NAMBA MAALUMU YAZINDULIWA KUCHANGIA MFUKO WA UKIMWI

October 21, 2017
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa namba maalumu ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi.  Wanaoshuhudia kulia kwake ni Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na  Mwenyekiti wa Bodi ya mfuko huo, Godfrey Simbeye. Kushoto kwa Mhagama ni Waziri wa TAMISEMI, Suleiman Jafo na anayemfuatia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Khamis Mwinyimvua.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (katikati) akifurahia pamoja na viongozi wenzake  mara baada ya uzinduzi huo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akimkabidhi hundi ya sh. milioni 660 Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Suleiman Jafo akimkabidhi hundi ya sh. milioni 200 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera ( kulia) kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Mererani. 
 Mwenyekiti wa bodi wa mfuko, Godfrey Simbeye akizungumza kabla ya uzinduzi wa namba hizo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk Leonard Maboko akizungumza kwenye tukio hilo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akitoa hotuba katika tukio hilo.
 Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera akisisitiza jambo baada ya kukabidhiwa hundi yake.

WANAFUNZI WATAKIWA KUJITENGA NA MATUMIZI YA SIMU NA TV YASIYO SAHIHI

October 21, 2017
Na Binagi Media Group
Shule za Eden ni za kutwa na bweni zikijumuisha shule ya Awali, Msingi na Sekondari zilizopo Jijini Mwanza.

Katika matokeo ya darasa la saba mwaka huu, wanafunzi wote wa Eden wamefaulu mtihani wao kwa kiwango cha juu na kuwa miongoni mwa shule tatu bora mkoani Mwanza zilizofanya vizuri.

Jana Oktoba 21,2017 ilikuwa siku ya Mahafali ya saba ya shule ya Sekondari Eden iliyopo Mandu Kata ya Nyakato Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza ambapo Meneja wa Shule za Eden anaeleza ubora wa shule hizo.
Wahitimu wa shule ya sekondari Eden iliyopo Mandu Kata ya Nyakato Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza wakiwa kwenye mahafali ya saba ya shule hiyo jana
Mkurugenzi wa shule za Eden, Joseph Mbabazi aliwataka wanafunzi kuzingatia maadili mema waliyofundishwa shuleni hapo wakati na baada ya mtihani wao wa kidato cha nne hatua ambayo itawaepusha na vishawishi na hivyo kutimiza ndoto yao kimasomo. Aidha aliwahisi pia wazazi na walezi kuzingatia malezi bora kwa watoto wao
Meneja wa shule za Eden, Mwl.Charllote Mbabazi akizungumza kwenye mahafali hayo
Mgeni rasmi, Mdhibiti wa ubora wa shule Kanda ya Ziwa Michael Cheyo, akizungumza kwenye mahafali hayo
Baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri shuleni hapo wakipokea zawadi
Mgeni rasmi akipokea zawdi kutoka kwa Mkurugenzi wa shule za Eden
Mgeni rasmi akisalimiana na Mkuu wa shule ya sekondari Eden
Wahitimu wa shule ya sekondari Eden wakipokea vyeti kutoka kwa mgeni rasmi
Meza Kuu
Wahitimu wa Eden sekondari wakionyesha michezo mbalimbali
Bonyeza HAPA kutazama picha zaidi za mahafali

WAKUU WA MASHIRIKA NA TAASISI ZA UMMA WABADILISHANA UZOEFU JIJINI DAR ES SALAAM

October 21, 2017
Mwenyekiti wa muda wa kundi la wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji  wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania, (TIC), Bw.Geoffrey Idelphonce Mwambe, (aliyesimama) akizungumza na baadhi ya wakuu wakuu hao, kwenye kikao cha kubadilishana uzoefu kwa nia ya kuongeza ufanisi ili kwenda sambamba na kasi ya serikali ya awamu ya tano. Mkutano huo ulifanyika makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam Oktoba 20, 2017
Mwenyekiti wa muda wa kundi la wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji  wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania, (TIC), Bw.Geoffrey Idelphonce Mwambe, (aliyesimama) akizungumza na baadhi ya wakuu wakuu hao, kwenye kikao cha kubadilishana uzoefu kwa nia ya kuongeza ufanisi ili kwenda sambamba na kasi ya serikali ya awamu ya tano. Mkutano huo ulifanyika makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam Oktoba 20, 2017. Kulia ni Katibu wa muda wa kundi hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, (HELSB), Bw. Abdul –Razak Badru


 Bw.Geoffrey Idelphonce Mwambe
 Bw. Abdul –Razak Badru
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchni, (TAA), Bw.Richard Mayongela, (kulia), akizungumza kwenye kikao hicho. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Magzeti ya Serikali, (TSN), Dkt. Jim Yonazi, na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bw.Laurean Bwanakunu.

Mkurugenzi Mkuu wa  Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, akizungumza kwenye kikao hicho. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, Bw. Edwin Rutageruka.

MPINA NA WAZIRI WA OMAN WAZUNGUMZIA MASUALA UWEKEZAJI WA VIWANDA KATIKA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI

MPINA NA WAZIRI WA OMAN WAZUNGUMZIA MASUALA UWEKEZAJI WA VIWANDA KATIKA SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI

October 21, 2017
DSC_0015
Katika picha, wa pili kushoto Mhe. Luhaga Mpina Waziri wa Mifugo na Uvuvi akizungumzia suala ya uwekezaji wa viwanda katika sekta ya mifugo wa pili kulia ni Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salim Al Ismail, akimsikiliza kwa makini. Kulia ni Balozi wa Oman nchini Mhe. Ali Mahroqi, na kushoto ni Katibu Mkuu Uvuvi Dkt. Yohana Budeba.
DSC_0018
Kushoto Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salim Al Ismail, akimtembeza Mhe. Luhaga Mpina Waziri wa Mifugo na Uvuvi katika meli ya Oman baada ya mazungumzo yalohusu sekta ya Mifugo na Uvuvi Dar es Salaam leo.
IMG_20171021_095809
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina kulia akijadili jambo na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Mhe. Salim Al Ismail, baada ya kuuonyeshwa mandhali ya meli ya Oman iliyotia nanga katika bandari ya Dar es Salaam.
IMG_20171021_110657
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina kulia akijadili jambo na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Mhe. Salim Al Ismail, baada ya kuuonyeshwa mandhali ya meli ya Oman iliyotia nanga katika bandari ya Dar es Salaam.
IMG_20171021_111352
Wakiwa katika picha ya Pamoja ,Waziri wa Mifugo na Uvuvi  Mhe. Luhaga Mpina, Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salim Al Ismail, Balozi wa Oman Nchini Mhe. Ali Mahroqi, Katibu Mkuu wa Wizara Uvuvi Dkt Yohana Budeba na watumishi wa Wizara hiyo baada ya Mawaziri hao kufanya mazungumzo kuhusiana na sekta ya Uvuvi na Mifugo leo ndani ya meli ya Oman iliyotia nanga katika bandari ya Dar es salaam.
…………………………………………………………..
NA; MWANDISHI MAALUM
Waziri anayeshughlia masuala ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amekutana na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salim Al Ismail na kujadili suala zima la uwekezaji wa viwanda katika Sekta ya Mifugo na Uvuvi.
Katika Mazungumzo hayo Waziri Mpina amemueleza  Waziri huyo wa uwekezaji wa Oman kuwa Tanzania imekuwa ikizalisha nyama kwa kiasi cha tani 36 kwa siku na imekuwa ikifanya biashara kwa kuuza tani za nyama ambazo hazijakatwa katika nchi za falme za kiarabu ikiwemo Oman, na wakati umefika sasa kwa nchi hizi mbili kushirikiana kwa pamoja katika Sekta hii kwa Oman kuwekeza katika Viwanda vya ndani vya nyama kwa kuendeleza viwanda vilivyopo na hata kujenga Viwanda vipya, akitolea mfano ujenzi wa kiwanda cha nyama cha Ruvu ambao umefikia 51% kukamilika.
“Tunataka viwanda vyote vya nyama vya ndani vikidhi mahitaji na kuweza kuuza nyama nje ya nchi”. Alisema Mpina.
Kwa upande wake Waziri Salim Al Ismail alipoelezwa kuhusu viwango na madaraja mbali mbali ya nyama nchini na mmoja wa mtaalam kutoka wizara hiyo, alisema kuwa Oman ipo tayari kuwekeza katika sekta ya viwanda vya nyama na kuisaidia Tanzania kutafuta soko la Marekani kupitia Oman kwani nchi hiyo ya Falme za kiarabu ina cheti  na kibali kilichothibitishwa na mamlaka ya chakula na dawa cha Marekani, “Tunaweza kuchukua nyama kutoka Tanzania na kuingiza Marekani bila kulipa Ushuru, tunapaswa kuwa na vyeti halali ili kuweza kupata soko katika nchi nyingine, Alisema Waziri Ismail.”
Waziri Ismail aliendelea kusema kuwa, Makampuni Binafsi kutoka Oman yapo tayari kufanya biashara katika eneo hili hivyo ni wakati wa Tanzania sasa kuonyesha utayari.
“Hizi bidhaa za nyama ni lazima zitoke kwenu sababu sisi hatuna maji wala majani ya kulisha mifugo kama ngombe, mbuzi na kondoo ambao huchinjwa kwa wingi baada ya Hijja. Alisisitiza.”