Benki ya UBA Tanzania wazidi kung'ara wiki ya huduma kwa wateja

October 03, 2017
 Afisa huduma kwa wateja wa Benki ya UBA Tanzania, Bi Stella Matau akifurahia kumuhudumia mmoja wa wateja wao wakubwa aliyefika katika benki hio huku benki hio ikiendelea kung'ara katika kutoa huduma bora kwa wateja kwa wakati wote
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya UBA Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wateja wao waliofika katika benki hio kwaajili ya kupata huduma za kibenki
Meneja Uendeshaji wa Benki ya UBA Tanzania, Bw Chriss Byaruhanga (wa Kwanza kushoto) akikata keko na baadhi ya wateja wao ikiwa ni ishara ya kuendeleza shamrashamra za wiki ya huduma kwa wateja ambapo wateja hao wameisifu benki hio kwa kutoa huduma bora wakati na sio kwa kipindi cha kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Meneja Uendeshaji wa Benki ya UBA Tanzania, Bw Chriss Byaruhanga akigawa keki kwa baadhi ya wateja na wafanyakazi wa benki hio ikiwa ni ishara ya kuzindua wiki ya huduma kwa wateja.
Mmoja wa wateja wa benki ya UBA Tanzania akipata huduma ya kuweka pesa 
Mkuu wa idara ya masoko wa benki ya UBA Tanzania, Brendasia Kileo akigawa keko kwa mmoja wa wateja waliokuwa wakipata huduma ndani ya benki mapema leo ikiwa ni muendelezo wa wiki ya Huduma kwa wateja
Wiki ya huduma kwa wateja inaendelea huku benki ya uba tanzania ikiendelea kutoa huduma bora na zenye kutimiza malengo ya wateja wao huku kituo chao cha huduma kwa wateja kikiendelea kushika hatamu kwa wateja wao kwa kuwapa huduma bora masaa 24. Uba Bank ambao hivi karibuni walijidhatiti tena kwa kuanzisha kituo cha huduma kwa wateja kwa masaa 24 wamezidi kuwapatia huduma bora wateja wao bila kuangalia kuwa ni wiki ya huduma kwa wateja wao Hutoa huduma bora siku zote.
Uba bank wanafurahi kuwahudumia wateja wao siku zote huku wiki ya huduma kwa wateja ikiendelea kuwa sehemu tu ya kuendeleza kutoa huduma bora kwa wateja.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN UZINDUZI WA MAKUMBUSHO MPYA YA OLDUVAI - NGORONGORO

October 03, 2017

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro, wengine pichani  ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) pamoja na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kulia). ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipiga makofi pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) pamoja na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kulia) mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipata maelezo mbali mbali kuhusu maisha ya binadamu na wanyama wa kale kutoka kwa Mhifadhi wa Mambo ya Kale kutoka Makumbusho ya Taifa Dkt. Agness Gidna mara baada ya kufungua Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia historia kuhusu maisha ya binadamu na wanyama wa kale iliyopo kwenye Makumbusho ya Olduvai mara baada ya kufungua Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia uzinduzi wa tovuti na mtanzao wa bure wa Hifadhi ya Ngorongoro mara baada ya kufungua Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.
:Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akihutubia mara baada ya kufungua kufungua Makumbusho mapya ya mambo ya kale katika bonde la Olduvai ndani ya hifadhi ya Ngorongoro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 33 WA JUMUIYA YA TAWALA ZA MITAA TANZANIA (ALAT) JIJINI DAR ES SALAAM LEO

October 03, 2017
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akiongea machache wakati wa kuanza kwa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Bw. Gulma Hafeez Muccadam akisoma risala yao mbele ya Rais Dkt magufuli wakati wa kuanza kwa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Suleiman Jaffo mbele ya Rais Dkt magufuli wakati wa kuanza kwa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Waziri Mkuu Mhe Kassim majaliwa akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kufungua wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifungua wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na meza kuu wakipata picha ya kumbukumbu na wadau wa maendeleo na wafadhili wakuu wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) baada ya kuufungua katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Makamu Mwenyekiti wa ALAT Bw. Stephen Mhapa baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Mstahiki Meya wa Dar es salaam Mhe. Isaya Mwita Baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.

SBL yatoa bajaji kwa wasambazaji wake bora

October 03, 2017

Meneja usambazaji wa SBL kanda ya Dar es salaam , Malila Mmasi akikabidhi funguo kwa mwakilishi wa kampuni ya Smart  Builders wakati wa makabidhiano kwa kampuni  nne zinazofanya vizuri katika usambazaji wa bidhaa zinazozalishwa na SBL,bajaj yenye thamani ya shilingi milion 3.9 kila moja kwa ajili ya kurahisisha shughuli zake za usambazaji, kwa ujumla bajaj hizo zina thamani ya sh milioni 15.6. Hafla ya makabidhiano zilifanyika mapema leo katika ofisi za makao makuu SBL Temeke Jijini Dar es salaam.
Meneja usambazaji wa SBL kanda ya Dar es salaam , Malila Mmasi akikabidhi mwakilishi wa kampuni ya Mount Cameroon.

Meneja usambazaji wa SBL kanda ya Dar es salaam , Malila Mmasi akikabidhi mwakilishi wa kampuni ya  kimori investment mara ya kuibuka mshindi wa msambazaji bora katika hafla iliyofanyika mapema leo Jijini Dar es salaam.

Maandalizi ya utafiti wa mafuta Ziwa Eyasi, Tanganyika yaanza

October 03, 2017

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, (mbele) akiongoza kikao kilichoshirikisha wataalam kutoka Uganda,  Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na  Madini, Shirika la Maendeleo  ya Petroli  Tanzania (TPDC) na Mamlaka  ua Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA) kabla ya kuanza ziara katika Ziwa Eyas Wembere lililopo mkoani  Singida.
Wataalam kutoka ,  Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na  Madini, Shirika la Maendeleo  ya Petroli  Tanzania (TPDC) na Mamlaka  ua Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA) wakifuatilia maelekezo  yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo  pichani).
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Robert Kasande (kulia) pamoja na wataalam kutoka Uganda wakifuatilia ufafanuzi  uliokuwa unatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo  pichani)
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi  Juliana Pallangyo (kushoto mbele) akieleza jambo katika kikao hicho.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akielezea hali ya utafiti wa mafuta na gesi nchini.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Robert Kasande akifafanua jambo katika kikao hicho.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Nishati na Madini, Asteria Muhozya (kulia) akibadilishana mawazo na Meneja Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki, Salum Mnuna katika kikao hicho

MWENGE WA UHURU WAZINDUA DUKA LA BIMA YA AFYA LA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA

October 03, 2017
 Sehemu ya muonekana kwa ndani duka la Bima ya Afya la Halmashauri ya Jiji la Tanga
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akiwa nje ya duka hilo akisubiri mapokezi ya mwenge wa uhuru kwenye duka hilo
 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akiwa na watumishi wa mfuko huo mara baada uzinduzi wa duka hilo katikati ni Macrina Clemence ambaye ni Afisda Matekelezo wa Mfuko huo na kulia ni Daktari Luiza Mtafi 
 Sehemu ya watumishi wa NHIF Mkoani Tanga katikati ni daktari Luiza Mtafi kushoto ni Afisa Madai NHIF Mary Daniel na kulia ni Afisa Matekelezo,Macrina Clemence
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kulia akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu wakifuatilia uzinduzi huo

WANACHAMA WA MTANDAO WA KIJANI KIBICHI TANZANIA WAKAGUA SHAMBA LA UWEKEZAJI MKUBWA WA KILIMO CHA PAPAI RUAHA, IRINGA

October 03, 2017
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita) Mkakati wa  Dkt. Kissui Stephen  Kissui akielezea malengo ya ziara YA Wakulima wanachama wa mtandao huo walipowasili katika  eneo la shamba  hilo lililopo Ruaha- Kware, wilayani Kilolo, mkoani Iringa, patakapolimwa zao la kibiashara la Papai. Kushoto kwake ni  Mkurugenzi Mtendaji na  Mwanzilishi wa mtandao huo, Adam Ngamange, Wa pili kushoto ni Afisa Mtendaji Kilimo na Mifugo wa Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo, John Mchopa, na Mwenyeji wa Shamba hilo na mkulima wa Ruaha, Amani Matinya.  

Dk. Kissui amesema lengo ya ziara hiyo ni kuwaonesha Wakulima wanachama wa Mkikita  mashamba wanayotarajia kuanza kulima kwa mkataba pia kuutangaza mtandao huo ili watu waanze kuwaza kijani na kila mtu arudi kwenye kilimo.

Alisema kama mtu hawezi kulima mwenyewe kuna wataalamu mbao watawekwa shambani kwa gharama nafuu ambao wataweza kuendeza mashamba hayo.

Pia,  Dk. Kissui alisema wanatumia mbegu za kisasa zinazozalisha mara tatu zaidi na mbolea za Organic  ambazo hazina madawa na haziharibu ardhi ili kuhakikisha vizazi na vizazi viweze kufurahia.

Alisema pia Mkikita husaidia kutafuta  masuala ya masoko duniani kabla ya kuanza kulima zao husika.

"Sisi tunaanza kutafuta masoko ya ndani na nje na baadaye tunawaaunganisha wakulima kwenye masoko" Alisema Kissui.
Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA) wakiwasili Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo, Mkoa wa Iringa wakati wa ziara ya kujionea shamba lenye ekari 3000 kwa ajili ya kuwekeza Kilimo cha PAPAI.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mkikita, Adam Ngamange akielezea miradi ya kuhamasisha kilimo na ufugaji kibiashara wakati wa ziara ya kutembela shamba kwa ajili ya kuwekeza kilimo cha PAPAI Ruaha -Kware Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania, Adam Ngamange alisema katika mtandao wanafanya miradi ya uhamasishaji kilimo na ufugaji kibiashara.

Alisema waligundua Watanzania wengi wanalima lakini si kibishara ambapo wameanza na miradi mitano katika maeneo maalum kama Ruaha  ambako waendesha kilimo cha Papai kwa kufuata taratibu zote za msingi  za kilimo hai.

Aliongeza kuwa mradi huo utakaoanza na ekari 384 zitakazogawanywa katika mafungu ya ekari 32 na kupandwa katika utaratibu wa kili mwezi mara moja ili waweze kusambaza papai kwenye masoko makubwa.
 Wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania wakitembelea na kukagua shamba kwa ajili ya kuwekeza kilimo cha PAPAI.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui (katikati) amueleza jambo Mwenyeji wa Shamba hilo na mkulima wa Ruaha, Amani Matinya.  
 Mwenyeji wa Shamba hilo na mkulima wa Ruaha (alienyosha mkono), Amani Matinya akiwaonesha wanachama wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania ukumbwa shamba hilo na mbinu zinazotumika kumwagilia.