulioandaliwa na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, kushoto ni Mkurugenzi wa Sayansi na Teknolojia Prof. Evelyn Mbede .
Mkurugenzi wa Sayansi na Teknolojia Prof. Evelyn Mbede, akiwasalimia wajumbe wa warsha ya kupitia marejeo ya mfumo wa Taifa wa sayansi,teknolojia na ubunifu ulioandaliwa na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Prof. Patrick Makungu, Katika ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na wa mwisho kulia ni Naibu katibu Mkuu waWizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia John Mngodo .
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Prof. Patrick Makungu, akisema hotuba ya kumakribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(Hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa warsha ya ubunifu wa sera ya Taifa katika Sayansi na Teknolojia iliandaliwa na Wizara ya Mawasilano,Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali ambao ni wajumbe wa mkutano wa ubunifu wa sera ya taifa ya Sayansi na teknolojia ilifanyika katika hoteli ya Kunduchi jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa na Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia.(Picha na Lorietha Laurence- Maelezo)
Waziri wa Maji Prof. Maghembe azindua Madhimisho ya 27 ya Wiki ya Maji Kitaifa

Waziri wa Maji Prof. Maghembe azindua Madhimisho ya 27 ya Wiki ya Maji Kitaifa

March 17, 2015

1
Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe akiakata utepe kuashiria uzinduzi wa Maadhimisho ya 27 ya Wiki ya Maji Kitaifa yanayofanyika katika mji wa Musoma mkoani Mara.
5
Waziri wa Maji Prof. Maghembe akihutubia wananachi.
2
Mkemia wa Wizara ya Maji, Rocho Mkole akitoa maelezo kwa Waziri wa Maji Prof. Maghembe wakati alipotembelea banda la wizara hiyo
3
Mhandisi wa Mazingira wa Idara ya Rasilimaji za Maji kutoka Wizara ya Maji, Eng. Modest Zakari akitoa maelezo kwa Waziri Prof. Maghembe kuhusu kilimo cha umwagiliaji.
4
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe akiangalia kifaa cha kupimia maji kwenye banda ya kampuni ya kampuni ya NFOSYS PS, huku Msambazaji Mkuu wa Wizara Crepi Bulamu na wataalamu wa kampuni hiyo na wakishuhudia.
  6
Burudani
……………………………….
Hussein Makame-MAELEZO
ZAIDI ya wananchi Milioni 7 wamepatiwa maji safi na salama katika miji ya mikoa, wilaya na miji midogo nchini kutokana na kuboresha huduma za majisafi na uondoaji majitaka mijini.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Maji Kitaifa yanayofanyika katika shule ya Msingi Mkendo mjini Musoma mkoani Mara.
Prof. Maghembe amesema uboreshaji huo ni kujenga, kukarabati na kupanua miundombinu ya majisafi katika miji mikuu ya mikoa, wilaya, miji midogo na miradi ya maji ya kitaifa.
AlisemaSerikali kupitia Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji imejenga miradi mipya 663 imejengwa katika vijiji 10 kwa kila halmashauri nchini na miradi 68 ya upanuzi na ukarabati kupitia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
“Utekelezaji huo umekamilisha miradi 731 iliyopangwa kutekelezwa na unajumuisha miradi 390 ambayo haikukamilika katika mwaka wa fedha 2013/2014” alisema Prof. Maghembe na kuongeza:
“Kuanzia mwezi Julai 2013 hadi mwezi Desemba 2014, jmla ya miradi ya maji 674 ilijengwa na kukamilika.Idadi hii inatokana na ujezni wa miradi mipya 433 ya vijiji 10 katika kila halmashauri na miradi mingine 241 ya upanuzi na ukarabati”
Alifafanua kuwa miradi hiyo imevipatia maji vijiji 900 na jumla ya vituo vya kuchotea maji 18610 vilivyojengwa ambavyo vinahudumia watu 4,568,402 na kuanzisha vyombo vya watumia maji 560.
“Usimamizi huo imepelekea kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama vijijini kutoka asilimia 40 Julai 2013 hadi asilimia 53.08 za sasa” alisema Profesa Maghembe.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kapteni Mstaafu Aseri Msangi aliwataka wananchi kutunza vyanzo vya maji ili kuhakikisha kuwa wanapata maji kwa muda wote.
Alikizungumzia hali ya maji Kapteni Mstaafu Msangi alisema kwa sasa upatikanaji wa maji vijijini ni asilimia 46.3 wakati maeneo ya mijini upatikanaji wa maji ni asilimia 53.5.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mbogo Futakamba aliwaasa wananchi, mashirika na wadau wote wa sekta ya maji kuunga mkono jhudi za kuboresha huduma za maji hapa nchini.
Alisema lengo la maadhimisho hayo ni kuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi watambue kuwa maji ni rasilimali muhimu katika kupiga vita umasikini na kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi.
Waziri Prof. Maghembe alisema Madhumuni ya Maadhimisho ya Wiki ya Maji ni kuhamasisha, kutoa elimu kwa umma kuhusu Sekta ya Maji na kusisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki katika mipango ya utunzaji wa rasilimali za maji na uhifadhi wa mazingira.
Maadhimisho ya 27 ya Wiki ya Majiyamebeba Kaulimbiu isemayo “Maji kwa Maendeleo Endelevu” ambapo yataambatana na uzinduzi au uwekaji mawe ya msingi ya miradi ya maji ikiwemo mradi mkubwa wa Maji wa mji wa Musoma.
Naibu Waziri wizara ya afya na ustawi wa jamii atembelea ujenzi wa hospitali ya rufaa ya kanda ya kusini

Naibu Waziri wizara ya afya na ustawi wa jamii atembelea ujenzi wa hospitali ya rufaa ya kanda ya kusini

March 17, 2015

1
Msanifu majengo Peter Laiser akiwaonesha ramani ya mchoro wa ujenzi huo.(Picha zote na wizara ya afya na ustawi wa jamii)
4 5
Muonekano wa jengo la wagonjwa wa nje(mapokezi) la hospitali ya rufaa ya kanda ya kusini mikoani mtwara.hadi kukamilika jengo hili litagharimu shilingi billioni 4 na litakua ni la ghorofa tatu.
MAMA SALMA KIKWETE AZURU LINDI/ AHUTUBIA MKUTANO MKUBWA LINDI MANISPAA, AKABIDHI BATI 100 NA VYOMBO VYA BENDI SHULE YA SEKONDARI ANGAZA

MAMA SALMA KIKWETE AZURU LINDI/ AHUTUBIA MKUTANO MKUBWA LINDI MANISPAA, AKABIDHI BATI 100 NA VYOMBO VYA BENDI SHULE YA SEKONDARI ANGAZA

March 17, 2015


1
Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Mwantumu Mahiza mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Lindi tarehe 15.3.2015 kuanza ziara ya kikazi ya siku 5 kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM.
11
Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama Cha Mapinduzi na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa Manispaa ya Lindi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kata ya Mikumbi tarehe 16.3.2015.
53
Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkabidhi kadi ya CCM Ndugu Shaibu Rajabu Matola mara baada ya kujiunga na chama hicho. Ndugu Matola ni miongoni mwa vijana 200 waliojiunga na Chama Cha Mapinduzi na kukabidhiwa kadi katika mkutano huo.
4
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Mwantumu Mahiza akisisitiza jambo wakati akiwahutubia mamia ya wana CCM na wananchi wa Lindi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Mikumbi katika Manispaa ya Lindi tarehe 16.3.2015.
10
Taswira mbalimbali za mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Mikumbi, Manispaa ya Lindi na kuhutubiwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete tarehe 16.3.2015.
13
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa Mama Salma Kikwete akikabidhi bati 100 na vifaa vya bendi kwa uongozi wa Shule ya Sekondari Angaza iliyoko katika Manispaa ya Lindi tarehe 16.3.2015. Anayepokea kwa niaba ya shule hiyo ni Mkuu wa Shule Mwalimu Upendo Muro (wa tano kutoka kulia) akiwa pamoja na Ndugu Ashimun Mzava, Afisa Elimu Sekondar, Manispaa Lindi wa nne kutoka kulia) na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo. Aliyesimama wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Lindi Bwana Abdallah Ulega.

Picha na John Lukuwi