Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Mheshimiwa Paul C. Makonda Leo Mei 18, 2017 akizungumza Na Watendaji wa
Sekta ya Ardhi Na Ujenzi wanaohudumu katika Manispaa za Ubungo,
Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la Dar es
salaam ametoa maelekezo 17 ya kuzingatia katika utendaji wao.
*1.*Watendaji wa Sekta ya Ardhi
Na Ujenzi Kushughulikia migogoro ya ardhi Na Ujenzi ili wananchi
wasipeleke malalamiko yao ngazi za juu.
*2.*Watendaji wa Sekta ya Ardhi
Na Ujenzi Wameagizwa kutoa vibali vya Ujenzi ndani ya mwezi mmoja Na
zoezi hilo lianze Mwezi wa sita mwaka huu 2017. Mwanzoni mwa mwezi wa
Saba kuzinduliwa teknolojia ambayo wananchi watapata taarifa zao za
Ardhi kwenye mtandao Jambo ambalo litafanya Dar es salaam kuwa kiganjani
mwa wananchi.
*3.*Wakuu wa Idara katika Sekta
ya Ardhi Na Ujenzi kuhakikisha wanatoa taarifa kuhusu Mipango ya Idara
kwenye vyombo vya habari kwa kuwatumia maafisa habari kwani tayari wana
mahusiano Na waandishi mbalimbali katika vyombo vyombo vya habari.
*4.*Wakuu wa Idara ya Ardhi Na
Ujenzi kutoa TAARIFA ya maeneo yote ya wazi yaliyotolewa Hati, Na
kujitokeza haraka kwa wote waliotoa Hati za maeneo ya wazi kama wapo.
*5.*Wakuu wa Idara ya Ardhi Na
Ujenzi kusimamia haraka upimaji wa maeneo yote ya Umma kama kama vile
Shule, Hospitali, Na Masoko kama alivyoagiza Waziri wa TAMISEMI sambamba
Na kutoa Mikakati wa Upimaji.
*6.*Wakuu wa Idara ya Ardhi Na
Ujenzi kuhakikisha ufanisi Na bidii ya utendaji inaongezeka hususani
mikakati ya kuhusisha wapimaji binafsi wanaotambulika kwani Mji ukipimwa
vyema Madiwani watafurahi lakini pia itakuwa njia rahisi ya kuepuka
migogoro ya Ardhi.