KOREA KUSINI KUJENGA DARAJA LA KISASA LA SALANDER JIJINI DAR ES SALAAM LITAGHARIMU SH.BILIONI 100.4

November 18, 2014




*MOTO WATEKETEZA SOKO LA BIDHAA ZA UTAMADUNI LIJULIKANALO KAMA MT.MERU CURIOS & CRAFTS MARKET JIJINI ARUSHA.

November 18, 2014

Baadhi ya bidhaa zilizoteketea kwa moto katika SOKO la bidhaa za utamaduni lijulikanalo kwa jina la MT.MERU CURIOS& CRAFTS MARKET usiku wa kuamkia leo. 
 Wakazi wa Jiji la Arusha wakiangalia namna moto ulivoathiri soko hilo.
Bango la Soko hilo.
Hali si swari kabisa sokoni hapo.
Wengine wakiangalia kama watabahatika kuokoa chochote.
Wengine wakiokota mabaki ya mabati yaliyoungua.



Sehemu ya Wafanyabiashara wa SOKO la bidhaa za utamaduni lijulikanalo kwa jina la MT.MERU CURIOS & CRAFTS MARKET wakiwa wameduwaa bila kujua la kufanya mara baada ya Soko hilo kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo na kuunguza bidhaa zote za wafanya biashara zililopo katika soko hilo

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo ameagiza uchunguzi wa kina kufanyika kufuatia soko la wafanyabiashara wa Vinyago na bidhaa mbalimbali za kitalii la Maasai Market kuteketea kwa moto.

Mulongo ambaye alifatana na kamati ya Ulinzi na Usalama alishangaa kuona maduka hayo ambayo yapo jirani na Kikosi cha Zima Moto kushindwa kuzima moto na kusababisha hasara kwa wananchi.

"Sitakubali kuona uzembe unaendelea katika mkoa wetu,lazima watu wawajibishwe kwa uzembe hasa Kikosi cha kuzima moto ambao mko karibu na Ofisi za Chama Cha mapinduzi wilaya yalipo maduka haya"amesema Mulongo

Chanzo cha moto bado hakijaweza kufahamika huku maduka hayo yapatayo 188, huku yakiwa hayajaunganishwa na Umeme kwa lengo la kuepusha hatari ya moto kwani bidhaa nyingi ni vinyago vinavyotengenezwa kwa mbao.
Habari picha kwa hisani ya Othmani michuzi blog

KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI MKOA WA MANYARA CHAFANYIKA MJINI BABATI

November 18, 2014

 Baadhi ya wajumbe wa kikao cha ushauri cha Mkoa wa Manyara, (RCC) wakifuatilia kikao hicho kilichofanyika jana mjini Babati na kuongozwa na Mkuu wa mkoa huo Elaston Mbwilo.
 Ofisa elimu wa Mkoa wa Manyara, Ibrahim Mbang'o na baadhi ya wajumbe wakifuatilia jambo kwenye kikao cha ushauri cha mkoa huo (RCC) kilichofanyika jana mjini Babati.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara, Christina Mndeme (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Anatory Choya, wakiwa kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa huo (RCC) kilichofanyika jana mjini Babati
Rais Dk.Shein akutana na Uongozi wa Chama cha wapatholojia Tanzania.

Rais Dk.Shein akutana na Uongozi wa Chama cha wapatholojia Tanzania.

November 18, 2014

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na ujumbe wa Chama cha Wapatholojia wa Tanzania walipofika Ikulu Mjini Zanzibar  kwa ajili ya Kujitambulisha kwa Rais leo (wa pili kulia) Mwenyekiti wa Chama hicho Dk. Charles Massambu,[Picha na Ikulu.]Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na ujumbe wa Chama cha Wapatholojia wa Tanzania walipofika Ikulu Mjini Zanzibar  kwa ajili ya Kujitambulisha kwa Rais leo (wa pili kulia) Mwenyekiti wa Chama hicho Dk. Charles Massambu,[Picha na Ikulu.] unnamed 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na ujumbe wa Chama cha Wapatholojia wa Tanzania walipofika Ikulu Mjini Zanzibar  kwa ajili ya Kujitambulisha kwa Rais leo (wa pili kulia) Mwenyekiti wa Chama hicho Dk. Charles Massambu,[Picha na Ikulu.]
WAZIRI MKUU NA MATUKIO BUNGENI DODOMA LEO

WAZIRI MKUU NA MATUKIO BUNGENI DODOMA LEO

November 18, 2014


unnamed
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wabunge wa Viti Maalum, Amina Makilagi (kulia) na Mary Chatanda kwenye jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Novemba 18, 2014. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
unnamed1 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Mary Nagu akiwasilisha  Muswada wa Marekebisho ya Sheria  ya Ubia Baina ya Sekta  ya Umma na Sekta Binafsi wa mwaka 2014, bungeni mjini Dodoma Novemba 18, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
TATIZO LA MSONGAMANO WA MAGARI DAR KUTATULIWA

TATIZO LA MSONGAMANO WA MAGARI DAR KUTATULIWA

November 18, 2014

unnamed
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli(kulia),akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu ujenzi wa daraja lenye urefu wa kilometa 7.5 litakaloanzia eneo la Aghakani na kuishia Coco beach, ujenzi huo unaotarajiwa kuanza mapema mwakani na unafadhiliwa na Serikali ya watu wa Korea Kusini ,lengo ni kupunguza msongamano wa magari katika daraja la Serender,kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Dkt. Juma Iyombe. (Picha Lorietha Laurence –Maelezo)
………………………………………………………………………………………..
 Na Beatrice Lyimo -Maelezo
Zaidi ya Bilioni 110 zinatarajia kutumika katika ujenzi wa daraja lenye urefu wa kilometa 7.5 ili kupunguza msongamano wa magari  jijini Dar es Salaam.  
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli alisema daraja hilo litaanzia  eneo la Aghakani na kuishia Coco beach.
Waziri Dkt. Magufuli alisema daraja hilo litakalojengwa kwa msaada wa  Serikali ya Korea Kusini litakuwa  na njia nne na barabara mbili za huduma kwa kila upande lenye  uwezo wa kupitisha magari elfu 61 kwa siku .
“Serikali ya Korea Kusini imemaliza mradi wa ujenzi wa daraja la Kikwete pamoja na barabara ya Malagalasi Mkoani Kigoma na sasa tumewaomba waendelee kutoa  msaada kwa ajili ya ujenzi wa barabara mkoani Dar es Salaama ili kupunguza msongamano wa magari”, alisema Dkt. Magufuli.
Kwa upande wake  Mtendaji Mkuu kutoka TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale  amebainisha kuwa wataalamu kutoka Korea Kusini wameshafanya Upembuzi yakinifu uliomalizika hivi karibuni, hivyo ujenzi wa daraja hilo unatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwaka ujao.
Aliongeza kuwa daraja hilo litakalofahamika kwa jina la  New Salender Bridge litaunganishwa na barabara ya Ally Hassan Mwinyi kutokea Aghakani na kwa upande mwingine litaunganishwa na barabara ya Chole iliyopo Masaki.
Serikali imeweka mikakati mingi ya kupunguza msongamano wa foleni za magari kwa kuanzisha ujenzi mbadala wa barabara za juu unaotarajiwa kujengwa maeneo ya TAZARA,Mbagala rangi tatu hadi gerezani, kuanzishwa kwa kivuko cha Dar es Salaam hadi  Bagamoyo.
Pia utafanyika utanuzi wa  barabara nyingine za Dar es salaam kwenda Morogoro kupitia Chalinze na ile ya  Morocco hadi Mwenge na  Bagamoyo hadi Msata.
KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AMALIZA ZIARA YAKE JIMBO LA MTAMA

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AMALIZA ZIARA YAKE JIMBO LA MTAMA

November 18, 2014

 01 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Bernard Membe Mbunge wa jimbo la Mtama na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa wakati alipowasili katika Kiwalala Kituo cha Ufugaji cha Masister cha Narunyu ambapo ameshiriki kazi ya kukamua maziwa akiwa katika ziara yake ya kikazi ya mikoa ya Lindi na Mtwara akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali lakini pia  kuhimiza uhai wa Chama cha Mapinduzi CCM, Katibu mkuu Kinana katika ziara hiyo anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa,Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MTAMA -LINDI)3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kukamua maziwa katika kituo cha uugaji cha Masister cha Narunyu Mtama mkoani Lindi wakati alipotembelea kituo hicho.02Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi ya Masister mara baada ya kuwasili katika kituo hicho katika jimbo la Mtama mkoani Lindi.1 
Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo la Mtama wakiwa katika kikao cha ndani wakizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana . 7 
Mbunge wa jimbo la Mtama na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Maifa Mh. Bernard Membe akizungumza na wajumbe wa mkutano huo huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisikilizia wa pili kutoka kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi.   18 
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi. kushoto na Mbunge wa jimbo la Nchinga Mh. Said Mtanda wakicheza ngoma za asili ya kabila la Kimakonde wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika kata ya Chiuta jimbo la Mtama mkoani Lindi19 
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika mkutano huo. 24 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Chiuta leo. 23 
Mbunge wa jimbo la Mtama Mh. Bernard Membe akizungumza na wananchi wa jimbo lake katika kata ya Chiuta leo.

MWANAMUME MMOJA AUAWA NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA MTONI

November 18, 2014
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 18.11.2014.
  • MWANAMUME MMOJA AUAWA NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA MTONI NA WATU WASIOFAHAMIKA WILAYANI KYELA.
MWANAMUME MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA HENRY AMBAKISYE (60) MKAZI WA KIJIJI CHA KANDETE ALIKUTWA AMEUAWA NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA MAJINI KATIKA MTO KANDETE NA WATU WAWILI AMBAO BADO HAWAJAFAHAMIKA MAJINA WALA MAKAZI YAO.
 MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA KATIKA MTO HUO MNAMO TAREHE 17.11.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA KANDETE, KATA YA KAJUNJUMELE, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA.
 AWALI MNAMO TAREHE 15.11.2014 MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU WAKATI MAREHEMU ANATOKA NGOMANI AKIWA NA MWANAMKE MMOJA AITWAYE KISA KIMA (48) MKAZI WA KAPWILI ALIVAMIWA  NA KISHA KUSHAMBULIWA NA WATU HAO. AIDHA MWANAMKE HUYO BAADA YA KUONA HALI HIYO ALIKIMBIA NA KUTOWEKA ENEO LA TUKIO.
 MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NA MAJERAHA YA KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI UTOSINI.  CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI UGOMVI WA KUGOMBEA MWANAMKE.  KISA KIMA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA MAHOJIANO ZAIDI KUHUSIANA NA TUKIO HILO. AIDHA JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI ZINAENDELEA.
 Imesainiwa na:
          [BARAKAEL N. MASAKI – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
 IGP MANGU AONGEZA ASKARI KITETO

IGP MANGU AONGEZA ASKARI KITETO

November 18, 2014
E88A9486
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Ernest Mangu akimsikiliza Diwani wa Kata ya Matui Wilayani Kiteto Bw.Athuman Kidawa wakati alipofanya ziara wilayani humo kufuatia kuwepo kwa migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji iliyosababisha kutokea mapigano yaliyosababisha kutokea kwa  vifo.kushoto ni Afisa tarafa wa Matui Bw.Eliakimu Ndelekwa.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)E88A9514
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Ernest Mangu akizungumza na wananchi  wa Kata ya Matui Wilayani Kiteto wakati alipofanya ziara wilayani humo kufuatia kuwepo kwa migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji iliyosababisha kutokea mapigano yaliyosababisha kutokea kwa  vifo. (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)E88A9421
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Ernest Mangu akizungumza na Mtendaji wa Kijiji cha Chekanao, Kata ya Kiperesa , Wilayani Kiteto Bw.Omar Ndee (kulia) wakati alipofanya ziara wilayani humo kufuatia kuwepo kwa migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji iliyosababisha kutokea mapigano yaliyosababisha kutokea kwa vifo.Katikati ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Deusdedit Nsimike pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw.Japhet Chafu (Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Kiteto.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu ameahidi kuongeza idadi ya Askari katika kijiji cha Chekanao, kata ya Kiperesa wilayani Kiteto Mkoani Manyara kufuatia wananchi katika kijiji hicho kujitolea nyumba kwa ajili ya kuishi Askari kwa lengo la kuimarisha usalama katika maeneo yao kufuatia kuwepo kwa migogoro ya ardhi inayosababisha kutokea kwa mauaji.
IGP Mangu aliyasema hayo jana wakati alipokuwa katika ziara Wilayani Kiteto ya kujionea uharibifu uliojitokeza pamoja na kutafuta ufumbuzi wa migogoro hiyo iliyopelekea kutokea kwa vifo vya wakulima na wafugaji hivi karibuni katika wilaya hiyo ambapo watu kadhaa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana na vurugu hizo.
Alisema kufuatia kuwepo kwa umbali mrefu wa kituo cha Polisi na kijiji hicho atahakikisha askari wa kudumu wanakuwepo ili kushirikiana na wananchi katika kuwabaini wahalifu wanaofanya vurugu na kuendeleza migogoro hiyo ambapo wananchi nao waliahidi kujenga kituo cha Polisi.
Kwa upande wake Mtendaji wa Kijiji cha Chekanao Bw.Omar Ndee alisema wamekuwa wakipata shida kutokana na umbali mrefu wa kituo cha Polisi jambo ambalo limekuwa likifanya kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu vinavyochangiwa na migogoro ya ardhi katika wilaya ya Kiteto.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji hicho Japhet Chafu alilishukuru Jeshi la Polisi kwa kuimarisha usalama kijijini hapo tangu kutokea kwa mauji ya wakulima na wafungaji ambapo alibainisha kuwa bila kuwepo wao hali ingekuwa mbaya zaidi kutokana na kutokuwepo na muafaka baina ya wakulima na wafugaji.
“IGP hawa askari wako wasingekuwepo hapa usingekuta mtu lakini tunawashukuru sana hawa askari kwa kuwa hivi sasa hali ya usalama imerejea na hata shambani tumeanza kwenda” Alisema Bw.Chafu.
IGP Ernest Mangu alitumia ziara hiyo kuzungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, Wakaguzi wa Tarafa pamoja na Askari Kata ili kutafuta ufumbuzi wa migogoro hiyo na kuimarisha hali ya ulinzi na usalama.