JIJI LA ARUSHA LANUFAIKA NA MIRADI YA BARABARA, ELIMU NA AFYA .

JIJI LA ARUSHA LANUFAIKA NA MIRADI YA BARABARA, ELIMU NA AFYA .

May 02, 2017
unnamed
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo afungua barabara ya Mahakama – St. James  wakati wa ziara yake Jijini hapa.
A
Jiwe la Msingi lililowekwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwenye barabara ya Mahakama – St. James
A 1
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(Pili kulia) akiwa na Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Jiji pamoja na Katibu wa CCM Wilaya wakikagua barabara ya Oljoro – Kisimani(4Km) iliyojengwa kwa kiwango cha Changarawe.
A 2
Kutoka Kulia ni Mhandisi wa Majengo Samwel Mshuza akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(Pili Kulia) ramani ya Kituo cha Afya Muriet kinachojengwa kwa mapato ya ndani ya Halomashauri ya Jiji.
A 3
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (mbele) akikagua ujenzi wa kituo cha Afya Muriet.
………………
Jiji la Arusha lina Mtandao wa barabara zenye urefu wa Km 334 na kati ya hizo barabara za Lami ni Km 86.7 tu na zilizobakia ni Changarawe pamoja na  barabara za udongo. Tangu Halmashauri hii ilipopata hadhi ya kuwa Jiji imeanza kutekeleza mkakati wa ujezi wa barabara za Lami kila mwaka  wa Fedha  kwa kutumia mapato ya ndani.
 Halkadhalika           Halmashauri imeendelea kutafta miradi kutoka Tamisemi na Mfuko barabara ili kuongeza mtandao wa barabara za Lami pamoja na changarawe kufanya mji huu kuendana na hadhi ya Jiji.
Mwaka wa Fedha 2016/2017 Halmashauri imeendelea na kazi ya uboreshaji wa miundombinu kwa kujenga barabara za Lami atika Maeneo ya Mahakamani – Kaloleni (0.65Km), Unga Ltd – Muriet (5.9 Km), Bp – Sunflag –Njiro (0.85) ambazo zote zimegharmu zaidi Tsh Bil 7 kutoka Mapato ya ndani, Mfuko wa barabara pamoja na Mradi wa Tscp.
Miradi yoyte ta barabara imefunguliwa, kukaguliwa na kutembelewa  na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo  wakati wa ziara yake iyokamilika mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo pia aliweza kufungua barabara ya Oljoro Kisimani iliyojengwa kwa kiwango cha changarawe (4 Km) pamoja na Ujenzi wa Daraja la Oljoro.
Kupitia ziara hiyo Mhe. Gambo ameweza kufungua madarasa 17 kwa niaba ya madarasa 60 ya Shule za Msingi yaliyojengwa, madarasa 7 kwa niaba ya madarasa 15 ya Sekondari na kutembelea ujenzi wa vituo vya Afya 2 maeneo ya Muriet na Moshono ambavyo vyote ujenzi wake umeanza kwa mwaka huu wa Fedha

WAZIRI LUKUVI AZINDUA MPANGO KABAMBE MTWARA

May 02, 2017
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi amefanya uzinduzi wa Mpango Kabambe (Master Plan) ya 2015-2035 Mkoani Mtwara . 
 
Katika shughuli hiyo Mh. Lukuvi aliwataka watendaji wa Mtwara katika sekta ya ardhi kwa kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa Bi. Halima Dendego kuhakikisha kuwa wanafuata Master Plan hiyo ili kuweza kuipanga Mtwara na kanda ya kusini yote vizuri hatimaye kufikia Tanzania yenye uchumi wa kati na Viwanda.

Katika ziara hiyo, mbali na kuzindua mpango kabambe pia alifanya ukaguzi katika mifumo ya ukusanyaji wa kodi ofisi za ardhi za halmashauri ya manispaa ya Mtwara ili kuhakikisha makusanyo ya kodi ya ardhi yanafanyika kwa malengo mahususi.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendego akiongea na wananchi mbele ya Waziri Lukuvi, alimhakikishia Mheshimiwa Waziri kuwa atasimamia utekelezaji wa mpango kabambe kikamilifu kwa maendeleo ya watu wa Mtwara  na watanzania kwa ujumla.

Katika uzinduzi huo Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango Miji na Vijiji, Bi. Imaculate Senje ameeleza kuwa uzinduzi huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza au koundoa kabisa tatizo la migogora ya ardhi mkoani mtwara, na kuchochoea fursa za uwekezaji, hivyo amewapa rai wananchi wa Mtwara kufuata mpango huo kwa maendeleo ya taifa.

Pia Ndugu Hamza Sikamkono Afisa Mipango Miji Manispaa ya Mtwara ameeleza kuwa dira ya mpango kabambe huo ni kuwa na mji mahiri wenye uchumi wa mafanikio ambao hutoa kazi na fursa za kutosha na kuvutia uwekezaji.

Afisa huyo ameeleza mpango huo umegusa maeneo ya Naumbu, Mjimwema, Nanguruwe na Ziwani ukigusa huduma zote za kijamii ikiwemo shule na hospitali na shughuli za kiuchumi yakiwemo maeneo ya viwanda na uwekezaji.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evodi Mmanda Baada ya kuwasili mkoani humo.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akizindua mpango kabambe mkoani Mtwara na Mkukabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendego.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akikagua mfumo wa ukusanyaji wa kodi ya pango la ardhi katika Halmashauri ya Mtwara ili kuhakikisha makusanyo ya kodi yanafanyika kwa ukamilifu.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akikagua masijala ya ardhi halmashauri ya Manispaa ya Mtwara na kuwataka Maafisa Ardhi kuweka kumbukumbu za Hati Miliki za Ardhi katika mpangilio mzuri ili kuepusha migogoro ya ardhi..
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akiongea na wananchi wa mkoa wa Mtwara katika uzinduzi wa Mpango Kabambe Mkoani hapo.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi (wapili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendego (wakwanza kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evodi Mmanda (wakwanza kulia), Mwenyekiti wa CCM Mtwara Ndugu Muhamed Sinani (wapili kulia) wakiwa katika uznduzi huo.
 Wananchi wa Mkoa wa Mtwara wakifuatilia Uzinduzi wa Mpango Kabambe (Master Plan) ya Mtwara.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango Miji na Vijiji Bi. Imaculate Senje akizungumza katika Uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Mtwara.
Ndugu Hamza Sikamkono Afisa Mipango Miji Manispaa ya Mtwara akizungumza katika Uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Mtwara.

BALOZI SEIF AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA MCT

May 02, 2017

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Uongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) uliofika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kubadilishana nao mawazo. Kulia ya Balozi Seif ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Bwana Kajubi Mukajanga na Kushoto ya Balozi ni Mkuu wa Ofisi ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) upande wa Zanzibar Bibi Shifaa Hassan .
Mkuu wa Ofisi ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) upande wa Zanzibar Bibi Shifaa Hassan akifafanua jambo mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif walipokutana nae kwa mazungumzo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Bwana Kajubi Mukajanga Kulia ya Balozi Seif akielezea mikakati ya Baraza la Habari Tanzania inavyofanya kazi Zanzibar katika kuhakikisha Maadili ya Habari yanazingatiwa na Wana Habari wote Nchini.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Bwana Kajubi Mukajanga akimkabidhi Balozi Seif Vitabu mbali mbali vilivyochapishwa na Baraza hilo kuhusu Tasnia ya Habari Tanzania.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa juu wa Baraza la Habari Tanzania mara baada ya kubadilishana mawazo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Bwana Kajubi Mukajanga na Muandishi wa Makala wa MCT Yussuf Mpinga.


Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Ofisi ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) upande wa Zanzibar Bibi Shifaa Hassan, Muhariri wa Machapisho wa MCT Khamis Mzee na Mkuu wa Kitengo cha Rasilmali Watu cha MCT Bivi Ziada Kilobo. Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inasubiri kuyapokea kwa ajili ya kuyafanyia kazi mapendekezo yatakayowasilishwa ya Rasimu ya Sera ya Habari Zanzibar katika kuona Sekta ya Habari Nchini inakuwa imara.

Alisema Taasisi zinazohusika na jukumu la kusimamia masuala hayo ni vyema zikahakikisha kwamba zinaharakisha mapendekezo hayo ili ile dhana ya Uhuru wa kupata Habari bila ya kuogopa inapatikana.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo yake na Uongozi wa Baraza la Habari Tanzania { MCT } ulioongozwa na Katibu Mtendaji wake Bwana Kajubi Mukajanga aliokutana nao hapo Afisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeahidi kutoa kila aina ya msaada katika kuona Sekta hiyo muhimu kwa jamii inawajibika ipasavyo katika kuwapasha Habari Wananchi.
RAIS DKT MAGUFULI AREJEA DAR ES SALAAM LEO BAADA YA KUHITIMISHA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU MKOANI KILIMANJARO

RAIS DKT MAGUFULI AREJEA DAR ES SALAAM LEO BAADA YA KUHITIMISHA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU MKOANI KILIMANJARO

May 02, 2017


das1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiswasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Aprili 2, 2017 akitokea mkoani Kilimanjaro alikokuwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
das2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Aprili 2, 2017  akitokea mkoani Kilimanjaro alikokuwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
das3
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar es salaam baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Aprili 2, 2017  akitokea mkoani Kilimanjaro alikokuwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
das4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar es salaam na kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya mkoa huo Kamishna Simon Sirro baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Aprili 2, 2017 akitokea mkoani Kilimanjaro alikokuwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
das5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar es salaam na kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya mkoa huo Kamishna Simon Sirro baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Aprili 2, 2017 akitokea mkoani Kilimanjaro alikokuwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
PICHA NA IKULU
…………………………………………………………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 02 Mei 2017, amemaliza ziara ya siku Tatu mkoani Kilimanjaro, ambapo akiwa mkoani hapa pamoja na mambo mengine alikuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani – Mei Mosi.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro – KIA, Rais Magufuli ameagwa na viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Said Mecki Saidick..
Jaffar Haniu,
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU,
Moshi, Kilimanjaro.
02 Mei, 2017
MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA KUMI NA TANO MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MEI 2, 2017.

MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA KUMI NA TANO MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MEI 2, 2017.

May 02, 2017
PIX1-Mhe.Spika akiongoza Bunge
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai  akiongoza kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
PIX2-Naibu waziri wa Fedha akizungumza
 Naibu Waziri  wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt,Ashatu Kijaji  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
PIX3-Mhe.Masauni
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamadi Masauni akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
PIX4-Mhe Kigwangalla
Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wazee na Watoto Mhe.Dkt Khamis Kigwangala akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
PIX5-Ole Nasha
Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.William Ole Nasha akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
PIX6-Juma jafo
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI Mhe.Selemani  Jafo akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
PIX7-Mhe.Muhongo
Waziri  wa Nishati na Madini Mhe.Prof.Sospeter Muhongo  akitolea ufafanuzi  hatua  zilizochukuliwa na Serikali juu ya Tetemeko la ardhi lilitokea Mkoani Kagera ivi Karibuni katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.PIX8-Mama kikwete na hawa ghasia
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe. Salma Kikwete na Mbunge wa Mtwara Vijijini (CCM) Mhe. Hawa Ghasia  wakijadili jambo  katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
PIX9-Mhagama na Jafo
 Waziri wa Sera,Bunge,Kazi ,Vijana ,Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama  akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI Mhe.Selemani  Jafo  katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
PIX11-Mhe.Peneza
 Mbunge wa Viti Maalum(CHADEMA) Mhe.Upendo Peneza akiuliza swali katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
PIX12-Mhe.Mabula akijibu swali
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
Z
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM) Mhe.Peter Serukamba akizungumza jambo na Mbunge wa Nzega Mjini Mhe.Hussein Bashe katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
Z 1
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Haki,Maadili na madaraka ya Bunge  Mhe.Almas Maige akisoma hoja za kamati hiyo kuhusu Shauri la kudharau Mamlaka ya Spika linalowahusu Mhe.Freeman Mbowe,Mhe Halima Mdee  na Mhe.Ester Bulaya na Shauri la kuingilia Uhuru  na Haki za Bunge linalowahusu Bw.Paul Makonda na Pastory Mnyeti katika kikao cha kumi na tano cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 2, 2017.
Picha Zote na Daudi Manongi- Dodoma MAELEZO,DODOMA
FAINALI YA KOMBE LA FA,SIMBA NA MBAO FC KUPIGWA MJINI DODOMA MEI 28.

FAINALI YA KOMBE LA FA,SIMBA NA MBAO FC KUPIGWA MJINI DODOMA MEI 28.

May 02, 2017
simba-vs-mbao-fc_dhgu8a1ys6nq1ny5m5d92i0r2
Hatimaye fainali ya Kombe la Shirikisho kati ya Mbao FC dhidi ya Simba itafanyika Mei 28 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Msemaji wa TFF, Alfred Lucas amethibitisha kwamba uwanja utakuwa ni Jamhuri.
“Kweli ni Jamhuri, awali ilikuwa ni droo lakini sasa moja kwa moja tumetangaza Jamhuri,” alisema leo.
Awali, kupitia mitandao ya kijamii, Rais wa TFF, Jamal Malinzi alitangaza uwanja utakaochezewa mechi utapatikana kupitia droo.
Malinzi alisema droo itafanyika ndani ya siku chache zijazo jambo ambalo lilizua mjadala mkubwa kati yake na mashabiki ambao walioenkana kumshangaza.
MASAUNI AFANYA KIKAO NA WAJUMBE WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI, JIJINI DAR ES SALAAM

MASAUNI AFANYA KIKAO NA WAJUMBE WA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI, JIJINI DAR ES SALAAM

May 02, 2017
A
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wajumbe wa Baraza lake pamoja na Wadau wa Kampuni ya Afritrack ambayo iliwasilisha katika kikao hicho Mfumo wa Ulipaji wa Tozo wa Papo kwa Papo kwa kutumia mashine za umeme. 
A 1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya Afritrack, Subel Sharif (kushoto) wakati alipokua anawasilisha mada katika kikao cha Wajumbe wa Baraza hilo, kuhusu Mfumo wa Ulipaji wa Tozo wa Papo kwa Papo kwa kutumia mashine za umeme. 
A 2
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Mafunzo na Uenezi wa Baraza hilo, Henry Bantu wakimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya Afritrack, Subel Sharif (hayupo pichani) wakati alipokua anawasilisha mada katika kikao cha Wajumbe wa Baraza hilo, kuhusu Mfumo wa Ulipaji wa Tozo wa Papo kwa Papo kwa kutumia mashine za umeme. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

VIDEO: KONGAMANO LA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI, KITAIFA JIJINI MWANZA.

May 02, 2017

Fuatilia yaliyojiri kwenye Kongamano la Wanataaluma na Wadau wa Habari kuelekea Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2017, lililofanyika kitaifa Jijini Mwanza.

Kilele cha Maadhimisho hayo ni kesho Mei 03,2017 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli.
#BMGhabari
Tazama hapa picha

BANZI AONYA BIASHARA ZA MAGENDO

May 02, 2017
ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Tanga, Mhashamu Anthony Banzi ameitaka serikali  kuzibiti biashara za magendo kwani madhara yake ni makubwa kiuchumi kutokana na bidhaa za hapa nchini kutopata soko uhakika.

Banzi aliyasema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na Blog ya Tanga Raha hii ambapo alisema bila kuwepo kwa jitihada za makusudi bidhaa za ndani zitakuwa zikikosa soko hali itakayopelekea kushuka kwa viwango vya uzalishaji badala ya kuongezeka kila wakati.

Alisema suala hilo lina madhara makubwa kiuchumi hivyo mamlaka husika zihakikishe zinalivalia njuga kwa vitendo ikiwemo kuwa mstari wa mbele kupambana nalo ili kuweza kuondosha.

Aidha pia aliwataka watanzania kuunga mkono na jitihada za kupambana na kwa kupiga vita biashara za magendo kutokana na kusababisha bidhaa zetu kukosa soko la uhakika na hivyo kuchangia uzalishaji kushuka.

“Watanzania lazima tuwe wazalendo na bidhaa ambazo zinaza lishwa hapa nchini kwa kuzipa nafasi kubwa ikiwemo kuachana na zile za magendo kwani madhara yake ni makubwa “Alisema Askofu Banzi.

Aidha alisema suala hilo ni moja kati ya mambo ambayo Serikali
inapaswa kulisimamia kwa waledi mkubwa ili liweza kuwa na tija ikiwemo kutoa elimu juu ya athari zake kwa jamii kila wakati.

“Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli ipo makini
kuendeleza watu wake kwa kuangalia namna ya kuwajali hivyo nashauri tufundishwe uzalendo kuanzia shule za msingi mpaka vyuo vikuu”Alisema

Akizungumzia suala la Uvuvi haramu,Askofu Banzi alisema madhara yake ni makubwa hasa kwa vizazi vijazo iwapo hakutakuwa na juhudi za makusudi za kupambana na suala hilo kwa vitendo wakati huu.

“Watu wanatumia uvuvi haramu hii ni hasara kwa Taifa na vizazi vijavyo hasa kiuchumi hivyo jambo hilo lianze kuweka mikakati kabambe ya kulitokomeza kabla halijaleta athari “Alisema.

Aidha pia alishauri kuwepo na utaratibu maalumu kwa wavuvi ambapo kila atakayekwenda kuvua baharini awe na kibali ili kuzibiti uharibifu wa mazingira kuchuma mali kwa kufuja.

RAIS DKT MAGUFULI AREJEA DAR ES SALAAM LEO BAADA YA KUHITIMISHA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU MKOANI KILIMANJARO

RAIS DKT MAGUFULI AREJEA DAR ES SALAAM LEO BAADA YA KUHITIMISHA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU MKOANI KILIMANJARO

May 02, 2017
das1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiswasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Aprili 2, 2017 akitokea mkoani Kilimanjaro alikokuwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
das2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Aprili 2, 2017  akitokea mkoani Kilimanjaro alikokuwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
das3
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar es salaam baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Aprili 2, 2017  akitokea mkoani Kilimanjaro alikokuwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
das4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar es salaam na kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya mkoa huo Kamishna Simon Sirro baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Aprili 2, 2017 akitokea mkoani Kilimanjaro alikokuwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
das5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dar es salaam na kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya mkoa huo Kamishna Simon Sirro baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Aprili 2, 2017 akitokea mkoani Kilimanjaro alikokuwa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
PICHA NA IKULU
…………………………………………………………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 02 Mei 2017, amemaliza ziara ya siku Tatu mkoani Kilimanjaro, ambapo akiwa mkoani hapa pamoja na mambo mengine alikuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani – Mei Mosi.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro – KIA, Rais Magufuli ameagwa na viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Said Mecki Saidick..
Jaffar Haniu,
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU,
Moshi, Kilimanjaro.
02 Mei, 2017
Maadhimisho Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Yaanza Mwanza

Maadhimisho Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Yaanza Mwanza

May 02, 2017
Mtaalamu wa Mawasiliano nchini, Innocent Mungy akiwasilisha mada kwenye kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza. Kongamano hilo lililoanza leo Mai 2, 2017 linamalizika kesho Mei 3. Mkurugenzi wa Wakfu wa Vyombo vya Habari nchini 'TMF', Ernest Sungura akiwasilisha mada kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza. Baadhi ya wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari wakiwa kwenye kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd, Francis Nanai akichangia mada katika mkutano huo. Mmiliki wa Kampuni ya Sahara Media Group, Antony Diallo akichangia hoja kwenye kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza. Kongamano hilo lililoanza leo Mai 2, 2017 linamalizika kesho Mei 3. Baadhi ya wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari wakiwa kwenye kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza. Baadhi ya wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari wakiwa kwenye kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza. Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-Tanzania, Salome Kitomari akifuatilia mijadala mbalimbali kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza. Kongamano hilo lililoanza leo Mai 2, 2017 linamalizika kesho Mei 3 linashirikisha wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari. Baadhi ya wanataaluma ya habari na wadau anuai wa vyombo vya habari wakiwa kwenye kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2017 linalofanyika jijini Mwanza.